UCHAGUZI MDOGO: Shaka Hamdu Shaka asema CCM itakubali matokeo yoyote Jimbo la Amani kwani hata hivyo kabla ya Uchaguzi imeshinda kata 7 Kati ya 12

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,546
2,177
IMG-20221216-WA0186.jpg

IMG-20221216-WA0187.jpg
CCM YASEMA IPO TAYARI KWA USHINDI AMANI, KATA SABA

Shaka aeleza mwenendo wa kampeni umetoa mwangaza kushinda kwa kishindo

Na MWANDISHI WETU

WAKATI wananchi katika Jimbo la Amani, Zanzibar na kata saba zilizopo kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara, Kesho wakipiga kura kuchagua mbunge na madiwani, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kimeridhishwa na mwenendo wa kampeni na kinatarajia kupata ushindi.

Taarifa iliyotolewa na CCM na kutiwa saini na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ilisema tathimini kuhusu kampeni iliyofanywa na Chama imeonyesha zilikwenda vizuri.

"CCM imeridhishwa kwa kiasi kikubwa na mwenendo wa kampeni zake za uchaguzi mdogo zilizozinduliwa tarehe 1, Desemba, 2022 na zinazo kamilika leo 16, Desemba, 2022. (jana).

"Kampeni hizi mpaka sasa zimefanywa kwa weledi na umahiri mkubwa. Mwenendo wake umekuwa mzuri sana na CCM ina uhakika wa kushinda kwa kishindo cha zaidi ya asilimia 90," alisema Shaka katika taarifa hiyo kwa umma.

Alisema CCM ikiongozwa na wagombea wake mahiri imefanya kampeni nzuri kupitia mikutano ya hadhara, kukutana na makundi ya wazee, vijana na wanawake na kunadi sera zake kama zilivyoainishwa katika Ilani yake ya Uchaguzi ya 2020 - 2025.

UBUNGE AMANI

Kwa mujibu wa Shaka, kuhusu kiti cha ubunge Jimbo la Amani Zanzibar, CCM ilimteua Abdul Yussuf Maalim kupeperusha bendera yake na kwamba Chama kinaamini atapata ushindi mkubwa kwa kuwa anakubalika.

Aidha, Shaka alisema pia Chama kinashiriki uchaguzi katika kata saba kati ya 12 kwa upande wa Tanzania Bara ambazo ni Majohe (Dar es Salaam), Mwamalili (Shinyanga) Njombe (Njombe), Vibaoni, Mnyanjani (Tanga), Mndubwe (Mtwara) na Dunda (Pwani).

Mbali na hizo, alisema kaata tano kati ya 12 tayari CCM imeshinda kwa kupita bila kupingwa ambazo ni Dabalo (Dodoma), Ibanda (Mbeya), Misugusugu (Pwani), Kalumbeleza (Rukwa) na lukozi (Tanga).

TUTAKUBALI MATOKEO

Shaka alieleza kuwa Hata hivyo Chama kipo tayari kupokea matokeo yoyote katika uchaguzi huo kwa kuwa CCM ndicho Chama kilichobeba na kusimamia demokrasia ya kweli ya vyama vingi nchini.

Uchaguzi mdogo katika jimbo la Amani unafanyika leo kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Marehemu Mussa Hassan.

===
 
Awamu ya sita wanaosusia Uchaguzi ni watu wasio na uwezo tu ama,

1. Wa kifedha

2. Kisera
 
Sisi CHADEMA sio Kama tunasusia ila hatuna hela na tunaogopa aibu kwakuwa hatujui nguvu ya Chama chetu kwa sasa alisikika kamanda mmoja toka Ubungo, Je huu ndio Ukweli wenyewe?
Hao watu uliowataja wanahali Ngumu Sana
 
Sisi CHADEMA sio Kama tunasusia ila hatuna hela na tunaogopa aibu kwakuwa hatujui nguvu ya Chama chetu kwa sasa alisikika kamanda mmoja toka Ubungo, Je huu ndio Ukweli wenyewe?
Aaah wapi? Kwa matatizo yaliyopo nchini hata bila kampeni mtu mwenye akili timamu hawezi pigia kura CCM? Yaani mtu apigie kura mgao na ufisadi?
 
Kwa nini CCM,inatoa tamko la kukiri kukubali kushindwa au kushinda uchunguzi mdogo wa udiwani kata ya Amani,na mgombea wake anatajwa.Ni muziki mnene huko Amani au mambo ya muungano.
Tunawatakia uchaguzi mwema,wananchi wa kata hizo, wafanye uchaguzi kwa amani na bila ghiriba.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kwa nini CCM,inatoa tamko la kukiri kukubali kushindwa au kushinda uchunguzi mdogo wa udiwani kata ya Amani,na mgombea wake anatajwa.Ni muziki mnene huko Amani au mambo ya muungano.
Tunawatakia uchaguzi mwema,wananchi wa kata hizo, wafanye uchaguzi kwa amani na bila ghiriba.
Ni vile CCM hii ya Sasa ni Ukweli na Uhakika
 
Back
Top Bottom