CHADEMA tuondoleeni wasiwasi huu kama kweli mtaweza kuongoza Tanzania.!

Umeandika vyema kuwa watu wana imani na CHADEMA siyo na TUNTEMEKE! ndiyo maana alisema arumeru CHADEMA hatutashinda na TUKASHINDA! Watanzania wana imani na CHADEMA hawajui TUMTEMEKE. Na mimi naamini huyu mtu hayupo ndani ya CHADEMA, yuko nje, maana anavyaanfikaga huwa havina ukweli wowote,na havitofautiani na propaganda za magamba ambazo tumezizoea! Ila angalizo lako ni la uzalendo na nimelikubali.
 
Pamoja sana mkubwa.Intelejensia ya chama inapaswa kuwa macho masaa 24
 
Umeandika vyema kuwa watu wana imani na CHADEMA siyo na TUNTEMEKE! ndiyo maana alisema arumeru CHADEMA hatutashinda na TUKASHINDA! Watanzania wana imani na CHADEMA hawajui TUMTEMEKE. Na mimi naamini huyu mtu hayupo ndani ya CHADEMA, yuko nje, maana anavyaanfikaga huwa havina ukweli wowote,na havitofautiani na propaganda za magamba ambazo tumezizoea! Ila angalizo lako ni la uzalendo na nimelikubali.

Hakika amefanya uzalendo wa hali ya juu
 
uzalendo upi hapo?maana mzee anapiga ruzuku ya chama na akisemwa tu kosa.bigup sana Tuntemeke
Mbona M.K.W.E.R.E anapiga ruzuku za Chama, Serikali, WAMA na za Wafadhili kwa kwenda kubembea na misibani kila kukicha, na akisemwa tu bundi kama wewe hamuoni kosa?
 
Watu wa namna hii hawakosekanagi kwenye maisha.......ziko njia nyingi za kudeal nao na mojawapo ni kuwaacha kama madhara yake hayana mashiko.....
 
Nikisoma watu wote wanavyochangia kwa kila thread ya inayohusu CDM ninaamini kwamba chama hiki kiko damuni mwa Watanzania
 
Shukrani sana mleta mada. Ila binafsi madhara ya Tuntemeke siyaoni maana habari zake huwa hazina ushahidi, na kwasasa watanzania wameishajua maana ya neno propaganda, hata aliyeko kule Nduku-Kahama lazima aulize ushahidi!!

Huyu ni wakupuuza tu, hizi tuhuma ni za kupikwa tu na zinaishia kujaza saver Jf!!

Pamoja na hayo hii haiwafanyi viongozi wetu kufanyia kazi mapendekezo yako ili kukomesha ushetani huo!!!

LONG LIFE CDM NEVER GIVE UP!!
 
Nimeyapenda sana maoni yako.Natamani Dr Slaa na Mbowe wawe wameona mjadala huu.
 
100% namfahamu tuntemeke na kundi lake, sema ukimtaja tuntemeke jina lake humu unaweza ukala ban,
in short Tuntemeke ni mtu wa makao makuu ya chama, ana kundi lake ambalo linaundwa na VIJANA wale failures wa uchaguzi wa BAVICHA, fatilia comments zao humu utajua nini nakiongelea, hata post zinazohusu yule makamu wa BAVICHA aliemtetea Shibuda, tuntemeke ndio huwa anazileta na kumsifia sana, sasa how comes TUNTEMEKE muasi awe anamshabikia mtu ndani ya CDM na wakati Tunte na kundi lake hawaitakii mema CDM?
Chunguza kwa umakini uhusiano wa wale wahanga walioshindwa uchagzui wa BAVICHA na tuntemeke ndio mtatambua mm naongelea nini.
Tunawajua hawa watu wakuu na hali lipo wazi kabisa.
 
DR SLAA Njoo na majibu hapa na utueleze kama kweli ana daiwa na chadema mil 140,mimi sitaki kumhukumu Tuntemeke kuwa anaongea majungu,kumbukeni tuntemeke huyo huyo alianzisha kashifa ya mbowe kuuzia chadema fuso bovu kwa mil 500 jambo ambalo lilikua la kweli!
 
