ridhiwani kikwete na jakaya kikwete ni majina tu wala hawana undugu wowote
CCM isiyo na Udini wala ukanda hii hapa:Mawaziri wakuu 10 tangu uhuru 8 kati yao wakristo, J.K. Nyerere, Joseph Sinde Warioba, Cleopa Msuya, Fredrick Sumaye, Samwel John Malecela, Edward Lowassa, na Mizengo Kayanza Peter Pinda na WAISLAMU wawili tu Salim Ahmed Salimu na Rashid Mfaume Kawawa (Hii si bahati Mbaya). CCM NI CHAMA CHA KIDINI!
Hizo hasira sasa sijui utaenda chama gani Chadema nako utakutana Tundu Lissu, Christian Lissu, Philemon Ndesamburo, Owenya Ndesamburo, Mke mkubwa wa Dr Slaa, Rose Kamili Slaa.
Vipi hawa sio ndugu zako Josephat Manyerere, Vicent Nyerere, Leticia Nyerere.
Monday, 01 October 2012 08:08 |
HALMASHAURI Kuu ya CCM imepitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za Umoja wa Vijana (UVCCM), huku majina ya watoto wa vigogo yakijichomoza kwenye kinyanganyiro hicho. Orodha ya majina hayo iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela inaonyesha baadhi ya majina ya watoto wa vigogo hao ambao wameteuliwa kuwania nafasi mbalimbali. Wagombea walioteuliwa ni Mboni Mahita, mtoto wa aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Zabein Muhita; Ahmed Nyanganyi ambaye ni mtoto wa Balozi Mustafa Nyanganyi; Antony Mavunde, mtoto wa aliyekuwa Meya wa Dodoma, Peter Mavunde na Lulu Abbas Mtemvu, mtoto wa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu. Wengine ni Halima Bulembo, mtoto wa Abdallah Bulembo ambaye ni kada mkongwe wa CCM na hivi sasa anawania Uenyekiti wa Wazazi Taifa, Stanley Bendera, mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na mtoto wa Mbunge wa zamani wa Morogoro Kusini Mashariki, Semindu Pawa, Rashid Semindu Pawa. Katika orodha hiyo licha ya watoto wa vigogo, wamo baadhi ya wanasiasa maarufu vijana ambao nao wamepitishwa na Nec-CCM akiwamo Meya wa Manisapaa ya Ilala, Jerry Silaa. Kwa mujibu wa orodha hiyo, walioteuliwa kuwania nafasi ya Mwenyekiti Taifa ni Sadifa Juma Khamis, Rashid Simai Msaraka na Lulu Msham Abdallah ambao wote wanatoka Zanzibar. Kwa upende wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, walioteuliwa ni aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Tahliso), Paul Makonda, Mboni Mhita na Ally Salum Hapi. Wajumbe wa Halmashauri Kuu kupitia UVCCM wajumbe watakaojaza nafasi sita bara, waliofanikiwa kupenya ni 31 akiwamo Silaa. Kwa upande wa UVCCM Zanzibar viti vinne, yamepitishwa majina 22 kuwania nafasi hizo. Wagombe wa Baraza Kuu Taifa viti vitano bara inawaniwa na watu 40 wakiwamo Wazanzibari 14. |
Ndugu wanajamvi,ndani ya uongozi wa CCM majina haya hapa chini yataongoza vijana huku wakiwa wanajiandaa kufanyiwa mpango na kuandaa mtandao wa kuchukua nchi siku za usoni.nayo ni:-
1.Ridhiwan Jakaya Mrisho kikwete
2.Ashura Hussein Ally Hassan Mwinyi
3.Shariffer Ghalib Bilal
4.Irene mizengo Pinda Mtoto wa Mkulimwa wa Sumbawanga
5.Fred Edward Lowassa
6.Felister Job Ndugai
7.Jalome Pius Msekwa
8.Beny Samwel Sita
9.Judith Wilson Mukama.
