Chaguzi za CCM: Undugunisation au majina kufanana tuu?

Mwali kwanza nikupe pole... Ila tu ukweli wa mambo ni kuwa katika Siasa jina lako linapoashiria wewe ni mtoto ama una Uhusiano na mkubwa fulani basi ni rahisi sana wewe kuwa mkubwa pia. Tumeona hata vile chama kuu pinzani cha CCM kinavofurahia watoto wa wakubwa hao wakijiunga...

Anafunguliwa headline kabisa... "Mtoto wa Fulani ajiunga", Kazi ipo kwa wale ambao wanataka vyeo na ni watoto wa nobody in the name of politics...

Thom malenga Lukuvi ni ndugu wa William Lukuvi.
 
taarifa kutoka dodo zinasema jk wa awamu hii ameingiza watatu kutoka familia yake katika uongozi ndani ya ccm nikajaribu kufikiria jk wa ukweli angeingiza wangapi kama angesimamia kupitisha majina ndani ya uongozi ccm.
tujadili bila jazba wala kejeli kwa sababu hata kwenye mpira kuna familia za mpira na nyingine ni mmoja tu alifanikiwa kucheza mpira kwa mafanikio.je jk wa sasa ni familia ya kina njohole na jk wa zamani ni ya kina lunya.
 
ndugu yangu wala huitaj kuumiza kichwa kwani kila mtu anasimama kwa nafsi yake. but kwangu mimi ningeona kama ingekuwa busara amwambaie mkewe awe nje ya siasa ili kulinda heshima ya familia. amwache mtoto kwani yeye hana neno.

sijui kwanin sipend tu huyu mama kuingia kuwepo kwenye siasa lakn sababu zangu za msingi ni hizi hapa.
kwanza kabisa sio mwanasiasa kwani hawez kujieleza wala hata kuongea kwa kuamsha hisia kwa watu na pia hata usomaji wake wa hotuba ni wa kiwango cha chini sana.

pili anataiwa astaafu sasa alee famailia yake manake kwa kurudi siasan ni wazi kwamba anatengeneza uwanja wa kuruhusu baba aendeleze jahaz la kuchakachua tu.

tatu huko msoga angeweza kufanya kazi nyingine kama anavyofanya mama Anna Mkapa huko Lushoto ambazo zingemletea heshima kuliko hizi za kudhalilishana kwa maneno ya kejeli na kashfa.

nne aangalie waliomtanulia wako wapi? na je ajiulize kwann wako walipo ndipo atakapoona kwamba kuwa nje ya siasa kunakuza reputation yake kuliko ndani kwa wakati huu.

mfano mzuri naamin kikwete angependa sana kama baada ya ile miaka mitano ya kwanza angekaa pembeni pasi kuingia kipind hiki cha pili.
 
taarifa kutoka dodo zinasema jk wa awamu hii ameingiza watatu kutoka familia yake katika uongozi ndani ya ccm nikajaribu kufikiria jk wa ukweli angeingiza wangapi kama angesimamia kupitisha majina ndani ya uongozi ccm.
tujadili bila jazba wala kejeli kwa sababu hata kwenye mpira kuna familia za mpira na nyingine ni mmoja tu alifanikiwa kucheza mpira kwa mafanikio.je jk wa sasa ni familia ya kina njohole na jk wa zamani ni ya kina lunya.
hIVI WEWE UNAIJUA ccm HII LEO AU ni raia wa kuomba uhamiaji? Wewe angalia toka enzi za sukita ni kina nai walikuwa ma directors na walikuwa ni watoto wa kina nani? Kulitokea ajira banki kuu iliyojaa watoto wa viongozi wa CCM tuu, nakushangaa kulalamikia leo wakati gemu lilianza tokea 1947!!!!
 
Huyu hajarithishwa na mtu yeyote. Katumia nguvu yake mwenyewe kufika pale alipo.

enzi zake joseph nyerere,joseph butiku na shemeji yao lawrance gama[rip] ama mlikuwa wadogo ama baadhi yetu tumesahau ?
 
Hiyo ndiyo timu ya ushindi ya ccm 2015, kati kikwete, pembeni Ridhiwani na nyuma salma. Hapo hakuna mpinzani atakayepenya. Raha ya mtu mwongo ni kwanza hujidanganya mwenyewe, ndipo hufuatia mwingine.

Kikwete alisema anawaweka vijana, Je Filikunjombe, Kigwangala, Mpina na Bashe ni wazee kuliko yeye? Na

Lowassa, Chenge na Sitta ni vijana kwake?Kikwete haya wee, aibu yako hiyo, lichama kufia kiganjani mwako.
 
undugu upo hadi ulaya ..ila mimi nisingekuwa na shida kama wangeleta undugu ila wapige kazi tatito lao wanaleta undugu ili kula , kuiba ,kulindan, kupeana vyeo na vitu kama hivyo.
 
Wewe hujui kitu, hao waliambulia cheo hicho kwa kuwa asilimia kubwa vile vyeo muhimu vilikuwa vinashikiliwa na Waislamu.

Tupe seti yote ili tukuelewe. Wakati hao wakishikilia uwaziri mkuu, rais alikuwa nani, makamu wa rais alikuwa nani, mkuu wa majeshi alikuwa nani, mkuu wa polisi alikuwa nani, mkuu wa Tiss alikuwa nani, nk. Weka majina hapa na dini zao ili tujadili hoja yako vizuri.
 
Masahihisho, sio watatu ni wa nne, Ridhwan Jakaya Mrisho Kikwete Bagamoyo ujumbe wa Nec ni mtoto wa Mwenyekiti, Salma Kikwete mjumbe wa Nec lindi mke wa mwenyekiti, Mohamed kikwete Mwenyekiti wa wilaya ya Bagamoyo, Mwanaisha kikwete uenyekiti wa uwt pwani anapambana na DKT fatma Ameir Gama.

Tuje kwa Nyerere Joseph Nyerere alikuwa ndugu wa damu wa mwl nyerere na alishawahi kushika vyeo vingi kabla ya kifo chake ikiwemo uenyekiti wa CCM Marana Joseph Butiku alikuwa katibu kiongozi wa Ikulu pia ni mwana ukoo wa Familia ya Nyerere.

Katika hili la undugu Benjamin William Mkapa ndio mtu asiekuwa na doa hili, Nyerere,Mwinyi na Kikwete wanatofautiana kiwango lakini wote waliingiza wa nyumbani kwenye nafasi za kiutumishi na kichama.
 
Ametumia Cheo chake kupitisha wana familia yake,,, na alisema kina bashe na kingwangalla wanakimbilia nini NEC? Sasa na yeye sijui ndio pangy pakavu tia mchuzi?
 
Du! hii nimechekeka kidogo, hata Salma Rashidi Kikwete hana nasaba yoyote na Jakaya Mrisho Kikwete. Ila wote (Salma na Ridhiwani) wamepita bila kupingwa.
 
Labda bibie kaona vyema asiitaje familia ya mzee. Lakini walio wengi wajanja, na wanaridhika tu wakiwa na uhakika wa kula, kuvaa, matibabu na kulala. Ni familia ya mfano haijawahi kutokea.
 
Do we think at the same levels? Kuna wengine hawana true assessment of the situation au wanadharau nini jamii inaona na kutaka au wanaamini wao pekee ndio wanashikilia hatma ya lolote litakalotokea kesho kwahiyo hakuna shida kuingiza michezo kama hiyo kwenye siasa. Kwa vyovyote vile, kuna gharama za kufanya hivyo mbele ya safari hasa pale ambapo power itashift.
 
taarifa kutoka dodo zinasema jk wa awamu hii ameingiza watatu kutoka familia yake katika uongozi ndani ya ccm nikajaribu kufikiria jk wa ukweli angeingiza wangapi kama angesimamia kupitisha majina ndani ya uongozi ccm.
tujadili bila jazba wala kejeli kwa sababu hata kwenye mpira kuna familia za mpira na nyingine ni mmoja tu alifanikiwa kucheza mpira kwa mafanikio.je jk wa sasa ni familia ya kina njohole na jk wa zamani ni ya kina lunya.

hajali kuwa wapinzani watatumia huo udhaifu wa kifamiliya kuiangusha ccm? huyu ni mwenyekiti ansiye na vision
 
Back
Top Bottom