Chaguzi za CCM: Undugunisation au majina kufanana tuu?

Huyu hajarithishwa na mtu yeyote. Katumia nguvu yake mwenyewe kufika pale alipo.

Kwa kufahamu au kutofahamu, fedha za Nimrod Mkono zimemsaidia sana Makongoro kisiasa huko kwao dhidi ya wakina Chambiri!!
 
Ongezea haya,

Uvccm ,Angela Mwanri,Deogratius Ndejembi,Halima Bulembo,Jonas Nkya vs Yule naibu waziri wa zamani Afya,
Wazazi kuna ,Abdalah Bulembo,Adam Kighoma Malima
 
Nimepitia majina ya walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
CCM, naona kama kama vile jina langu limekatwa. Lakini nimekutana na
majina mengi yanafanana hasa surnames kiasi cha kujiuliza kama jina
langu limekatwa kwa kuwa jina langu la mwisho halifananii kabisa na
majina mengine kwenye hiyo orodha. Nafikiria kubadilisha jina sasa,

maana naona CCM na Chadema mtindo mmoja tuu. Kama kule Zanzibar naona
ni dili kama ukiwa na surname ya Vuai. Pia katika uchambuzi wangu
inaelekea majina ya kichaga ni machache sana kulinganisha na mengine.
Sijui kama yamekatwa au wachaga wamehamia kwingine.

Inawezekana kabisa wagombea hawana undugu wowote maana surnames kama
Mollel (Arusha) Vuai (Zanzibar) na Wambura (Mara) ni mengi kiasi.
Lakini kuna majina either wote wanagombea au jina lina uhusiano na
vigogo wa sasa au wa zamani wa CCM. Baadhi ya majina yanayofanana

niliyoyakuta kwenye orodha kama yanavyoonekana hapo chini. Majina
mengi kutoka Zanzibar na Arusha nimeyakata mimi mwenyewe maana
yanafanana mno lakini inawezekana kabisa sio ndugu.
Kama umeona
mengine, ongezea tafadhali.

Salma Rashidi KIKWETE
Mwanaisha Halfani KIKWETE
Mohamed Mrisho KIKWETE
Ridhiwani Jakaya KIKWETE
Hawa ni ndugu na Jakaya Kikwete (M/Kiti wa CCM taifa) au ni majina tuu?

Vita Rashidi Kawawa
Zainab Rashid Kawawa
Hawa wana uhusiano wowote na Rashid Kawawa?

Bayoum Awadhi KIGWANGALLA
Hamisi Andrea Kigwangalla (mbunge wa Nzega) – coincidence tuu ya
majina? Hamisi Andrea Kigwangalla kakatwa anyway.

Saumu Mohamed BENDERA
Denis William BENDERA
Stanley J. BENDERA
Saum Mohamed BENDERA
Any connection with Joel Bendera hasa huyu Stanley J. BENDERA?

William John MALECELA
Anne Kilango MALECELA
Definitely hapa hakuna ubishi kuwa wana connection na John Malecela

Lulu Abbas MTEMVU
Abbas MTEMVU (mbunge wa Temeke) – jina tuu au ni ndugu?

Ahmed Mustafa NYANG’ANYI
Uhusiano na Mustafa NYANG’ANYI (alikuwa mkuu wa mkoa wa DSM)?

Sophia Mnyambi SIMBA
Ulanga Agathon SIMBA
Connection na Idd Simba?

Aisha Omar Kigoda
Abdallah Omari KIGODA
Mashallah (God willed it)

Stanley Haule KOLIMBA
Ndugu na Horace Kolimba (kiongozi wa zamani wa CCM)?

Janeth Maurice Masaburi
Connection yoyote na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi?

Halima Mohamed MUDHIHIR
Undugu wowote na Mudhihir Mohamed Mudhihir aka kisiki cha mpingo?

Abdul Sued KAGASHEKI
Connection na waziri Khamis Suedi Kagasheki?

Beatrice Kasanda MASANILO
Any connection na mchungaji mstaafu Masanilo wa JF?

Na mwisho, Dalaly Peter KAFUMU (55) (huyu nilisoma kuwa baada ya
kushindwa ile kesi yake ya ubunge alisema kuwa ataachana na mambo ya
siasa lakini naona anagombea. A u-turn?

