Maundumula
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 7,553
- 3,070
Chadema kutoa maamuzi au kutoa tamko?
Maamuzi yametolewa na mahakama!
Maamuzi yametolewa na mahakama!
Mkutano gani!
Unachosema ni kweli, lakini kwa suala la hukumu hii juu ya Lema haifai kuwa sehemu ya kumbukumbu za sheria za nchi hii. Ninaimani kwa suala hili mahakama ya rufaa itakataa kutumiwa na CCM, na serikali yake na hivyo majaji wataona aibu na kumrudishia Lema Ubunge wake.Uhuru wa mahakama ni rahisi kuutamka kwa nadharia kuliko Kutenda. Kama kuna mtu atafanya utafiti juu ya uteuzi wa Majaji sina Shaka hatashangaa juu ya vigezo vinavyotumika kuwateua waheshimiwa hawa. Jibu la chagamoto hii ni Kwenye katiba mpya.
Kwa mujibu wa M Kiti wa CDM Mhe Freman Mbowe, CDM itatoa kauli rasmi jumamosi hii, kama kitakata rufaa au kitakubali maamuzi ya mahakama. Hii inatokana na kwamba kukubali uamuzi wa mahakama kunaweza kutafsiriwa kama uamuzi huo uko sahihi kabisa. Mhe amesama wanaheshimu taratibu za mahakama, lakini wamepokea uamuzi huo kwa mshituko mkubwa. Ili kuonyesha ulimwengu kwamba hawakutendewa haki basi wanaweza kuamua kukata rufaa. Aliongeza kwamba hawaogopi uchaguzi lakini haki lazima iheshimiwe.
Dr Bana amesema kuna uwezekano mkubwa sana wa CDM kulirudisha jimbo hilo kwa sabau ni ngome kubwa ya CDM
(Mahojiano Redio ya Ujermani leo saa 12)
Soma pendekezo la Mwana JF (Atigi) hapa chini: