CHADEMA waamua kuchimba visima 11 Igunga na Kafumu haonekani tena Igunga!

asante kwa kuiweka clear zaidi. Naona pro-CDM hawatengi muda wa kufikiria.
chadema ni chama makini ndio maana Sabodo katoa ofa ya visima ktk majimbo yote sio magamba waliokubuhu kufisadi misaada ya inayotolewa nchi za hisani na saizi bila aibu wanataka kutafuna fedha ya DOWANS.
 
Tuacha ushabiki, Kiongozi gani anaweza kuleta maendeleo ndani ya wiki mbili. Ni mapema sana kumsemea Kafumu.
Maendeleo hayaletwi na viongozi, kama unatarajia maendeleo ya wanaigunga kuletwa na Kafumu basi umepotea. Kafumu alikwenda Igunga kutafuta uhalali wakujilimbikizia ukwasi na sio vinginevyo. Kazi ya viongozi wakiwamo wabunge ni kuunganisha nguvu za wananchi kujiletea maendeleo yao wenyewe.
 
Hii tabia ya CDM kupokea pesa hovyo kwa matajiri watakuja kujuta.

Huyu muhindi ni mafia anajua anachokifanya kwanza Pro-CDM-JF wanafuata mkumbo hawajuhi Sabodo anafanya kazi gani

pole sana imekuuma.Unataka wananchi wafe kwa kukosa maji safi na salama.
 
Ujue CDM-JF wengi ni mambumbu wa siasa hii habari wote wanakubaliana.

Eti CDM waamua kuchimba visima.. hakuna hata mwenye kuuliza source pesa zinatoka wapi

funga domo lako.Ulitaka hizo hela apeleke kwenye vyama vya mafisadi?
 
Kila kitu kinahitaji mipango madhubuti ili kufikia malengo.

Naamini kuwa Kafumu anajipanga, kwakuwa matatizo ni mengi lazma apange mikakati madhubuti.
Alitakiwa awe amepanga mikakati hata kabla ya kukusudia kugombea na sio baada ya kuchaguliwa. Baada ya kuwa mbunge ingekuwa utekelezaji wa mikakati hiyo. Lakini kwakuwa alikwenda Igunga kutafuta uhalali wa kujilimbikizia ukwasi basi mkakati wake umekuwa kurudi Dar na kupokewa na wakwasi wenzake, na kinachofuata ni kuanza kujipendekeza kwa mkuu wa kaya ili amteuwe kuwa waziri wa madini ili aendelee kuneemeka.
 
Visima vyenyewe vitaandikwa Don by Sabodo, Sio Chadema. Hapa ni Sabodo ndie anayechimba visima kwa kupitia ukandarasi wa CHADEMA. Mwenye akiri atajua hili lakini Mbumbumbu Atani Quote With negative and bias comments.
 
Muanzisha thread naona unajiliwaza wewe na Magwanda wenzeko..hii habari nimeisoma kwenye gazeti la Mwananchi la leo.

Visima 200 vitachimbwa na Sabodo kwenye majimbo yote ya wabunge wa CDM.

Hakuna pesa yoyote CDM wametoa.

Magwanda wanapongezana tu..Ha! Ha! Ha! Mnachekesha

maneno ya uongo hivi inabidi yafutwe na mods!
 
Visima vyenyewe vitaandikwa Don by Sabodo, Sio Chadema. Hapa ni Sabodo ndie anayechimba visima kwa kupitia ukandarasi wa CHADEMA. Mwenye akiri atajua hili lakini Mbumbu Atani Quote With negative and bias comments.

pole umechemsha kisonoko!
 
Dk Slaa anena
Dk Slaa amesema chama hicho kinatarajia kuchimba visima vya maji 11 katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora ikiwa ni wiki takriban mbili tangu kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo uliofanyika Oktoba 2.

Dk Slaa alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kukabidhi mchanganuo wa namna walivyogawa mradi wa utekelezaji wa visima 200, vilivyotolewa na Sabodo kwa lengo la kuchimbwa katika majimbo tofuati wanakotoka wabunge wa Chadema.

Alisema lengo la kutekeleza mradi huo wa maji katika Jimbo la Igunga limetokana na ziara aliyoifanya katika vijiji 98, vilivyopo katika jimbo hilo na kugundua wananchi wake wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji.

“Katika mpango kazi wetu, tumepanga kuchimba visima 11 katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, hii imetokana na ziara yangu katika vijiji 98 ambapo niligundua kuwa wakazi hao wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji,”alifafanua Dk Slaa.

Chadema kilishika nafasi ya pili katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, kwa aliyekuwa mgombea wake, Joseph Kashindye kupata kura 23,260 sawa na asilimia 44.3, nyuma ya mgombea wa CCM, Dalaly Kafumu aliyeshinda kwa kura 26,484 kati ya 52,487 halali zilizopigwa, sawa na asilimia 50.4.