Narudia tena, kama umeona mengine, ongezea tafadhali.

hapo kwenye rangi,huyu nimeliona jina lake kwenye list ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya shahada ya pili pale udsm mwaka huu,,,,M.A EDUCATION
 
Vipi Pepe Kale wa Bongo, AKA Le Muntuz, Le Baharia, Mzee wa Wassup na ha ha ha ha ha ha william W. Malecela?
 
Last edited by a moderator:
hapo kwenye rangi,huyu nimeliona jina lake kwenye list ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya shahada ya pili pale udsm mwaka huu,,,,M.A EDUCATION
You gotta be kidding me bwana! M.A.????
 
ndugu yangu wala huitaj kuumiza kichwa kwani kila mtu anasimama kwa nafsi yake. but kwangu mimi ningeona kama ingekuwa busara amwambaie mkewe awe nje ya siasa ili kulinda heshima ya familia. amwache mtoto kwani yeye hana neno.

sijui kwanin sipend tu huyu mama kuingia kuwepo kwenye siasa lakn sababu zangu za msingi ni hizi hapa.
kwanza kabisa sio mwanasiasa kwani hawez kujieleza wala hata kuongea kwa kuamsha hisia kwa watu na pia hata usomaji wake wa hotuba ni wa kiwango cha chini sana.

pili anataiwa astaafu sasa alee famailia yake manake kwa kurudi siasan ni wazi kwamba anatengeneza uwanja wa kuruhusu baba aendeleze jahaz la kuchakachua tu.

tatu huko msoga angeweza kufanya kazi nyingine kama anavyofanya mama Anna Mkapa huko Lushoto ambazo zingemletea heshima kuliko hizi za kudhalilishana kwa maneno ya kejeli na kashfa.

nne aangalie waliomtanulia wako wapi? na je ajiulize kwann wako walipo ndipo atakapoona kwamba kuwa nje ya siasa kunakuza reputation yake kuliko ndani kwa wakati huu.

mfano mzuri naamin kikwete angependa sana kama baada ya ile miaka mitano ya kwanza angekaa pembeni pasi kuingia kipind hiki cha pili.

Ndugu yangu, hapa ni kujaribu kulinda vyote walivyofanikiwa kukusanya wakatiu mzee akiwa madarakani. Akikaa pembeni wanaweza kumsahau halafu mambo yakabadirika, hivyo ni bora kuwamo kuwamo you never know, na kwakuwa kuna wengi wamewekwa tayari kwa maandaliza ya kulipa fadhila. Inatia kichefu chefu lakini ndipo tulipofikia.. unataka WAMA ife?
 
You gotta be kidding me bwana! M.A.????

kweli kabisa,inaonesha amemaliza OPEN MWAKA JANA,,,,,USIFANANISHE NA MWANAASHA NI MWANAISHA MWALI,ingia web ya udsm nenda kwenye selection za postgraduate then nenda kwenye M.A education full time,
coz nami niliomba hii kitu ndo nikaona
 
hivi hakuna waliofeli darasa la saba wakachukua majina ya wengine, ambayo bado hayajafutwa kwenye NECTA, huyu mwanahaisha JK ni mdogo sana anawezaje kugombea?
 
kweli kabisa,inaonesha amemaliza OPEN MWAKA JANA,,,,,USIFANANISHE NA MWANAASHA NI MWANAISHA MWALI,ingia web ya udsm nenda kwenye selection za postgraduate then nenda kwenye M.A education full time,
coz nami niliomba hii kitu ndo nikaona
Nashindwa kuingia, weka link basi au snapshot tafadhali.
 
Hizo hasira sasa sijui utaenda chama gani Chadema nako utakutana Tundu Lissu, Christian Lissu, Philemon Ndesamburo, Owenya Ndesamburo, Mke mkubwa wa Dr Slaa, Rose Kamili Slaa.

Vipi hawa sio ndugu zako Josephat Manyerere, Vicent Nyerere, Leticia Nyerere.

Mkuu Ritz, tambua kwamba ccm imekuwa madarakani kwa muda mrefu, stile iliyotumika kwenye usaili siyo iliyotakiwa kufanywa na chama makini kama ccm. hii inadhihirisha jinsi kikwete alivyochoka akili na kuigeuza ccm chama cha ukoo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom