CHADEMA yaiiga ODM kuhusu Sera ya Majimbo

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Ili kujiandaa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA leo wapo Jijini mwanza ili kuweza kuibua mchakato wa kuiboresha sera yake ya majimbo ambayo kilijinadi nayo kwenye uchaguzi mkuu wa 2005.

Katika kufanya mchakato huo ulioandaliwa na Kurugenzi ya Bunge na Halimashauri -kitengo cha sera na utafiti wakishirikiana na kurugenzi ya vijana , wameweza kuandaa rasimu ya sera hiyo kwa ajili ya kuibua mjadala wa kitaifa.

Viongozi wakuu wa CHADEMA wanategemewa kuhudhuria Kongamano hilo ambqalo linafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Mwanza leo hii.

Yupo mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, pamoja na Makamu mwenyekiti Bara . wengine ni pamoja na mkurugenzi wa vijana taifa John Mnyika, Danda JUJU ambaye ni afisa mwandamizi kurugenzi ya Bunge nba halimashauri kitengo cha sera na utafiti.

Nitawawekea rasimu ya mjadala huo hapo chini.
 
Pia wanategemewa kufungua ofisi ya Vijana CHADEMA mkoani mwanza eneo la Nyegezi, hii ni ofisi ambayo vijana wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mt. Augustine waliitafuta wenyewe na kuchangishana ili kuhakikisha kuwa wanapata mahali pa wao kujadili na kutoa mawazo yao juu ya hatima ya taifa lao Tanzania.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

RASIMU YA SERA YA MFUMO MPYA WA UTAWALA
“SERA YA MAJIMBO”

“Nguvu na Mamlaka kwa Umma”


IDARA YA UTAFITI NA SERA –TAIFA
MEI 2008

YALIYOMO

Dibaji ........................................................................................................................... 4

Shukrani ..................................................................................................................... 6

Utangulizi .................................................................................................................... 7

SURA YA KWANZA

TATHIMINI YA MFUMO WA SASA WA UTAWALA

1. Maana ya mfumo wa utawala ..................................................................... .8

2. Mfumo na muundo wa sasa wa utawala.................................................... 8

3. Udhaifu wa mfumo wa sasa wa utawala na matokeo yake ...................9

4. Asili ya mfumo wa sasa wa utawala .............................................................10

SURA YA PILI

HOJA ZA KUWA NA SERA YA MFUMO MPYA WA UTAWALA - SERA YA MAJIMBO ................................................................................................. 21

SURA YA TATU

DIRA, DHUMUNI, NA MALENGO YA SERA YA MFUMO MPYA WA UTAWALA “SERA YA MAJIMBO” .......................................................................22

1. Dira......................................................................................................................15

2. Dhumuni kuu....................................................................................................15

3. Malengo mahsusi..............................................................................................15

SURA YA NNE

MATAMKO YA SERA YA MFUMO MPYA WA UTAWALA
“SERA YA MAJIMBO”
1. Mfumo Mpya wa Utawala ............................................................................17

2. Muundo Mpya wa Serikali Kuu.................................................................18

3. Muundo Mpya wa Serikali za Majimbo.....................................................20.

4. Mgawanyo wa Raslimali katika Serikali za Majimbo ............................21.

5. Mgawanyo wa Majukumu katika Serikali za Majimbo ..........................22

6. Mawasiliano ya kiutendaji ............................................................................23

7. Muundo Mpya wa Serikali za Mitaa............................................................21

8. Vyombo vya uwakilishi katika Mfumo Mpya wa Utawala ....................22.

9. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .......................................... 25

10. Mabaraza ya jimbo ...........................................................................................26

11. Mabaraza ya halmashauri ..............................................................................27.

SURA YA TANO

MCHAKATO WA KUANZISHA MFUMO MPYA WA UTAWALA
“UTAWALA WA MAJIMBO”

1. Kuanzisha mjadala wa kitaifa ............................................................................30

2. Kuandika rasimu ya Katiba Mpya.......................................................................

3. Kukusanya maoni ya wananchi ..........................................................................35.

4. Kupeleka muswada wa Katiba Mpya Bungeni ..................................................

5. Kuanzisha Mfumo Mpya wa Utawala kwa awamu ........................................24.

DIBAJI.

Ndugu Watanzania Wenzangu,

Miaka 47 ya uhuru na umaskini wetu inatosha kwa kila mmoja wetu, kukiri kwa nia njema kabisa, kuwa tumekwama. Kwamba, maadui watatu ambao sote kama taifa tulinuia kuwatokomeza; ujinga, umaskini, na maradhi, wametushinda!.

Taifa lolote lililokwama linahitaji mabadiliko. Mabadiliko hayo huweza kuja kwa njia mbili. Ama kwa mtindo wa kutumia nguvu, yaani mapinduzi (revolution), au kwa mtindo wa amani, yaani mageuzi (reforms).

Ni dhahiri kuwa sote tunapendelea mabadiliko kwa njia ya amani, yaani ‘reforms’. Tangu tumepata uhuru, Tanzania imefanyiwa ‘majaribio’ mengi sana ya kisiasa, kijamii na hata ya kiuchumi, lakini ‘majaribio’ haya hayakutukwamua. Bado tumekwama!.
Yako maeneo machache tuliyopiga hatua kama taifa. Lakini mafanikio machache tuliyopata hayalingani na utajiri wa asili wa nchi yetu. Aidha, mafanikio kidogo ya wakati tulionao ni sawa tu na umaskini wa wakati huu tulionao maana mafanikio haya hayalingani kabisa na umri wa miaka 46 ya uhuru wetu.
Ni kweli subira huvuta heri, lakini subira inapoendelea kutumbukiza taifa kwenye lindi la umaskini, subira hii hukaribisha shari!
Ni rahisi kufikiria kuwa kukwama kwetu leo ni tunda la ufisadi wa viongozi. Ni kweli hili linachangia. Hata hivyo tukumbushane historia kidogo.
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliongoza taifa hili kwa miaka 25. Alikuwa kiongozi aliyependwa sana na watu. Hakuwa fisadi na wala serikali ya awamu yake haikuwa ya kifisadi. Pamoja na uadilifu wa Mwalimu, bado nchi hii, ilikwama sana kiuchumi na hivyo kimaendeleo!
Ni dhahiri kuwa kutokomeza ufisadi pekee si suluhisho pekee la kuipeleka nchi yetu kwenye neema. Tunahitaji kufanya mageuzi makubwa zaidi ya kutokomeza ufisadi.Mageuzi yanayolikwamua taifa lolote huanzia kwenye mageuzi ya kifikra.
Naam! Baada ya kutafiti na kutafakari kwa kina, kwa upande mmoja tulibaini kuwa ukubwa wa nchi yetu na utajiri wake wa asili vimelemaza taifa letu. Kwa upande wa pili, tulibaini na hivyo kuamini kuwa mfumo wetu wa utawala umeshindwa kutumia rasilimali watu na maliasili yetu kwa maendeleo ya taifa.
Tutafakari kwa pamoja masuala haya kwa kina kisha tuchukue uamuzi wa kufanya mabadiliko ya mageuzi (reforms). Wakati umetutupa sana lakini tusiwe tayari muda utupite zaidi. Tuyazingatia haya;
Kwamba mfumo wetu wa utawala ndiyo chimbuko la umaskini na kukwama kwetu.Kwamba hata ukimleta ‘malaika’ ukamweka Ikulu awe Rais wa Tanzania, kwa mfumo wetu wa utawala uliopo, lazima atakwama!Kwamba utajiri wetu wa asili ndio utatumika kama chanzo cha kubomoa mshikamano wa taifa. Kwamba, kwa matendo ya watawala wetu, ni wazi kwamba wamemsahau Mungu!Kwamba amani yetu ni tete!
Ndugu Watanzania Wenzangu, Rasimu ya Sera hii imefanya tafakari ya kina ya masuala haya. Haikuishia hapo. Imetoa ufumbuzi wa kifikra kwa kuzingatia uhalisia. Nachukua fursa hii kuzindua rasmi mchakato wa kukusanya maoni kwa ajili ya kuifanyia marejeo(reviews) sera ya Mfumo Mpya wa Utawala(Sera ya Majimbo); rasimu hii isaidia kuchochea mjadala kufikia azma hiyo.
Kwamba, mfumo mpya wa utawala “utawala wa majimbo, ndio jibu la msingi la kukwama kwetu.
Hima tuweke kando itikadi na tofauti zetu, turuhusu utashi na maono yetu kwa maslahi ya taifa letu. Kisha tuukubali ukweli na kuchukua uamuzi kwa maslahi ya Taifa letu.
Tumechelewa lakini bado tuna nafasi ya kufanya mabadiliko ya kasi yatakayovuka kasi ya kuchelewa kwetu. Amina!
Freeman Aikaeli Mbowe.

Mwenyekiti wa Taifa

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

SHUKRANI

Idara ya Uafiti na Sera – CHADEMA, inapenda kuwashukuru kwa dhati watu binafsi, asasi zisizo za kiserikali, taasisi na mashirika mbalimbali ambayo yamechangia kwa njia moja au nyingine kukamilika kwa rasimu ya sera hii.

Tunathamini michango yote ya kifikra iliyotolewa na wananchi wa kada mbalimbali walio wanachama na wasio wanachama wa CHADEMA katika mchakato wa kukusanya maoni yaliyowezesha kuandikwa kwa rasimu hii. Na tunapenda kutoa rai kwa wananchi wengi zaidi kuweza kutoa maoni yao mbalimbali kuhusu rasimu hii ili hatimaye tuweze kupitisha sera iliyoboreshwa zaidi.

Kwa nafasi ya kipekee kabisa nawajibika kuwashukuru wajumbe wa Kamati iliyoandaa rasimu hii. Hawa ni Mzee Masinde, ndugu Vincenti Bukuru na ndugu Kilian Nango kwa mchango wao uliotukuka.

Aidha, natambua na kuthamini kwa dhati mchango wa ndugu Edward E. Kinabo ulioboresha uchambuzi wao na kupelekea kukamilika kwa rasimu ya sera hii.

Ni haki kuwashukuru maofisa wote wa Idara ya Utafiti na Sera katika Kurugenzi ya Bunge na Halmashauri kwa kushirikiana na Kurugenzi ya Vijana kwa kutafiti na kupata matokeo mbalimbali yaliyojenga dhana na uhalisia wa sera hii.

Taifa na vizazi vyake vitawakumbuka kwa uzalendo wenu!

Idara ya Utafiti na Sera inaisambaza rasmi rasimu hii kwa umma ili kupata maoni ya wananchi kabla ya vikao vya kikatiba vya CHADEMA kuzingatia maoni hayo na kupitisha sera kamili itakayozinduliwa mwishoni mwa mwaka huu wa 2008.

Danda Juju Martin

AFISA MWANDAMIZI WA UTAFITI NA SERA –CHADEMA.

UTANGULIZI

Katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi dhumuni kuu la chama cha siasa ni kutafuta ridhaa ya kuongoza dola.

Sanjari na hili, chama cha siasa pia kina wajibu wa kujipanga kiitikadi na kisera juu ya namna bora ya kuongoza dola.

Aidha, wakati chama kikitafuta ridhaa ya kuongoza dola kinawajibika pia kutathmini ubora wa itikadi, dira, sera, mikakati na mipango iliyopo ili kuibua fikra mbadala za kushauri na kurekebisha mapungufu yaliyopo kwa maslahi ya taifa.

Kwa kipindi cha miaka 47 sasa, hatma ya maendeleo na mustakabali wa Tanzania, imekuwa ikitegemea mfumo na muundo wa utawala uliorithiwa kwa wakoloni baada ya uhuru.

Hiki kimekuwa ni kipindi kirefu kabisa cha kutathmini ubora na ufanisi wa mfumo huu katika kukidhi matakwa na matarajio ya wananchi.

Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa kikifanya tafiti na tafakari za kina juu ya chanzo kikuu cha umaskini wa nchi hii.
Wakati umefika.

Wajibu wa CHADEMA wa kutoa suluhisho mbadala kwa umaskini wa nchi hii haukwepeki.

Tafiti ambazo chama hiki kimefanya na kushirikisha wananchi ndio zao la sera hii ya Mfumo Mpya wa Utawala “Sera ya Majimbo” ya mwaka 2008.

SURA YA KWANZA

TATHMINI YA MFUMO WA SASA WA UTAWALA

1.0 Maana ya Mfumo wa Utawala.

(1) “Mfumo wa utawala” kwa muktadha wa sera hii, ni uhusiano kati ya muundo wa vyombo mbalimbali vya uongozi wa umma ikiwa ni pamoja na mamlaka na wajibu wake kwa umma, na wajibu wa umma na mamlaka yake kwa upande wa pili, katika kuamua, kuendesha na hatimaye kufanikisha nia na matarajio ya umma wa eneo fulani la nchi na/au nchi husika kwa ujumla.

(2) Vyombo vinavyojenga utawala au uongozi wa umma ni serikali na ngazi zake mbalimbali mintaarafu serikali kuu na serikali za mitaa na idara zake, vikiwemo pia vyombo vya uwakilishi wa wananchi kama Bunge, na vyombo vinavyohusika na haki kama mahakama.

(3) Mamlaka na wajibu wa vyombo hivi pamoja na wajibu na mamlaka ya umma hubainishwa katika katiba ya nchi na sheria mbalimbali ambazo hutengenezwa na kuridhiwa na umma wa eneo au nchi husika.

(4) Kimsingi, majukumu makuu ya mfumo wowote wa utawala katika nchi ni kukuza maendeleo ya kiuchumi na kutoa huduma za jamii kama vile ulinzi na usalama wa raia, elimu, afya, maji, nishati na mengineyo.


2.0 Mfumo na Muundo wa sasa wa Utawala.

(1) Mfumo na muundo wa sasa wa utawala nchini umegawanyika katika ngazi kuu mbili; serikali kuu na serikali za mitaa.

(2) Serikali kuu imegawanyika katika sehemu kuu saba, nazo ni;

I. Ofisi ya Raisi – hii inajumuisha pia Bunge na Mahakama.
II. Ofisi ya Makamu wa Raisi.
III. Ofisi ya Waziri Mkuu.
IV. Wizara za sekta mbalimbali ikiwemo inayohusika na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
V. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
VI. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
VII. Ofisi ya Katibu Tarafa.


(3) Serikali za mitaa zimegawanyika katika ngazi kuu tano;

I. Halmashauri za wilaya/manispaa/jiji.
II. Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji.
III. Wakuu wa Idara katika Halmashauri. Idara hizi ni kama idara za mipango, kilimo, elimu, maji, maliasili, maendeleo ya jamii n.k).
IV. Ofisi ya Kata – hii huwa chini ya Katibu Kata na Kamati ya Maendeleo ya Kata.
V. Serikali ya Kijiji/Mtaa – hii huundwa pia na Ofisa mtendaji wa Kijiji na Halmashauri ya Kijiji.

(4) Serikali kuu na serikali za mitaa zina mahusiano na maingiliano makubwa katika utekelezaji wa majukumu yake. Kazi na majukumu ya serikali za mitaa zimeainishwa kwenye sheria ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982. Kwa mfano, sehemu ya 111 na 118 ya sheria za Mamlaka za Mijini (Urban Authorities) zimeainisha huduma zinazotolewa na serikali za mitaa kama ifuatavyo.

a) Huduma zinazotolewa na serikali za mitaa kwa usimamizi wa serikali kuu. Huduma hizi ni elimu ya msingi, huduma za afya, maendeleo ya kilimo na mifugo, maji, na ujenzi na ukarabati wa barabara.

b) Huduma zinazotolewa na kusimamiwa na serikali za mitaa yenyewe. Huduma hizi ni ukusanyaji wa taka, usafi wa mazingira, maegesho ya magari na vifaa vinginevyo, masoko na nyinginezo.


3.0 Udhaifu wa mfumo wa sasa wa utawala na matokeo yake.

(1) Mfumo wa sasa wa utawala ndiyo chanzo kikuu cha umaskini na kusuasua kwa maendeleo ya watu wa taifa hili. Hii ni kwa sababu ya mapungufu yafuatayo;

(2) Mfumo wa sasa wa utawala una mlundikano mkubwa wa ngazi mbalimbali za serikali na vyeo vingi visivyokuwa na ulazima wala tija kwa maendeleo ya watu. Kwa mfano, kumekuwa na migongano ya kiutendaji kati ya Serikali Kuu (Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya) na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa pande zote kufanya kazi katika eneo moja la kijiografia na katika jamii ile ile moja. Mlundikano huu wa ngazi nyingi za utawala umekuwa ukisababisha yafuatayo;

a) Kuwepo kwa utitiri mkubwa tena usio wa lazima wa viongozi na ofisi za serikali na hivyo serikali kujikuta ikitumia fedha nyingi zaidi kugharamia utawala kuliko maendeleo ya wananchi. Karibu kila mwaka bajeti ya serikali hutenga fedha nyingi mno kwa ajili ya utawala kuliko ile ya miradi ya maendeleo ya wananchi. Matokeo yake ni umaskini na kuendelea kusuasua kwa maendeleo ya watu.

b) Kuwepo kwa urasimu, uzembe na ucheleweshaji mkubwa wa kutoa huduma na kutekeleza mikakati na hivyo kusuasua kwa maendeleo ya watu.

