Chaguzi za CCM: Undugunisation au majina kufanana tuu?

Aaahgh Mwali bwana! mbona unafukunyuku nyingi?
Pale Maneromango tuna majina ya semeni 5, sikujua 4, Sikudhani 7, kufakunoga 6 na kila mtu ana ukoo wake.
Sasa wakiwania NEC utasemaje?

Hao unaosema hawana undugu, majina yanafanana tu!!!!!!
 
kwetu sisi wafugaji tukitaka kuchagua dume la mbegu huwa tunaangalia historia ya vizazi vinne nyuma, mama yake, baba yake, babu zake na bibi zake, kama ni ng'ombe walitoa maziwa kiasi gani, waliwezaje kuvumilia mazingira magumu kama vile upungufu wa majani na maji, walistahimili vipi magonjwa, kwa wale maksai walifanya je kazi bila kuchoka. kwa hiyo ukoo ulioweza kufikia vigezo ndio unaendelezwa. hata kwenye utawala sio kila mtu anaweza kuongoza. makabila na koo nyingine zina mikosi, kwa hiyo zile zilizoongoza kwa ufanisi ndio tutakazoendelea kuziendeleza. hata marekani wameonesha mfano. kama baba yako ni mchawi ni rahisi sana na wewe kuwa mchawi. lakini sio rahisi sana kwa mtoto wa askofu kuwa mganga wa Tunguri. kwa hili nawaunga ccm mkono. nadhani unaona jinsi Huseni mwinyi anavyoongoza vizuri wizira anazopangiwa, pia karume alivyoongoza vizuri zanzibar na kuondoa matatizo ya cuf. natarajia Rais ajae atatoka katika ukoo wa Nyerere na waziri mkuu atatoka katika ukoo wa Sokoine na Makamu wa Rais atatoka katika ukoo wa Abood jumbe na Rais wa Zanziba atatoka katika ukoo wa Ali hasani Mwinyi. hapo tutaendelea.
 
CCM isiyo na Udini wala ukanda hii hapa:Mawaziri wakuu 10 tangu uhuru 8 kati yao wakristo, J.K. Nyerere, Joseph Sinde Warioba, Cleopa Msuya, Fredrick Sumaye, Samwel John Malecela, Edward Lowassa, na Mizengo Kayanza Peter Pinda na WAISLAMU wawili tu Salim Ahmed Salimu na Rashid Mfaume Kawawa (Hii si bahati Mbaya). CCM NI CHAMA CHA KIDINI!

Twendako naona giza tu!
 
kweli nimekaa nikafikiria tunapoelekea...na ninaamini wala si pazuri...yani familia ya rais yote imeingia kwenye siasa, na wote ni wajumbe wa NEC?? DINGI mwenyekiti....mama mjumbe na mtoto(riz) naye mjumbe....chama kimeoza, na sasa kinanuka......kisipozikwa...uvundo utaenea hadi kwenye jina la nchi.........wasomi wamenielewa...........CURE IS URGENTLY NEEDED....2015 MBALI JAMANI..........
 
Hizo hasira sasa sijui utaenda chama gani Chadema nako utakutana Tundu Lissu, Christian Lissu, Philemon Ndesamburo, Owenya Ndesamburo, Mke mkubwa wa Dr Slaa, Rose Kamili Slaa.

Vipi hawa sio ndugu zako Josephat Manyerere, Vicent Nyerere, Leticia Nyerere.

Kama ngoma ni droo basi hiyo issue hata ikiondolewa au kuongezwa haina effect. Ni kama kujumlisha same figure pande mbili au kuiondoa.Equilibrium haigeuki.BY the way hadi uchaguzi mkuu propaganda za CCM zitakuwa agianst wao wenyewe.Na mbaya itawachukua muda kuwanyamazisha kasuku wao wasizirudie tena.
 



bot_tabimg.gif

Monday, 01 October 2012 08:08


Tausi Mbowe

HALMASHAURI Kuu ya CCM imepitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za Umoja wa Vijana (UVCCM), huku majina ya watoto wa vigogo yakijichomoza kwenye kinyang’anyiro hicho.


Orodha ya majina hayo iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela inaonyesha baadhi ya majina ya watoto wa vigogo hao ambao wameteuliwa kuwania nafasi mbalimbali.

Wagombea walioteuliwa ni Mboni Mahita, mtoto wa aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Zabein Muhita; Ahmed Nyang’anyi ambaye ni mtoto wa Balozi Mustafa Nyang’anyi; Antony Mavunde, mtoto wa aliyekuwa Meya wa Dodoma, Peter Mavunde na Lulu Abbas Mtemvu, mtoto wa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu.


