CHADEMA wanaomba michango ya wahanga wa Hanang halafu wameweka picha ya Mbowe kama ndiye mhanga mwenyewe

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,334
9,755
Ndugu zangu Watanzania,
Chadema.png

Nilishawaambieni na naendelea kuwaambieni kuwa CHADEMA ni matapeli na wababaishaji sana.leo hii wameanzisha kampeni wanasema ni kwa ajili ya kuwachangia wahanga wamafuriko ya hanang.lakini cha ajabu na kusikitishaa na kukatisha watu tamaa kuwachangia wameweka picha ya Mbowe kwenye bango lao.

Watu wanajiuliza kwa hiyo Mbowe ndiye mhanga? Ndiye amefiwa na ndugu zake? Ndiye anayechangiwa? Ndiye ambaye anakwenda kupokea pesa hizo na kuzipangia matumizi? Ndiye anayeneemeka na matatizo yaliyowapata wana Hanang? Kama yeye siyo mhanga sasa kwanini wameweka picha yake?

Nieleweke ya kuwa watu wanahoji haya baada ya kuwa na kumbukumbu mbaya ya kutafunwa kwa pesa za join the chain ,ambazo mpaka muda huu haieleweki zilikusanywa shilingi ngapi? Zilifanya kazi gani na zilibaki shilingi ngapi na zipo wapi?

Kwa hiyo wananchi na wafuasi wa CHADEMA wanaona ni muendelezo wa upigaji kama awali ambapo sasa chama kinataka kitumie fursa hiyo kupiga pesa kisawasawa na ndio maana wameweka na picha ya Mbowe mwenyewe mzee wa join the chain.

Kingine cha kushangaza ni kuwa wameweka namba ya simu kuwa ndio itakayo tumika kukusanya michango.sasa watu wana hoji na tunajiuliza je hiyo namba inapokea kiasi gani cha pesa ? Maana laini zingine zina kikomo cha kupokea miamala kwa siku. Pili kwanini CHADEMA kama wapo siriasi wasingefungua akaunti ya Benki?

Kwanini CHADEMA wanafanya vitu kihuni huni kiasi hiki utafikiri chama kilichoanzishwa jana? Hivi nani ameshikilia akili za CHADEMA kwa sasa? Nani mshauri wa CHADEMA kwa sasa? Mbona chama kinakwenda kama kipofu?

Hiyo laini ya simu inayopokea michango ni nani atakuwa anatembea nayo na kukaa nayo? Vipi huyo mtu akitoa au kuhamisha pesa na kufuta sms? Nani atajuwa? Nani atafuatilia ? Nani atahoji ?Nani atakuwa na imani na uhakika wa kiasi kitakachopatikana wakati mtu anayekaa na hiyo laini anaweza kutoa au kuhamisha pesa hata akiwa kwake tu?

Kazi iendelee mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nilishawaambieni na naendelea kuwaambieni kuwa CHADEMA ni matapeli na wababaishaji sana.leo hii wameanzisha

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Sijui inakuuma nini ,wewe sio mwanachama wa CHADEMA ,hutochanga ,CHADEMA wanaomba Michango kutoka kwenye wanachama wao na sio wa CCM Mshama uwe unaelewaa hi gamu inaendaje ,kama huwezi kuelewa hii ndogo uteuzi utauweza kweli na Najua hakuna MTU ATAKAYEKUPA UTEUZI
 
Wazee wa zamani jau sana, eti wanamsemo wao unasema "Jambo lisilokuhusu ya nini kulivalia Kibwebwe"

Wazee Jau sana!

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Back
Top Bottom