(3) Mfumo wa sasa wa utawala umelimbikiza madaraka makubwa na raslimali za maendeleo kwa serikali kuu ambayo kimuundo haipo karibu na wananchi kulinganisha na serikali za mitaa. Madaraka zaidi ya kiutawala na watumishi, madaraka ya kifedha, na madaraka ya kisiasa na kimaamuzi yote yamekuwa chini ya serikali kuu. Hili limekuwa na athari zifuatazo;

a) Nchi nzima bila kujali ufanisi imekuwa ikiendeshwa kutokea Dar-Es-Salaam ilipo Ikulu, wizara na ofisi mbalimbali za kiserikali na hivyo kutokuwepo uratibu mzuri wa shughuli za kimaendeleo.

b) Mapato yote kutoka vyanzo vikuu vya mapato yamekuwa yakichukuliwa na serikali kuu – Dar –Es-Salaam, na kutumiwa vibaya au kugawanywa vibaya kwa wilaya na mikoa na matokeo yake ni kuwa na maeneo mengi yenye utajiri wa raslimali lakini bado yapo kwenye lindi la umaskini. Mfano ni wilaya ya Geita, yenye utajiri mkubwa wa raslimali ya madini lakini watu wake ni maskini.

c) Serikali za mitaa zimekuwa zikipokea zaidi amri kutoka serikali kuu na hivyo kukosa umuhimu na uwezo wa kushughulikia maendeleo ya watu.

d) Viongozi wa serikali kuu wamekuwa na mwanya wa kufanya watakavyo kwa kutokuwepo udhibiti dhidi yao. Kwa mfano, waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa ana nguvu za kikatiba za kufanya maamuzi binafsi bila kupitia bungeni. Kwa mwanya huu huweza kufanya maamuzi binafsi kwa misingi ya kiitikadi pale ambapo mamlaka husika ya Serikali za Mitaa inapokuwa inaongozwa na chama tofauti na cha Waziri huyo mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
e) Kutokuwepo kwa udhibiti wa kutosha kwa viongozi wa serikali kuu pia kumekuwa kukichochea sana rushwa na ufisadi. Nafasi ya Bunge kufuatilia na kusimamia utendaji wa serikali kuu imekuwa ikiathiriwa na baadhi ya sheria zinazotoa mamlaka kwa mawaziri kufanya maamuzi makubwa bila kupitia Bungeni, mathalani mikataba ya madini kuwa siri kati ya serikali na kampuni husika.

(4) Mfumo wa sasa wa utawala umepoka nguvu na mamlaka ya umma na kuwapa watawala dhamana ya kuutawala umma bila ridhaa yake. Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya huteuliwa na Rais. Kiutendaji wanawajibika kwa Rais kupitia Waziri Mkuu. Wakuu wa mikoa wana mamlaka na madaraka ya kisiasa na kiuendeshaji/kiutendaji na ya kipolisi (kama kutoa amri mtu kukamatwa na kushtakiwa). Kama alivyo Waziri kwa Wizara yake ndivyo alivyo pia mkuu wa mkoa kwa mkoa wake, na mkuu wa wilaya na wilaya yake. Wote wanamwakilisha Rais katika maswala ya kisiasa na ya uendeshaji wa shughuli za Serikali. Lakini tofauti na Waziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawatokani na ridhaa ya wananchi. Hili limekuwa na athari zifuatazo;

a) Limeweka uwezekano kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutimiza zaidi maslahi yao, ya vyama vyao na hasa maslahi ya Raisi anayewateua kuliko kutimiza haja na matakwa ya wananchi wanaowatawala.

b) Wananchi wamekuwa wakishindwa kuwahoji na kuwawajibisha Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa kuwa wakuu hawa hawapatikani kupitia chaguzi ambazo zingetoa fursa hiyo bali huteuliwa na Raisi.

c) Wakuu wa Mikoa na Wilaya wamekuwa na madaraka dhidi ya mamlaka za serikali za mitaa ambazo viongozi wake hupatikana kwa ridhaa ya wananchi kupitia chaguzi za serikali za mitaa.

d) Kwa hali hii serikali kuu imekuwa ikifinya demokrasia na kukwaza uhuru wa serikali za mitaa katika kutimiza wajibu wake kwa wananchi. waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa ana nguvu za kikatiba za kufanya maamuzi binafsi bila kupitia bungeni. Kwa mwanya huu huweza kufanya maamuzi binafsi kwa misingi ya kiitikadi pale ambapo mamlaka husika ya Serikali za Mitaa inapokuwa inaongozwa na chama tofauti na cha Waziri huyo mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.

(5) Kumekuwa na mapungufu katika uundaji wa wilaya na mikoa. Ibara ndogo ya (2) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977 ndiyo inatoa madaraka kwa Rais kuunda mikoa hata hivyo haikuainisha vigezo vya msingi vya kuzingatiwa katika kuamua eneo fulani kutamkwa kuwa Mkoa. Aidha mkoa kama taasisi haukupewa majukumu mahsusi ya kikatiba. Badala yake ni mkuu wa mkoa binafsi anayepewa majukumu kikatiba na majukumu hayo kufafanuliwa zaidi katika sheria ya Tawala za Mikoa No. 19 ya 1997. Uundaji wa wilaya nao hauna vigezo vya msingi vinavyoeleweka kisheria. Kwa sababu hii baadhi ya mikoa imekuwa ikiundwa si kwa sababu ya kurahisisha maendeleo ya wananchi bali kuwagawa na kuwatawala kirahisi kwa manufaa ya chama kilicho madarakani (CCM).

(6) Mfumo wa sasa wa utawala haukidhi haja ya demokrasia ya vyama vingi. Demokrasia ya vyama vingi inatoa uwezekano wa kutokea vyama tofauti vinavyongoza serikali za mitaa tofauti. Pia vyama tofauti vinaweza kuongoza serikali kuu na baadhi ya serikali za mitaa. Katika mazingira ya aina hii siyo rahisi mkuu wa mkoa au wilaya aliyechaguliwa na Rais wa chama kimoja kwa misingi ya kiitikadi kutoa ushirikiano kwa serikali za mitaa zinazoongozwa na vyama tofauti na kile cha Rais wa nchi. Historia imedhibitisha hivyo na mfano halisi ni wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu inayoongozwa na CHADEMA tangu kipindi cha 2001 hadi 2005. Kiini cha mgogoro katika Wilaya hii ni mitazamo ya kiitikadi kati ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ambao ni wana-CCM.

(7) Kwa mfumo wa sasa timu za Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ni sawa na timu ya Mawaziri. Itakapotokea CCM kushindwa uchaguzi na chama kingine kushika madaraka, wakuu wote wa mikoa na wilaya ambao wote ni wenye itikadi ya CCM watafutwa kazi na wapya wenye itikadi ya chama kilichoshinda kuteuliwa. Hatua hii ina athari kubwa mbili;

a) Ni mzigo mkubwa kwa taifa kuwalipa wakuu hawa mafao ya utumishi wao.
b) Taifa litapoteza uzoefu wa wakuu hawa walioujenga kupitia mafunzo mbali mbali ya kiutawala kwa gharama za umma. Kuingiza timu mpya isiyo na uzoefu wa uendeshaji wa shughuli za kiserikali na za kiutawala kwa ujumla ni kurudisha maendeleo ya jamii nyuma.