Wengine ni Halima Bulembo, mtoto wa Abdallah Bulembo ambaye ni kada mkongwe wa CCM na hivi sasa anawania Uenyekiti wa Wazazi Taifa, Stanley Bendera, mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na mtoto wa Mbunge wa zamani wa Morogoro Kusini Mashariki, Semindu Pawa, Rashid Semindu Pawa.


Katika orodha hiyo licha ya watoto wa vigogo, wamo baadhi ya wanasiasa maarufu vijana ambao nao wamepitishwa na Nec-CCM akiwamo Meya wa Manisapaa ya Ilala, Jerry Silaa.


Kwa mujibu wa orodha hiyo, walioteuliwa kuwania nafasi ya Mwenyekiti Taifa ni Sadifa Juma Khamis, Rashid Simai Msaraka na Lulu Msham Abdallah ambao wote wanatoka Zanzibar.


Kwa upende wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, walioteuliwa ni aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Tahliso), Paul Makonda, Mboni Mhita na Ally Salum Hapi.


Wajumbe wa Halmashauri Kuu kupitia UVCCM wajumbe watakaojaza nafasi sita bara, waliofanikiwa kupenya ni 31 akiwamo Silaa.


Kwa upande wa UVCCM Zanzibar viti vinne, yamepitishwa majina 22 kuwania nafasi hizo.

Wagombe wa Baraza Kuu Taifa viti vitano bara inawaniwa na watu 40 wakiwamo Wazanzibari 14.




 
CCM - CULT PARTY; Sasa unaona ni kwanini Wanatumia NGUVU za DOLA kuitesa CHADEMA...

Unaona ni kwanini hawaisumbui CUF ? Sababu CUF ni rahisi kupewa tonge la UGALI na DAGAA na kukaa

kimya
Angalia SERIKALI YA MPITO huko Zanzibar ni SWAFI; hata kama kulikuwa na MABOMU BUBUBU

yaliendekezwa
Sio kwa CUF kwa UAMSHO!!! Sasa MTASEMA CCM YALETA DEMOKRASIA YA UKWELI?
 
Ndugu wanajamvi,ndani ya uongozi wa CCM majina haya hapa chini yataongoza vijana huku wakiwa wanajiandaa kufanyiwa mpango na kuandaa mtandao wa kuchukua nchi siku za usoni.nayo ni:-

1.Ridhiwan Jakaya Mrisho kikwete
2.Ashura Hussein Ally Hassan Mwinyi
3.Shariffer Ghalib Bilal
4.Irene mizengo Pinda Mtoto wa Mkulimwa wa Sumbawanga
5.Fred Edward Lowassa
6.Felister Job Ndugai
7.Jalome Pius Msekwa
8.Beny Samwel Sita
9.Judith Wilson Mukama.
10.Dickson Membe
11.Debora Mark Mwandosya
12.Hawa Abdallah kigoga.

Kama huu utaratibu ungekuwa wa chama kingine Sijui,wapenzi wa ccm zote mbili A & B level ya kina Duni wangetoa tamko gani.
 
Wamekosea sana kudhani hivyo, theirs will be different times altogether!
 
Ndugu wanajamvi,ndani ya uongozi wa CCM majina haya hapa chini yataongoza vijana huku wakiwa wanajiandaa kufanyiwa mpango na kuandaa mtandao wa kuchukua nchi siku za usoni.nayo ni:-

1.Ridhiwan Jakaya Mrisho kikwete
2.Ashura Hussein Ally Hassan Mwinyi
3.Shariffer Ghalib Bilal
4.Irene mizengo Pinda Mtoto wa Mkulimwa wa Sumbawanga
5.Fred Edward Lowassa
6.Felister Job Ndugai
7.Jalome Pius Msekwa
8.Beny Samwel Sita
9.Judith Wilson Mukama.
10.Dickson Membe
11.Debora Mark Mwandosya
12.Hawa Abdallah kigoga.

Kama huu utaratibu ungekuwa wa chama kingine Sijui,wapenzi wa ccm zote mbili A & B level ya kina Duni wangetoa tamko gani.

let me tell you guys! The one who owns gold makes the rule,unaijua uganda?mke wa rais,watoto wa rais,wakwe wa rais wameshika sehemmu nyeti,angalia rwanda watoto wa kagame,congo aliyerithi nchi ni mtoto wa aliyekuwa rais kabila,north korea rais aliyepo ni mtoto wa rais aliyefariki,marekani angalia ukoo wa bush kuanzia baba yao,watoto ,MY FRIENDS HUWEZI KUZUIA UPEPO KUVUMA,BALI ELEKEA UPANDE UNAPOENDA UPEPO.
 