10.Dickson Membe
11.Debora Mark Mwandosya
12.Hawa Abdallah kigoga.
Kama huu utaratibu ungekuwa wa chama kingine Sijui,wapenzi wa ccm zote mbili A & B level ya kina Duni wangetoa tamko gani.
Nimepitia majina ya walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
CCM, naona kama kama vile jina langu limekatwa. Lakini nimekutana na
majina mengi yanafanana hasa surnames kiasi cha kujiuliza kama jina
langu limekatwa kwa kuwa jina langu la mwisho halifananii kabisa na
majina mengine kwenye hiyo orodha. Nafikiria kubadilisha jina sasa,
maana naona CCM na Chadema mtindo mmoja tuu. Kama kule Zanzibar naona
ni dili kama ukiwa na surname ya Vuai. Pia katika uchambuzi wangu
inaelekea majina ya kichaga ni machache sana kulinganisha na mengine.
Sijui kama yamekatwa au wachaga wamehamia kwingine.
Inawezekana kabisa wagombea hawana undugu wowote maana surnames kama
Mollel (Arusha) Vuai (Zanzibar) na Wambura (Mara) ni mengi kiasi.
Lakini kuna majina either wote wanagombea au jina lina uhusiano na
vigogo wa sasa au wa zamani wa CCM. Baadhi ya majina yanayofanana
niliyoyakuta kwenye orodha kama yanavyoonekana hapo chini. Majina
mengi kutoka Zanzibar na Arusha nimeyakata mimi mwenyewe maana
yanafanana mno lakini inawezekana kabisa sio ndugu.
Kama umeona mengine, ongezea tafadhali.
Salma Rashidi KIKWETE
Mwanaisha Halfani KIKWETE
Mohamed Mrisho KIKWETE
Ridhiwani Jakaya KIKWETE
Hawa ni ndugu na Jakaya Kikwete (M/Kiti wa CCM taifa) au ni majina tuu?
Vita Rashidi Kawawa
Zainab Rashid Kawawa
Hawa wana uhusiano wowote na Rashid Kawawa?
Bayoum Awadhi KIGWANGALLA
Hamisi Andrea Kigwangalla (mbunge wa Nzega) coincidence tuu ya
majina? Hamisi Andrea Kigwangalla kakatwa anyway.
Saumu Mohamed BENDERA
Denis William BENDERA
Stanley J. BENDERA
Saum Mohamed BENDERA
Any connection with Joel Bendera hasa huyu Stanley J. BENDERA?
William John MALECELA
Anne Kilango MALECELA
Definitely hapa hakuna ubishi kuwa wana connection na John Malecela
Lulu Abbas MTEMVU
Abbas MTEMVU (mbunge wa Temeke) jina tuu au ni ndugu?
Ahmed Mustafa NYANGANYI
Uhusiano na Mustafa NYANGANYI (alikuwa mkuu wa mkoa wa DSM)?
Sophia Mnyambi SIMBA
Ulanga Agathon SIMBA
Connection na Idd Simba?
Aisha Omar Kigoda
Abdallah Omari KIGODA
Mashallah (God willed it)
Stanley Haule KOLIMBA
Ndugu na Horace Kolimba (kiongozi wa zamani wa CCM)?
Janeth Maurice Masaburi
Connection yoyote na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi?
Halima Mohamed MUDHIHIR
Undugu wowote na Mudhihir Mohamed Mudhihir aka kisiki cha mpingo?
Abdul Sued KAGASHEKI
Connection na waziri Khamis Suedi Kagasheki?
Beatrice Kasanda MASANILO
Any connection na mchungaji mstaafu Masanilo wa JF?
Na mwisho, Dalaly Peter KAFUMU (55) (huyu nilisoma kuwa baada ya
kushindwa ile kesi yake ya ubunge alisema kuwa ataachana na mambo ya
siasa lakini naona anagombea. A u-turn?
Narudia tena, kama umeona mengine, ongezea tafadhali.