4.0 Asili ya Mfumo wa sasa wa Utawala

(1) Asili ama chimbuko la mfumo huu wa utawala Tanzania ni mfumo wa utawala wa kikoloni uliotawala nchi hii kabla ya uhuru wa Tanganyika (1961) na Zanzibar (1964). Hili linathibitika kwa kuzingatia historia kama ifuatavyo;

a) Dhana na muundo wa sasa wa “Tawala za Mikoa” hauna tofauti na “Tawala za Kijimbo” za wakoloni waingereza. Wakati wa ukoloni wa Waingereza tawala za mikoa tulizo nazo leo ziliitwa tawala za majimbo. Maneno “Jimbo” na “Mkoa” kimsingi yana maana moja. Yote yana maana ya “eneo” katika mgawanyo wa nchi kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za Serikali/utawala. Maneno haya hutumika kwa kubadilishana. Neno “Jimbo” lilibadilishwa baada ya uhuru na neno “Mkoa”. Hata hivyo, ni dhahiri kuwa kubadilishwa kwa matumizi ya neno “Jimbo” kuwa “Mkoa” ulikuwa ni uamuzi wa kisiasa tu uliolenga kuwafanya wananchi kuondoa fikra za “utawala” wa kikoloni. Kwa bahati mbaya kubadilishwa kwa neno “Jimbo” kuwa “Mkoa” hakukuondoa tofauti za kimsingi kati ya tawala zetu za mikoa na zile tawala za majimbo ya kikoloni.

b) Makamishna wa majimbo na wilaya waliteuliwa na mamlaka ya utawala wa Uingereza kupitia Ofisi ya makoloni. Makamishna wa majimbo waliwajibika kiutendaji kwa Gavana. Makamishna wa majimbo walikuwa na mamlaka na madaraka ya kisiasa, ya kiuendeshaji/kiutendaji, ya kipolisi na hata ya kimahakama. Walikuwa na mamlaka na madaraka juu yetu pasipo hiari yetu kama tu walivyo wakuu wa mikoa na wilaya wa leo.

c) Chimbuko la Tawala za Serikali za mitaa za sasa ni Serikali za mitaa za wakati wa ukoloni. Kuwepo kwa makamishna wa mikoa na wilaya wakati wa ukoloni kama wawakilishi wa utawala wa kikoloni chini ya Gavana, lilitokana na wakoloni kutowaamini wenyeji kujiongoza. Kwa hiyo wakati wa ukoloni Tawala za Serikali za Mitaa ziliwajibika kwa wakuu wa majimbo na wilaya. Hata sasa bado wakuu wa mikoa na wa wilaya wamepewa mamlaka na madaraka fulani juu ya Serikali za Mitaa.


SURA YA PILI

HOJA ZA KUWA NA SERA YA MFUMO MPYA WA UTAWALA
“SERA YA MAJIMBO” TANZANIA.

1. Tanzania bado imeendelea kuwa moja ya nchi maskini sana duniani licha ya kuwa taifa huru kwa miaka 47 sasa. Muda huu ungetosha kabisa kulifanya taifa hili pamoja na watu wake wapige hatua kubwa kimaendeleo. Kinyume chake kipindi cha miaka 47, kimethibitisha kuwa;

a) Sera na mikakati mingi ya maendeleo ya jamii na kiuchumi imejaribiwa na kukwama au kuleta mafanikio kidogo na ya taratibu mno. Hata sasa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA) hauonekani kubadili hali ya maisha ya watu kwa kasi inayostahili. Nchi imepewa mikopo na misaada mingi sana tangu uhuru na hata kufutiwa madeni lakini bado ni maskini. Kukwama na kusuasua kwa sera na mikakati mingi ya kimaendeleo tena ndani ya kipindi kirefu kabisa cha miaka 47 sasa, kunaibua haja ya msingi ya kuutazama upya mfumo wa sasa wa utawala.

b) Taifa limekuwa likiendelea taratibu mno na wakati huo huo kukiibuka matabaka kati ya walio nacho na wasionacho na kutoa dalili mbaya kwa mustakabali wa amani, umoja na mshikamano wa taifa hili. Hili pia linaibua haja ya kuutazama upya mfumo wa sasa wa utawala.

c) Ufisadi na rushwa vimekuwa ni moja ya matatizo makubwa na ya muda mrefu ndani ya serikali hali inayoibua haja ya kuutazama upya mfumo wa sasa wa utawala ili kuweza kujenga udhibiti wa kutosha dhidi ya matatizo haya.

2. Mfumo wa sasa wa utawala ulishaonesha udhaifu mkubwa tangu miaka ya mwanzoni baada ya uhuru lakini hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa hazijaweza kuondoa kiini cha tatizo. Mathalani, kutekelezwa kwa Mpango wa Madaraka Mikoani, na Mipango ya Maboresho ya Serikali za Mitaa, vyote havijaweza kupeleka nguvu na mamlaka kwa umma vya kutosha wala kuongeza ufanisi wa kutosha katika kuwaongoza watu kupata maendeleo.

3. Mfumo wa sasa wa utawala ulirithiwa na kuigwa na viongozi kutoka katika mfumo wa utawala wa kikoloni, ukaandikwa kwenye katiba na katiba hiyo kupitishwa na viongozi tu. Wananchi hawakupewa haki yao ya kuelimishwa na kutoa maoni. Hili pia linaibua haja ya wananchi kupewa haki ya kuandika katiba yao pamoja na mambo mengine itabainisha kwa ridhaa yao namna bora ya jinsi wanavyotaka kujiongoza.
4. Tanzania ni nchi kubwa sana. Ina ukubwa wa kilometa za mraba laki tisa na arobaini na tano elfu (945,000 km2). Ukubwa huu ni zaidi ya ukubwa wa nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Lesotho na Swaziland zikichanganywa pamoja. Tanzania ina watu milioni 38 ikiwa ni nchi ya 38 kati ya nchi 195 za dunia kwa wingi wa watu . Katika Afrika, Tanzania ni ya saba kwa wingi wa watu ikizidiwa na Nigeria (yenye watu milioni 132), Misri (milioni 79), Ethiopia (milioni 75), Kongo (milioni 63), Afrika Kusini (milioni 44) na Sudan (yenye watu milioni 41). Ukubwa huu wa nchi unajenga hoja za kuwa na mfumo mbadala wa utawala kama ifuatavyo;

b) Kuna haja ya kuwa na mfumo mbadala wa utawala utakaochochea ufanisi na maendeleo ya haraka kwa kupeleka madaraka karibu zaidi na wananchi badala ya kila kitu kuidhinishwa, kutekelezwa na kusimamiwa na utawala wa serikali kuu ulio katika eneo moja tu la nchi (Dar –Es-Salaam).

c) Kuna haja ya kuwa na mfumo mbadala wa utawala utakaotoa kwanza uhuru kwa watu kutumia raslimali zinazopatikana katika maeneo yao kujiletea maendeleo na wakati huo huo kufidia maeneo yatakayoonekana kupungukiwa raslimali, badala ya raslimali kutoka pembe zote za nchi kulimbikizwa Dar-Es-Salaam.

d) Kuna haja ya kuwa na mfumo mbadala wa utawala utakaokidhi zaidi haja na matakwa ya demokrasia ya vyama vingi ili kuchochea maendeleo ya haraka na kuepuka hatari ya taifa kutumbukia kwenye migogoro ya kisiasa katika siku zijazo.

1. Mfumo wa sasa wa utawala umesababisha kero kadhaa za muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar kwa kipindi cha miaka 44 sasa (tangu mwaka 1964). Mathalani upande wa Zanzibar umekuwa ukilalamika kuwa unapunjwa kimapato, na kumezwa sana kihadhi na kimamlaka na upande wa bara na kwa upande mwingine watu wa Tanzania bara nao wamekuwa wakilalamika kuwa Zanzibar imepewa nafasi kubwa kwenye muungano kuliko ukubwa wake. Kero hizi zinajenga hoja ya kutazama upya mfumo wetu wa utawala katika ngazi ya muungano ili kuepusha nchi kutumbukia kwenye migogoro mikubwa ya kisiasa katika siku zijazo.


SURA YA TATU

DIRA, DHUMUNI, NA MALENGO YA SERA YA MFUMO MPYA WA UTAWALA “SERA YA MAJIMBO”

1. Dira.
“Kuwa na taifa linaloendelea kwa haraka na kwa usawa, lenye haki, umoja na mshikamano wa kweli”

2. Dhumuni Kuu.
“Kujenga mfumo na muundo wa utawala unaotoa nguvu na mamlaka zaidi kwa umma katika kujiongoza na kutumia raslimali zao kwa usawa kujiletea maendeleo”.

