Chama kipya chasajiliwa Tanzania

ipo haja ya kufuta vingine ambavyo kuanzishwa kwake hakuna maana yoyote,sawa maana inaweza kuwepo (katiba ya chama husika) lakini madhumuni yake kupitwa na wakati.
 
nadhani km si mtoto wakambo huyu sijui!,ila wenye akili TANZANIA WAPO WATAMG'AMUA TU.Baba akiwa ni yuleyule hata ukimbadilisha jina la baba ake huwezi kumbadilisha tabia zake
 
Chadema sio chama ww , ni wanaharakati. Na kuna mpango wa kukifuta kwenye orodha ya vyama vya siasa isajiliwe kwenye wizara ya mambo ya ndani ambapo wanaharakati walio na NGOs zao ndiko wanakosajiliwa na cdm ikasajiliwe huko

Halafu unajiita Genius Brain
 
Msajili wa vyama vya siasa nchini ndugu John Tendwa amekisajili kwa muda Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) kikiwakilishwa na mwenyekiti wa muda ndugu WALESI MAYUNGA.

Hii ni habari njema kabisa. Sioni tatizo la kuendelea kuanzisha vyama ukizingatia kwamba ndio kwanza tumetimiza miaka 20 tokea mfumo wa vyama vingi uanze. Vyama vingi vya upinzani vilivyosasa vimethibitisha kuwa ni CCM "B" (Ikiwemo NCCR-Mageuzi)Watanzania bado wanahitaji chama cha kweli cha upinzani, ambacho ndio kitakuwa mkombozi wa Umma, kwahiyo wenye nia ya dhati waendelee kuanzisha tu vyama, na ni matumaini yangu kuwa vyama vyote halisi na vyenye nia ya kweli vitaungana mbele ya safari na kukamilisha MAZIKO ya CCM.

Suala jingine la msingi hapa kama kweli tunataka udhibiti wa kuanzishwa vyama, basi ni kuwa na sheria ya wagombea binafsi, ili watu wenye uwezo wagombee bila zengwe. Kwa hali ilivyosasa, njia ya kwenda ikulu ni kupitia chama cha siasa tu na kama vyama vilivyopo ni longolongo, basi watu hawana budi kuendelea kuanzisha vyama vyenye misingi madhubuti na kuhakikisha ile "virus" ya CCM haingii ndani ya chama na kuvuruga kila kitu.
 
magamba watakaojitoa 2015 wakitoswa kupokelewa cdm, ndio wamejiandalia mallalio watakapo pumzika kugombania ruzuku
 
Huu ni mkakati mahsusi wa kuibomoa CDM 2015, nyuma ya chama hiki kipya kuna vigogo wengi ambao wanajua fika 2015 hawana lao CCM wala CDM. Imekaa kama CCJ vile, lengo ni kudeflect kura ili kuwa na vyama vingiiiiiiiiiii vitkavyonyang'anyana kura ili kuipunguzia nguvu CDM.

km vile ulikuwa mawazon mwangu, once nimesoma heading niliwaza hvo hvo! dah. . . .
 
Hii kauli ni ya kuhifaadhiwa sana moyoni na tunaichunguza sana tu ijapokua Mkigoma-Mzanzibari huyu ninayo mashaka sana kama aatakua aamepata kibali kuwa 'NAPE' wa Zitto Kabwe kiaina!!!

chama cha zitto kabwe, huku kigoma tunajiandaa kuhamia chama zitto, ukabila wa chadema umetuchosha.
 
Huyu ndio alitangaza kuwa atavifuta vyama visivyo na muelekeo, naona anaendelea kusajili vyama kama njugu. Hivi vyote ni njama ya Chama Cha Madhaifu aka CCM kupunguza spidi ya CHADEMA, kazi yao ni kusajili vyama utitiri vikifadhiliwa na wao wenyewe au vigogo wezi ndani ya chama chao kuhakikisha ukombozi wa taifa hili unacheleweshwa.
 
Hao hawana lolote!! wanataka kuwapotezea watu station/hot topic zinazojadiliwa saizi na vyombo vya habari na umma wa watanzania.....then watu wabadili topic,hatudanganyiki!!!
 
chama cha zitto kabwe, huku kigoma tunajiandaa kuhamia chama zitto, ukabila wa chadema umetuchosha.

Kama cdm iliyotambaa Nchi nzima mnadai ni ya ukabila, hiyo ya kgm tu si itakuwa ya UKA-JAAAA. Sidhani kama kuna Mha mjinga kiasi cha kukimbilia chauma kwa 7bu ya ukabila. Na hata hili jina la Zitto mnalitumia tu sidhani kama amewatuma.
UKEBHURA JOGO UKAMARA IBHINONKO.
 
Back
Top Bottom