Chadema wako aware

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
naomba kila mpenda mabadiliko aelewe chadema wako macho tena yamefunguka yote kabisa na wanajua kabisa ccm wana intelligent ya kizamani ya kuvuruga vyama vingine
yule mzee shibuda ilikuwa na mojawapo ya intelligent ya kizamani ya ccm,japo walivyoanza hakuna aliyejua:peep:
 
Sidhani kama wapo makini. Mbona wamewachukua some senior government Intelligence officers kuwa members wa kamati kuu?
 
mbw anachofanya n kuhakikisha kuwa anawateua watakao mlinda,yaani unakosoa ccm na kisha unaishi kama ccm tena zaidi yake,...na ww roseregia tukisema umetumwa utabisha?
 
kama unategemea mabadiliko kupitia chadema umekosea, wanatumia udhaifu wako wa kufikiria na kukudanganya kuwa ni wapambanaji.sina haja ya kutibua ladha yako kwao lamsingi endelea kuwasoma na mwisho utaelewa kama hakuna mpambanaji
 
wapo aware na nini? ni vizuri kujadili hali halisi.
hii taarifa ipo kwenye global publishers soma na comments zake


MOTO WAWAKA CHADEMA, NI VITA YA KAMBI ZA MBOWE, ZITTO

VITA vya makundi vimezidi kuviandama vyama vikubwa vya siasa nchini, ambapo sasa hali si shwari ndani Chadema, ambako kunadaiwa kuwepo mkakati wa kumng'oa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.

Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, anadaiwa kuponzwa na msimamo wake kupinga ununuzi wa magari mitumba yenye thamani ya Sh480 milioni ya Chadema.

Hali hiyo ilijitokeza katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichoketi juzi Jumamosi chini ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kikao ambacho pia kilimg'oa John Shibuda katika nafasi ya kukaimu uenyekiti mkoa wa Shinyanga. Shibuda ambaye ni mbunge wa Maswa Magharibi ameondolewa baada ya kukalia nafasi hiyo takriban kwa siku nne tu tangu ateuliwe, kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Shinyanga Philip Shelembi ambaye alizikwa April 27, 2011.

Chanzo cha mvutano
Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha Kamati Kuu na kuthibitishwa na baadhi ya wajumbe wa kikao hicho zinasema kuwa mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, ndiye alianzisha mvutano wa kutaka Zitto ang'olewe kutokana na kupinga wazo la kununua magari chakavu kutoka India.

Chanzo chetu cha uhakika kilidokeza kuwa mashambulizi dhidi ya Zitto yalianza pale alipounga mkono hoja ya Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo ambao walinukuliwa wakisema kwamba, isingekuwa sahihi kwa chama hicho kinachopinga ufisadi kufanya ufisadi kwa kununua magari chakavu wakati wamekuwa wakiibana serikali isifanye hivyo.

Baada ya Zitto kuunga mkono hoja hiyo, vyanzo hivyo nifafanua kuwa ndipo vurugu zilipoanza kwani Lema alianza kumrushia vijembe akisema kwamba Zitto ni tatizo na kwamba amekuwa akimtetea Shibuda.

Habari zinasema baadhi ya wajumbe walisema hoja ya Lema haikuwa na nguvu ya kumshutumu Zitto kwani Shibuda ni mbunge halali wa Chadema.

Duru zaidi za kisiasa kutoka ndani ya kikao hicho zinasema wakati mvutano huo ukiendelea, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alikuwa kimya huku kwa mara ya kwanza Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akiwa mmoja wa wajumbe waliomtetea Zitto.

"Wakati Lema akisema hivyo, Dk Slaa wakati wote alikuwa kimya na hakusema chochote. Mnyika alisimama na kumtetea Zitto kwa mara ya kwanza, na katika utetezi pia alikuwepo Grace Kiwelu," kiliweka bayana chanzo hicho.

Katika majibizano hayo inadaiwa ulifika wakati Zitto alisimama na kumwambia mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kwamba mpango mkakati wake huo wa kujenga mtandao utakuja kumgharimu katika siku za usoni."Zitto alimwambia Mbowe mpango wake huo wa kujenga mtandao ungekuja kumletea matatizo hapo baadaye, "kilisema chanzo hicho kikimnukuu Zitto ndani ya kikao.