3. Malengo Mahsusi.
(1) Kupunguza ukubwa wa serikali kuu kimuundo na kimajukumu pamoja na gharama zake za uendeshaji na kuachia raslimali nyingi kutumika moja kwa moja kwa maendeleo ya wananchi.

(2) Kurahisisha uongozi wa nchi kwa kuiunganisha mikoa kuwa majimbo ambayo viongozi wake watapatikana na kuongoza kwa ridhaa ya wananchi.

(3) Kupunguza urasimu wa kufikia maamuzi na kuongeza ufanisi na usimamizi wa karibu zaidi katika utoaji huduma kwa jamii chini ya tawala za majimbo.

(4) Kuondoa matabaka kwa kuweka mgawanyo mzuri na matumizi mazuri ya raslimali kati ya eneo moja la nchi na lingine.

(5) Kuimarisha mfumo na muundo wa Serikali za Mitaa kwa kuingiza ngazi ya Mkoa katika muundo huu.

(6) Kuondoa migongano ya kiutendaji kati ya Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa pande zote kufanya kazi katika eneo moja la kijiografia na katika jamii ile ile moja.

(7) Kuanzisha vyombo vya uwakilishi wa wananchi ndani ya utawala wa majimbo na kuboresha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(8) Kuimarisha utawala wa kidemokrasia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa.
(9) Kutanua na kuimarisha huduma za mahakama na vyombo vya usalama.
(10) Kuondoa kero za muungano kwa kuboresho mfumo na muundo wake.

SURA YA NNE

MATAMKO YA SERA YA MFUMO MPYA WA UTAWALA
“SERA YA MAJIMBO”


1. Mfumo Mpya wa Utawala.

“Ili kuwa na taifa linaloendelea kwa haraka na kwa usawa, lenye haki, umoja na mshikamano wa kweli”, tutapeleka nguvu na mamlaka zaidi kwa umma katika kujiongoza, kujiamulia mambo yao na kutumia raslimali zao kujiletea maendeleo. Tutafanya yafuatayo;

a) “Tutashirikisha wananchi katika kutafuta ufumbuzi wa kero zote za muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar kwa kupitia upya mfumo na muundo wake”.

b) “Tutabadili mfumo wa sasa wa utawala na kuanzisha mfumo mpya wa utawala utakaokuwa na muundo mpya wa serikali kuu na serikali za majimbo. Serikali za mitaa zitakuwa sehemu ya serikali za majimbo’’.

c) Mtiririko wa mfumo mpya wa utawala na muonekano wake utakuwa hivi;

Serikali Kuu:Mamlaka za Majimbo/Mikoa Mamlaka za sasa za Serikali za

Mitaa (Mamlaka za Wilaya na za Mijini) Mamlaka za Vijij/Mitaa

Jamii za watanzania wa Vijijini na Mijini.


2. Muundo Mpya wa Serikali Kuu.

2.0 “Tutapunguza ukubwa wa serikali kuu ya sasa, majukumu yake na gharama zake za uendeshaji na kuongeza ufanisi katika uongozi wa nchi kwa kufanya yafuatayo”;
a) Tutadumisha na kuboresha utendaji wa Ofisi ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuijengea uwezo mkubwa wa uratibu. Tutaongeza uhuru wa Mahakama na wigo wa huduma zake.
b) Tutadumisha na kuboresha utendaji wa Ofisi ya Makamu wa Raisi.
c) Tutaondoa ofisi na cheo cha Waziri Mkuu na kubakisha viongozi wawili tu wa juu wanaochaguliwa moja kwa moja na wananchi – Raisi na Makamu wa Raisi. Majukumu yote ya Waziri mkuu na ofisi yake yataongezwa kwenye orodha ya majukumu ya Makamu wa Raisi kama msaidizi mkuu wa Raisi.
d) Tutapunguza wizara nyingi za sasa na majukumu yake yatahamishiwa ngazi ya serikali za majimbo na kubakiza wizara nne tu katika serikali kuu, ambazo ni;Wizara ya Ulinzi na Usalama, Wizara ya Mambo ya Ndani (ikiwamo Uhamiaji),Wizara ya Fedha, na Wizara ya Mambo ya Nje.
e) Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, na Ofisi za Tarafa zitafutwa na majukumu yake yatahamishiwa katika serikali za majimbo na kutekelezwa na mamlaka za serikali za mitaa. Hii ni kwa sababu maeneo yote ya Kiwilaya na Tarafa kwa sasa yamo katika mipaka ya mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mujibu wa sheria Na. 7 ya 1982 na Na.8 ya 1982 ya mamlaka za wilaya.
2.1 Kimsingi majukumu makuu ya serikali kuu yatakuwa ni;
a) Uundaji wa sera za kitaifa kwa kushirikisha serikali za majimbo.
b) Uwekaji viwango vya huduma kitaifa.
c) Usimamizi wa Taasisi na miundo mbinu za kitaifa kama vyuo vikuu, Hospitali kuu za rufaa, Barabara kuu na mengineyo.
d) Ufuatiliaji wa uzingatiwaji wa sera, sheria, miongozo ya Kitaifa na viwango vya huduma kwa Umma wa vijijini na mijini.
3.Muundo Mpya wa Serikali za Majimbo

“Tutarahisisha uongozi wa nchi na kupeleka nguvu na mamlaka kwa umma kwa kuiunganisha mikoa kuwa majimbo ambayo yataongozwa na Wakuu wa Majimbo watakaopatikana kwa ridhaa ya wananchi kwa njia ya chaguzi za kidemokrasia. Kwa kufanya hivyo tutapunguza urasimu wa kufikia maamuzi na kuongeza ufanisi na usimamizi wa karibu zaidi katika utoaji huduma kwa jamii chini ya tawala za majimbo”.

“Kutaundwa majimbo manane kwa kuunganisha mikoa na wilaya mbalimbali kwa vigezo vya ukaribu na uhalisia wa kijiografia na kiuchumi, kama ifuatavyo;

a) Jimbo la Kaskazini litaundwa na Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.
b) Jimbo la Kusini litaundwa kwa kuunganisha mikoa ya Lindi na Mtwara.
c) Jimbo la Ziwa litaundwa kwa kuunganisha mikoa ya Kagera, Mwanza, Shinyanga na Mara.
d) Jimbo la Mashariki – mkoa wa Tanga na visiwa vyake.
e) Jimbo la Pwani -litaundwa kwa kuunganisha Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar- es-salaam.
f) Jimbo la Kati litaundwa na Mikoa ya Dodoma na Singida.
g) Jimbo la Magharibi litaundwa na mikoa ya Tabora, Rukwa na Kigoma.
h) Jimbo la Nyanda za Juu Kusini litaundwa kwa kuunganisha Mikoa ya Iringa na Mbeya.

“Majimbo yote yatapewa uhuru wa kutosha “semi autonomous “ wa kujiamulia na kutekeleza mambo yake isipokuwa kwa mambo yatakayosimamiwa na serikali kuu tu.

4. Mgawanyo wa Raslimali katika Serikali za Majimbo.

Majimbo yatapewa nguvu na mamlaka ya kukusanya mapato na kutumia sehemu kubwa ya mapato hayo kwa maendeleo ya wananchi na kugharamia shughuli za utawala wa jimbo husika. Tutazingatia pia utaratibu huu;

a) Kutawekwa kanuni maalum itakayobainisha sehemu ya mapato ambayo kila jimbo kutegemea na wingi wa raslimali na vyanzo vyake vya mapato, itachangia kwenda Hazina ya Serikali Kuu.

b) Hazina ya Serikali Kuu itagharamia uendeshaji wa serikali kuu na itakuwa ikifidia yale majimbo yatakayoonekana kuwa na uchache wa raslimali na vyanzo vya mapato ili kuhakikisha kuwa majimbo yote yanaendelea kwa usawa.

c) Kutawekwa kanuni ya mgawanyo wa vyanzo vya mapato na usimamizi wa ukusanyaji wake utakaoainisha wazi wazi, maeneo ambayo uongozi wa jimbo na Halmashauri za Wilaya/Miji zitahusika navyo.

d) Ugawaji wa mapato yanayokusanywa na kila mamlaka za serikali za mitaa utaangaliwa upya na kuweka kanuni nzuri itakayozingatia uwiano wa uwezo wa kifedha wa kutoa huduma katika kila mamlaka. Kwa kanuni hiyo, tutahakikisha kuwa kunakuwa na viwango sawa vya msingi vya utoaji huduma muhimu kitaifa.

5. Majukumu katika Serikali za Majimbo.

Tutatengeneza mgawanyo mpya wa majukumu, kwanza kati ya Uongozi wa Majimbo na Serikali Kuu, kwa maana ya wizara za kisekta, na pili kati ya Serikali za Mitaa za sasa na Uongozi wa Majimbo kama ifuatavyo;

a) Majukumu ya sasa ya serikali kuu kupitia wizara zake mbalimbali yatakuwa chini ya idara, wizara, au vyombo maalum vitakavyoundwa na uongozi wa majimbo kwa ajili ya kutekeleza majukumu hayo isipokuwa tu kwa majukumu ya wizara kuu nne zitakazobaki chini ya serikali kuu. Kwa mfano, baada ya uongozi wa majimbo kuanza, uendeshaji wa; Elimu ya sekondari na ukaguzi wa elimu ya msingi, shughuli za ugani katika kuendeleza kilimo na mifugo, shughuli za kusimamia usambazaji pembejeo, kuendeleza kilimo cha umwagiliaji kwa wakulima wadogo na wakati, hospitali za sasa za wilaya na mkoa, usimamizi na hifadhi ya mazingira pamoja na usimamizi wa hifadhi za misitu, na mengineyo, vyote vitakuwa chini ya serikali za majimbo.

b) Watendaji wengi wa taaluma za kisekta ambao sasa wapo Wizarani na wanashughulikia majukumu ya kiwizara mikoani, watahamishiwa katika mfumo wa uongozi wa majimbo ili kuimarisha utendaji na usimamizi wa kitaaluma wa utoaji huduma zitakazosimamiwa na uongozi wa majimbo.

c) Kimsingi Uongozi wa Majimbo utakuwa ukisimamia utekelezaji wa sera za kitaifa kwa kuzingatia mazingira ya kila jimbo, utasimamia utoaji huduma kwa jamii katika Jimbo kwa kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa za ngazi ya kati na utasimamia ushirikishaji jamii katika mipango ya maendeleo na utoaji huduma kwa kushirikiana na mamlaka za Serikali za Mitaa za ngazi ya kati.

d) Mamlaka na madaraka ya sasa ya Mkuu wa Mkoa, yaani yale ya kisiasa na ya uendeshaji serikali yatahamishiwa kisheria kwa mamlaka ya uongozi wa Jimbo na siyo tena kwa mtu au ofisi binafsi katika utumishi wa serikali kuu kama ilivyo sasa kwa Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya.Kwa kufanya hivi, Serikali za majimbo zitapunguza mikondo ya sasa ya utoaji amri kwa serikali za mitaa kutoka mikondo mitatu, yaani Waziri, Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya hadi mmoja tu wa Serikali Kuu kupitia serikali ya jimbo.

6. Mawasiliano ya kiutendaji.

a) Mawasiliano ya sasa kati ya Serikali Kuu, kupitia wizara husika na Serikali za Mitaa, yatapitia Mamlaka za Majimbo ambazo zitakuwa viungo kati Serikali Kuu na Mamlaka za chini na za kati za Serikali za Mitaa.

b) “Mamlaka ya Jimbo yatapewa kisheria madaraka ya kusimamia na kuratibu kwa ukaribu zaidi, shughuli za mamlaka za chini za Serikali za Mitaa ndani ya maeneo ambayo sasa ni mikoa”.


7. Muundo Mpya wa Serikali za Mitaa
Serikali za mitaa zitakuwa sehemu ya serikali za majimbo na zitawasiliana na serikali kuu kupitia uongozi wa jimbo. Muundo mpya wa serikali za mitaa utahusisha ngazi zifuatazo;

a) Halmashauri za wilaya/Miji.
b) Wakuu wa Idara katika Halmashauri. Idara hizi ni kama idara za mipango, kilimo, elimu, maji, maliasili, maendeleo ya jamii n.k).
c) Ofisi ya Kata itakayokuwa chini ya Katibu Kata na Kamati ya Maendeleo ya Kata.
d) Serikali ya Kijiji/Mtaa itakayoundwa pia na Ofisa mtendaji wa Kijiji na Halmashauri ya Kijiji.


8. Vyombo vya uwakilishi katika Mfumo Mpya wa Utawala.
Ili kuhakikisha nguvu na mamlaka ya umma vinakuwepo, mfumo mpya wa utawala utakuwa na vyombo vya uwakilishi wa wananchi ambavyo wajibu wake utakuwa ni kuwakilisha wananchi, kutunga sheria na kupitisha sera, na kusimamia utendaji na uadilifu wa serikali katika ngazi husika. Vyombo hivi ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo litatimiza wajibu wake katika ngazi ya taifa, Mabaraza ya Majimbo ambayo yatatimiza wajibu wake ndani ya tawala za majimbo, mabaraza ya halmashauri za wilaya/miji, na mabaraza ya halmashauri za vijiji.

9. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

a) “Kutakuwa na Bunge moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo wabunge wake watapatikana kutoka upande wa Zanzibar, na kutoka ndani ya majimbo manane ya Tanzania Bara kwa njia ya chaguzi za demokrasia ya vyama vingi’’.

b) “Mfumo wa sasa wa uchaguzi utafanyiwa marekebisho ili kuunda majimbo mapya ya uchaguzi ambayo kupitia hayo wabunge kutoka pande zote watakuwa wakipatikana na kuwakilisha wananchi kwa uwiano unaofaa” .

c) “Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litaendelea kuwa chini ya Ofisi ya Raisi lakini Katiba na sheria zinazolihusu zitapitiwa upya na kuboreshwa ili kulipa uhuru, nguvu na mamlaka zaidi ya kutimiza wajibu wake bila kuathiriwa na serikali kuu”.

d) “Wajibu wa Bunge hili utakuwa ni kupitisha maamuzi ya kitaifa, kusimamia utendaji na uadilifu wa serikali kuu, na kuwakilisha maslahi na matakwa ya wananchi katika ngazi ya kitaifa” .


10. Baraza la Jimbo.

a) “Tutaanzisha baraza moja la wawakilishi katika kila jimbo ambalo wajumbe wake watapatikana kutoka ndani ya maeneo ambayo sasa ni mikoa kwa njia ya chaguzi za demokrasia ya vyama vingi”.

b) “Mfumo wa sasa wa uchaguzi utafanyiwa marekebisho ili kuwezesha kupatikana kwa wajumbe wa baraza la jimbo kwa uwiano unaofaa”

c) “Wajibu wa Baraza la Jimbo utakuwa ni kupitisha sera na maamuzi ya jimbo husika, kusimamia utendaji na uadilifu wa serikali ya jimbo, na kuwakilisha maslahi na matakwa ya wananchi wa jimbo husika.



11. Mabaraza ya Halmashauri za Wilaya au Miji.

a) “Tutadumisha na kuboresha muundo wa sasa wa mabaraza ya halmashauri za wilaya na miji pamoja na chaguzi za demokrasia ya vyama vingi ili kupata madiwani wake kwa haki na usawa zaidi”.

b) “Wajibu wa mabaraza ya halmashauri za wilaya/miji utakuwa ni kupitisha maamuzi, kusimamia utendaji na uadilifu wa halmashauri, na kuwakilisha maslahi na matakwa ya wananchi katika eneo husika la halmashauri”.


12. Mabaraza ya Vijiji.

a) Tutadumisha na kuboresha muundo na majukumu ya sasa ya mabaraza ya vijiji.

SURA YA TANO

MCHAKATO WA KUANZISHA MFUMO MPYA WA UTAWALA
“UTAWALA WA MAJIMBO”
1. Kuanzisha Mjadala wa Kitaifa.

b) “Ili kufanikisha uanzishwaji wa mfumo mpya wa utawala “utawala wa majimbo” tutaitisha mjadala wa kitaifa utakaoelimisha na kushirikisha wananchi katika kutathmini mfumo wa sasa wa utawala na kujadili haja na namna ya kuanzisha mfumo huu mpya wa utawala unaopendekezwa”.

c) “Mjadala wa kitaifa juu ya mfumo wa utawala utaitishwa kupitia njia mbalimbali za kufikia wananchi kwa kadri zitakavyoonekana zinafaa, mathalani mikutano ya hadhara ya wananchi, mikutano maalum ya asasi zisizo za kiserikali na wadau wa kada mbalimbali, matumizi ya vyombo vya habari, na njia nyinginezo”.

d) “Lengo la mjadala wa kitaifa litakuwa ni kupata maoni ya wananchi juu ya mfumo mpya wa utawala na masuala mbalimbali ya kikatiba na kisheria. Matokeo ya mjadala huu yatatumika kuandika katiba rasimu ya Katiba Mpya”.

2. Kukusanya maoni ya wananchi.

“Tutaendesha mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi nchi nzima juu ya ya rasimu ya Katiba Mpya na Mfumo Mpya wa Utawala “Utawala wa Majimbo” unaopendekezwa” .

3. Kupeleka muswada wa Katiba Mpya Bungeni.

“Tutaandaa muswada juu ya katiba mpya na mfumo mpya wa utawala “utawala wa majimbo” na kuuwasilishwa Bungeni ili kujadiliwa zaidi na kuidhinishwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

4. Kuanzisha Mfumo Mpya wa Utawala.

“Tutaunda tume ya wataalamu itakayopendekeza na kusimamia uanzishwaji wa mfumo mpya wa utawala kwa awamu na kuidhinishwa na vyombo halali kikatiba. Na hatimaye Tanzania itakuwa chini ya mfumo mpya wa utawala, “utawala wa majimbo”
 
Last edited:
Wadau mnaombwa kutoa maoni yenu kama sehemu ya mchakato huu ili kuelekea Tanzania tunayoitaka ama tunayoifikiria siku zijazo.

Mchakato huu umeanza mapema ili kuweza kuwahusisha wanajamii wengi zaidi ,nami nashukuru kupata fursa ya kupewa nakala hii nami ntatoa mchango wangu wa mawazo na wengine hima tushiriki , na haswa wale ambao kila siku wanasema kuwa kazi ya upinzani sio kukosoa tuu bali ni kuonyesha wanataka kutufikisha wapi naamini sasa watapata fursa ya kueleza mawazo yao kwa kina ,.
 
Mkoa wa RUVUMA utakuwa jimbo gani?

Warioba wakati akihojiwa na gazeti la Raia mwema alisema kuwa "sasa sera nyingi hazitokani na wananchi ndiyo maana kuna lugha ya kusema tuwaelimishe wananchi" swali lako truevoter limenipeleka kwenye nadharia hii ya warioba iliyojenga kufahamu mantiki yake kwamba sera zisizotokana na wananchi hazitekelezeki wala hazitakubalika!

Hivi hayo majimbo yatagawanywa kwa utashi wa wananchi au kwa utashi wa wanasiasa,na vigezo vya kuyagawa vitakuwa ni nini. Na je hayo majimbo chimbuko lake ni nini? kwa mfano kwa nini Ruvuma isiwe kwenye jimbo la kusini badala ya Jimbo la nyanda za juu kusini?!!

Na kama Kikwete akiamua kuongeza mikoa mwaka huu kwa kukubaliana na maombi yaliyopelekwa kwake,mikoa hiyo itavunjwa kukianzishwa majimbo? Na labda tuambiwe mapema kabisa itachukua muda kiasi gani kuanzisha majimbo hayo, na gharama zake zimekadiriwa ziwe shilingi ngapi na zitapatikanaje.
 
Warioba wakati akihojiwa na gazeti la Raia mwema alisema kuwa "sasa sera nyingi hazitokani na wananchi ndiyo maana kuna lugha ya kusema tuwaelimishe wananchi" swali lako truevoter limenipeleka kwenye nadharia hii ya warioba iliyojenga kufahamu mantiki yake kwamba sera zisizotokana na wananchi hazitekelezeki wala hazitakubalika!

Hivi hayo majimbo yatagawanywa kwa utashi wa wananchi au kwa utashi wa wanasiasa,na vigezo vya kuyagawa vitakuwa ni nini. Na je hayo majimbo chimbuko lake ni nini? kwa mfano kwa nini Ruvuma isiwe kwenye jimbo la kusini badala ya Jimbo la nyanda za juu kusini?!!

Na kama Kikwete akiamua kuongeza mikoa mwaka huu kwa kukubaliana na maombi yaliyopelekwa kwake,mikoa hiyo itavunjwa kukianzishwa majimbo? Na labda tuambiwe mapema kabisa itachukua muda kiasi gani kuanzisha majimbo hayo, na gharama zake zimekadiriwa ziwe shilingi ngapi na zitapatikanaje.


Ndugu yangu maswali yako yote isipokuwa swali moja la gharama yamejibiwa kwenye rasimu hiyo hapo juuu tafadhali chukua muda kidogo na usome ndipo uanze kuulizia ufafanuzi ......

Kuhusu gharama unajua kuuendesha mkoa mmoja leo ni kiasi gani? rejea bajeti ya mwaka jana utaona mzigo wa kuendesha mikoa ambayo kimsingi hawana kazi kwani kazi zote zinafanywa wilwyani pamoja na kwenye halimashauri husika .

Kunaa maana gani kwa mkoa wa DSM kuwa na afisa nyuki, misitu n.k ile hali hivyo vitu havipo?

Kuna haja gani kwa Mkoa wa Singida kuwa na afisa uvuvi wa mkoa?
 
Nakubaliana na Sera za majimbo.
Kwa maoni yangu hapa sasa hata wananchi wa vijijini watakumbukwa na umuhimu wao kuonekana!
Hizi ndio grassroot movements towards developmental achievements hence prosperity!
Ni serikali ndogo ndogo ambazo mfumo na malengo yake itakuwa ni kufanya kazi karibu zaidi na wananchi kwenye shughuli za kimaendeleo na uwezekano mkubwa wa wananchi kuweza kunufaika na uendelezwaji wa rasilimali zao ikiwa ni pamoja na msisitizo kwenye kuitumia ardhi vyema kwenye shughuli za kilimo.
Huu ni mfumo ambao utapelekea kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa Taifa kwasababu utawaweka wananchi karibu zaidi na viongozi wake wakati wa utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo.
So far naona mgawanyo wa majimbo umeweka balance nzuri sana kwani kila jimbo linaonyesha kuwa na uwezo wa kuendeleza shughuli za kimaendeleo bila ya kuwa na wasiwasi wa kuwa nyuma kimaendelo.
Utaratibu huu wa sera za majimbo utawasaidia wananchi kuweza kunufaika na rasilimali zao huku pia serikali za majimbo hayo zikiweza kushirikiana na Serikali kuu kuweza kuisadia katika utekelezaji wa sera za kimaendeleo kwa kushirikiana na tawala zote zenye kuwawakilisha wananchi!
Haya nakubali mjadala uanze....
 
wamecherewa na sera zao za kukopi na kupaste

sera hizo haziisaidii tanzania ya leo, na wala hazihitajiki


kumanipata mkongwe?
 
wamecherewa na sera zao za kukopi na kupaste

sera hizo haziisaidii tanzania ya leo, na wala hazihitajiki


kumanipata mkongwe?

Mi naona badala ya kuja na kauli zako za kimwalimu mwalimu hapa ni heri usome mapendekezo yaliyotolewa hapo juu...Uyatafakari then ujibu accordingly kwa ni kivipi zimepitwa na wakati!
Kumanielewa?
 
Kwa taarifa yako sera hizi ndizo zenye kuifaa Tanzania kama tukizijadili hapa!
 
a) Jimbo la Kaskazini litaundwa na Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.
b) Jimbo la Kusini litaundwa kwa kuunganisha mikoa ya Lindi na Mtwara.
c) Jimbo la Ziwa litaundwa kwa kuunganisha mikoa ya Kagera, Mwanza, Shinyanga na Mara.
d) Jimbo la Mashariki – mkoa wa Tanga na visiwa vyake.
e) Jimbo la Pwani -litaundwa kwa kuunganisha Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar- es-salaam.
f) Jimbo la Kati litaundwa na Mikoa ya Dodoma na Singida.
g) Jimbo la Magharibi litaundwa na mikoa ya Tabora, Rukwa na Kigoma.
h) Jimbo la Nyanda za Juu Kusini litaundwa kwa kuunganisha Mikoa ya Iringa na Mbeya.

Majimbo yote yamekaa safi!
Ila naomba msaada hapo kwenye highlight ya herufi g.
Tabora Rukwa na Kigoma ni mikoa iliyoko nyuma kimaendeleo!
Tunataka kuona kuwa ni shughuli gani na resources gani zitakazoweza kuwasukuma!
Naelewa ni mikoa ambayo ni tajiri na hivyo nataka kujua ni kwanini ilibaki nyuma na sera hizi zitaweka mkazo gani ambao utaweka wazi kuwa sasa haya maeneo nayo yatapata maendelo kutokana na utajiri wao wa ardhi na vitega uchumi vingine!
 
