Jaji Francis Mutungi ailima barua CHADEMA, ataka ijieleze ndani ya siku 5

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,729
218,289
Msajili wa Milele wa Vyama vya siasa nchini Tanzania , Francis Mutungi , ameokota taarifa mitandaoni ambako inadaiwa kuna video ya Aibu ya kiongozi wa ccm inasambaa mitandaoni .

Sasa Mtukufu Mutungi moja kwa moja kaisingizia Chadema.

---
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekiri kupokea barua kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, inayowataka wajielezea ndani ya siku tano, tangu kupokea barua hiyo.

Kwa kujibu wa barua hiyo ambayo bado haijawekwa hadharani ilipokelewa na chama hicho tangu Oktoba 2, 2023 mchana, kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ikitaka wajielezea kwa madai ya kurekodi maudhui ya video ya kumdhalilisha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

CCM inakishutumu chama hicho cha upinzani, ikidai kimerekodi maudhui ya video hiyo na kuyasambaza kwenye mitandao yake ya kijamii, pamoja na ya wafuasi wake, maudhui ambayo yanaashiria kutengenezwa kwa makusudi kwa lengo la kutaka kumshushia hadhi kiongozi wao.

Mwananchi Digital ilipomuuliza Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kuhusu barua hiyo, amekiri ni kweli japo aligoma kufafanua kwa madai yupo likizo.
"Siwezi kulifanunua jambo hili kwa undani niko likizo," amesema.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amekana chama hicho kuhusika na suala hilo huku akieleza hata mitandao ya chama hicho haijarekodi taarifa zinazoelezwa kupitia barua ya msajili.

"Toka nilipopokea barua hiyo Oktoba 2, 2023 nimepitia mitandao rasmi ya kijamii ya Chadema sijaona video hiyo. Nafahamu pia Chadema haijatengeneza video yenye maudhui kama hayo yanayolalamikiwa," amesema Mnyika.

Mnyika amedai Ofisi ya Msajili inaendelea kupokea malalamiko hayo kutokana na kanuni kandamizi za maadili ya vyama vya siasa za mwaka 2019 zilizotokana na marekebisho mabaya ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2019.

"Tunaendelea kutaka Katiba Mpya itakayowezesha kuwa na taasisi huru ikiwamo ofisi huru ya Msajili wa Vyama na kutungwa kwa sheria mpya ya vyama itakayolinda demokrasia, uhuru na haki za vyama vyama vya siasa," amesema.
 
Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania , Francis Mutungi
Heshima kitu cha bure, position ya Msajili wa vyama vya siasa ni lazima ishikwe na mtu mwenye title ya Jaji mstaafu, hivyo kumtaja lazima uiweke title yake proper, ile title kama ya udakitari wa heshima, it's a real title kama ya Dr, Adv, CPA. Eng. Prof. etc kumuita Francis Mutungi bila Jaji Francis Mutungi ni kumdharau!.
Nafasi nyingine zinazishikwa na Jaji mstaafu ni Mwenyekiti wa NEC, Mwenyekiti wa Tume ya Maadili na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Acha dharau!. And this is not the first time!, kiburi sii maugwana!.
P
 
Heshima kitu cha bure, Msajili wa vyama vya siasa ni Jaji mstaafu, hivyo kumtaja lazima uiweke title yake proper, ile title kama ya udakitari wa heshima, it's a real title kama ya Dr, Adv, CPA. Eng. Prof. etc kumuita Francis Mutungi bila Jaji Francis Mutungi ni kumdharau!. Acha dharau!. And this is not the first time!, kiburi sii maugwana!.
P
Vyeo vya mbeleko ni watu wanaojipendekeza tu wanaweza kutumia kama sehemu ya utambulisho.
 
Heshima kitu cha bure, Msajili wa vyama vya siasa ni Jaji mstaafu, hivyo kumtaja lazima uiweke title yake proper, ile title kama ya udakitari wa heshima, it's a real title kama ya Dr, Adv, CPA. Eng. Prof. etc kumuita Francis Mutungi bila Jaji Francis Mutungi ni kumdharau!. Acha dharau!. And this is not the first time!, kiburi sii maugwana!.
P
Heshima inatengenezwa na muhusika. kuna vitu ukivifanya vinakuvunjia heshima mwenyewe.. ndio maana wanasema heshima haiobwi ni automatic..wewe unamwombea heshima ......isitoshe huyo mtu ni jaji lakini ukiangalia mwenendo wake toka akalie hicho kiti huwezi kusema huyu mtu alifika level ya ujaji maana amekuwa akitekeleza mambo kisiasa zaidi kuliko proffessional.
 
