CHADEMA tuondoleeni wasiwasi huu kama kweli mtaweza kuongoza Tanzania.!

Asante mkuu, mada nzuri na uwasilishaji maridhawa.

CHADEMA hawajaanza kwa haya ya Tuntemeke, nadhani waleteleza nyuma ya hapo; mfano suala akina Shibuda na la Zitto muda huu. Walipaswa wachukue hatua thabiti na za wazi, kama ilivyofanya kwa wale madiwani wa Arusha (of coz simaanishi kuwafukuza, namaanisha ni muhimu watende na ionekane wamefanya kwa sababu zenye kuelekweka na sahihi).

Napata taswaira ya kuwa kwa namna moja au nyingine CHADEMA hawajajui vizuri nafasi yao katika nyoyo na hisia za Watanzania walio wengi (ambao wamechoshwa na umaskini na usanii wa ccm na sasa wako tayari kuchukua hatua za kuachana na ccm na mambo yake yote!).

Of coz kuna suala la propaganda na kuchafuana ktk siasa za Tz, lakini hawa viongozi lazima waje hadharani na kusema kitu aidha wakubali au wakanushe lakini sio kukaa kimya.
Najua wengi watasema muda muafaka bado lakini when do we really know (precisely) that the time is right?
Kwanza nimshukuru mtoa mada kwa kuliweka hili wazi pengine watasikia, na pili nikushukuru Reagan kwa kuniwahi kulisema hili.

Ukweli ni kuwa Chadema wamezembea sana katika kupata ushauri, kuufanyia kazi na kutoa maamuzi.
Tumelizungumza mara nyingi na kuwatahahadhirisha juu ya mtafaruku unaonyemelea chama.
Mtafaruku hautokani na wananchi wanaounga mkono chama bali watu wachache wenye uchu wa madaraka.

Kuanzia alipofukuzwa Kafulila tulisema kuwa hakuwa peke yake, yeye alikuwa msemaji tu lakini nyuma yake kulikuwa na nguvu kubwa sana ya wanasiasa. Tukashauri ufanyike uchunguzi wa kina na waliohusika wachukuliwe hatua hata kama ni onyo lakini liwepo katika kumbu kumbu.

Mgogoro wa Uenyekiti haukuonekana kuisha na hilo limebaki donda.
Ukaja mgogoro wa madiwani, hakika walifanya kwa shinikizo lakini wao kama viongozi hawakuwa tayari.
Walichukua hatua kwakua political base yao ilitikisika na kunyong'onyea.
Hata hivyo tulidhani ulikuwa mwanzo mzuri.

Likaja suala la Kiongozi mmoja kujifungamanisha na CCM huku akikonekana wazi kukaidi misimamo ya chama. Tukatahadharisha kuwa hatari kubwa si kiongozi ni kundi la wafuasi wake ambalo anazidi kulijenga badala ya kujenga chama.

Likaja la Shibuda nalo likamalizwa kiaina tu bila kuwa na hatua zozote za kinidhamu.
Hili likazua mtafaruku kati ya mwenyekiti BAVICHA na Makamu wake. Ilishangaza sana kuona hata pale makamu mwenyekiti alipoonekana wazi kushindwa kumudu nafasi yake, kutoa matamako kwa kutumwa na kukiingiza chama katika mtafarauku, Chadema wamekaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea.

Mlolongo wote huo umezidi kujenga kundi la 'uasi' na kulipa nguvu zaidi.
Ukifuatilia kwa undani, mara baada ya mtafaruku wa Wabunge kule Kigoma kumekuwa na jitihada za kumsafisha kiongozi mwenye tuhuma. Hapa ndipo Tuntemeke na kundi lake wanapoingia kwa madai yanayokiyumbisha chama.

Tatizo la Chadema ni lile lile la CCM, la kutotaka kuudhi baadhi ya viongozi. Nasikitika kusema utayari wa kusimamia misingi, kanuni na sheria za chama hautoi mwanga wa matumaini nje ya yale tuliyoyazoea kwa miaka 50.

Kwa mwendo wa Chadema wa sasa, miaka 2 ijayo ni mingi sana kushuhudia anguko lake.
Haya yote yanafanyika kwa kukusudia kwasababu haiwezekani Chadema wafanye uchunguzi wakuitikisa serikali washindwe kujua nani anakigawa chama na kwanini. Haiwezekani!

Kinachotokea ni Chadema kujenga utamaduni wa chama cha viongozi na si taasisi ya kisiasa.
Mwaka 2010 tuliwahi kuwaambia Chadema, ni lazima chama kiwe taasisi na siyo one man show!

Chadema sasa hivi ni chama kinachojiandaa kutwaa dola. Tumeona hazina kubwa sana ya viongozi, wengine wakifanya kazi wenyewe na kwa mapenzi yao. Nilishangaa kuona Iringa kijijini kuna watu wanajenga ofisi za chama kwa jitihada zao.
Hawa ndio wakombozi wa kweli, na inatia shaka pale ambapo Chadema inadhani mtu au watu fulani ni bora zaidi kuliko umma wa Watanzania unaowaubiri kwa ukombozi.

Hali ilipo ni tete sana, pengine washabiki, wanachama na manazi hawtapenda kusikia haya. Kwasisi tunaokusudia kuisadia nchi bila kujali itikadi zetu tunasima na kusema wazi hali ni tete.

Sijui wataanzaje kumtaka Tuntemeke athibitishe au achukuliwe hatu huku Juliana wa BAVICHA akiwa salama! huo ni mfano tu lakini yapo mengi yatayowakwaza katika maamuzi kwasababu ya kushindwa kusimamia misingi, kanuni na sheria kuanzia mwazO.

Ni kwa muktadha huo Chadema inapita katika kipindi kigumu sana, wasioitakia CDM mema sasa wamekaa mkao wa kusambaratisha.Ukweli na usemwe!
 
Mkuu umeandika maneno mazito sana.Naamini Dr Slaa na Mbowe wanaona maneno haya mazito na ushauri ulioenda shule.
 
TUNTEMEKE kumbe yuko ivoooooo eeeeeh aseee REST IN PEACE JAMAAANGU
 
Hivi wakati Slaa alivyo wataja mafisadi alikua na nia ya kuharibia serikali au alikua anatuonyesha waovu yanayo fanyika? Sasa tuntemeke kututoa maovu ya CDM imekua kosa.

kukosoa sio kosa, ila inategemea unafanya ukosoaji huo kwa mtindo upi. nafikiri mtoa mada ameweka wazi njia sahihi za kidemokrasia za mwanachama kutumia pale anpoona kuwa wenzie wanavuruga na sio kwenda kuropokaropoka in public alafu at the same tym ati wewe ni member wa chama. huko ni kung'ata na kupuliza; haijengi ila inabomoa.

Slaa anapoponda ufisadi unaofanyika na serikali kwa umma, kumbuka yeye siyo sehemu ya serikali, yeye ni mpinzani, so it is very ryt kwa yeye kufanya hivyo. mdau usichanganye habari, Tuntemeke ni sumu, that's just too obvious.

chama kinapokuwa na vijikundi visivyo rasmi kama hivi tutarudi kulekule.....
 
Asante mkuu kwa bandiko lako zuri.Limenibariki sana
 
Back
Top Bottom