Binafsi nina maswali mawili,
La kwanza linahusiana na usemi wa Mheshimiwa Mbowe aliposema haya:- Kwamba mfumo wetu wa utawala ndiyo chimbuko la umaskini na kukwama kwetu. Kwamba hata ukimleta ‘malaika' ukamweka Ikulu awe Rais wa Tanzania, kwa mfumo wetu wa utawala uliopo, lazima atakwama! Kwamba utajiri wetu wa asili ndio utatumika kama chanzo cha kubomoa mshikamano wa taifa. Kwamba, kwa matendo ya watawala wetu, ni wazi kwamba wamemsahau Mungu!Kwamba amani yetu ni tete!

Maneno haya yanazua hoja yangu kubwa kwamba Mheshimiwa Mbowe mwenyewe anakiri kwamba nchi yetu haiwezi kuiendelea hata akiletwa MALAIKA.. chini ya mfumo huu sasa hapa pananipa taabu sana!..Hivi kubwe hawa viongozi wetu wanapofanya UFISADI sababu kubwa ni mfumo wa utawala nchini ama ni wao wenyewe kuwa na tamaa ya Utajiri kwa kutumia madaraka yao. Hii inawaondolea lawama hawa viongozi wachafu na pengine kuwapa sababu ya kujitetea wanapofuja mali ya Umma. Je, hata yeye anaamini kumbe hawezi kuongoza nchi ktk mfumo huu then why amehusika ktk chaguzi iliyopita chini ya mfumo mbovu uliopo!
Binafsi sikubaliani na maelezo hayo kwani ni mfumo huu huu uliokuwepo wakati wa Nyerere na hapakuwa na Mafisadi ambao ndio chachu ya maendeleo yetu..Nyerere hakuweza kutuendeleza kiuchumi kwa sababu kazi yake kubwa ilikuwa kujenga UMOJA wetu na kuweka msingi wa uzalishaji nchini - MIUNDOMBINU...Miaka 25 ya kujenga miundombinu haiwezi kutohesabika kama ni maenedleo ati kwa sababu tu haikuweza kuzaa matunda. Mjenzi wa nyumba yeyote huona maendeleo ya ujenzi wa nyumba hiyo pindi anapoanza kuweka msingi wa jengo na sio lazima hadi siku atakapo anza kupangisha ndio tuseme kafanya jambo la maana..
Uchumi wetu tumeufuja sisi wenyewe kwa kuchagua viongozi wabaya wenye tamaa ya Utajiri wa haraka na sio mfumo wa Majimbo hata kidogo.

Swala la pili:-
Bado nashindwa kuelewa nafasi ya Zanzibar kama nchi yenye Uhuru wake na iliyoungana na Bara ktk mfumo huu wa majimbo...
Je, wao watakuwa kama jimbo tu la Muungano ambao awali ulihusu nchi mbili?
Ukubwa na udogo wa nchi hauwezi kuwa sababu ya mgawanyiko Bara hali Zanzibar hakuna sera inayo restore Zanzibar national sovereignty..
Je, Zanzibar kama nchi hawatapata mwanya wa kuomba kuvunja Muungano kwa sababu kuundwa kwa Majimbo ni moja ya Ukiukaji wa sheria za kutambua nchii huru hizi (sovereignty) zilizoundwa hapo awali na kuwekewa mkataba?.
 
Sera ya majimbo

May I get a summary of what this is all about?

Ni uundwaji wa serikali za majimbo ambapo badala ya serikali kuu kuchukua mapato yote kutoka kwa wananchi..Tunahakikisha kuwa pasenti flani ya kutosha inabaki kuwasadia kwenye shughuli zao za kimaendelo na za kijamii kama vile maji hospitali nk!
Badala ya mapato hayo kwenda kwa mafisadi..Sasa yatawasaidia wananchi kwa kuwaweka karibu zaidi na viongozi wao!
Hakuna tena cha kusubiri Mkuu aseme...Bali tutakuwa na watu wa kuwashika mashati pale mambo yanapokuwa hayaendi vile wananchi wanataka!
 
Jamani CHADEMA mbona tunarudishana nyuma mimi nadhani huu utawala wa majimbo tulishapitia enzi za mkoloini na ukafeli.
Au nyinyi wenzetu emeona tusichokiona? tuoneshane
 
Binafsi nina maswali mawili,
La kwanza linahusiana na usemi wa Mheshimiwa Mbowe aliposema haya:- Kwamba mfumo wetu wa utawala ndiyo chimbuko la umaskini na kukwama kwetu. Kwamba hata ukimleta ‘malaika' ukamweka Ikulu awe Rais wa Tanzania, kwa mfumo wetu wa utawala uliopo, lazima atakwama! Kwamba utajiri wetu wa asili ndio utatumika kama chanzo cha kubomoa mshikamano wa taifa. Kwamba, kwa matendo ya watawala wetu, ni wazi kwamba wamemsahau Mungu!Kwamba amani yetu ni tete!

Maneno haya yanazua hoja yangu kubwa kwamba Mheshimiwa Mbowe mwenyewe anakiri kwamba nchi yetu haiwezi kuiendelea hata akiletwa MALAIKA.. chini ya mfumo huu sasa hapa pananipa taabu sana!..Hivi kubwe hawa viongozi wetu wanapofanya UFISADI sababu kubwa ni mfumo wa utawala nchini ama ni wao wenyewe kuwa na tamaa ya Utajiri kwa kutumia madaraka yao. Hii inawaondolea lawama hawa viongozi wachafu na pengine kuwapa sababu ya kujitetea wanapofuja mali ya Umma. Je, hata yeye anaamini kumbe hawezi kuongoza nchi ktk mfumo huu then why amehusika ktk chaguzi iliyopita chini ya mfumo mbovu uliopo!
Binafsi sikubaliani na maelezo hayo kwani nina hakjina ni mfumo huu huu uliokuwepo wakati wa Nyerere na hapakuwa na Mafisadi ambao ndio chachu ya maendeleo yetu..Nyerere hakuweza kutuendeleza kwa sababu kazi yake kubwa ilikuwa kujenga UMOJA weutu na kuweka msingi wa uzalishaji nchini MIUNDOMBINU...Miaka 25 ya kujenga miundombinu haiwezi kutohesabika kama ni maenedleo ati kwa sababu tu haikuweza kuzaa matunda. Mjenzi wa nyumba yeyote huona maendeleo ya ujenzi wa nyumba hiyo sio lazima hadi siku atakapo anza kupangisha ndio tuseme kafanya jambo la maana..
Uchumi wetu tumeufuja sisi wenyewe kwa kuchagua viongozi wabaya wenye tamaa ya Utajiri wa haraka na sio mfumo wa Majimbo hata kidogo.

Swala la pili:-
Bado nashindwa kuelewa nafasi ya Zanzibar kama nchi yenye Uhuru wake na iliyoungana na Bara ktk mfumo huu wa majimbo...
Je, wao watakuwa kama jimbo tu la Muungano ambao awali ulihusu nchi mbili?
Ukubwa na udogo wa nchi hauwezi kuwa sababu ya mgawanyiko Bara hali Zanzibar hakuna sera inayo restore Zanzibar national sovereignty..
Je, Zanzibar kama nchi hawatapata mwanya wa kuomba kuvunja Muungano kwa sababu kuundwa kwa Majimbo ni moja ya Ukiukaji wa sheria za kutambua nchii huru hizi (sovereignty) zilizoundwa hapo awali na kuwekewa mkataba?.

Mkandara kitu ambacho kimenifanya nisapoti mfumo huu ni kwasababu malengo yake yamewekewa msisitizo kwenye maendeleo zaidi ya mamlaka ya utawala!
Badala ya kusubiri udikteta wa Rais wa jamhuri wa kuamua kila nafsi ifanye nini..Tunakuwa tumewapa wananchi ukaribu na serikali kwa kuzitumia tawala wakilishi kama za majimbo!
Hapa kwenye sera hii uhuru wa kweli wa mwananchi kwenye kujiletea maendeleo umezingatiwa na unyonyaji utapigwa kumbo kwa sababu wote tutashiriki kwenye shughuli za kimaendeleo kwa karibu zaidi!
Na si tu kushiriki..Bali pia kuona matunda yake!
 
Back
Top Bottom