CHADEMA pelekeni taarifa kwa Spika mubashara, mmeilinda vyema heshima ya chama chenu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mimi si mwanachama wa CHADEMA. Ni mwanachama wa CCM tangu miaka ya 80 nilipohitimu Chuo Kikuu. Tangu kumaliza utumishi wangu ndani ya Serikali na chama, nimebakia kuwa mwanachama mtiifu wa chama changu-nikishirikishwa mipango mbalimbali ya kichama na kiserikali katika kushauri na kuitekeleza kupitia vijana wetu chamani. Nimekuwa wakati wote mfuata utaratibu na kuwa na nidhamu kwa CCM yangu ingawa huusema ukweli.

Chama ni kikubwa kuliko mtu au watu fulani. Hakuna awaye yeyote, mwanachama wa CCM au chama kingine cha siasa, ambaye ni mkubwa kuliko chama. Mtu huwa na nguvu ya kuongea na kutenda kupitia chama, nje ya chama chake mtu huyo si kitu. Katika muktadha huo, kila mwanachama wa chama huulinda UANACHAMA wake kwa nguvu kubwa. Huulinda kwa kuwa na nidhamu-hata iliyochanganyika na woga; hekima, utii na busara. Masikio huwa hayakizidi kichwa!

Nikiwa huku Kigoma, nimefuatilia Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA uliofanyika Mlimani City huko Dar es Salaam. Nilizifuatilia ajenda zake lakini kubwa ni kuwahusu akina-Halima Mdee na wenzake 18. Baraza Kuu limeridhia kufukuzwa kwao uanachama wa CHADEMA na Kamati Kuu ya chama hicho. Yaani, Baraza Kuu limetupilia mbali rufaa za yeyote kati yao ambaye alipinga uamuzi wa Kamati Kuu. Sasa wamefukuzwa na Mamlaka ya juu kabisa ya CHADEMA.

Kama mwanasiasa mbobevu na mpenda demokrasia, uamuzi juu ya akina Halima Mdee NIMEUFURAHIA na NAUPONGEZA. Sababu yangu ni ujumbe unaobebwa na uamuzi huo: nidhamu kwanza, umaarufu baadaye. Wahusika walipaswa kujishusha kabla ya jana. Kusimama katika ubatili na kuutetea kumewaponza. Sasa wamevuna walichopanda. Watetezi wao Serikalini na Bungeni hawapo na hawawezi kuwasaidia tena. Heshima na nidhamu ni vitu vya bure. Hakuna mkubwa kuliko chama chake!

Nawashauri CHADEMA, siku watakayopeleka taarifa ya kufukuzwa uanachama kwa akina Halima Mdee, walifanye jambo hilo mubashara. Hatutaki tena kumsikia Spika au Katibu wa Bunge akikana kupokea barua ya CHADEMA. Hatutaki kuona tena jambo hili linaendelea. Taarifa ipelekwe Bungeni; Spika awaondoe akina Halima Mdee Bungeni halafu CHADEMA waamue kupeleka Wabunge wengine wa viti maalum au la.

Royal Tour!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Ujiji, Kigoma)
 
Nawashauri CHADEMA, siku watakayopeleka taarifa ya kufukuzwa uanachama kwa akina Halima Mdee, walifanye jambo hilo mubashara. Hatutaki tena kumsikia Spika au Katibu wa Bunge akikana kupokea barua ya CHADEMA.
Ushauri kuntu
 
Ni uamuzi sahihi, wasingewafukuza wangekigawa Chama na hata malalamiko yao ya awali kwamba Spika wa Bunge ndiye aliyekuwa akiwalinda yangekuwa batili, Mimi nilitegemea hili kutokea, isitoshe hawa wakata Rufaa walizidisha sana mbwembwe kiasi kwamba hadi ilikuwa kero.

Lakini pia wanatakiwa waweke wazi ni nani aliyeteua hayo majina yao ili wakiwakilishe Chama? Vinginevyo nawakaribisha huku Umoja Party, karibuni tukijenge Chama.
 
nidhamu kwanza, umaarufu baadaye. Wahusika walipaswa kujishusha kabla ya jana. Kusimama katika ubatili na kuutetea kumewaponza.
Yes, Wote tulitegemea baada tu ya kamati kuu kuwafuta wangeachie Ubunge wao feki fasta na kuwa watiifu kwa chama huku wakisubiri rufaa zao, lakini ikawa tofauti wakawa na kiburi chao na kuendelea kuwa bungeni huku wakijua fika wao hawana uwakilishi wa chama chochote.

Kwa kweli hamna namna, siku 40 zishafika - cha msingi waanze maisha ya kisiasa.
 
Asante mkuu. Mimi siyo mshabiki wa chadema au CCM. ila napenda siasa za ushindani wa mawazo mbadala. ukiangalia siasa zetu za CCM zimetudumaza kimawazo na hata kimaendeleo kwa sababu hakuna uwajibikaji.

Ukiwa na upinzani imara (siyo lazima uwe madarakani) inasaidia kuwa na mawazo mbadala yenye tija kwa taifa.
 
Back
Top Bottom