CHADEMA waamua kuchimba visima 11 Igunga na Kafumu haonekani tena Igunga!

Tuacha ushabiki, Kiongozi gani anaweza kuleta maendeleo ndani ya wiki mbili. Ni mapema sana kumsemea Kafumu.
kweli wewe ni mzee,hadi unaouvivu hata kufikiri.kunatatizo gani?kwa kafumo hatakuanza utekelezaji wa awali wa ahadi zake?na kwenda dar kupumzika.akumbuke kashinda bahatimbaya tu.kama haamini asubiri 2015.
 
Dk Slaa anena
Dk Slaa amesema chama hicho kinatarajia kuchimba visima vya maji 11 katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora ikiwa ni wiki takriban mbili tangu kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo uliofanyika Oktoba 2.

Dk Slaa alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kukabidhi mchanganuo wa namna walivyogawa mradi wa utekelezaji wa visima 200, vilivyotolewa na Sabodo kwa lengo la kuchimbwa katika majimbo tofuati wanakotoka wabunge wa Chadema.

Alisema lengo la kutekeleza mradi huo wa maji katika Jimbo la Igunga limetokana na ziara aliyoifanya katika vijiji 98, vilivyopo katika jimbo hilo na kugundua wananchi wake wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji.

“Katika mpango kazi wetu, tumepanga kuchimba visima 11 katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, hii imetokana na ziara yangu katika vijiji 98 ambapo niligundua kuwa wakazi hao wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji,”alifafanua Dk Slaa.

Chadema kilishika nafasi ya pili katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, kwa aliyekuwa mgombea wake, Joseph Kashindye kupata kura 23,260 sawa na asilimia 44.3, nyuma ya mgombea wa CCM, Dalaly Kafumu aliyeshinda kwa kura 26,484 kati ya 52,487 halali zilizopigwa, sawa na asilimia 50.4.

Habari zinasemekana kuwa baada ya Kafumu wa CCM kushinda ubunge tayari ameisha weka makazi ya kudumu Mbezi beach Dar es Salaam na kuwaacha wananchi wa Igunga wakifa na njaa na kuhangaika huku na kule kutafuta maji,,,hiki kitendo kimefanya CHADEMA waamue kuanza kuwatekelezea mradi wa visima 11 vya maji wananchi wa Igunga japo hawakushinda ndani ya hilo jimbo kwani kipindi cha kampeni Dr Slaa aliona ni kiasi gani wanachi wa Igunga wanavyoteseka na uhaba wa maji..

Badili heading/kichwa cha habari kiwe Sabodo kuchimba visima IGUNGA. Kwa sababu anayekwenda kuchimba visiama hivyo ni Sabodo si CHADEMA. Kumbukumbu zangu zinaonyesha Sabodo ni kada wa CCM si CHADEMA lakini kwa kuwa ni mwanademokarasia amekuwa akiichangia CHADEMA ikli kuipa nguvu ya kutoa ushindani kuliko ilivyo hivi sasa (dhaifu).
 
Chama cha magamba wametumia zaidi ya bil 3 kwenye uchaguzi huo kwa muda wa mwezi 1 wa kampeni zao,wanaonekana kuwa na hela za kutumia hovyohovyo.Kwa nn sio kwenye mambo ya msingi kama ya kutatua kero za wananchi?
Kingeshinda chama kingine ingekuwa sahihi kuwapa muda lkn sio ccm!
Na nyie watu wa Igunga na tabora kwa ujumla YOU ARE BREAKING OUR HEART! kumbukeni enzi za mzigo mzito mbebeshe myamwezi zimeshaisha.
Mlikuwa mnalialia RA alipokuwa anajivua gamba.Amewaletea nn kwa miaka yote aliyokaa zaidi ya kuwaletea umasikini kwenu na nchi nzima?
Mnaudhi sanaaana nyie! Kwenye biblia imeandikwa yesu alikuja kuwakomboa watu katka utumwa wa dhambi lakn watu wakamuua hatimaye.Na nyie ndo walewale wa kuridhka na matatizo.NDUHU TABU GETE! NAHENE MIJAMPOLA!

na wananchi wengine walizirai daah,nimependa lugha gongana kama mkazo,labda wataacha kuzirai.
 