Kung'olewa kwa Shibuda
Mbali ya Zitto, Kamati Kuu hiyo pia iliazimia kutengua nafasi ya Shibuda, kukaimu nafasi ya uenyekiti ya Chadema mkoa wa Shinyanga.Vyanzo hivyo viliongeza kwamba, kabla ya mpango huo genge linalompinga Zitto lilimshutumu kwamba alikwenda Shinyanga na kushirikiana na baadhi ya wanachama kumweka Shibuda ili kutimiza ajenda zao.

Mvutano huo unaondelea ndani ya Chadema unazidi kukiweka chama hicho kinachokua na kuwa na malengo ya kukamata dola katika wakati mgumu kutokana na makundi mawili, huku moja likimuunga mkono Zitto na jingine Mbowe.

Zitto na Shibuda ni viongozi ambao wamekuwa wakikumbwa na misukosuko ndani ya Chadema na mara kadhaa Zitto amenusurika kung'olewa katika nafasi zake za uongozi kutokana na kile kinachodaiwa ni hulka yake ya kutofautina na wenzake hata katika mambo yenye maslahi kwa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Kauli za Zitto, Shibuda
Zitto alipoulizwa na Mwananchi jana jioni kuhusu tafrani hiyo alisema "….tafadhali sana, naomba nisiongee chochote kwa sasa, hiki ni kipindi cha kukijenga chama, si kipindi cha kuonyesha umma kwamba Chadema kuna mgogoro".

Pale mwandishi alipomhoji zaidi alisema "…tafadhali naomba nikupigie baadaye" kisha kukata simuKwa upande wake Shibuda alikiri kusikia taarifa hizo na kuongeza kwamba, anasubiri apate taarifa rasmi kwani yeye alipewa heshima hiyo na wanachama wa Shinyanga kupitia vyombo vyao vya maamuzi.


COMMENTS

CHADEMA VIPI.... MBONA MNATAKA KUWA ZIMA MOTO.... "MBOWE KULIKONI SAUTI YA ZEGE HIYO NDO MIHIMILI UKICHEZA CHAMA KITAFULIA "...MAGARI YA MTUMBA YATAKIFIKISHA WAPI CHAMA ZAIDI YA KASHFA ....
Comment by faith colly 2 hours ago
mbowe huna sababu ya kumchukia zitto umtumie vizuri utaona matunda yake!! chuki ya nn?
Comment by layla 3 hours ago
Mbowe chuki alokua nayo nikuona kua Zitto kila nafasi anayo gombania Mbowe na zitto anaigombania hiyo ndio tatizo na pia Udini mwingi sana CHADEMA, Mbowe watakutia ilaa wenzio ebu tuliza ushakua mtu mzima na mwenye kuheshimika,wape vijana wako nafasi wafanye kazi,Na kwa sasa Mbowe unampa sana nafasi Mnyika sababu unataka kumuondoa Zitto lakini jua unafanya makosa na humtendei haki Zitto, Lipi alolifanya la ajabu mpaka mumnadi kwa sanaaaaaa mangapi amejitolea kwa CHADEMA? Vyama vyengine wanamtaka usisahau Mbowe kua huyo kijana anajua mpaka mvunguni kwako, ushakua mtu unaeheshimika kwahiyo tumia busara unapoongea na vijana wako.
Comment by Timothy Mbulakwao 3 hours ago
NILIKUWA NIMEANZA KUKIKUBALI CHAMA, LAKINI TO BE HONEST HIYO COMPONENT 1 YA MBOWE SIIPENDI HATA KIDOGO. MIGOGORO MINGI SANA YA CHADEMA UKIANGALIA CHANZO NI YEYE. HATAKI KUTHAMINI MAWAZO YA WENGINE PIA. FIKRA ZAKE ZIKIPINGWA KIDOGO TAYARI ANATISHIA KUWANG'OA WENZAKE KWENYE NYEDHIFA ZAO.
LAKINI NINACHOKIONA NI MBIO ZA HUKU TUENDAKO. ANAHISI KAMA AKINA KABWE WATAMFUNUKA KWA UMAARUFU NA NGUVU NDANI YA CHAMA. NDIO MAANA MUDA WOTE ANAJITAHIDI KUWAKATA KAULI KATIKA MAWAZO NA HOJA ZAO. NAWASHAURI TENA WASITHUBUTU KUMPENDEKEZA AKASIMAMA KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA URAISI HATA SIKU MOJA. NEXT TIME WAMWACHE BABU AJARIBU TENA BAHATI YAKE THEN WAJARIBU WENGINEO.
Comment by Muhili Komba 4 hours ago
Mnajua hapa ni propaganda iliyoandaliwa ili chama kisambaratike ili ccm waseme si mnaona wenyewe kwa wenye wanagombana.hiyo ndio siri kuna watu baraa hao walisoma urusi hizi zile za soviet.
Comment by hamza salum 4 hours ago
mungu anusuru,kwani hiki ndo chama tunachotegemea kuleta upinzani na kufanikiwa kuingia madarakani sasa mkianza hivyo,ndoto zitakua hazitimii
Comment by William Jotham 4 hours ago
Laana hii jamani itaisha lini ktk nchi hii ya Kambarage. Tulidhani Chadema wanaweza kuwa suruhisho la matatizo ya UFISADI, sasa nawao ndo wanaelekea hukohuko!!!!!!!Mbowe anaonekana ni DICTATOR kwanini asiwasikilize akina zitto.Zitto anayosema ni halali. Mh.Slaa okoa jahazi maana hao vijana wako wanahitaji discpline ya hali ya juu,wanakiua chama tulichokuwa tunatarajia kitukomboe. Wote mnajifanya kumuenzi mwl.Nyerere lakini hamna kitu,ndo maana anawalaani mnaojifanya kumuenzi.Chadema kaeni chini mjenge chama chetu. KIDUMU CHAMA CHA DEMOKRASIA!!!!!!! Zidumu fikra za VITA VYA UFISADI>>>>.
Comment by Haji Hashimu 7 hours ago
ni kweli tatizo la migogolo ndani ya Chadema ni Mbowe, kwani amekuwa mtu wa kupendwa kufuatwa kwa kila kitu anachosema au ongea, hawa wengine kama Godbless Lema ni wasiojua chochote wao kazi yao ni kufuata kila kitu anachosema Mbowe. Wasipokuwa makini Mbowe anaweza kukiaribu chama badala ya kujenga.
Comment by ikk 7 hours ago
Kabwe, Shibuda.. Ninyi sio wanafamilia/Ukoo. Mta fanyiwa fitna mpaka mkimbie!
Comment by Timothy Mbulakwao 8 hours ago
huyo ndo mbowe. Chama ni kizuri lakini ubabe wa Mbowe, asiyetaka kupingwa kwa kila anachokifanya au kukisema ni tatizo. Na hizo ni element za udictator kwani yeye anadhani mara zote mawazo yake ni sahihi kuliko ya wengine. Chonde msijekumsimamisha kugombe aupresdent 2015 Mtaua chama na mtawapa nguvu sana CCM. Huu ni ushauri wa bure.
 
Nasikitishwa na Mwenendo wa CDM kwa sasa! Nashauri viongozi waache tofauti zao jamani bado mapema mno na safari ndefu!
 
kama unategemea mabadiliko kupitia chadema umekosea, wanatumia udhaifu wako wa kufikiria na kukudanganya kuwa ni wapambanaji.sina haja ya kutibua ladha yako kwao lamsingi endelea kuwasoma na mwisho utaelewa kama hakuna mpambanaji


Madaliko tayari yameanza ndugu, fukuza-fukuza & magamba ndani ya ccm, cheque ya dowans ilivyokuwa ngumu kutoka, muswada wa katiba umerudishwa (kwa aibu ya karne), na sukari nayo imeshuka bei. CHADEMA -TWANGA KOTE-KOTE:)
 
CDM,bado makini tu hata mseme vp,hayo ni mapito tu,bado safu ya wapambanaji na wapigania haki za wanyonge iko imara!CHADEMA,CHADEMA!Daima pamoja
 
Hii ni pure propaGANDA, na watu wapo kazini hapa!!
Lakini amini usiamini, huu ni usanii wa kitoto unaopandwa hapa, na utafanyiwa kazi fasta!
 
Hii ni pure propaGANDA, na watu wapo kazini hapa!!
Lakini amini usiamini, huu ni usanii wa kitoto unaopandwa hapa, na utafanyiwa kazi fasta!
Hii nguvu inayotumiwa na CCM humu JF ingetumika kubuni mbinu za maendeleo lingekuwa jambo la heri lakini kama mbinu ni hizi za kuja kuudhi wanachama wa JF kwa kupinga chochote na kujaza page za thread kwa hoja za mabishano tu kamwe hawatafanikiwa.
 
