Chadema; tutawaunga mkono wanaotetea wananchi bukoba.

Nam...

Member
Nov 11, 2011
51
16
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, amesema kuwa chama hicho kitaendelea kuwatetea wananchi wake na kutowakumbatia mafisadi, kwa kuhakikisha wanafichua siri za watu hao.

Ametolea mfano manispaa ya Bukoba, kuwa CHADEMA inawaunga mkono madiwani waliosimamishwa na uongozi wa CCM mkoa kwa kutokuwa na imani na Meya, kwani wamegundua ufisadi ndani ya manispaa hiyo, lakini baadhi ya viongozi wa CCM wanataka kuwafukuza kwa maslahi ya uongozi ndani ya chama akasema haitakubalika.

Ameongeza kuwa CHADEMA haina mpango wowote kisiasa na Kagasheki ambaye ni mbunge wa jimbo hilo, lakini akasema katika hili CHADEMA inamuunga Kagasheki mkono kwani anatetea wananchi, hivyo chama kisibebe hoja ya Kagasheki kama ya CCM.
 
Madiwani waliofukuzwa ndiyo wanaowahujumu wananchi wa bukoba.

Binafsi nikiwa mpenzi wa CDM,nawashauri viongozi wangu kutojiingiza kichwa kichwa ktk mgogoro wa madiwani wa Bkb. Kama watafanya uchunguzi makini mtagundua madiwani wanaojidai kutetea maslahi ya wananchi wa Bkb,wengi wao ni vibaka wazoefu ambao hawastahili kuongoza hata kitongoji!
 
Back
Top Bottom