CHADEMA kutoa uamuzi wa maamuzi ya Mahakama Jumamosi NMC Arusha

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
3,153
697
Kwa mujibu wa M Kiti wa CDM Mhe Freman Mbowe, CDM itatoa kauli rasmi jumamosi hii, kama kitakata rufaa au kitakubali maamuzi ya mahakama. Hii inatokana na kwamba kukubali uamuzi wa mahakama kunaweza kutafsiriwa kama uamuzi huo uko sahihi kabisa. Mhe amesama wanaheshimu taratibu za mahakama, lakini wamepokea uamuzi huo kwa mshituko mkubwa. Ili kuonyesha ulimwengu kwamba hawakutendewa haki basi wanaweza kuamua kukata rufaa. Aliongeza kwamba hawaogopi uchaguzi lakini haki lazima iheshimiwe.

Dr Bana amesema kuna uwezekano mkubwa sana wa CDM kulirudisha jimbo hilo kwa sabau ni ngome kubwa ya CDM

(Mahojiano Redio ya Ujermani leo saa 12)

Soma pendekezo la Mwana JF (Atigi) hapa chini:
Hukumu iliyotolewa ya kumvua ubunge Mh. Lema haikutarajiwa kwa kuzingatia mwenendo wa kesi. Katika hali hii ni lazima Chadema kwa kushirikiana la Lema wakate rufaa kupinga hukumu hii. Sababu za kupinga hukumu ni kubwa kiasi kwamba Lema kwa kusaidiwa na Chadema lazima wakate rufaa

Haki haikutendeka

Hukumu ya kumvua Ubunge Lema siyo ya haki kwa kuzingatia mwenendo wa kesi. Hakuna ushahidi iliotolewa ambao haukuacha shaka yoyote kuwa Lema alitenda kosa la kumtukana Batilda. Na hata kama ushahidi usingeacha shaka yoyote hicho kinachoitwa tusi si kosa la kumvua ubunge Lema. Mwanasiasa yoyote anayegombea inabidi mwenendo wake wa maisha uhojiwe li kuona kama anaweza kushika madaraka ya kisiasa. Hata kama ushahidi mzito ungeonyesha kuwa Lema alidodosa maisha ya mgombea, hiyo haiwezi kuwa kosa la kumvua Ubunge. Wote tunatambua namna maisha ya wagombea wa Chadema yanavyohojiwa wakati wa chaguzi Mbalimbali, za ubunge na uraisi. Na hii ni haki kwa wananchi kujua, siyo kosa. Pamoja na mapungufu ya kutungwa kwa kosa, pia hakuna uthibitisho wa nguvu wa hicho kinachoitwa kosa kuwa Lema alikifanya. Ni ushahidi wa kutunga wa maneno, hakuna ushahidi wa maandishi wala sauti katika mkanda wala CD kuwa Lema alitoa matamshi yaliyotungiwa mashitaka

Kutekeleza M4C (Movement for change)- Vuguvugu la mabadiliko
Chadema lazima kielekeze vuguvugu la mabadiliko la M4C lililozinduliwa huko Arumeru katika maeneo yote. Kwa wananchi, kwa wabunge, kwa wana-CCM na katika mhimili wa Mahakama. Kwa sasa, Chadema kimpatie Lema kazi ya kutekeleza mikakati ya M4C wakati rufaa ya kupinga hukumu imekatwa. Lema hatakosa kazi ya kufanya katika chama wakati kesi ya rufaa inaendelea au wakati wa kusubiri kupangiwa kesi. Lema hana cha kupoteza kwa kukata rufaa kwa sababu tangu alipoamua kujiunga na Chadema alijiunga siyo kwa ajili ya kutafuta ufahari au mali bali kusaidia kuondoa ukandamizaji wa CCM. Ndiyo maana alikubali kukaa mahabusu ili kupinga ukandamizaji wa Polisi. Watanzania wote wanaojiunga na Chadema wanachagua kutetea wananchi, wanamapenzi na nchi yao na hawakimbiliii mali, wanaokimbilia mali za kifisadi hujiunga na CCM. Wanaojiunga na Chadema ni watu ambao wameweka rehani hata maisha yao wenyewe kwa ajili ya kuitetea na kuilinda nchi yao dhidi ya ufisadi na dhuluma ya CCM na serikali yake.

Kutathmini mhimili wa Mahakama
Kwa kukata rufaa Chadema kitaweza kutathmini mwenendo wa mhimili wa mahakama. Tunataka kujua kama jaji Gabriel Rwakibarila aliyetoa hukumu ametumiwa na CCM na serikali yake kama yeye binafsi au imehusisha mtandao wa majaji wengine katika mhimili wa mahakama. Tunajua kuwa kuna wanasheria ambao wamekuwa wakitumiwa na wanasiasa mafisadi kuhujumu uchumi wa nchi kwa kusaini mikataba ya kifisadi. Mikataba yote ya kifisadi imehusisha wanasheria wasiokuwa na uchungu na nchi yetu. Tumejua kwa mwenendo wa kesi ulivyokuwa kwamba jaji huyo ametumika na CCM kutekeleza azima yao. Tunajua jinsi Lema alivyokuwa mwiba bungeni kwa waziri wa mambo ya ndani na pia waziri mkuu pinda na jeshi la polisi. Siyo ajabu kwa CCM na Serikali yake kumtumia huyo jaji ili kumkomoa Lema na Chadema. Kwa Chadema kukata rufaa wananchi tutajiridhisha kama muhimili wa mahakama utalinda hadhi yake kwa kutengua hukumu hiyo isiyo ya haki. Kama itaibariki tutakuwa tumetambua tatizo kwa ujumla wake na kuwatambua kwa majina majaji wanaoshiriki katika kuua demokrasia na hivyo kuwa target ya M4C. Tunaamini kuwa mahakama ya rufaa italinda hadhi yake kwa kutengua humu hiyo isiyo ya haki ili mhimili wa mahakama na taaluma ya sheria visidhalilishwe.

Kutunga sheria zenye hadhi
Kwa kutata rufaa, Chadema na Lema watakuwa wamesaidia wananchi kukataa sheria dhalili. Maana kwa kuiacha hukumu hiyo kama ilivyo, itaingia kwenye kumbukumbu za sheria na hivyo kuwa sehemu ya nukuu katika taaluma ya sheria na katika muhumili wa mahakama. Tunataka Chadema ifanye kwa vitendo kukataa sheria za ovyoovyo na hasa tunapoelekea kutunga katiba mpya.
 
the so called Dr. banna, anajikomba komba kwa jamii kwa mambo yaliyo dhahiri ili kujaribu kujitengenezea credibility, akafie mbali huko, atuache wenyewe.
 
BBC 7:01

Lema amesikitishwa sana, lakini anasema anaweza kuwa mbunge kwa kukata rufaa. Lakini ningependa zaidi kurudi kwa wananchi. Lakini mambo yote Jomamosi (Mbowe)
 
Mh Lema anasema hata kesho uchaguzi ukirudiwa atashinda (VOA 7:30). Alijua kwamba matokeo yatatenguliwa hata kabla ya kuingia mahakamani.
 
Hukumu iliyotolewa ya kumvua ubunge Mh. Lema haikutarajiwa kwa kuzingatia mwenendo wa kesi. Katika hali hii ni lazima Chadema kwa kushirikiana la Lema wakate rufaa kupinga hukumu hii. Sababu za kupinga hukumu ni kubwa kiasi kwamba Lema kwa kusaidiwa na Chadema lazima wakate rufaa

Haki haikutendeka

Hukumu ya kumvua Ubunge Lema siyo ya haki kwa kuzingatia mwenendo wa kesi. Hakuna ushahidi iliotolewa ambao haukuacha shaka yoyote kuwa Lema alitenda kosa la kumtukana Batilda. Na hata kama ushahidi usingeacha shaka yoyote hicho kinachoitwa tusi si kosa la kumvua ubunge Lema. Mwanasiasa yoyote anayegombea inabidi mwenendo wake wa maisha uhojiwe li kuona kama anaweza kushika madaraka ya kisiasa. Hata kama ushahidi mzito ungeonyesha kuwa Lema alidodosa maisha ya mgombea, hiyo haiwezi kuwa kosa la kumvua Ubunge. Wote tunatambua namna maisha ya wagombea wa Chadema yanavyohojiwa wakati wa chaguzi Mbalimbali, za ubunge na uraisi. Na hii ni haki kwa wananchi kujua, siyo kosa. Pamoja na mapungufu ya kutungwa kwa kosa, pia hakuna uthibitisho wa nguvu wa hicho kinachoitwa kosa kuwa Lema alikifanya. Ni ushahidi wa kutunga wa maneno, hakuna ushahidi wa maandishi wala sauti katika mkanda wala CD kuwa Lema alitoa matamshi yaliyotungiwa mashitaka

Kutekeleza M4C (Movement for change)- Vuguvugu la mabadiliko
Chadema lazima kielekeze vuguvugu la mabadiliko la M4C lililozinduliwa huko Arumeru katika maeneo yote. Kwa wananchi, kwa wabunge, kwa wana-CCM na katika mhimili wa Mahakama. Kwa sasa, Chadema kimpatie Lema kazi ya kutekeleza mikakati ya M4C wakati rufaa ya kupinga hukumu imekatwa. Lema hatakosa kazi ya kufanya katika chama wakati kesi ya rufaa inaendelea au wakati wa kusubiri kupangiwa kesi. Lema hana cha kupoteza kwa kukata rufaa kwa sababu tangu alipoamua kujiunga na Chadema alijiunga siyo kwa ajili ya kutafuta ufahari au mali bali kusaidia kuondoa ukandamizaji wa CCM. Ndiyo maana alikubali kukaa mahabusu ili kupinga ukandamizaji wa Polisi. Watanzania wote wanaojiunga na Chadema wanachagua kutetea wananchi, wanamapenzi na nchi yao na hawakimbiliii mali, wanaokimbilia mali za kifisadi hujiunga na CCM. Wanaojiunga na Chadema ni watu ambao wameweka rehani hata maisha yao wenyewe kwa ajili ya kuitetea na kuilinda nchi yao dhidi ya ufisadi na dhuluma ya CCM na serikali yake.

Kutathmini mhimili wa Mahakama
Kwa kukata rufaa Chadema kitaweza kutathmini mwenendo wa mhimili wa mahakama. Tunataka kujua kama jaji Gabriel Rwakibarila aliyetoa hukumu ametumiwa na CCM na serikali yake kama yeye binafsi au imehusisha mtandao wa majaji wengine katika mhimili wa mahakama. Tunajua kuwa kuna wanasheria ambao wamekuwa wakitumiwa na wanasiasa mafisadi kuhujumu uchumi wa nchi kwa kusaini mikataba ya kifisadi. Mikataba yote ya kifisadi imehusisha wanasheria wasiokuwa na uchungu na nchi yetu. Tumejua kwa mwenendo wa kesi ulivyokuwa kwamba jaji huyo ametumika na CCM kutekeleza azima yao. Tunajua jinsi Lema alivyokuwa mwiba bungeni kwa waziri wa mambo ya ndani na pia waziri mkuu pinda na jeshi la polisi. Siyo ajabu kwa CCM na Serikali yake kumtumia huyo jaji ili kumkomoa Lema na Chadema. Kwa Chadema kukata rufaa wananchi tutajiridhisha kama muhimili wa mahakama utalinda hadhi yake kwa kutengua hukumu hiyo isiyo ya haki. Kama itaibariki tutakuwa tumetambua tatizo kwa ujumla wake na kuwatambua kwa majina majaji wanaoshiriki katika kuua demokrasia na hivyo kuwa target ya M4C. Tunaamini kuwa mahakama ya rufaa italinda hadhi yake kwa kutengua humu hiyo isiyo ya haki ili mhimili wa mahakama na taaluma ya sheria visidhalilishwe.

Kutunga sheria zenye hadhi
Kwa kutata rufaa, Chadema na Lema watakuwa wamesaidia wananchi kukataa sheria dhalili. Maana kwa kuiacha hukumu hiyo kama ilivyo, itaingia kwenye kumbukumbu za sheria na hivyo kuwa sehemu ya nukuu katika taaluma ya sheria na katika muhumili wa mahakama. Tunataka Chadema ifanye kwa vitendo kukataa sheria za ovyoovyo na hasa tunapoelekea kutunga katiba mpya.
 
Wakuu,naomba wanaofahamu sheria za uchaguzi wanijuze.Je baada ya Lema kupigwa chini,ataruhusiwa kugombea tena Arusha kwa uchaguzi mdogo?Naomba nijuzwe Tafadhali wakuu
 
Sioni sababu kukata rufaa mahakama zetu tunazijua, leo wanaweza wakakata rufaa wakajifanya wameipokea kazi ikawa dana dana mpaka 2015,, pia wanaweza rufaha ikatolewa mapema lakini Lema akazuiwa kugombea pia.
 
Nimeeleza kuwa kama mahakama ya rufaa itabariki hukumu tutakuwa tumewajua kwa majina majaji wanaotumiwa na CCM na serikali yake, na hata kutumika kwa mahakama kwa ujumla na CCM. Hivyo tatizo litakuwa limeeleweka kwa upana wake. Hata hivyo kuna uwezekano kuwa wataona aibu na kulinda hadhi ya mahakama hivyo kutengua hukumu. Kama watapiga danadana hadi 2015, tutaelewa kuwa mahakama kwa ujumla wake inatumika kisiasa na hivyo itakuwa target ya M4C.
 
Lengo lako nini?
Nimeeleza sababu kwenye post ikiwemo kusahihisha hukumu isiyo ya haki ili mahakama isigeuzwe kuwa kichaka cha wanasiasa na majaji walafi. Naamini viongozi wa Chadema watajadili hukumu hii na kukata rufaa kwa kuzingatia maelezo niliyoyatoa kwenye post.
 
Si walifanya makusudi basi na sisi tufanye makusudi yale yale. Nataka CCMwaje Arusha wahukumiwe na wananchi kwa kuendekeza ujinga wao.
 
Mahakama ni muhimili wa inchi pia acha CDM waueshim na kurudi kwa uma wa A town wafanya hukumu yao,uwezi shinda rufaa.
 
Tuutathimini mwenendo wa mahakama? Hata mtoto mdogo haitaji kufanya utafiti kujua kwamba hukumu iliyotolewa imepikwa! Nafikiri huo muda wa tathmini utafuata baada ya uchaguzi kufanyika na Lema akiwa kesharejea bungeni?
 
Back
Top Bottom