Karamagi amesema Chama Cha Mapinduzi kitaisimamia Serikali kuhakikisha inaendelea kuboresha na kuweka Mazingira wezeshi kwa Wawekezaji

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
CCM YAENDELEA KUVUTIA WAWEKEZAJI MKOA KAGERA.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Kagera, ndugu Nazir M. Karamagi amesema Chama Cha Mapinduzi kitaisimamia Serikali kuhakikisha inaendelea kuboresha na kuweka Mazingira wezeshi kwa Wawekezaji ambao wana mchango mkubwa katika maendeleo kwa Wananchi na Utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Ameeleza hayo katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapunduzi yaliyofanyika katika uwanja wa Nyakahanga wilaya ya Karagwe ambapo maadhimisho hayo yaliambatana na ziara ya kutembelea
Wawekezaji na kukagua miradi ya maendeleo wilaya Karagwe.

Karamagi akiwa ameongoza Viongozi wa CCM Mkoa Kagera kutembelea Ujenzi wa Kiwanda cha Kahama Fresh Ltd cha kuchakata Maziwa na kusindika nafaka, amempongeza Mwekezaji kwa mpango wa kukopesha ng’ombe na kutoa mbegu kwa wananchi watakaowezesha upatikanaji wa malighafi ya kiwanda hicho.

“Kazi yetu kama Chama ni kuhakikisha tunawalinda Wawekezaji, kwa kuhakikisha tunapiga hodi Serikalini na kuhakikisha Wizara husika inatatua matatizo ya Wawekezaji na kumaliza Vikwazo na changamoto zote zinazowakabili” amesema Karamagi.

Karamagi amesema Uwekezaji una mchango mkubwa kwa kuchangia pato la Taifa, kutoa ajira pamoja na kusaidia wananchi kuwa na uhakika wa soko la mazao mbalimbali yanayotumika kama malighafi katika viwanda.

Aidha, Katika maadhimisho hayo Chama cha Mapinduzi kimetembelea ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe lenye thamani ya Shilingi Bilioni 3.5, pamoja na mradi wa Maji Omururongo wa Kayanga wenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.3.

Kwa Upande wake, Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Karagwe Innocent Bashungwa ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuufungua mkoa wa Kagera kwa mtandao wa Barabara ambayo inasaidia Wananchi na Wawekezaji katika shughuli zao.

Bashungwa amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya Nyakahanga - Nyaishozi kuelekea Benaco wenye thamani ya bilioni 92.9 na miradi mingine ya Barabara ambazo zilikuwa hazipitiki ambapo zaidi ya bilioni 7.3 imetengwa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara kupitia TARURA.

Amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho za kupata Mkandarasi atakayejenga kwa kiwango cha lami barabara ya Omugakorongo ambayo inaunganisha Mkoa Kagera na nchi ya Uganda.
 
Attachments

  • IMG-20240202-WA0695.jpg
    IMG-20240202-WA0695.jpg
    373.4 KB · Views: 2
  • IMG-20240202-WA0692.jpg
    IMG-20240202-WA0692.jpg
    166.8 KB · Views: 2
  • IMG-20240202-WA0684.jpg
    IMG-20240202-WA0684.jpg
    423.1 KB · Views: 2
  • IMG-20240202-WA0678.jpg
    IMG-20240202-WA0678.jpg
    495.1 KB · Views: 2
  • IMG-20240202-WA0674.jpg
    IMG-20240202-WA0674.jpg
    508.3 KB · Views: 2
  • IMG-20240202-WA0672.jpg
    IMG-20240202-WA0672.jpg
    167.2 KB · Views: 2

CCM YAENDELEA KUVUTIA WAWEKEZAJI MKOA KAGERA.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Kagera, ndugu Nazir M. Karamagi amesema Chama Cha Mapinduzi kitaisimamia Serikali kuhakikisha inaendelea kuboresha na kuweka Mazingira wezeshi kwa Wawekezaji ambao wana mchango mkubwa katika maendeleo kwa Wananchi na Utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Ameeleza hayo katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapunduzi yaliyofanyika katika uwanja wa Nyakahanga wilaya ya Karagwe ambapo maadhimisho hayo yaliambatana na ziara ya kutembelea
Wawekezaji na kukagua miradi ya maendeleo wilaya Karagwe.

Karamagi akiwa ameongoza Viongozi wa CCM Mkoa Kagera kutembelea Ujenzi wa Kiwanda cha Kahama Fresh Ltd cha kuchakata Maziwa na kusindika nafaka, amempongeza Mwekezaji kwa mpango wa kukopesha ng’ombe na kutoa mbegu kwa wananchi watakaowezesha upatikanaji wa malighafi ya kiwanda hicho.

“Kazi yetu kama Chama ni kuhakikisha tunawalinda Wawekezaji, kwa kuhakikisha tunapiga hodi Serikalini na kuhakikisha Wizara husika inatatua matatizo ya Wawekezaji na kumaliza Vikwazo na changamoto zote zinazowakabili” amesema Karamagi.

Karamagi amesema Uwekezaji una mchango mkubwa kwa kuchangia pato la Taifa, kutoa ajira pamoja na kusaidia wananchi kuwa na uhakika wa soko la mazao mbalimbali yanayotumika kama malighafi katika viwanda.

Aidha, Katika maadhimisho hayo Chama cha Mapinduzi kimetembelea ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe lenye thamani ya Shilingi Bilioni 3.5, pamoja na mradi wa Maji Omururongo wa Kayanga wenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.3.

Kwa Upande wake, Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Karagwe Innocent Bashungwa ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuufungua mkoa wa Kagera kwa mtandao wa Barabara ambayo inasaidia Wananchi na Wawekezaji katika shughuli zao.

Bashungwa amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya Nyakahanga - Nyaishozi kuelekea Benaco wenye thamani ya bilioni 92.9 na miradi mingine ya Barabara ambazo zilikuwa hazipitiki ambapo zaidi ya bilioni 7.3 imetengwa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara kupitia TARURA.

Amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho za kupata Mkandarasi atakayejenga kwa kiwango cha lami barabara ya Omugakorongo ambayo inaunganisha Mkoa Kagera na nchi ya Uganda
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2024-02-02 at 13.23.05(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-02 at 13.23.05(1).jpeg
    495.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-02 at 13.23.04.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-02 at 13.23.04.jpeg
    663.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-02 at 13.23.03(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-02 at 13.23.03(1).jpeg
    166.8 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-02 at 13.23.04(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-02 at 13.23.04(1).jpeg
    405.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-02 at 13.23.07.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-02 at 13.23.07.jpeg
    508.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-02 at 13.23.02(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-02 at 13.23.02(1).jpeg
    377.3 KB · Views: 2
Back
Top Bottom