CHADEMA kutoa uamuzi wa maamuzi ya Mahakama Jumamosi NMC Arusha

...mahakama ya wananchi inafaa zaidi. Umaarufu wa chama unazidi kupaa. Kwenda tena mahakamani ni kupoteza muda na nafasi ambayo imetolewa kuwapiga msasa wananchi kwa vitendo. Kama ingekuwa shule, basi hoi ni "remidial class.
Umaarufu wa chama utaendelea kwa sababu M4C imezinduliwa Arumeru ili itekelezwe. Wakati rufaa inaendelea wananchi watamchangia Lema kupitia M4C ili aendelee kuwatumikia wananchi na wakati huo huo kukiongezea chama umaarufu zaidi na kukiimarisha. Hukumu hiyo ya kosa la kutunga na lisilokuwepo itatengeliwa na mahakama ya rufaa kama wakiona umuhimu wa kulinda hadhi ya mahakama kuu na ya rufaa na muhilimili wa mahakama kwa ujumla.
 
Hii serikali ni ya ovyo sana! Ngoja ije katiba mpya; 2015 ccm itashindwa hata kuwa chama kikuu cha upinzani!!!!!
 
Kwanza heading yako haijakaa vizuri. Hakuna kosa kwa chama chochote (except CCM) au mtu wa kada yoyote kutawala AR. Tatizo ni ufisadi wa CCM wanaofanya kupitia AR. CDM or any contestant out of CCM inawakosesha mianya ya kuwanyonya wanaAR.
 
Huu ni upotoshaji wa magamba, kajipange upya CDM hawapotoshwi, rufaa ipo kwa wananchi, kwa unafikiri tumesahau porojo za Mahakama kuhusu mgombea binafsi aliyoshinda Mch. Mtikila na mahakama ya rufaa kusema ikatungwe sheria ya kurusu mgombea binafsi, badala ya kutafsiri iliyopo inasemaje. Hiyo ndio ilikuwa kazi ya mahakama ya rufaa!!!!!. Rufaa ipo kwa wananchi uelewe hilo, na si kesi ya ngedere umpelekee nyani
 
Ikumbukwe kuwa msingi mzima wa kesi ni kuwa Lema alimdhalilisha Batilda Burian katika mojawapo ya mikutano ya kampeni. Kwamba, kuna maneno aliyasema ambayo yalikuwa ni ya udhalilishaji. Sasa hilo ni jambo linalowezakujadiliwa. Wale ambao mmesikiliza hukumu maswali yafuatayo yamejibiwa vipi. Binafsi sijaweza kuchukua msimamo wa hukumu yenyewe bila kuisoma vizuri na kuelewa reasoning ya jaji:

a. Mahakama imejuaje kuwa Batilda alidhalilishwa? - Bila kumuuliza yeye wanajuaej kuwa alijisikia kudhalilika. Vipi kama aliona ni ujinga tu wala haikumdhalilisha? Hivi mtu mwingine anaweza kwenda kusema "x ameibiwa" wakati yule ambaye anadaiwa kuibiwa anaona kila kitu chake kipo salama?

b. Imethibitishwa nini kuhusu alichosema Lema ambacho ni cha udhalilishaji? Alisema maneno gani, lini na wapi na ni ushahidi gani kuwa aliyasema hayo? Kwa mfano watu watatu wakija na walikuwepo kwenye mkutano wakasema hawakusikia maneno hayo na watu wengine watatu ambao walikuwepo kwenye mkutano huo wakasema walimsikia mahakama inaamua vipi kuwa hao watu watatu wanaosema walisikia wanasema kweli?

c. Binafsi kwa kweli sijashtushwa sana na Lema kuvuliwa ubunge - kama kuna ushahidi wa kutosha sidhani kama mahakam ailikuwa na uchaguzi mwingine- kilichonishtua zaidi na kinachonisumbua ni kuwa inaonekana hukumu ilishajulikana mapema zaidi almost a week kabla. Hili ni geni sana kwenye mahakama zetu. What happened?

Mwanakijiji umenielewa vema sana. Hukumu hii haikubaliki na kuweza kuingizwa katika vitabu vya sheria. Njia ya kuifuta ni kukata rufaa. Sidhani kama mahakama ya rufaa itakubali kutumika namna hii kwa kosa la kutunga na lisiloweza kumvua ubunge, kama huyo jaji alivyotumika.
 
mimi siwashauri CHADEMA kuta rufaa mahakamani bali kwa wananchi kwa kuomba tena kura
na kuthibitiishakua lema ndo mbunge halali wa arusha mjini panoja na wao kumvua.
Labda tu hapa kiuzalendo nitakosolewa juu ya garama haswa fedha nyingi zitakazo tumika
katika kurudia uchaguzi huu na muda mwingi wa kufanya maendeleo unaopotea katika siasa.
Vinginevyo naamini kwa zaidi ya asilimia 90 kua ukirudiwa uchaguzi hata sasa hivi, chadema sio tu tunashinda bali tunashinda kwa kuwaacha ccm gape kubwa sana.
 
WanaJF,

Niko Iringa, poleni na mshtuko mdogo kuhusu ubunge wa Mh. Lema kutenguliwa. Ninachofurahi ni kwamba ndani ya dk kama 30, baada ya hukumu kutolewa, nilipata taarifa haraka kutoka karibu kila kona ya nchi hii, Kigoma - Dsm; Mtwara - Arusha, Kagera n.k. Hakika utandawazi wa habari ni muhimu katika mambo kama haya!

Kazini jana, kazi hazikuendelea. Na hapo ndipo nilipopata swali hili: "Aliyetoa uamuzi kesi ya Lema ni mwanaCHADEMA?

Nina uhakika kila mahali kulitokea majadiliano na mabishano makubwa kuhusu uamuzi huu. Iringa, tukiwa na kada maarufu wa CCM Iringa, kanda ambaye mara nyingi huonyesha ujasiri katika matukio ya kisiasa, jana ilikuwa mara yangu ya kwanza kumsikia akisema wazi kwamba uamuzi uliyofanyika ni hatari. Hata nilipomuuliza vizuri kwa nini ni hatari, alitaja sababu zifuatazo:
  1. Mkoa wa Arusha ni ngome kubwa sana ya upinzani, hasa mapenzi makubwa yako kwa CHADEMA.
  2. Wiki haijaisha tangu Arumeru ichukuliwe na CHADEMA (1/4/2012) baada ya uchaguzi mdogo, kufuatia kifo cha Mh. Jeremia Sumari, hukumu tarehe 5/4/12.
  3. Kutokana na mwenendo wa kisiasa Arusha, maamuzi hayo yanawatia pressure kubwa sana jeshi la polisi.
  4. Mwamuzi ameamua kuwatia pressure CCM, kwani pia iko wazi kabisa hapajawepo muafaka wa uongozi wa manispaa kutokana na mvutano wa CHADEMA na CCM kuhusu meya wa manispaa.

Sasa, nimependa nilete mada hii kwenu wanaJF mtoe mawazo yenu. Ninachojua mimi, katika saikolojia ya mtu, hata kama mahakama ni muhimili huru unaojitegemea, ndani ya mtu, katika matendo kusudifu, huwezi kujua anawaza nini. Inawezekana mwamuzi wa kesi hii anajua namna gani wanaCCM walivyo sasa, hivyo akaamua kweli kuwatia pressure zaidi, la, inawezekana sheria imefanya kazi yake.

Kwa mawazo ya kada huyu wa CCM Iringa, anasema suala la Lema, na hali halisi ya kisiasa Arusha, wadau zaidi ya mahakama zingekutana kufanya maamuzi ya busara, hata baada ya mieizi sita kutoa hukumu tangu uchaguzi wa Arumeru kufanyika, ili kuondoa pressure ya CCM kuanguka. Pia, kungekuwepo mashauriano yanayolenga kuleta sura nzuri kuhusu hukumu ya Lema kwani kwa uchaguzi wa Arumeru ghaph ya CCM katika duru za kisiasa nchini imeshuka sana, ikiwa imeshusha zaidi wasifu wa Mh. Mkapa nchini.

Simtetei Mkapa, mwamuzi wa kesi, wala siisifu CHADEMA, tunataka kujenga maantiki ya mwenendo wa mambo ya kisiasa nchini kwa kuangalia matukio haya. Nguvu ya asili (natural forces) ya mienendo ya mambo mengi huhusisha kuzaliwa, kukua, na kufa. Yawezekana CCM inakufa kwani ilizaliwa ikakua. Yamkini, CHADEMA inakua, na hii itasaidiwa na matukio mengi ya kufa kwa CCM.

Mawazo yenu tafadhali.

Perecy Ugula,
MwanJF Mchanga,
Iringa
Niandikie: ugulapp@yahoo.co.uk
Nipigie: +255 766 082388
 
Hadhi ya mahakama miongoni mwa watu makini Tanzania iliisha pale ilipokubali kutumiwa katika suala la kuruhusu mgombea binafsi. Tanzania hakuna mahakama huru tena (hata Jaji Mkuu kasema hilo) na heshima yake imekwenda na maji. Kila mtu anajua rushwa ilivyoota mizizi na kushamiri mahakamani na uhuru wake unavyoingiliwa na serikali. Hivyo pamoja na faida zote za kukata rufaa, kwa hili, hapana. Rufaa bora ni kwa wananchi.
Nimekuelewa, katika suala la demokrasia, ambalo wananchi wanachagua halafu jaji anabadilisha maamuzi ya wengi, hili ni suala la kujiridhisha mahakama ya rufaa. Nakwambia kama mahakama ya rufaa haitatengua maamuzi ya huyo jaji, M4C itaishukia mahakama. Nguvu ya wananchi itaishikisha adabu mahakama. Chadema na Lema wakate rufaa ili tuimukike mahakamu ya rufaa pia na muhimili mzima wa mahakama
 
Mwanakijiji umenielewa vema sana. Hukumu hii haikubaliki na kuweza kuingizwa katika vitabu vya sheria. Njia ya kuifuta ni kukata rufaa. Sidhani kama mahakama ya rufaa itakubali kutumika namna hii kwa kosa la kutunga na lisiloweza kumvua ubunge, kama huyo jaji alivyotumika.

Mkuu Atigi. Mimi ndiyo sijakuelewa. Kwa sasa hivi wengi wetu tunafikiria namna na njia ya kulirudisha
mikononi mwa Chadema jimbo la Arusha mjini. Wewe umejikita zaidi kwenye maswala ya mahakama na integrity yake. Au una ajenda ingine isiyoonekana waziwazi?
 
yani huyo jaji wa magamba ataisoma! kwani kabala ajatulia jimbo limerudi!
 
Hakuna ubishi kuwa hukumu ile ina madhaifu kisheria na Lema akikata rufaa atashinda ila hukumu hiyo itabatilishwa 2014!. Time consuming for nothing!.

Baadhi ya lugha zinazodaiwa ni za udhalilishaji are facts na zina fall kwenye sheria za madai na sio jinai!.

Mfano mtu akiwa tipwa tipwa ukamuita 'wee tipwa tipwa' ana haki ya kulalamika kuwa amedhalilishwa but its a fact!.

Its a fact kuwa Batilda ni mwanamke na hakuna Lwaigwanan wa kike!.

Its fact Batilda kama mwanamke aliyeolewa kwa ndoa na ana mahusiano yasiyo ya kawaida nje ya ndoa huitwa ma..ya!.

Labda pia its a fact ile mimba ilikuwa sio ya mumewe bali ya yule Mzee wangu!.

Tuisubirie nakala ya hukumu ili tuichambue logic ya jaji katika kufikia maamuzi ila vyovyote iwavyo rufaa wasikate unless kwa kutoka rufaa kutamfanya Lema ame kubali kosa ambalo litatumiwa kama msingi wa kumwekea pingamizi!.

Wito wangu kwa Chadema, chonde chonde msije kunfanyia Lema kile mlicho mfanyia Mwera kule Tarime mkaishia kuitoa Tarime kama sadaka kwa sadakalawe!.
Pasco nawe unaionea huruma Chadema? Mimi sioni kama kuna kupoteza muda. Nimeeleza vema namna Chadema na Lema watakavyoendelea na kazi za M4C wakati rufaa inaendelea. Kushinda rufaa kwa Lema ni ushindi wa wananchi wote maana hatuwezi kama nchi kuruhusi sheria za ovyoovyo kuingia kwenye vitabu vya sheria. Ikumbukwe kuwa hukumu za ovyo kama hizi zikiachwa bila kukatiwa rufaa zinaingizwa kwenye vitabu vya sheria.
 
maamuzi magumu n makini huwa yanafanywa na chadema tu, kwa kuwa ndiyo yenye watu makini
 
kumhusisha Mwalimu katika mijadala yetu haitasaidia na si busara! ila magamba watatambua!
 
WanaJF, Katika pitia pitia hotuba za Mwalimu JK Nyerere nimekutana na hii hotuba yake aliyoitoa katika mkutano mkuu wa kumchagua mgombea wa chama cha mapinduzi, 1995. Sikilizeni ni hotuba yenye kushiba mambo yanatoa vuguvugu la kutaka kututenganisha watanzania. Karibuni katika mjadala!!
Mwalimu Nyerere Mkutano Mkuu 1995
 
Mkuu Atigi. Mimi ndiyo sijakuelewa. Kwa sasa hivi wengi wetu tunafikiria namna na njia ya kulirudisha
mikononi mwa Chadema jimbo la Arusha mjini. Wewe umejikita zaidi kwenye maswala ya mahakama na integrity yake. Au una ajenda ingine isiyoonekana waziwazi?
Kukata rufaa kuna sababu nyingi na za msingi. Na kama mahakama itaona aibu na kurudisha hadhi yake Lema atarudishiwa ubunge wake. Soma kwa makini sababu nilizoandika za kukata rufaa
 
kuna watu wametumwa kupima upepo hapa.gambaz hao.uchaguzi urudiwe na hakuna kukata rufaa ili aibu yao iwe juu yao na watoto wao.
Dogo, soma sababu nilizoeleza utaelewa vema. Hukumu hii haikubaliki bika kukatiwa rufaa.
 
Kaka endapo CCM watamteua Millya kama kawaida yao yataibuka makundi ndani ya chama na hapo Chadema watapeta!Hata hivyo kwa sisi tuliopo Arusha mjini tunaiona hali ya siasa ndani ya mji huu.CCM watavuna aibu nyingine ya mwaka! Kwa ushauri wangu wtakaoumia ni sisi walala hoi kwa sababu CCM watatumia dola kutafuta ushindi hivyo tutarajie mauaji pamoja na vijana kuwekwa ndani (mahabusu) na kujaa vituo vya polisi.Naomba ni "dikree" interest mimi ni NEUTRAL.
 
Back
Top Bottom