Chama cha wasiokuwa na ajira

MY LOVE

Senior Member
Oct 17, 2012
161
68
wanajamii wa TZ, tatizo la ajira linazidi kuwa kubwa na tabaka la wenye nacho na wasionacho linazidi kuwa kubwa, hii inatokana na ukweli usiojificha kwamba waliotokea kwenye familia za viongozi au matajiri ndio wanaopata ajira hata kama hawana sifa.
Pia nasikia kuwa serikali haina hela ndio maana hawatoi ajira.

PENDEKEZO

  • Naamini vijana tusiokuwa na ajira tupo wengi sana, na viongozi wetu hawajali maana wakwao wanapata ajira mdebwedo, kwa hiyo tuungane tuwe na chama ambacho kitaweza kutoa PICHA HALISI ya tatizo la ajira. Labda wanaweza kuona ni serious issue.
  • chama hicho kiwe na viongozi kutoka kila Profession
  • Chama hicho kichunguze taratibu zote na vigezo vinavyo tumika ktk kutoa ajira
  • Chama hicho kishawishi serikali kupunguza matumizi makubwa ya fedha yasiyokuwa na ulazima ili hicho kidogo kinacho patikana tugawane wote. mfano; magari ya kifahari kwa viongozi, semina na tume ambazo huwa ni uwizi mtupu kwani nyingine hazifanyiwi kazi zinabaki kwenye makaratasi tu, na......... na........
  • Pia vijana wataelimishana juu ya kujiajiri na kukabiliana na changamoto za maisha.

NAAMINI KWA PAMOJA TUKIAMUA CHAMA HIKI kitakuwa na wanachama wengi na kitakuwa na nguvu kuliko vya kisiasa maana wanachama wake ni VIJANA na wana NGUVU kimwili na kiakili.
 
Good idea but ! umeshawahi kujiuliza chama cha wenye ajira (vyama vya wafanyakazi) tu vyenyewe vinalumbana na serikali miaka yote na malengo yao yote hayajawahi kutatuliwa na serikali, Je hicho cha waliokosa ajira watakisikiliza kweli? Ndoto zako ni njema tuu kwa serikali mpya ijayo.Vinginevyo kitakuwa hakina nguvu!
 
kama vp nendeni habari maelezo, tangazeni nia na tarehe ya kuchoma moto vyeti vyenu kwa kua havijawasaidia chochote. naamini watapay attention na wanaweza kuwakumbuka.
ni mtazamo tu msikasirike washkaji haya mawazo tu
 
kama vp nendeni habari maelezo, tangazeni nia na tarehe ya kuchoma moto vyeti vyenu kwa kua havijawasaidia chochote. Naamini watapay attention na wanaweza kuwakumbuka.
Ni mtazamo tu msikasirike washkaji haya mawazo tu

mawazo yako ni finyu
 
wanajamii wa TZ, tatizo la ajira linazidi kuwa kubwa na tabaka la wenye nacho na wasionacho linazidi kuwa kubwa, hii inatokana na ukweli usiojificha kwamba waliotokea kwenye familia za viongozi au matajiri ndio wanaopata ajira hata kama hawana sifa.
Pia nasikia kuwa serikali haina hela ndio maana hawatoi ajira.

PENDEKEZO

  • Naamini vijana tusiokuwa na ajira tupo wengi sana, na viongozi wetu hawajali maana wakwao wanapata ajira mdebwedo, kwa hiyo tuungane tuwe na chama ambacho kitaweza kutoa PICHA HALISI ya tatizo la ajira. Labda wanaweza kuona ni serious issue.
  • chama hicho kiwe na viongozi kutoka kila Profession
  • Chama hicho kichunguze taratibu zote na vigezo vinavyo tumika ktk kutoa ajira
  • Chama hicho kishawishi serikali kupunguza matumizi makubwa ya fedha yasiyokuwa na ulazima ili hicho kidogo kinacho patikana tugawane wote. mfano; magari ya kifahari kwa viongozi, semina na tume ambazo huwa ni uwizi mtupu kwani nyingine hazifanyiwi kazi zinabaki kwenye makaratasi tu, na......... na........
  • Pia vijana wataelimishana juu ya kujiajiri na kukabiliana na changamoto za maisha.

NAAMINI KWA PAMOJA TUKIAMUA CHAMA HIKI kitakuwa na wanachama wengi na kitakuwa na nguvu kuliko vya kisiasa maana wanachama wake ni VIJANA na wana NGUVU kimwili na kiakili.

Wàzo zuri muanzisha uzi, ila icje ikawa unataka ujiajiri kwa ada zetu za uanachama maana tusio na ajira kimsingi ni wengi sasa kweli wote tukijiunga kwenye huu umoja wako hata tukilipa fee 500 kwa mwezi aaah si haba milioni hukosi kwa mwezi halaf unapotelea Mgeta huko Milimani!
 
hilo ni wazo tu, sina nia ya kuanzisha chama, ila kwa wanaoweza na wakaona inafaa wanaweza endelea, ( Waandishi wa habari wasiokuwa na ajira wanachama chao)
 
naomba nwe mkuu wa kitengo cha HR....halafu unajua mwisho wa siku itakua hatupati kabisa ajira..we angalia mtu kamaliza 2010 mpaka leo unadhan atakua anakumbuka kila kitu? Coz huko ktk interview maswali wanauliza mambo ya class tu c kukomoana huku...
 
Mtaji mkubwa katika maisha ni akili zetu wenyewe. Kwa wale waliokwenda shule, vidato, chuo, nk bila shaka mtaji wao ni mkubwa kwa sababu elimu yao ni kubwa na hata uwezo wa kufikiri na kuona opportunities ni mpana. Ni vema vijana tujiajiri kwa kutumia elimu zetu badala ya kusubiri serikali ituajiri. Namini tukishughulisha na kazi yoyote ile na kwa malengo maalumu baada ya muda tutafanikiwa tu. Hakuna serikali inaweza kuajiri kila mtu au kila msomi duniani.
 
Sifa kubwa ya mwanachama itakuwa ni kutokuwa na ajira.
Huoni kuwa hilo litakuwa ni tatizo.
Hapo viongozi wa hicho chama hawatakubali kuajiriwa tena
 
Back
Top Bottom