Chama cha wanaume wazee Tanzania chazinduliwa

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Na WMJJWM, Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amevitaka Vyama vinavyoshughulika na masuala ya Wazee nchini kufanya kazi kwa karibu na Mabaraza ya kisera ya Wazee kupitia mwongozo wa Kitaifa uliozinduliwa tarehe 6 Oktoba 2023 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wazee kitaifa mkoani Geita.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Chama cha Wazee Wanaume Tanzania iliyofanyika jijini Dodoma Oktoba 27, 2023, Waziri Dkt. Gwajima pia amesisitiza Asasi na Vyama vyote vya Wazee nchini kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sera, Sheria, Miongozo na Mipango ya Serikali huku wakizingatia Katiba zao bila kuingilia majukumu ya mamlaka nyingine au vyama vingine pamoja na kuwa na mikakati ya kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli zao kikamilifu.

Kuhusu kudhibiti mmomonyoko wa maadili Waziri Dkt Gwajima amesema, Chama hicho pia kina wajibu wa kuchochea Malezi chanya ya Watoto na Vijana, huku wajumbe wa Chama hicho wakiwa mfano kwenye kuwajibika kukemea mmomonyoko wa maadili katika jamii unaosababishwa na kukosa malezi stahiki.

Ameziahidi Asasi na vyama vyote vya Wazee kuwa, Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano ambapo amezitaja baadhi ya juhudi zinazofanywa na Serikali kuwa ni pamoja na Kuunda mabaraza ya ushauri wa masuala ya wazee ambayo ni kiungo cha kisera kati ya jamii ya wazee wa makundi mbalimbali na Serikali.

Aidha, kwa kushirikiana na majukwaa ya wazee serikali imeweza kufanya mapitio ya Sera ya wazee ya mwaka 2003 na kuja na rasimu ya sera mpya ya wazee ya mwaka 2023 ambayo iko kwenye hatua za mwisho.

Akitoa salaam za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Gerard Mongela amewataka wazee kuwa sehemu ya kusaidia maendeleo ya nchi kwa kuendelea kuwa washauri wazuri na kuwafungulia mlango vijana wanaotumikia taifa.

"Viongozi vijana wanahitaji sana hekima ya wazee, chini ya Uongozi wa Rais Samia mkawe kielelezo, muendelee kutoa ushauri bila kuchoka. Kupitia Chombo chenu, mtumie taaluma zenu muweke kwenye maandishi ili iwe kumbukumbu" amesema Mhe. Mongela

Akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wazee Wanaume Joseph Laizer amebainisha kwamba Chama hicho kimetokana na kuwa na malalamiko mengi ya kusahaulika kwa wazee hasa katika huduma za afya na maadili.

"Tumeamua kurudi kule tulipotoka, tujaribu kurudisha maadili vijijini, watoto wetu wanaposoma wanabadilika na kusahau jadi yao" amesema Laizer

Kwa upande wake Katibu Mwenenzi wa Chama cha Wazee Wanaume John Sagata akiwasilisha risala ya chama hicho amesema lengo la chama hicho ni kuungana wanaume wazee katika kujadili masuala yanayowahusu ambapo hadi sasa kina jumla ya wanachama 23146 katika mikoa 22 nchini.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dodoma Mchungaji Paulo Mpolo amebainisha kuwa, Baraza la Wazee ndio linabeba wazee wote wa kike na wa kiume hivyo amekiomba chama cha Wazee na vyama vingine vyote kushirikiana katika kuwatetea wazee.

"Kazi ya kutengeneza malezi na maadili yoyote ni kazi ya wazee, tulijisahau tukaacha kuwasaidia watoto wetu juu ya maadili yetu ya Kiafrika. Tuamke sasa na tukatae kuitwa tumepitwa na wakati, tusaidie kizazi chetu." amesema Mzee Mpolo.

Source: Jambo TV
View attachment 2794890View attachment 2794891View attachment 2794892View attachment 2794893
 
Soon uzee unakuja na nitakuwa mwanachama wao. Hebu watueleze sifa za kuwa mwanachama wa chama cha wazee wanaume tuone kama tunakidhi matakwa yao
 
Naomba namna ya kujiunga nami nijiunge mapema sana nigombee na ukatibu wa wazee
 
Daaa, watu wazima weshtuka, wameona upepo ulishavuma na kuachwa wapweke, now weona bora watafute umoja wa kupeana moyo na hata siku ya giza ilifika.

Maana huko mitaani, makanisani, misikitini kote ni kutengwa so bora uwe kwenye chama likitokea la kutokea wanakuja fasta!.
 
Ni jambo jema Ila ni onyo kwa vijana.Vijana watengeneze kesho yao njema ili wasije kutembea na mikongojo kama mawakili wao.Bali waitumie mikongojo kutembea kwa mikogo huku wanapiga miluzi laini.
 