Kuapishwa kwenyewe bado halafu aanze tuu nyie viazi kweli kafumu ni mbunge mteule bado hajawa mbunge kamili subirini akiapishhwa muone mziki wa CCM

Acha ujinga wewe? Umeulizwa mbunge aliyekuwepo amekaa madarakani kwa muda gani?! Toa jibu!
 
We masaburi, Dr Slaa ametoa tamko na Sabodo amefadhili. Ni jukumu la chama kuamua lielekeze wapi misaada iliyopokelewa. Nyie magamba mkipata misaada kama hii ni dili mnapeleka kwa mahawara zenu kama mnavyowapa ukuu wa wilaya na mikoa. Watu wameamua kupitishia katika mikono sahihi.
Tulia kidogo halafu fuatilia hii conversation imetokea wapi, maana unachokifanya ni kunipiga risasi askari mwenzako.
 
Hii tabia ya CDM kupokea pesa hovyo kwa matajiri watakuja kujuta.

Huyu muhindi ni mafia anajua anachokifanya kwanza Pro-CDM-JF wanafuata mkumbo hawajuhi Sabodo anafanya kazi gani
 
Kuapishwa kwenyewe bado halafu aanze tuu nyie viazi kweli kafumu ni mbunge mteule bado hajawa mbunge kamili subirini akiapishhwa muone mziki wa CCM

Duh!!! Mkuu, kweli ukidhamiria na akili zikakutuma kwa dhamira na si reality utatoa majibu mepesi kwa maswali magumu. Majibu yatakayowashangaza great thinkers. Mkuu, yule RA alitoka chama gani? Na je kwa kipindi chote cha ubunge wake pale Igunga aliendelea kuwa mteule tu bila kuapishwa na ndiyo sababu iliyomfanya ashindwe kuwapati maji watu wake? Kweli kazi ipo humu ndani ya JF!!!
 
CCM hawana jipya kwani RA amekaa muda mrefu na mpaka sasa ni shida na aibu igunga? au alikuwa bado hajaapishwa? hakua mb wa ccm? Ninacho jua mimi mbunge wa wananchi igunga ni kashindye, hoyo kafumu ni mbunge wa ccm tena huko dar, muache aungane na kina david matayo ambao huonekana jimboni kipindi cha kampeni tu.

kaenda kusherehekea miaka 50 ya uhuru na ushindi mkuu.wananchi msubirini atakuja!
 
Hapa CDM wanajaribu kuona ni kundi lipi la watz ni la kuwasaidia kwanza kutokana na shida walizonazo,,, wameamua kuwachimbia visima hata kama siyo jimbo wanaloliongoza kwani siasa na utekelezaji ni kitu tofauti,,, kiongozi makini ni yule anayejua shida za watz na siyo kuwaangalia wale waliompa jimbo kuongoza,,, Ingekuwa ni ccm imeshindwa hapo Igunga ingeamua hata kuwakatia umeme hata mwezi mzima mie nawajua sana hawa jamaa,,,,
 
Ujue CDM-JF wengi ni mambumbu wa siasa hii habari wote wanakubaliana.

Eti CDM waamua kuchimba visima.. hakuna hata mwenye kuuliza source pesa zinatoka wapi
 
Hii tabia ya CDM kupokea pesa hovyo kwa matajiri watakuja kujuta.

Huyu muhindi ni mafia anajua anachokifanya kwanza Pro-CDM-JF wanafuata mkumbo hawajuhi Sabodo anafanya kazi gani

Hapo kwenye wekundu pana jambo. Hivi mkuu, ni lazima uchangie kila thread unayokutana nayo humu ndani ya JF? Kwa nini usuwe kama wale wanaosema " nilikuwa napita tu" wakaenda zao. Kama wewe humjui Mzee Sabodo basi ni mvivu wa kusoma au hata kusikiliza siasa na development issues za Tanzania. Huyu ni mzalendo halisi, ambaye yuko tayari kugawana alichonacho na wasionacho. Mfano mzuri ni wa hivyo visima vya maji ambavyo alivitangaza mapema kabisa mwa mwaka huu, na kuwataka wahitaji walete proposals zao kwake ili bodi aliyoiteua iyapitie na kutoa maamuzi. Na ni mwana CCM mwenzako kama wewe nawe ni wa CCM.
 