Kwani mnashangaa nini?kutokujua fitina za ccm?ni mara ngapi CDM kimeandamwa na scandal kama hizi za kutengenezwa na CCM?jamani mbona tunakuwa wepesi wa kusahau? hebu tujikumbushe jamani tusidandie tu hoja,hii ndo siasa na ndo kazi ya propaganda,kama una roho nyepesi nakushauri kaa pembeni uwe mtazamaji vinginevyo nawe utapotea

kwetu sie tuliosoma political science haya mambo si ya ajabu kwa siasa zenye kuhusisha jamii ya watu wasiokuwa na elimu ya kutosha kupembua mambo kama ya watanzania

huyu anayesema Mbowe asipewe nafasi ya urais 2015 hili kalipata kutoka wapi,mbona 2010 alikaa pembeni?alafu tunaomba mtambue tokea CDM imeanza rekodi zinaonesha chama kimekua kkpanda chini ya Mbowe,angelikuwa hafai si tungeliona chama kinashuka viwango zaidi?tufikiri zaidi kuliko kuongea
 
Kwani mnashangaa nini?kutokujua fitina za ccm?ni mara ngapi CDM kimeandamwa na scandal kama hizi za kutengenezwa na CCM?jamani mbona tunakuwa wepesi wa kusahau? hebu tujikumbushe jamani tusidandie tu hoja,hii ndo siasa na ndo kazi ya propaganda,kama una roho nyepesi nakushauri kaa pembeni uwe mtazamaji vinginevyo nawe utapotea

kwetu sie tuliosoma political science haya mambo si ya ajabu kwa siasa zenye kuhusisha jamii ya watu wasiokuwa na elimu ya kutosha kupembua mambo kama ya watanzania

huyu anayesema Mbowe asipewe nafasi ya urais 2015 hili kalipata kutoka wapi,mbona 2010 alikaa pembeni?alafu tunaomba mtambue tokea CDM imeanza rekodi zinaonesha chama kimekua kkpanda chini ya Mbowe,angelikuwa hafai si tungeliona chama kinashuka viwango zaidi?tufikiri zaidi kuliko kuongea

Mbowe is the Best CEO for CHADEMA! hata watu wasipokubali lakini ni ukweli, mbona NCCR kipo chali? Mbona CUF kipo chali?
 
Umejitaid kuona kuona kuwa chadema wapo macho lakini sina uhakika kama kwel na wewe macho yako yote yapo waz kuwachunguza chadema vizuri.mimi ninachoomba ni tuendelee kuwachunguza hawa ndugu zetu
 
ukifuatilia trend nyingi utaona kuwa ni watu walewale wanataka kukwamisha CHADEMA kuexcel. Kumbuka ile walk out against President. Kumbuka Maandamano ya Arusha. Na kumbuka maanadamano ya kanda ya ziwa. Kote huku walijaa sababu. Sasa leo hii watu wako msibani na hata hawajazika walishaanza kupeana vyeo. Je kunanii? Naamini hata wenyeji wa Shinyanga waliwashangaa haraka hii ya kurithishana madaraka. Mimi naamini Mbowe is the best Party Chairperson, si tu kwa upinzani, bali hata ukilinganisha na chama tawala. Nadhani wenyeviti wengine wanatakiwa wacopy na kupaste model yake. Ndo maana utaona pamoja na mikiki mikiki mingi CHADEMA imeendelea kukua exponentially. Nadiriki kusema kuwa pengine angekuwepo mwenyekiti mwingine hii growth tusingeiona. Ndo maana wabaya wake wanastruggle kwa nguvu zote kumharibia.
 
Kwa kweli mambo ya propaganda siyo mchezo jamani. Habari ya Kikao cha kamati kuu ya CDM yaliandikwa na vyombo vya habari na humu JF kwa namna ambayo utagundua kuwa ni kitu ambacho kimeandaliwa kabla hata ya kikao chenyewe na habari zenyewe zinaonyesha mwelekeo fulani. Kitu cha ajabu hadi leo sijasikia uongozi wa CDM ukitoa tamko lolote kuhusu kikao hicho.
 
Nasikitishwa na Mwenendo wa CDM kwa sasa! Nashauri viongozi waache tofauti zao jamani bado mapema mno na safari ndefu!
Ha ha ha propaganda munaziweza hamsomi thread zilizoeleza ukweli ya nini kili jiri jitahidini labda mutaweza baada ya kutoa magamba yenu mukianza na mwenyekiti wenu wa chama cha magamba
 
hivi zito bado hajazoea madaraka ? Habadiliki na asinichukie kwani mm muislamu mwenzake manake ugonjwa wake udini , yaani hata akichangia hoja kikao cha ndani anatangaza ? Umaarufu gani anaotamani mbona anajulikana tz yote hata kipindi cha bunge c unaonekana badilika kaka
 
Back
Top Bottom