Mahakama kutoa uamuzi wa Kesi ya Halima Mdee na wenzake Desemba 14

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,718
218,266
Screenshot_2023-10-24-17-23-11-1.png
Wakati baadhi ya Walalamikaji hao wameanza kuvaa sare za ccm , huku wengine wakihutubia kwenye Majukwaa ya CCM, imetangazwa kwamba hukumu ya kesi yao dhidi ya Chadema itatolewa Desemba 14 2023.

Ikumbukwe kwamba Halima Mdee na wenzake , akiwemo Dada yangu Sophia Mwakagenda walifungua kesi kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema.

===============

Hatma ya Mdee na wenzake 18 kujulikana Desemba 14, 2023

Desemba 14, 2023 saa nane na nusu mchana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepanga kutoa hukumu ya kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Halima Mdee na wenzake 19 ambao walifutwa uanachama katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Uamuzi huo umetolewa Oktoba 24, 2023 na Jaji Cyprian Mkeha wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kupangiwa hukumu.

Wakili wa upande wa wajibu maombi, Wakili Deogratias Mahinyira kwa niaba ya wenzake amesema Hukumu ya kesi hiyo imepangwa kutolewa ikiwa ni baada ya pande zote kukamilisha mawasilisho kama ilivyoelekezwa na Mahakama.

"Shauri leo lilikuwa linakuja kwa ajili maelekezo ya Mahakama (necessary orders), kwa sababu tarehe ya mwisho Mahakama ilikuwa imeeleza baada ya shauri kusikilizwa kwamba leo tuje Mahakama ijiridhishe kama pande zote zimeweza kufanya mawasilisho yake ya mwisho ili Mahakama iweze kupanga tarehe ya uamuzi," amesema Wakili Deogratias Mahinyira.

Halima Mdee ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na wenzake 18 walifungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama, kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review).

Kesi hiyo ilifunguliwa ikiwa ni muda mfupi baada ya Baraza Kuu la Chadema kuunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho wa kuwafukuza uanachama.

Ikumbukwe Juni 2022 Mahakama Kuu Dar es Salaam ilitupilia mbali maombi ya Halima Mdee na wenzake kutokana na kuwepo kwa kasoro kuhusu jina la mjibu maombi wa kwanza, lakini walifungua shauri ambalo linatarajiwa kutolewa hukumu.

Itakumbukwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson alisema hawezi kutangaza kuwa nafasi za Wabunge hao wa Viti Maalum zipo wazi kabla ya taratibu za Kimahakama kukamilika.
 
View attachment 2791423

Wakati baadhi ya Walalamikaji hao wameanza kuvaa sare za ccm , huku wengine wakihutubia kwenye Majukwaa ya ccm , imetangazwa kwamba hukumu ya kesi yao dhidi ya Chadema itatolewa Desemba 14 2023.

Ikumbukwe kwamba Halima Mdee na wenzake , akiwemo Dada yangu Sophia Mwakagenda walifungua kesi kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema .
Heri wahamie CCM wakachukue nafasi za miccm isiyo na akili hata kijiko, SEMA wakifika huko nako wataacha akili Tena watatumia za CCM
 
View attachment 2791423

Wakati baadhi ya Walalamikaji hao wameanza kuvaa sare za ccm , huku wengine wakihutubia kwenye Majukwaa ya ccm , imetangazwa kwamba hukumu ya kesi yao dhidi ya Chadema itatolewa Desemba 14 2023...
Mahakama ilisema hukumu yao ni mwezi huu wa 10, lakini hukumu Bado Hadi sasa. Hapo wanacheza na muda tu.
 
View attachment 2791423

Wakati baadhi ya Walalamikaji hao wameanza kuvaa sare za ccm , huku wengine wakihutubia kwenye Majukwaa ya ccm , imetangazwa kwamba hukumu ya kesi yao dhidi ya Chadema itatolewa Desemba 14 2023.

Ikumbukwe kwamba Halima Mdee na wenzake , akiwemo Dada yangu Sophia Mwakagenda walifungua kesi kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema .
Maadam maridhiano yamekufa then Chadema haiwezi kushinda kesi. Mahakama zetu zinapewa maelekezo na Rais so mood yake ndio inaamua kesi ikaaje.
 
Yaani hicho kipindi ni cha maandalizi kuelekea uchaguzi mkuu. Hiyo hukumu ni non sense haina impact kwa chadema kama mahakama itaamua ni kweli walikiuka ubunge wao kutoka kwenye chama chao. Fasta watakubaliana na hukumu hiyo ya kuvuliwa uanachama wa chadema na wengi watajiunga ccm kisha kupatiwa majimbo ya kugombea au kupata teuzi zingine ndani ya serikali ya ccm na maisha yao ya kisiasa yakaendelea
 
Bora iwe hivyo ili wakaendelee na siasa za kizandiki.
 
Bora iwe hivyo ili wakaendelee na siasa za kizandiki.
Mwanachama kama halima mdee yule ni likely atakuwa product ya ccm na aweza akatafutiwa jimbo kama gwajima hatampisha kawe. Kuna kuna bulaya na matiko zile nazo ni asset za ccm typically hazitakaa bure bila kufanya kazi ya za siasa. Wakikosa ubunge watalambishwa hata ukuu wa watalambishwa
 
Wakati baadhi ya Walalamikaji hao wameanza kuvaa sare za ccm , huku wengine wakihutubia kwenye Majukwaa ya CCM, imetangazwa kwamba hukumu ya kesi yao dhidi ya Chadema itatolewa Desemba 14 2023.

Ikumbukwe kwamba Halima Mdee na wenzake , akiwemo Dada yangu Sophia Mwakagenda walifungua kesi kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema .
Rest assured mheshimiwa jaji atakuwa mgonjwa hiyo siku, itahirishwa mpaka february mwaka wa kimahakama.
Hawa ni wabunge wa CCM na ni wahujumu uchumi kwakuwa wanaigiza kuwa CHADEMA.
Nijuacho mimi hawa wanakula mamilioni ya fedha zinazolipwa na walemavu kama kodi, zinazolipwa na vipofu, albino na maskini huku wao wakisafiri na fist class kwenda kuuza nchi huko DP.

Watasomesha watoto FEZA na Hopc, watasomesha IST na ulaya lakini nakuhakikishieni nlaana hii itawafuta wao na vizazi vyao.
Mungu hawezi achia hili jambo eti siasa, watalipa tu.
 
Back
Top Bottom