Mkuu nilishamuonya mwenzako mapema kwamba CCM haiwahusu hii thread.
 
100% namfahamu tuntemeke na kundi lake, sema ukimtaja tuntemeke jina lake humu unaweza ukala ban,
in short Tuntemeke ni mtu wa makao makuu ya chama, ana kundi lake ambalo linaundwa na VIJANA wale failures wa uchaguzi wa BAVICHA, fatilia comments zao humu utajua nini nakiongelea, hata post zinazohusu yule makamu wa BAVICHA aliemtetea Shibuda, tuntemeke ndio huwa anazileta na kumsifia sana, sasa how comes TUNTEMEKE muasi awe anamshabikia mtu ndani ya CDM na wakati Tunte na kundi lake hawaitakii mema CDM?
Chunguza kwa umakini uhusiano wa wale wahanga walioshindwa uchagzui wa BAVICHA na tuntemeke ndio mtatambua mm naongelea nini.
Tunawajua hawa watu wakuu na hali lipo wazi kabisa.

Intelejensia ya chama inapaswa kufanya kazi kuwaondoa hawa wajinga wanaotaka kuua chama.Wilfred Lwakatare fanya kazi yako!
 
Shukrani sana mleta mada. Ila binafsi madhara ya Tuntemeke siyaoni maana habari zake huwa hazina ushahidi, na kwasasa watanzania wameishajua maana ya neno propaganda, hata aliyeko kule Nduku-Kahama lazima aulize ushahidi!!

Huyu ni wakupuuza tu, hizi tuhuma ni za kupikwa tu na zinaishia kujaza saver Jf!!

Pamoja na hayo hii haiwafanyi viongozi wetu kufanyia kazi mapendekezo yako ili kukomesha ushetani huo!!!

LONG LIFE CDM NEVER GIVE UP!!

Asante kwa ushauri wako.Naamini viongozi wanapitia kwa umakini maoni yenu.
 
WanaJF

Ni ukweli ulio dhahiri kwamba chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kwa sasa kimejijengea imani kubwa kwa watanzania kiasi kwamba wananchi wameanza kuamini kwamba kumbe hata bila CCM nchi inaweza kusonga mbele.Ni jambo la kuwapongeza viongozi wakuu wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wake Dr Wilbroad Slaa kwa kufanikisha imani hiyo kwa chama chao.

Hata hivyo kumeanza kujitokeza mashaka kutoka kwa wananchi mbalimbali kutokana na mashambulizi mbalimbali hasa ya kashfa dhidi ya viongozi wakuu wa chama hicho hususan Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa yanayotolewa na wanaodai ni watu walioko ndani ya uongozi wa CHADEMA.

Watu hao wanaosambaza kashfa hizo kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii wamekuwa wakiongozwa na mtu anayejiita TUNTEMEKE anayedai yuko ndani ya uongozi na anafanya kazi makao makuu ya chama.Kwa vyovyote vile hili kundi kamwe haliwezi kuwa na nia njema na chama hicho kwa sababu katika hali yoyote kama wewe ni kiongozi una nia njema na chama chako huku ukiwa huridhishwi na matendo ya wenzako unapaswa kufanya mambo mawili kati ya yafuatayo:Kwanza kuyasema mabaya ya viongozi wenzako ndani ya vikao halali na Pili kama hatua zisipochukuliwa inakubidi utoke hadharani unajiuzulu nafasi zote na kutangaza kwa wananchi mabaya ya viongozi wako.Haiwezekani hata kidogo na wala haikubaliki katika demokrasia ukiwa hadharani kuwachekea viongozi wako na ukiwa gizani unatangaza kuwaangamiza.Huo ni UASI. Kamwe UASI haukubaliki katika chama chochote iwe ni CHADEMA,CUF,NCCR wala CCM

Kilichotushangaza sisi wengine hata kuamua kulisemea hili ni ukimya wa viongozi wa CHADEMA.Vurugu hizi za kundi linaloongozwa na TUNTEMEKE zina karibu mwaka sasa na inafikia mahali baadhi ya wananchi wanaanza kuamini hizo tuhuma zinapoanza kusambazwa tena kwa ustadi mkubwa.CHADEMA imekuwa sikuzote ikijipambanua kama chama chenye Intelejensia ya hali ya juu sana ni kwanini wasitumie ukachero wao kuwabaini WAASI hawa wote na kuwafukuzilia mbali? Huyu TUNTEMEKE katika uchaguzi mdogo wa Arumeru alitoa siri zote za vikao vya CHADEMA kwenye mitandao mbalimbali na kujiapiza ni lazima chama chake anachodai kukitetea kishindwe! Matokeo ya uchaguzi ule sasa ni historia!