Habari zinasemekana kuwa baada ya Kafumu wa CCM kushinda ubunge tayari ameisha weka makazi ya kudumu Mbezi beach Dar es Salaam na kuwaacha wananchi wa Igunga wakifa na njaa na kuhangaika huku na kule kutafuta maji,,,hiki kitendo kimefanya CHADEMA waamue kuanza kuwatekelezea mradi wa visima 11 vya maji wananchi wa Igunga japo hawakushinda ndani ya hilo jimbo kwani kipindi cha kampeni Dr Slaa aliona ni kiasi gani wanachi wa Igunga wanavyoteseka na uhaba wa maji..
Songa mbele mtu wangu Dr Slaa wa ukweli CDM sio ngonjela za Kafumu na Mchemba kwenye majukwaa ni vitendo!!!!!!!!!!Watanzania wanaona hiyo, press pia tangaza wacha ubaguzi!!!!!!!!!!
 
Wana ivy ga msitegemee kitu toka ccm zile kangana t-shirt ndio Kila kitu tayari let's meet 2015 sawa?
 
Wewe acha porojo za kitoto wewe ni nani humu JF unapangia watu cha kuongea.

Wewe unataka posts zote unazisoma humu JF zikufurahishe, nakushauri fungua Forum yako kama Malaria Sugu.

Huko ndio utakuwa unapangia watu vitu vya kuongea, kama kazi yako JF ni kuelekeza watu, mbona umeshindwa kumshauri huyu CDM-Kata mwenzako alioandika hii Heading ya uwongo kwenye hii thread.

Wewe unajua kama Sabodo anauza ile kitu?


-
Kama unazo taarifa nyeti kama hizo unangoja nini kufanya kazi za polisi jamii? Au unajua kuzitete sera za CCM bila kutumia akili hata kidogo.
 
Julius Mtatiro aliwai kusema wakati wa uchaguzi wa Igunga kuwa na hapa namnukuu.."Mkichagua ovyo ovyo haipaswi kuja kulalamika ovyo ovyo kwasababu ya uchaguzi wenu wa ovyo ovyo" mimi nadhani hiki ndicho walichokichagua wana-Igunga na wanapaswa wavune walichopanda...kwa upande wa pili,nakipongeza chama changu CDM kwa uamuzi huu wa hekima kwa kuamua kuonyesha kuwa chama cha siasa sio kupiga domo tu kama wengine wanavyofanya,bali ni kutumikia wanachi kwa kuondoa kero zao na matatizo yao......vinginevyo wana-Igunga wataona madhara ya kuchagua ovyo ovyo...........
Tafadhari wahurumie wana Igunga, si wote waliochagua chama cha maghamba bali walionewa, mara shahda zinunuliwe shauri ya njaa.Mara majina ya watu hakuna kwenye vituo vya kupigia kura. Vijana wanahangaika, makada wanauwawa wengine wanapigwa mabomu na polisi watoke kwenye vituo bila kupiga kura.Huo uchaguzi wa Igunga haukuwa wa haki ulikuwa ubabe na vitisho tuu!!!!!!!!!!!
 
Chadema wana majukumu gani nchini??? Na ni mradi wa kwanza kuufanya kama utafanyika kweli..kwani sabodo si ndio mfadiri. Acheni maneno kanga na muache siasa za kitoto. Ni mimi nisie na chama

Pole sana kwa kukosa upeo wa kufikiri. CCM imewagharimu takribani billion tatu kwa kuutafuta ubunge hapohapo IGUNGA. Hivi bado tu unaamini wataleta maendeleo bila kurudisha kile walichokipoteza? Yaani Mbunge wenu ana wakati mgumu sana kutekeleza hizo ahadi kwani baada ya kumnunulia wapiga kura asitegemee tena fungu la ghafla labda ajitolee pesa yake binafsi. Na hiyo itakuja tena wakati wa kutafuta kura.
 
maneno ya uongo hivi inabidi yafutwe na mods!

Narudia tena kusema pesa ya kuchimbia visima 200 anatoa Sabodo.

CDM hawatoi hata senti huo ndio ukweli.

Tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa, soma magezeti ya leo ndio utajua ukweli hapa mnadaganganya tu CDM-JF.

Ukurasa wa mbele wa Tanzania Daima Gazeti la CDM kuna picha Dr. Slaa, akimpa Sabodo, karatasi ya mchanganuo wa gharama za visima, ili Sabodo atoe pesa
 
Na hizi pesa zingepitia THE MAGAMBA' S international, Hakika zingechakachuliwa na kupeleka misaada kwenye misaada. Jamani adui wa maendeleo sugu TZ MAGAMBA haihitaji tochi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom