CHADEMA yaibwaga CCM Arumeru Mashariki; CCM Yakubali kushindwa (Zaidi ya kura 6,000)

Hatimaye Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Arumeru amemtangaza Bw. Joshua Nassari kuwa Mbunge Mteule wa jimbo hilo kufuatia ushindi wake mnono dhidi ya mgombea wa CCM Bw. Siyoi Summari. Joshua Nassari amepata kura 32,972 sawa na asilimia 54.91 ya kura zilizopiwa. Hii inaendana na makisio yangu ambayo yalitabiri ushindi wake wa karibu asilimia 50!

[video=youtube_share;zjUI5AbO-Jk]http://youtu.be/zjUI5AbO-Jk[/video]

Mtandao wa JamiiForums waweza kutangaza kwa uhakika kabisa kutokana na vyanzo makao makuu ya Jimbo huko Arumeru Mashariki kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi mdogo ambapo mgombea wake Bw. Joshua Nassari ameibuka kidedea baada ya kumbwaga vibaya mgombea wa CCM Bw. Siyoi Sumari. Matokeo yanaonesha hadi hivi sasa baada ya zaidi ya asilimia 80 ya vituo vyote kuripoti CDM imeshinda kata 14 dhidi ya 3 za CCM.

Chama cha Mapinduzi tayari kimekuballi kushindwa na kutoa pongezi kwa mgombea wa CDM.

CDM imeshinda kwa zaidi ya kura 6000


MATOKEO OFFICIAL:

Kura halali - 60038

CHADEMA 32,972 - Joshua Nassari (Mbunge Mteule)
CCM 26,757 - Siyoi Sumari


Vyama vingine:

AFP 139
UDP 18
TLP 18
DP 77
UPDP 22
NRA 35




My Take:
Bila ya shaka Uongozi wa taifa wa CDM hauna sababu ya kujiuzulu kwa wakati huu! Upepo umevuma upande wao na mtumbwi unaelekea kwenye ushindi 2015!

Kutoka kwa Zitto (FB)

zitto-status.jpg


HATIMAYE SIOI ASHINDWA KUOA.
Niwapongeze sana wanaChadema popote pale mlipo nchini kwa ushindi mnono katika chaguzi zetu
zote tulizozifanya na kuibuka na ushindi mnono.UKO wapi Rais mstaafu B W.MKAPA na mbwembwe zako za
kwenda kutoa lugha zisizofaa hasa ukizingatia wewe kama baba ulitakiwa uwashauri na si kama ulivofanya
sasa wewe unaaibika siku nyingine wakikutuma CCM kataa aibu zako hizo.
Yuko wapi Waziri mkuu mstaafu MHESHIMIWA Edward Ngoyayi Lowasa tunakujaTarehe kumikama mlivyokuwa mmepanga siku ya kumwapisha SIOI SUMARI.Wapi Mheshimiwa MB OLENYAKULE OLESENDEKA,Wapi Mwigulu MSHEMBA,hakika Chadema wanastaili pongezi sana kwani nguvu mliyoitumia katika uchaguzi wa Arumeru Mash ya kugombea jimbo ni sawa na kutumia bunduki kuua mbu.Ukiwaangalia wanaChadema walikuwa kama vile watoto Yatima kwani kwa kawaida mtu kama Rais alipaswa aballance mambo pande zote mbili na si vinginevyo. Joshua Nassari kamata jembe anza kazi vitendo vikaongee zaidi,na Wana Arumeru
watatujuza nakutakia kila la Heri.
 
Watanzania kilichofanyika ni uchaguzi tu; watu wa Arumeru bado wana matatizoyale yale waliyokuwa nayo jana. Baada ya furaha yote kwisha kinachokuja ni kumsaidia kijana kuongoza. Natumaini atakuwa na unyenyekevu na usikivu wa kuwa kiongozi mzuri. Binafsi namtakia kila la kheri na nitamsaidia kwa kadiri niwezavyo kumjenga kuwa kiongozi mzuri wa kitaifa.

Naona kijana ameanza kwa kasi kwani baada ya kutangazwa kuwa mbunge mteule tu amesema anaenda kufuatilia uchimbaji wa visima sijui kijiji gani. Anasema Ndesa alimuahidi kiasi fulani cha visima hivyo kazi inaanza mara moja.
 
Nina maswali mawili tu kwa yule **** swine mkubwa:
1) Nani alikua ana mimba CCM au CDM????
2) Nani amezalishwa tena kwa kisu maana uchungu uligoma,CCM au CDM???
 
mheshimiwa mwanakijiji, mimi niko karibu sana na eneo la tukio, pamoja na kufungua idadi kadhaa ya redio nimeyapata matokeo saa 12.50; wewe uliye nje ya nchi habari hizi unazipataje?

wewe kinachokuuma nini, uko ktk sistemu nini. Usimjibu huyu mtu mwanakijiji
 
jana wasira aliondoka haraka sana ...na hawakuagana na wenzake....mwigulu maka sasa haoni ile skafu yake ya shingoni

Mkuu hukumbuki maneno yaliyoandikwa na manabii kwenye Biblia; imeandikwa hivi, "Nitampiga mchungaji na kondoo watatawanyika". Katika hali hiyo wasubiri nini sasa!

Tatizo moja ni kwamba wanasiasa wetu wakishindwa hawawi wajasiri wa kujitokeza hadharani na kukubali matokeo - Concede defeat. Sioi amepata kura zaidi 26,000 japokuwa ameshindwa lakini angefanya uungwana kwa kukubali kushindwa hadharani na kuwashukuru wapiga kura badala ya kutokomea gizani bila kuaga - AWOL. Anaamua kuwaacha hata washabiki wake bila kujua ameenda wapi!

Hapa Arusha leo kazi hazifanyiki watu ni kusherehekea tu maofisini.
 
Peopleeeeeeeee's Poweeeeeeeeeeeeeeer. Yaani magamba yaendelee kushinda kule waliko watu wanaoona matatizo ya umasikini ni janga linaloletwa na Mungu. Ngoja walale wakiamka majimbo mengine yako meter 1000 kimaendeleo. Haya matatizo bado yako mikoa ya pwani na chakushangaza jiji la Dar es salaam nalo lina vilaza kadhaa ambao sijui tuwapige viboko waamke. Kwanza umeme, shida ya maji ilikuwa ni slaa kubwa ya magamba kuondoka jijini
Dsm ni tatizo sana katika mabadiliko ya nchi hii. Kila mtu anajiona kuishi Dar ni ujanja. Wengi hawana hata uelewa wa nini kinaendelea nchi hii. Na utakuta wale wachache wenye kuelewa na kukerwa na yanayoendelea hapa nchini ni wenye unafuu wa maisha, ajabu ni wenye dhiki kuona hiyo ni kawaida
 
Jamani nawapa pole sana CCM, Rejao na Sioi. Hungereni sana mwanakijiji, Dr Slaa, Mbowe na Mh Mbunge. Tanzania sasa mambo yanawezekana. Pole sana mzee Mkapa, haya mambo ni ya Taifa la leo.
 
Sasa nimeamini kumbe Mkapa/Lowassa ndio walikwenda kujazia kura za ushindi kwa Chadema ile siku ya mwisho pale Kikatiti!:smile-big:
 
Wao wana pesa sisi tuna Mungu.
Tulianza na Mungu tumemaliza na Mungu na Mungu ataendelea kutusimamia kila siku.
Hongera Chadema, hongera wananchi wa Arumeru Mashariki na hongera kwa watanzania wote
wenye mapenzi mema na nchi hii.
sasa ni M4C.
Mungu ibariki Chadema, Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom