CHADEMA yaiiga ODM kuhusu Sera ya Majimbo

Hawataki hilo lakini linakuja, hatuwezi sehemu zingine watu wanafanyakazi kama mchwa kwingine wanacheza bao tu!

Ha ha ha ha ha ha! Halafu ndio walalamishi na wachochezi wakubwa; tunaonewa, tunapunjwa, tunataka kujitenga. Bro; umegusa penyewe.
 
Victoria Province, North Province, Central Province, Coastal Province, South Province, unguja na Pemba!

Majimbo saba...
 
WENGI WANAFIKIRI UTAWALA WA MAJIMBO NI UKOMBOZI WA MAENDELEO,HUU SI UTAWALA.UTAWALA WA MAJIMBO UNASABABISHA UBAGUZI MKUBWA KATIKA NCHI,NI WAZI KABISA KUWA KUNA BAADHI YA MAJIMBO YATAKUWA DHAIFU NA HIVYO KAMWE HAYATAWEZA KUENDELEA,HIVYO KUSABABISHA EITHER KUDHARAULIWA KWA WATU WAKE AU WATU HAO KUHISI HAWANA UMUHIMU WA KUWA NI SEHEMU YA NCHI HIYO NA HIVYO KUWEZA KUAMUA VYOVYOTE HATA KUJITENGA.MIFANO MINGI YA SERIKALI ZA MAJIMBO IPO KAMA NIGERIA AMBAYO KILA SIKU MAJIMBO YAO YAPO VITANI TOKA MOJA HADI JINGINE,MFANO MWINGINE NI SUDAN NA MAJIMBO YAKE KAMA DARFUR,ABYEI NA SUDAN KUSINI HAPO KABLA ILIJULIKANA KAMA JIMBO LA JUBA, LEO HII WANAJITENGA. CHAMA KINACHOTAKA KULETA UJIMBO NDANI YA TANZANIA KINAJULIKANA CHIMBUKO LAKE NA UONGOZI ULIOPO PIA UNAJULIKANA KWA LENGO LAO LA MAJIMBO KWA KUJIONA KUWA WAO WATAKUWA MBELE NA HAWATAADHIRIKA VYOVYOTE KUTOKANA NA HISTORIA YA MAENEO YAO.KULE AMBAKO KULIBAKI NYUMA WANAJUA HAKUWAHUSU NA HIVYO HATA KUKIENDELEA KUWA NYUMA WAO SI HOJA. SERIKALI YA CCM INA LENGO LA KUWEKA USAWA WA KI MAENDELEO BILA KUBAGUA MAENEO.NA HII NDIO SERIKALI YENYE UTAWALA WA HAKI KWANI WATANZANIA NI WAMOJA.DHAHABU YA NYAMONGO INANUFAISHA MTWARA NA GESI YA MTWARA PIA INA FAIDA KWA TANGA BILA UKIRITIMBA WOWOTE. CHAMA CHENYE SERA ZA KUWAGAWA WATANZANIA KWA NJIA YOYOTE ILE NI CHA KUOGOPWA KAMA UKOMA.
ANGALIA HAPA CHINI JINSI SERA ZAO ZILIVYO.

"kwanza elewa baraza halitakuwa kubwa kiasi hiki! Pili, waziri atakuwa ni Executive tu bila kuingiliana na legislatures, nchi itakuwa ndani ya utawala wa majimbo, tukiwa na majimbo 8.mashariki (Dar, Moro, Pwani na Tanga), Kusini -Lindi Mtwara na Ruvuma, inyanda za juu kusini-Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa; Kati- Dom, Tabora na Singida; Kasikazini- Knjaro, Arusha na Manyara; Ziwa- Mara, Mwz, Simiyu, Geita,shy na Magharibi- Kigoma, Katavi na kagera while Visiwan- Zanzibar yote!

Wakuu wa mikoa wata chaguliwa huku nafasi ya mkuu wa wilaya ikifutwa, mbunge na Mkurugenzi wanatosha ku-run dunia, i mean wilaya! wilaya moja mbunge mmoja!

tupo wote hadi hapo!

afu marando, atorney general"- (MENDE DUME.)
 
Habari Ziada

Naomba utumie herufi ndogo kwenye kuandika. Nataka kuchangia lakini siwezi kusoma.