Ili usikatwe na jina lako liogopwe lazima utumia surname ya kigogo babuu. We hujasikia wenzio wanapitwa bila kupigwa?
 
Nimepitia majina ya walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
CCM, naona kama kama vile jina langu limekatwa. Lakini nimekutana na
majina mengi yanafanana hasa surnames kiasi cha kujiuliza kama jina
langu limekatwa kwa kuwa jina langu la mwisho halifananii kabisa na
majina mengine kwenye hiyo orodha. Nafikiria kubadilisha jina sasa,

maana naona CCM na Chadema mtindo mmoja tuu. Kama kule Zanzibar naona
ni dili kama ukiwa na surname ya Vuai. Pia katika uchambuzi wangu
inaelekea majina ya kichaga ni machache sana kulinganisha na mengine.
Sijui kama yamekatwa au wachaga wamehamia kwingine.

Inawezekana kabisa wagombea hawana undugu wowote maana surnames kama
Mollel (Arusha) Vuai (Zanzibar) na Wambura (Mara) ni mengi kiasi.
Lakini kuna majina either wote wanagombea au jina lina uhusiano na
vigogo wa sasa au wa zamani wa CCM. Baadhi ya majina yanayofanana

niliyoyakuta kwenye orodha kama yanavyoonekana hapo chini. Majina
mengi kutoka Zanzibar na Arusha nimeyakata mimi mwenyewe maana
yanafanana mno lakini inawezekana kabisa sio ndugu.
Kama umeona
mengine, ongezea tafadhali.

Salma Rashidi KIKWETE
Mwanaisha Halfani KIKWETE
Mohamed Mrisho KIKWETE
Ridhiwani Jakaya KIKWETE
Hawa ni ndugu na Jakaya Kikwete (M/Kiti wa CCM taifa) au ni majina tuu?

Vita Rashidi Kawawa
Zainab Rashid Kawawa
Hawa wana uhusiano wowote na Rashid Kawawa?

Bayoum Awadhi KIGWANGALLA
Hamisi Andrea Kigwangalla (mbunge wa Nzega) – coincidence tuu ya
majina? Hamisi Andrea Kigwangalla kakatwa anyway.

Saumu Mohamed BENDERA
Denis William BENDERA
Stanley J. BENDERA
Saum Mohamed BENDERA
Any connection with Joel Bendera hasa huyu Stanley J. BENDERA?

William John MALECELA
Anne Kilango MALECELA
Definitely hapa hakuna ubishi kuwa wana connection na John Malecela

Lulu Abbas MTEMVU
Abbas MTEMVU (mbunge wa Temeke) – jina tuu au ni ndugu?

Ahmed Mustafa NYANG’ANYI
Uhusiano na Mustafa NYANG’ANYI (alikuwa mkuu wa mkoa wa DSM)?

Sophia Mnyambi SIMBA
Ulanga Agathon SIMBA
Connection na Idd Simba?

Aisha Omar Kigoda
Abdallah Omari KIGODA
Mashallah (God willed it)

Stanley Haule KOLIMBA
Ndugu na Horace Kolimba (kiongozi wa zamani wa CCM)?

Janeth Maurice Masaburi
Connection yoyote na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi?

Halima Mohamed MUDHIHIR
Undugu wowote na Mudhihir Mohamed Mudhihir aka kisiki cha mpingo?

Abdul Sued KAGASHEKI
Connection na waziri Khamis Suedi Kagasheki?

Beatrice Kasanda MASANILO
Any connection na mchungaji mstaafu Masanilo wa JF?

Na mwisho, Dalaly Peter KAFUMU (55) (huyu nilisoma kuwa baada ya
kushindwa ile kesi yake ya ubunge alisema kuwa ataachana na mambo ya
siasa lakini naona anagombea. A u-turn?

Narudia tena, kama umeona mengine, ongezea tafadhali.



Mengine in Dickson Membe, Kambarage Wasira, Fredy Lowassa, Ashura Hussein Mwinyi, Benny Samwel Sita, Debora Mwandosya, Iren Pinda, Felster Ndugai, Sharifa Bilal, Hawa Kigoda, Judith Mukama na Jalome Msekwa
 
hivi ni sawa kurithishana uongozi kwa undungu? hata kama ni upole watanzania tunmezidi. nadhani ni wakati wa kuwa wakweli na kuachana na mambo ya kijinga kama hayo yanayofanywa na viongozi wetu. kwa suala kama hilo chama cha CCM mmebugi sana. naomba watanzania tulione hilo. kwa kherini.
 
Back
Top Bottom