Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,204
- 128,027
Shibuda hana madhara yoyote kwa sasa yuko sawa na Dr. Augustino Mrema lolote analosema tutakuwa busy na story na sms kama jana tulivyokuwa busy wakati wale wabunge wa CCM waliosokomezewa mic wachangie kwa lazima coz hawajawai kuongea tangu bunge lianze sasa wanapewa air time ya kujichoresha mbele ya wapiga kura wao juu ya swala hili la mswada wa katiba.Juzi wabunge watukufu wa CHADEMA walitoka ndani ya ukumbi wa bunge kwa sababu serikali na CCM wanataka kuburuza mchakato wa kupata katiba mpya. Mara ya kwanza wakati wa kukataa posho Mh. Shibuda aliwaponda na hakutoka nje kuungana na wenzake. Sasa ningependa kujua kama juzi naye alitoka nje, alikula pini au alikacha mapema.