Tatizo wazee wa siku hizi wahuni sana
Badala watulie na wake zao na familia wanahangaika na k mtaani
Wanaharibu ndoa zao kizembe mwishowe wanakuja kufa vibaya.just imagine unakutana na mzee wa miaka 55 kwenda juu eti anafutilia talaka.aya ukipewa unaenda wapi ?? Nani anakutaka jua lilivo kali mtaani?mbaya zaidi unakuta hata hela hana
Kuna mzee mmoja humu jf alinitongoza bna.hadi nilimuonea huruma.yaani yeye aliachana na mkewe kisa alimfumania
Jamàa kuna kipindi alikuwa na matender serikalini huko alikuwa vizuri.wakajenga na wife majumba nini wana watoto wakubwa tu wako vizuri
Ule utawala ukapita jamaa akashake vibaya mno akafunga ofisi wife dharau zikawa nyingi analala huko kwa kimada wake jamaa akaamua watengane ila watoto walikuwa side ya mama yao .jamaa akaenda kupanga huko analala chini miaka 57 .ananiambia miss njoo tuanze maisha eti.eti maisha gani naanza nae wakuu ?? Angesema tu labda tukamalizie maisha
Mwenzenu ana stress sasa hivi yuko 60 mi.nilishaanza maisha na wenye kuanza
Kwa umri huo angevumilia tu nyumbani kwake .kwani mke akigegedwa kuna nini??kujitesa kisa k ya mtu??

Sent from my SM-A725F using JamiiForums mobile app
 
Umeandika kama unakula matobholwa.Bado u-mtoto.Ulitaka akueleze yote ya chumbani na anavyojisikia mke wake kumsaliti kwa sababu ya kukosa fedha?
 
Miss Natafuta umeandika ponti sana kiukweli nimependa akili yako inavofikiria sure, I can not date a big mama kisa ana hela wakati mimi ni kijana.

Story za kulelewa na mashangazi nawashangaa sana vijana wanatamani mwanamke kisa ana pesa ni aibu sana.

Kikawaida mwanaume wa kweli anamtongoza mwanamke aliemtamani na kumpenda bila kujua ata anaitwa nani? Ama amesoma ajasoma? Ana kazi hana?

Wanaume wa sikuhizi wengi ni sifuri waite SUFURIA tena negative yaaani kumtongoza mwanamke kisa ana kazi huo ni upumbavu tena mkubwa sana.

Wanaume wajinga wajinga badilikeni hasa vijana wa 95+ kaka zenu hatuko hivo kuweni wanaume. Tafuteni pesa kuweni ngangari rasilimali za uma ni zetu sote ukiwa nazo chukua kajenge jamii yako.

Haya maisha bila mwiko huwezi kusonga mbele.@Miss Natafuta Haupendi pombe lakini una mguu wa bia ata usipoona siku zako mimi nitakutafutia.
 
Mambo yanazidi kuwa magumu aisee lazima tujitetee.
Kabisa, umestaafu bbt haujapelekwa na huku nyumbani unaombwa matumizi, ndo maana wazee wengi wanafanyakazi za ulinzi wa maduka ili wasilale tu nyumbani
 
Kuna vibabu vilinzi vya maduka azikiwe zinatandikia changudoa mabox kwa ujira wa buku, huku ni kudhalilishana. Muda mwingine vinapewa kazi za kupiga chabo polisi wakati show zikiendelea
 
Tatizo wazee wa siku hizi wahuni sana
Badala watulie na wake zao na familia wanahangaika na k mtaani
Wanaharibu ndoa zao kizembe mwishowe wanakuja kufa vibaya.just imagine unakutana na mzee wa miaka 55 kwenda juu eti anafutilia talaka.aya ukipewa unaenda wapi ?? Nani anakutaka jua lilivo kali mtaani?mbaya zaidi unakuta hata hela hana
Kuna mzee mmoja humu jf alinitongoza bna.hadi nilimuonea huruma.yaani yeye aliachana na mkewe kisa alimfumania
Jamàa kuna kipindi alikuwa na matender serikalini huko alikuwa vizuri.wakajenga na wife majumba nini wana watoto wakubwa tu wako vizuri
Ule utawala ukapita jamaa akashake vibaya mno akafunga ofisi wife dharau zikawa nyingi analala huko kwa kimada wake jamaa akaamua watengane ila watoto walikuwa side ya mama yao .jamaa akaenda kupanga huko analala chini miaka 57 .ananiambia miss njoo tuanze maisha eti.eti maisha gani naanza nae wakuu ?? Angesema tu labda tukamalizie maisha
Mwenzenu ana stress sasa hivi yuko 60 mi.nilishaanza maisha na wenye kuanza
Kwa umri huo angevumilia tu nyumbani kwake .kwani mke akigegedwa kuna nini??kujitesa kisa k ya mtu??

Sent from my SM-A725F using JamiiForums mobile app
dronedrake duuuh hiki kisa vipi. Kataa ndoa oyeee.
 
Kuhusu kudhibiti mmomonyoko wa maadili Waziri Dkt Gwajima amesema, Chama hicho pia kina wajibu wa kuchochea Malezi chanya ya Watoto na Vijana, huku wajumbe wa Chama hicho wakiwa mfano kwenye kuwajibika kukemea mmomonyoko wa maadili katika jamii unaosababishwa na kukosa malezi stahiki.
Mnataka kuwaua wazee bure, huku mnahamasisha miziki ya vichupi kwenye runinga halafu hapa mnajikosha ati maadili
 
"Viongozi vijana wanahitaji sana hekima ya wazee, chini ya Uongozi wa Rais Samia mkawe kielelezo, muendelee kutoa ushauri bila kuchoka. Kupitia Chombo chenu, mtumie taaluma zenu muweke kwenye maandishi ili iwe kumbukumbu" amesema Mhe. Mongela

1698433592684.png
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom