Hatimaye Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Arumeru amemtangaza Bw. Joshua Nassari kuwa Mbunge Mteule wa jimbo hilo kufuatia ushindi wake mnono dhidi ya mgombea wa CCM Bw. Siyoi Summari. Joshua Nassari amepata kura 32,972 sawa na asilimia 54.91 ya kura zilizopiwa. Hii inaendana na makisio yangu ambayo yalitabiri ushindi wake wa karibu asilimia 50!
[video=youtube_share;zjUI5AbO-Jk]http://youtu.be/zjUI5AbO-Jk[/video]
Mtandao wa JamiiForums waweza kutangaza kwa uhakika kabisa kutokana na vyanzo makao makuu ya Jimbo huko Arumeru Mashariki kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi mdogo ambapo mgombea wake Bw. Joshua Nassari ameibuka kidedea baada ya kumbwaga vibaya mgombea wa CCM Bw. Siyoi Sumari. Matokeo yanaonesha hadi hivi sasa baada ya zaidi ya asilimia 80 ya vituo vyote kuripoti CDM imeshinda kata 14 dhidi ya 3 za CCM.
Chama cha Mapinduzi tayari kimekuballi kushindwa na kutoa pongezi kwa mgombea wa CDM.
CDM imeshinda kwa zaidi ya kura 6000
MATOKEO OFFICIAL:
Kura halali - 60038
CHADEMA 32,972 - Joshua Nassari (Mbunge Mteule)
CCM 26,757 - Siyoi Sumari
Vyama vingine:
AFP 139
UDP 18
TLP 18
DP 77
UPDP 22
NRA 35
My Take:
Bila ya shaka Uongozi wa taifa wa CDM hauna sababu ya kujiuzulu kwa wakati huu! Upepo umevuma upande wao na mtumbwi unaelekea kwenye ushindi 2015!
Kutoka kwa Zitto (FB)
Watanzania kilichofanyika ni uchaguzi tu; watu wa Arumeru bado wana matatizoyale yale waliyokuwa nayo jana. Baada ya furaha yote kwisha kinachokuja ni kumsaidia kijana kuongoza. Natumaini atakuwa na unyenyekevu na usikivu wa kuwa kiongozi mzuri. Binafsi namtakia kila la kheri na nitamsaidia kwa kadiri niwezavyo kumjenga kuwa kiongozi mzuri wa kitaifa.
Udiwani songea ameshinda CDM, kiwira kashinda CDM, kirumba kashinda CDM, Tanga kashinda CUF.
Kwa kilatini kibovu
Vox Populi Vox Dei, Regnat Populus
Sauti ya Watu ni Sauti ya Mungu, Utawala wa Watu au (Acha Watu Watawale).
mheshimiwa mwanakijiji, mimi niko karibu sana na eneo la tukio, pamoja na kufungua idadi kadhaa ya redio nimeyapata matokeo saa 12.50; wewe uliye nje ya nchi habari hizi unazipataje?
jana wasira aliondoka haraka sana ...na hawakuagana na wenzake....mwigulu maka sasa haoni ile skafu yake ya shingoni
Jamani Rejao yuko wapi?
Dsm ni tatizo sana katika mabadiliko ya nchi hii. Kila mtu anajiona kuishi Dar ni ujanja. Wengi hawana hata uelewa wa nini kinaendelea nchi hii. Na utakuta wale wachache wenye kuelewa na kukerwa na yanayoendelea hapa nchini ni wenye unafuu wa maisha, ajabu ni wenye dhiki kuona hiyo ni kawaidaPeopleeeeeeeee's Poweeeeeeeeeeeeeeer. Yaani magamba yaendelee kushinda kule waliko watu wanaoona matatizo ya umasikini ni janga linaloletwa na Mungu. Ngoja walale wakiamka majimbo mengine yako meter 1000 kimaendeleo. Haya matatizo bado yako mikoa ya pwani na chakushangaza jiji la Dar es salaam nalo lina vilaza kadhaa ambao sijui tuwapige viboko waamke. Kwanza umeme, shida ya maji ilikuwa ni slaa kubwa ya magamba kuondoka jijini
BAADA YA MATOKEA HAYO tUNAOMBA MKAPA, LUSINDE NA WASIRA WATOE HOTUBA FUPI YA KUWASHUKURU WANANCHI:A S shade:....HEHEHEHEHEH