Angalia hapo kwenye red quote, kama ni mwana CCM ndiye amefadhili kuchimba visima inakuwaje mnasema CHADEMA wanachimba visima?
 
Mkuu inaonekana hata magazeti huwa husomi kwani una upungufu wa kujua siasa za tz japo unadakia kwa juu,,sourse ni gazeti la mwananchi
 
Jamani hayo matatizo ya maji Igunga ni tokea enzi za Ukoloni hadi leo hii sasa CCM inaongea upupu gani tena.

CCM imeshindwa na haifa, hizo fedha za Sabodo ni fedha ndogo sana ukilinganisha na fedha ambazo CCM inakusanya kutoka kwa Wahindi na wafadhili wake wa ndani na nje lakini fedha zinazoingia CCM zinaishia kuwa mitaji ya biashara kwa watoto na viongozi wa CCM. RA, EL na Kikwete pamoja na wizi wote waliofanya tumeambua Giza na umaskini mkubwa aliojionea Dr. Slaa huko Igunga, CCM huku wakijuwa wana Igunga hawana maji bado walikodi Helkopta mbili kwa ajili ya wizi wa kura na kuhadaa Umma bila hata mpango kazi wa maendeleo. CCM imeiba mabilioni ya shilingi lakini zaidi wanakimbia kuzificha katika accounts za nje ya nchni, mtu anaye tetea CCM ni mtu mfu kiakili si wakubishana naye ni wakuhurumia maana hajui alitendalo na ni mgonjwa.

Dr Slaa na Chadema ongereni sana, tupo nyuma yenu kama mlivyoona katika uchaguzi wa Igunga na katika mitandao yote ya Kijamii kuanzia JF, fb, twitter nk.
 
Hapo kwenye wekundu pana jambo. Hivi mkuu, ni lazima uchangie kila thread unayokutana nayo humu ndani ya JF? Kwa nini usuwe kama wale wanaosema " nilikuwa napita tu" wakaenda zao. Kama wewe humjui Mzee Sabodo basi ni mvivu wa kusoma au hata kusikiliza siasa na development issues za Tanzania. Huyu ni mzalendo halisi, ambaye yuko tayari kugawana alichonacho na wasionacho. Mfano mzuri ni wa hivyo visima vya maji ambavyo alivitangaza mapema kabisa mwa mwaka huu, na kuwataka wahitaji walete proposals zao kwake ili bodi aliyoiteua iyapitie na kutoa maamuzi. Na ni mwana CCM mwenzako kama wewe nawe ni wa CCM.

Wewe acha porojo za kitoto wewe ni nani humu JF unapangia watu cha kuongea.

Wewe unataka posts zote unazisoma humu JF zikufurahishe, nakushauri fungua Forum yako kama Malaria Sugu.

Huko ndio utakuwa unapangia watu vitu vya kuongea, kama kazi yako JF ni kuelekeza watu, mbona umeshindwa kumshauri huyu CDM-Kata mwenzako alioandika hii Heading ya uwongo kwenye hii thread.

Wewe unajua kama Sabodo anauza ile kitu?

-
 
Kuapishwa kwenyewe bado halafu aanze tuu nyie viazi kweli kafumu ni mbunge mteule bado hajawa mbunge kamili subirini akiapishhwa muone mziki wa CCM
Nipe kifungu cha katiba kinachosema kafumu ni mbunge mteule?
Kachaguliwa na aanze kazi swala kuapishwa ni la kwake watu wanataka kuona mabadiliko...
 
Tuacha ushabiki, Kiongozi gani anaweza kuleta maendeleo ndani ya wiki mbili. Ni mapema sana kumsemea Kafumu.

Je Miaka 50 au 15 aliyokaa RA haitoshi?, Nyota njema huonekana asubuhi. Uongozi Tanzania hivi sasa si kukimbilia Posho bali ni kufanya kazi za wananchi. Unapochaguliwa tu siko hiyo hiyo unatakiwa kuanza kazi maana uliomba mwenyewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom