CHADEMA yaiiga ODM kuhusu Sera ya Majimbo

Mambo ya kusema ni ukabila hayo ni kampeni chafu za CCM za kuwaogopesha wananchi kujaribu mbinu mpya za kulikwamua taifa!
Tume stuck na hatutaki kukubali!
Tunacheza tu kwenye matope!
ITS TIME TO GET OUT FROM IT!
 
Nataka nionyeshwe ni kivipi ukabila utapata nguvu chini ya sera hizi!
Na pia tuangalie kama tunaweza kurekebisha loophole ya namna hiyo kama ina exist!
Na kama hakuna uwezekano huo...Then hata mimi sitoweza kuisapoti hii sera ya majimbo kama ni kweli itapelekea migawanyo na ukabila!
Hapa kumbuka kuwa huu ni mjadala na si mabishano.
So mwenye data ashuke na si baseless accusations
 
Mambo ya kusema ni ukabila hayo ni kampeni chafu za CCM za kuwaogopesha wananchi kujaribu mbinu mpya za kulikwamua taifa!
Tume stuck na hatutaki kukubali!
Tunacheza tu kwenye matope!
ITS TIME TO GET OUT FROM IT!

Ukabila (au "ethnicity") siyo propaganda za CCM kama unavyodhania bali ni extension of (and is as real and powerful a force in the human race as) family, extended family and kinship as we know these.
 
Jmushi1
Mi bado nahitaji muda kuisoma rasimu hii kabla sijachangia sana. Lakini naikubali sana maana italeta maendeleo karibu sana na wananchi. Lakini pia nitaikubali na kuielewa kama viongozi wa majimbo Kama ilivyo kwa RC na DC watakuwa wamechaguliwa na wananchi wenyewe badala ya kuwa political posts ambazo watu wanagawana vyeo kwa undugu, urafiki, umbea, mapenzi na kadhalika. Hawa viongozi wakichaguliwa na watu watawajibika sana kusukuma maendeleo na ufisadi utashuka sana.
Kwa suala la ukabila mimi naona hilo wala si shida maana hata sasa utaratibu tulionao ni ukabila tupu. Angalia mikoa ilivyogawanywa kama si ukabila tu. angalia hata wilaya zote hapa nchini, zimegawiwa kikabila tupu. Sasa hawa wanaokuja kwa hoja hii bora wanyamaze maana majimbo yanaweza kubeba makabila mengi tu kuliko mikoa na wilaya zao zilivyo sasa ambapo zimegawanywa kikabila.
 
b) Kuna haja ya kuwa na mfumo mbadala wa utawala utakaochochea ufanisi na maendeleo ya haraka kwa kupeleka madaraka karibu zaidi na wananchi badala ya kila kitu kuidhinishwa, kutekelezwa na kusimamiwa na utawala wa serikali kuu ulio katika eneo moja tu la nchi (Dar –Es-Salaam).

c) Kuna haja ya kuwa na mfumo mbadala wa utawala utakaotoa kwanza uhuru kwa watu kutumia raslimali zinazopatikana katika maeneo yao kujiletea maendeleo na wakati huo huo kufidia maeneo yatakayoonekana kupungukiwa raslimali, badala ya raslimali kutoka pembe zote za nchi kulimbikizwa Dar-Es-Salaam.

d) Kuna haja ya kuwa na mfumo mbadala wa utawala utakaokidhi zaidi haja na matakwa ya demokrasia ya vyama vingi ili kuchochea maendeleo ya haraka na kuepuka hatari ya taifa kutumbukia kwenye migogoro ya kisiasa katika siku zijazo.

1. Mfumo wa sasa wa utawala umesababisha kero kadhaa za muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar kwa kipindi cha miaka 44 sasa (tangu mwaka 1964). Mathalani upande wa Zanzibar umekuwa ukilalamika kuwa unapunjwa kimapato, na kumezwa sana kihadhi na kimamlaka na upande wa bara na kwa upande mwingine watu wa Tanzania bara nao wamekuwa wakilalamika kuwa Zanzibar imepewa nafasi kubwa kwenye muungano kuliko ukubwa wake. Kero hizi zinajenga hoja ya kutazama upya mfumo wetu wa utawala katika ngazi ya muungano ili kuepusha nchi kutumbukia kwenye migogoro mikubwa ya kisiasa katika siku zijazo.

Hizo highlights ndio zinapelekea baadhi ya watu kuziita pesa zetu vijisenti!
Sasa si kwasababu zimekaa huko Dar es Salam bila matumizi huku technically zikimilikiwa na watu wachache kama kina Chenge huku wananchi wakifa kwa umasikini na magonjwa na njaa?
 
Na kwa kweli kama alivyosema Jmushi1 wanaoona hoja ya majimbo ni ukabila ni CCM ambao wao ndio waotumia kama ngao ya kupinga sera ya majimbo. Hilo halina ubishi. Lakini wamesahau kwamba kama ni ukabila basi wao ndio wameuzalisha maana mikoa na wilaya zimeganywa na zinaendelea kugawanywa kikabila hapo wanasemaje?
 
jmushi1,
Mkuu hii sio mara yangu ya kwanza kujadili swala hili, mapungufu nimeshayasema long time pamoja na kwamba hatukukubaliana na baadhi viongozi wa Chadema.
Hivyo nita deal la tatizo lililopo hapa usoni. Nimesema huwezi kumpasua mtu kichwa kwa sababu anaumwa mguu unless umefanya utafiti na kukuta kwamba swala hili linatokana na nerve fulani za kichwa kwenda miguuni.. Hili halijafanyika bado..
Sasa kama swala hili linahusiana na UCHUMI let's look at UCHUMI wenyewe..
Nchi yetu ni TAJIRI (raslimali) lakini watu wake ndio maskini kwa sababu kabla hata hatujapanda mbegu huwa zimeisha ibiwa.. Hivyo solution ya kugawa utajiri huo ktk majimbo utatoka wapi kama sio kugawana umaskini..Tumeshindwa kuzalisha kutokana na mikataba feki je majimboni kutazuia nini mikataba feki ikiwa kina Karamagi wapo kila kona kuiba mbegu zetu..Mkuu mnachoshindwa kuona wengi hapa ni kwamba Tanzania tunaibiwa mbegu zetu (Utajiri wa rasilimali) kabla hata hatujapandikiza, sasa huko Majimboni utawauzia nini ama fedha zipi zitakazo kwenda huko ikiwa mbegu hizi zinaibiwa kabla ya hata ya kuzijafika shambanii..tatizo kubwa la majimbo ni pale linapotazama zaidi mavuno wakati tatizo kubwa la uchumi wetu ni wizi na ulaji wa mbegu za kupandikiza uchumi huo. Hizi ni fedha za misaada toka nje fedha ambazo zimekusudiwa kujenga miundombinu yetu..tazama scandal zote zinahusu mabillioni ya fedha zinazotakiwa kuoteshwa ktk miradi mikubwa ya kitaifa. Trust me, kama tungekuwa tayari tuna kila kitu on line hakuna uhujumu uchumi any system could work na matatizo ya system moja yanaweza kuonekana kirahisi...

Tumeshindwa ukulima wenyewe kutokana na uongozi mbovu sasa hilo shamba hata tukiligawa vipi imeshindikana chini ya mfumo huu kwa sababu fedha haziwafikii wananchi wenye njaa, zinaliwa na baadhi viongozi..kwa hiyo kikwazo ni viongozi waliopo iwe CCM ngazi za Kitaifa, mikoa ama wilaya. wamejaribu madaraka ya wilaya na hizo halamashauri wamezuka kina Karamagi huko wilayani.. this alone ni ishara kubwa kwamba fisi wapo hata Ukerewe..
Tukiunda majimbo haya kutabadilisha kitu gani nafasi ya hawa viongozi kuendeleza mpango wao wa fedha hatowafikia wananchi?..
Mkuu haisaidii kitu ikiwa cheque yako utapewa wewe ama mke wako ikiwa mwizi wa cheque hizi ni mfanyakazi wa benki.. Fungua matawi mengi utakavyo haiwezi kusaidia isipokuwa unaongeza wezi ktk benki hizo kwani mfumo uliopo ndani ya Benki hizi unaruhusu mtu kughushi cheque za watu.
Hii ndio maana yangu na haina maana Majimbo ni sera mbovu laa hasha isipokuwa hai deal na the real issue hapa ikiwa diagnosis ya maradhi yetu (umaskini) haijafanywa..
Mfano ni kuwa Kama Karamagi kaweza kuiba toka serikali kuu atashindwa nini mtu mwingine mwenye mawazo kama Karamagi kuiba akiwa Jimboni... maanake tatizo letu sio mgao wa
 
Utaratibu wa central government kubakia wenye mamlaka kwenye shughuli zote za kimaendeleo ni mzigo mkubwa ambao unapelekea loopholes zinazotumiwa so often na Mafisadi!
Hapa accountability pia itakuwepo zaidi kwasababu wananchi watakuwa na uwezo zaidi wa kuwa monitor viongozi wao kwa ukaribu kuliko ilivyowahi kuwa before!!

Mkuu Jmushi1,

Nafikiri unachotakiwa kuongelea hapo ni kuimarisha halmashauri za wilaya na wala sio kuunda serikali nyingine ya jimbo.

Wakati tunaona umuhimu wa serikali ya mkoa haupo, nyie mnaongelea kuongeza level nyingine ya Kanda ambayo hata siku moja haiwezi kuwa karibu na wananchi.

Kwa maoni yangu hayo majimbo mnayoyasema yatakuwa ma middlemen ambao wanaongeza cost ya uendeshaji bila ku create au ku add any value kwa mwananchi aliyeko chini.

Nguvu kubwa sasa lazima iwekwe kwenye serikali za mitaa, hizo ndio ziko karibu na wananchi na zinaweza kuwawakilisha kwa ufanisi mkubwa zaidi.
 
Jmushi1
Mi bado nahitaji muda kuisoma rasimu hii kabla sijachangia sana. Lakini naikubali sana maana italeta maendeleo karibu sana na wananchi. Lakini pia nitaikubali na kuielewa kama viongozi wa majimbo Kama ilivyo kwa RC na DC watakuwa wamechaguliwa na wananchi wenyewe badala ya kuwa political posts ambazo watu wanagawana vyeo kwa undugu, urafiki, umbea, mapenzi na kadhalika. Hawa viongozi wakichaguliwa na watu watawajibika sana kusukuma maendeleo na ufisadi utashuka sana.
Kwa suala la ukabila mimi naona hilo wala si shida maana hata sasa utaratibu tulionao ni ukabila tupu. Angalia mikoa ilivyogawanywa kama si ukabila tu. angalia hata wilaya zote hapa nchini, zimegawiwa kikabila tupu. Sasa hawa wanaokuja kwa hoja hii bora wanyamaze maana majimbo yanaweza kubeba makabila mengi tu kuliko mikoa na wilaya zao zilivyo sasa ambapo zimegawanywa kikabila.

Safi sana na inabidi tujiepushe na hayo!
Na CCM wanaendelea kutugawanya ili iendelee kutawala base on devide and rule policies!
Hii system ya sasa ilikuwa ni ya mkoloni na bado serikali yetu wenyewe inaitumia dhidi yetu bila huruma!
Nakubali viongozi wawe wa kuchaguliwa!
 
Majimbo?

a. Tunapozungumzia Majimbo yanayojiendesha tunajaribu kumfuata mfano wa nani? Majimbo kama (states za Marekani); majimbo kama majimbo ya Canada (Provinces); majimbo kama mikoa ya Kenya?

b. Kuna uhusiano gani kati ya Majimbo (katika maana yake yoyote) na serikali Kuu? Hususan; mambo ya nje, usalama, raslimali, madini yanayopatikana kanda ya ziwa chini ya jimbo hilo yanafaida gani kwa jimbo la Kusini?

c. Je majimbo haya yatakuwa na Katiba zao (kama ilivyo Marekani) au yatajiongoza kwa mtindo wa sheria ipi? Kimsingi ni lazima kuwe na Katiba Mpya...

will continue
 
Mkuu Jmushi1,

Nafikiri unachotakiwa kuongelea hapo ni kuimarisha halmashauri za wilaya na wala sio kuunda serikali nyingine ya jimbo.

Wakati tunaona umuhimu wa serikali ya mkoa haupo, nyie mnaongelea kuongeza level nyingine ya Kanda ambayo hata siku moja haiwezi kuwa karibu na wananchi.

Kwa maoni yangu hayo majimbo mnayoyasema yatakuwa ma middlemen ambao wanaongeza cost ya uendeshaji bila ku create au ku add any value kwa mwananchi aliyeko chini.

Nguvu kubwa sasa lazima iwekwe kwenye serikali za mitaa, hizo ndio ziko karibu na wananchi na zinaweza kuwawakilisha kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Mkandara usi itetee system iliyoko sasa hivi kwasababu imeprove failure!
Kama wewe unasema system iliyoko inahitaji marekebisho..Then mwaga data how!?
Si mtu aliyeposti hii mada si ameposti ufanisi wa system tuliyonayo vs hii mpya?
 
Nchi yetu ni TAJIRI (raslimali) lakini watu wake ndio maskini kwa sababu kabla hata hatujavuna mali huwa imeisha ibiwa.. Hivyo solution ya kugawa utajiri huo ktk majimbo utatoka wapi kama sio kugawana umaskini..Tumeshindwa kuzalisha kutokana na mikataba feki je majimboni kutazuia nini mikataba feki ikiwa kina Karamagi wapo kila kona kuiba mbegu zetu..Mkuu mnachoshindwa kuona wengi hapa ni kwamba Tanzania tunaibiwa mbegu zetu (Utajiri wa rasilimali) kabla hata hatujapandikiza, sasa huko Majimboni utawauzia nini ama fedha zipi zitakazo kwenda huko ikiwa mbegu hizi zinaibiwa kabla ya hata ya kuzijafika shambanii..tatizo kubwa la majimbo ni pale linapotazama zaidi mavuno wakati tatizo kubwa la uchumi wetu ni wizi na ulaji wa mbegu za kupandikiza uchumi huo. Hizi ni fedha za misaada toka nje fedha ambazo zimekusudiwa kujenga miundombinu yetu..tazama scandal zote zinahusu mabillioni ya fedha zinazotakiwa kuoteshwa ktk miradi mikubwa ya kitaifa. Trust me, kama tungekuwa tayari tuna kila kitu on line hakuna uhujumu uchumi any system could work na matatizo ya system moja yanaweza kuonekana kirahisi...

Tumeshindwa ukulima wenyewe kutokana na uongozi mbovu sasa hilo shamba hata tukiligawa vipi imeshindikana chini ya mfumo huu kwa sababu fedha haziwafikii wananchi wenye njaa, zinaliwa na baadhi viongozi..kwa hiyo kikwazo ni viongozi waliopo iwe CCM ngazi za Kitaifa, mikoa ama wilaya..
Tukiunda majimbo haya kutabadilisha kitu gani nafasi ya hawa viongozi kuendeleza mpango wao wa fedha hatowafikia wananchi?..
Mkuu haisaidii kitu ikiwa cheque yako utapewa wewe ama mke wako ikiwa mwizi wa cheque hizi ni mfanyakazi wa benki.. Fungua matawi mengi utakavyo haiwezi kusaidia isipokuwa unaongeza wezi ktk benki hizo kwani mfumo uliopo ndani ya Benki hizi unaruhusu mtu kughushi cheque za watu.
Hii ndio maana yangu na haina maana Majimbo ni sera mbovu laa hasha isipokuwa hai deal na the real issue hapa ikiwa diagnosis ya maradhi yetu (umaskini) haijafanywa..
Mfano ni kuwa Kama Karamagi kaweza kuiba toka serikali kuu atashindwa nini mtu mwingine mwenye mawazo kama Karamagi kuiba akiwa Jimboni... maanake tatizo letu sio mgao wa

Swali: jee, wewe hapo ulipo upo tayari kumsaidia mzungu usiyemjua kwa hali na mali ili anufaike au ajinasue kwenye matatizo fulani aliyo nayo AU ndugu yako uliyezaliwa naye baba na mama mmoja?
 
Kama uko familiar na "Matrix stucture" na special project yetu kuwa ni maendeleo ya Taifa..Then hii ndio sera inayotufaa!
 
Mkandara usi itetee system iliyoko sasa hivi kwasababu imeprove failure!
Kama wewe unasema system iliyoko inahitaji marekebisho..Then mwaga data how!?
Si mtu aliyeposti hii mada si ameposti ufanisi wa system tuliyonayo vs hii mpya?

Kwanza niliyetoa hoja ni Mtanzania na wala sio Mkandara.

Pili kushindwa kwa serikali za mitaa kunatokana na capacity ndogo kwa viongozi na watendaji wa hizo halmashauri, kitu ambacho ni tatizo hata kwenye uongozi wa mkoa na itakuwa tatizo kwenye uongozi wa jimbo.

Tatu, halmashauri za wilaya bado zina nguvu kidogo sana na resources wanazopewa bado
ni kidogo ukilinganisha na majuku ambayo wanaweza kuyafanya.

Hayo matatizo hapo juu yanaweza kuwepo hata kwenye serikali za majimbo.

Ubaya wa majimbo kwa kulinganisha na serikali za mitaa ni kwamba itakuwa sawa na kutengeneza central government nyingine ambayo haitakuwa karibu na wananchi.

Kinachotakiwa ni kushughulikia matatizo yaliyopo kwani hata tukianzisha majimbo bado hayo matatizo yataendelea kutuandama tu.
 
Swali: jee, wewe hapo ulipo upo tayari kumsaidia mzungu usiyemjua kwa hali na mali ili anufaike au ajinasue kwenye matatizo fulani aliyo nayo AU ndugu yako uliyezaliwa naye baba na mama mmoja
Sijakuelewa mkuu, huyo mzungu nisiyemfahamu ndiye nani ktk hoja hii ya Majimbo?..
 
Sijakuelewa mkuu, huyo mzungu nisiyemfahamu ndiye nani ktk hoja hii ya Majimbo?..

Hapa najaribu kukuonyesha jinsi nguvu ya "undugu" (and by extension "ukabila" au "ethnicity "- albeit through closely related concepts of extended family and clanship) ilivyo na uhalisi na uhalali usiopingika katika mahusiano yote ya binadamu.
 
Sijakuelewa mkuu, huyo mzungu nisiyemfahamu ndiye nani ktk hoja hii ya Majimbo?..

Nafikiri alikuwa akimaanisha kwenye maamuzi ya uuzaji wa rasilimali zetu!
Maamuzi ambayo huwa yanamaliziwa Dar bila ya kuwashirikisha wazalendo!
 
Bado sikuelewi kabisa kwani sasa hivi hatuna Undugu? Hivi leo unaweza kunambia mtu kama Karamagi ni wa jimbo gani..na kesho chini ya Majimbo atakuwa jimbo gani..
 
Kwanza niliyetoa hoja ni Mtanzania na wala sio Mkandara.

Pili kushindwa kwa serikali za mitaa kunatokana na capacity ndogo kwa viongozi na watendaji wa hizo halmashauri, kitu ambacho ni tatizo hata kwenye uongozi wa mkoa na itakuwa tatizo kwenye uongozi wa jimbo.

Tatu, halmashauri za wilaya bado zina nguvu kidogo sana na resources wanazopewa bado
ni kidogo ukilinganisha na majuku ambayo wanaweza kuyafanya.

Hayo matatizo hapo juu yanaweza kuwepo hata kwenye serikali za majimbo.

Ubaya wa majimbo kwa kulinganisha na serikali za mitaa ni kwamba itakuwa sawa na kutengeneza central government nyingine ambayo haitakuwa karibu na wananchi.

Kinachotakiwa ni kushughulikia matatizo yaliyopo kwani hata tukianzisha majimbo bado hayo matatizo yataendelea kutuandama tu.

Sera ya majimbo itatuwezesha kuwa karibu na viongozi through smooth chain of commands na uwakilishi!
Badala ya Mwanakijiji kusubiri maamuzi ya rais kwenye utekelezaji wa sera muhimu za maendeleo..Wanakuwa na wawakilishi wenye nguvu kwenye maamuzi yenye kuhusika na shughuli za kimaendeleo!
 
Back
Top Bottom