Dawa ni kuendelea kuwaunga mkono CHADEMA hii italeta heshima na adabu kwa chama tawala

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,824
18,568
Kwanini viongozi wa nchi yetu wanakuwa na dharau kwa wananchi wakati mwingine? Ni kwasababu wanajua hata kama hawafanyi vizuri majukumu yao wataendelea kuwa madarakani tu.

Kwa wenzetu wa nchi zilizoendelea ni nadra kwa chama kukaa madarakani kwa zaidi ya vipindi viwili. Hata chama kikiongoza vizuri kiasi gani baada ya vipindi viwili kitapumzishwa na watapewa wapinzani.

Jambo hili huondoa utendaji mbovu ambao wakati mwingine ni kwasababu ya viongozi kukaa madarakani muda mrefu na kujisahau.

CCM wamejisahau na wamejenga mtandao wa watu flani wasio na hofu ya wananchi. Ili kuleta balance ya mambo, tuwaunge mkono CHADEMA. Nafurahi kwamba taratibu tunaanza tena kurudi kwenye demokrasia kama ilivyokuwa kabla ya uharibifu wa 2015-2021!
 
Hakuna kipindi ambacho ccm imechapa kazi na kutekeleza ilani za chama kama awamu hii ya sita.
Mashule ✔
Hospitali

Maendeleo kwa ujumla ✔
 
Back
Top Bottom