Thanks
 
Ziada unataka kusema utawala wa kimkoa kwamba hakuna mikoa dhaifu? Mbona inafahamika kuna mikoa mingine ni dhaifu na bado hatudharauliani? Mimi nafikiri umefanya haraka kuleta hoja bila kuifanyia utafiti, mifano uliyotaja ya Nigeria, Sudan nk haikidhi haja. Tatizo la Nigeria sio majimbo bali dini na mafuta, hata ukibadili utawala wa majimbo bila kushuhulikia tatizo la msingi bado vita vitaendelea
 
Mkuuu hiiiiko poa ila inabidi watz waujue kiundani,,, unajua sisi watz tuko nyuma sana kimawazo na kiuchambuzi kwan most of TZ citizens hawajui baya na zuri thats why wanazulumiwa bila kujua,,,,,
 
Sera ya majimbo ni mpango mzuri sana wa maendeleo kwa watanzania. Ni kupunguza gharama kwa serikali. Majimbo yapangwe bila
kuzidi ishirini. hapo ina maana tumeshapunguza mlolongo wa zamani wa wakuu wa mikoa wanaofika zaidi ya ishirini. na kila siku inaonge-
wa mikoa ambayo ni mapori tu. Na wakuu wa majimbo kuchaguliwa na wananchi kwa kupigiwa kura, kwa ufupi hayo yote ndio
yanayohitajiwa katika katiba mpya. Jambo na mfano mzuri ni wa kuigwa. Dunia ya sasa ndipo iliko kwenye kuwaletea wananchi hafueni
ya maisha.
 
Mi shabiki wa CDM. Siipendi hii sera ya majimbo kwa sbb ni divisive. Naunga sana mkono wa kuondoa cheo cha Mkuu wa Mkoa
 
Mi shabiki wa CDM. Siipendi hii sera ya majimbo kwa sbb ni divisive. Naunga sana mkono wa kuondoa cheo cha Mkuu wa Mkoa
Katika hayo majimbo yote, kila moja lina natural resources au means za kujiendesha....kwa hyo kukiwa na na majimbo kila zone watapamabana kuendeleza kwao, kuliko hii ya sass ya wilaya kusubiri mgao wa ruzuku toka dar
 
Ili kuwa na maendeleo ya haraka tunahitaji kuwa na Serikali ya Majimbo na si mkuu wa Mkoa na Wilaya, Mfumo umetutafuna tangu Uhuru hadi sasa tuseme basi na inatosha.

Kama CCM wameanza kuchukua Mengine kutoka CDM basi waichukue na Kulitekeleza hili hapa kabla ya 2015 ili wananchi wapate nafuu kwenye maisha.

Rasilimali zimejaa na hakuna wa kusimamia badala yake kila kiongozi wa CCM anajitahidi kuiba kwa miaka kama 50
 
Ni kweli mkuu majimbo yatasaidia sana kufanya ufuatiliaji wa karibu!
NAUNGA MKONO HOJA!
 
Ili kuwa na maendeleo ya haraka tunahitaji kuwa na Serikali ya Majimbo na si mkuu wa Mkoa na Wilaya, Mfumo umetutafuna tangu Uhuru hadi sasa tuseme basi na inatosha.

Kama CCM wameanza kuchukua Mengine kutoka CDM basi waichukue na Kulitekeleza hili hapa kabla ya 2015 ili wananchi wapate nafuu kwenye maisha.

Rasilimali zimejaa na hakuna wa kusimamia badala yake kila kiongozi wa CCM anajitahidi kuiba kwa miaka kama 50

Hoja ya majimbo imekuwapo toka chama kimeanzishwa! CCM wamekuwa wakitumia sera hii kama ni ya kibaguzi lakini kadri siku zinavyosonga mbele ukweli unajidhihiri kuwa ni sera murua kwa ustawi wa uchumi na maendeleo ya nchi hii!
 
yoyoyo!!!heshima kwenu wakuu,,,from New Delhi here na ninaunga mkono mfumo wa majimbo.LAKINI
1.kwa sababu chadema inaunga mkono serikali 3,basi ziundwe serikali ya Tanganyika,Zanzibar na Tanzania KWANZA.
2. cheo cha waziri mkuu kingebakia ili kusimamia serikali ya tanganyika yenye majimbo 8
majimbo ya tanganyika (WAZIRI MKUU=HEAD OF TANGANYIKAN GVT)
3.zanzibar ibakie kuwa na rais wake kama kiongozi wake mkuu
4.rais wa muungano wa tanzania na makamu wa rais wasimamie wizara za muungano kama mambo ya nje,fedha nk.
5.bunge,mahakama na serikali kuu viwe independent(bunge lisiwe chini ya rais kama ilivyopendekezwa.
6.mwisho mgawanyo wa majimbo ujikite zaidi ktk rasili mali zilizopo na idadi ya watu kuepuka majimbo mengine kuachwa nyuma kimaendeleo.nina wasiwasi na hilo jimbo la tanga
 
Back
Top Bottom