Si nia yangu kutoa utetezi kwa mtu yeyote kama ana kosa lolote lakini katika demokrasia ya kweli haikubaliki watu kujificha ndani ya vyama kwa unafiki huku wakila njama za kuangamiza vyama hivyo kwa siri.CHADEMA wanapaswa sasa kuchukua maamuzi magumu haraka iwezekanavyo kama wanataka kuendelea kulinda heshima yao waliyojijengea kwa wananchi.Nina Imani CHADEMA wana uwezo wa kuwatambua WAASI wote na kuwaondoa kabla hawajaleta madhara makubwa kwa chama hiki ambacho sasa ni tegemeo kuu na ndiyo mdomo wa wananchi.

Dr Wilbroad Slaa na Freeman Mbowe wanapaswa kuwathibitishia watanzania kwamba wako imara kwenye uongozi na kwamba hata wakikabidhiwa Taifa wanaweza kuliongoza bila kuruhusu UASI wowote ndani ya nchi.Ningependa kuwaambia waige mifano ya vyama vya CUF na NCCR ambavyo vimewatimua WAASI wao ambao walikuwa na nyadhifa kubwa za Ubunge sembuse hawa wa CHADEMA wanaoficha utambulisho wao chini ya TUNTEMEKE na kukiacha uchi chama chao huku wakipulizwa na viyoyozi vya chama hichohicho wanachokipiga vita makao makuu Kinondoni mtaa wa UFIPA.

Sisi wengine kazi yetu ni kutoa tahadhari kwamba CHADEMA wanapaswa kulinda kwa nguvu imani waliyojiwekea mbele ya Watanzania na kuchukua maamuzi ambayo yatakuwa ni ishara njema ya kulinda heshima ya chama hicho pendwa cha Watanzania.Dr Wilbroad Slaa na Freeman Mbowe tunawataka watuondolee wasiwasi wananchi kwamba tukiwapa nchi wanaweza kutuvusha salama.!

WanaJF karibuni kwa mjadala.
hilo pigia mstari uwezo wanao sio swala la kuuliza tena
 
Watu wa namna hii hawakosekanagi kwenye maisha.......ziko njia nyingi za kudeal nao na mojawapo ni kuwaacha kama madhara yake hayana mashiko.....

Mkuu kama kweli wapo ndani ya chama hawapaswi kuachwa.Dawa yao ni kufukuzwa tu.Alimradi kuwe na uthibitisho usiotia mashaka.
 
Hivi wakati Slaa alivyo wataja mafisadi alikua na nia ya kuharibia serikali au alikua anatuonyesha waovu yanayo fanyika? Sasa tuntemeke kututoa maovu ya CDM imekua kosa.

Uelewa wako mdogo. Kwani Dr. Slaa alikuwa ndani ya serikali au mwana CCM. Ungesema Sitta, Nape au Mwakyembe afadhali, ingawa hawa walizunguka tu baadhi ya mikoa kuuza sura, bila hata kuwataja mafisadi. Hii hoja inahusu mtu kunya ndani ya beseni la wali anaokula.
 
Kama kweli ni mwana CDM basi huyo ni mamluki na tutambaini muda si mrefu. Wakati huu ndio wakati ambao ccm wanafanya jambo lolote kwa gharama yoyote ili kujinusuru. ombi langu wana mageuzi wote tusirudi nyuma na wala mpuuzi asiturudishe nyuma. wakati huu ni wakati wa change either it's negative or positive we have to demand changes.

Huyu ajitokezed haradharani na aseme kuwa yeye ni cdm na kuna uozo abc
 
Back
Top Bottom