Msajili wa Milele wa Vyama vya siasa nchini Tanzania , Francis Mutungi , ameokota taarifa mitandaoni anbako inadaiwa kuna video ya Aibu ya kiongozi wa ccm inasambaa mitandaoni .

Sasa Mtukufu Mutungi moja kwa moja kaisingizia Chadema.

---
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekiri kupokea barua kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, inayowataka wajielezea ndani ya siku tano, tangu kupokea barua hiyo.

Kwa kujibu wa barua hiyo ambayo bado haijawekwa hadharani ilipokelewa na chama hicho tangu Oktoba 2, 2023 mchana, kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ikitaka wajielezea kwa madai ya kurekodi maudhui ya video ya kumdhalilisha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

CCM inakishutumu chama hicho cha upinzani, ikidai kimerekodi maudhui ya video hiyo na kuyasambaza kwenye mitandao yake ya kijamii, pamoja na ya wafuasi wake, maudhui ambayo yanaashiria kutengenezwa kwa makusudi kwa lengo la kutaka kumshushia hadhi kiongozi wao.

Mwananchi Digital ilipomuuliza Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kuhusu barua hiyo, amekiri ni kweli japo aligoma kufafanua kwa madai yupo likizo.
"Siwezi kulifanunua jambo hili kwa undani niko likizo," amesema.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amekana chama hicho kuhusika na suala hilo huku akieleza hata mitandao ya chama hicho haijarekodi taarifa zinazoelezwa kupitia barua ya msajili.

"Toka nilipopokea barua hiyo Oktoba 2, 2023 nimepitia mitandao rasmi ya kijamii ya Chadema sijaona video hiyo. Nafahamu pia Chadema haijatengeneza video yenye maudhui kama hayo yanayolalamikiwa," amesema Mnyika.

Mnyika amedai Ofisi ya Msajili inaendelea kupokea malalamiko hayo kutokana na kanuni kandamizi za maadili ya vyama vya siasa za mwaka 2019 zilizotokana na marekebisho mabaya ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2019.

"Tunaendelea kutaka Katiba Mpya itakayowezesha kuwa na taasisi huru ikiwamo ofisi huru ya Msajili wa Vyama na kutungwa kwa sheria mpya ya vyama itakayolinda demokrasia, uhuru na haki za vyama vyama vya siasa," amesema.
Aibu ya ccm wanalimwa barua chadema?
 
Heshima kitu cha bure, Msajili wa vyama vya siasa ni Jaji mstaafu, hivyo kumtaja lazima uiweke title yake proper, ile title kama ya udakitari wa heshima, it's a real title kama ya Dr, Adv, CPA. Eng. Prof. etc kumuita Francis Mutungi bila Jaji Francis Mutungi ni kumdharau!. Acha dharau!. And this is not the first time!, kiburi sii maugwana!.
P
Mbona wewe pale kwenye ballot paper uchaguzi wa Kawe 1- man- Vote, Mahere hakukuweka Wakili msomi au Adv Pascal Mayalla? Mkuu acha kuchanganya mambo
 
Heshima kitu cha bure, Msajili wa vyama vya siasa ni Jaji mstaafu, hivyo kumtaja lazima uiweke title yake proper, ile title kama ya udakitari wa heshima, it's a real title kama ya Dr, Adv, CPA. Eng. Prof. etc kumuita Francis Mutungi bila Jaji Francis Mutungi ni kumdharau!. Acha dharau!. And this is not the first time!, kiburi sii maugwana!.
P
Mkuu Pascal Mayalla heshima huwa hailazimishwi hata kidogo , wewe endelea kulamba viatu vyao ili ubarikiwe au uteuliwe , sisi tuache tuendelee kuwataja kwa majina yao ya ubatizo , halafu tukutane mbinguni ili Mungu aamue .

Kama nimekosea kisheria nipe kifungu cha makosa yangu na adhabu yake .
 
Heshima inatengenezwa na muhusika. kuna vitu ukivifanya vinakuvunjia heshima mwenyewe.. ndio maana wanasema heshima haiobwi ni automatic..wewe unamwombea heshima ......isitoshe huyo mtu ni jaji lakini ukiangalia mwenendo wake toka akalie hicho kiti huwezi kusema huyu mtu alifika level ya ujaji maana amekuwa akitekeleza mambo kisiasa zaidi kuliko proffessional.
Umemfumua ubongo
 
Back
Top Bottom