CHADEMA Kuitikisa Nyanda za Juu Kusini; Safari Kuanza kesho

picha za kanda ya ziwa tulizipata swadakta. ila picha za shinyanga kwenye mazishi ya comrade Shilembi haukuzirusha mh. Tafadhali bado tunazisubiri. Many thanks Regia. Aluta...........

Sikuwepo Msibani Kamanda.
 
wakati wao wakienda mbeya wanapopolewa na mawe, sisi (CDMA) tukienda tunapokelewa kama wafalme. ha ha haaaaa....:peace:
 
Chadema juu..................magamba chini sana.........tuko pamoja
 
Wana JF.

Heshima kwa wote.

Ile Ziara ya Maandamano ya Nyanda za Juu Kusini imewadia.Maandalizi yanaendelea vizuri na kesho ndio msafara unaoondoka kwa Convoy kuelekea Mkoani Mbeya.

Maandamano yenyewe yatazinduliwa Mbeya Mjini Siku ya Ijumaa tarehe 6 Mei, tunatarajia kufanya Ziara kwenye Mikoa ya Mbeya,Rukwa,Ruvuma na Iringa respectively.

Mkoa wa Morogoro tumeuondoa kwa sasa kwa kuwa kuna mvua nyingi na sehemu nyingine kuna mafuriko hivyo hatutaweza kufika maeneo yote, Morogoro tutakwenda baada ya Bunge la Bajeti.

Maandamano hayo kuongozwa na Viongozi Wakuu wa Chama. Makamanda Mbowe, Dr Slaa, Zitto na Arfi tukifuatiwa na Wabunge, Watendaji Makao Makuu, Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Majimbo.

Ziara inatarajiwa kuwa ya Siku 12 kila Mkoa ni siku tatu.

Kama kawaida nitajitahidi kuwahabarisha kila kitakachojiri kadiri ya uwezo wangu.
Nitaanza na Msafara wa kesho.

Aluta Continua

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

Mh.Regia,
Safi sana.Nawaomba Makamanda mkumbuke pia kutolea ufafanuzi madudu yaliyoingizwa katika mswaada wa uundwaji wa tume ya kutunga katiba, inavyoonekana wananchi hawajajua manufaa ya kupingwa kwa mswaada huo.Ni vema kwa sasa transparency ikatawala katika masuala ya kitaifa, CDM mnao wajibu wa kuwajulisha watanzania kwani Waziri na mwanasheria mkuu wamekuwa wakimumunya maneno hawasemi ukweli kuwa walikuwa na njama ya kupotosha mchakato.Naomba kuwasilisha.
 
regia Mtema, Mbeya na ukanda wa kusini ni wakuwekeza, kwani wapiga kura wake ni wengi na wanamamko kisiasa
 
Regia Magari mitumba musinunue kabisa nunueni hata moja lakini liwe jipya,mukinunua mitumba mutashwindwa kujitetea kwamba mumeenda kinyume na yale munayootuaminisha

Kitengo chenu cha mawasiliano kiwe live kutoa habari vijana wa Bavicha wanaweza kufanya kazi hiyo ya kutuhabarisha na kutuwekea picha hapa kila la heri mukawasalimie Akina Mbombo ngafu huko Mbeya
 
waambieni watu huko kwamba mnamlipa slaa milioni 15 na mnanunua magari mitumba ya mbowe

Wenzio wanaandika na kusoma magazeti ya uhuru na Mzalendo tu huku umepotea njia hutoshi unatakiwa kuwa mwelewa sana na akili timamu ndipo uwe katika blog hii.

 
naomba mtumie muda mwingi vijijini ili kutoa mwamsho unaotakiwa... wafungueni macho watu wa isimani mpaka ludewa mjini somo lishaeleweka kiasi
 
Wenzio wanaandika na kusoma magazeti ya uhuru na Mzalendo tu huku umepotea njia hutoshi unatakiwa kuwa mwelewa sana na akili timamu ndipo uwe katika blog hii.


Kuna watu ambao competence yao inakuwa hai wanapokuwa kwenye blogs kama global Publishers tu,Mzalendo na uhuru kwenye ishu za magazeti.They just want to hear CCM blah blah,yada yada yada!kazi ipo
 
Tuko pamoja kama samaki na maji au mizizi na ardhi, msisahau kuwa magamba hawajalala, mipango ya kuvuruga na kuchafua agenda ipo! Take care
 
I pray that the Lord will bless and protect you, and that he will show you mercy
and kindness. May the Lord be good to you and give you peace.”
Mwenyezi-Mungu awabariki na kuwalinda; Mwenyezi-Mungu awaangalie kwa wema, na kuwafadhili;Mwenyezi-Mungu awaonyeshe wema wake na kuwapa amani.
 
kama kawaida watu wa Arusha tupo pamoja nanyi siku zote:israel:
 
Waipelekeeeni salamu za ukombozi wa taufa lao, nenndeni kuwatoa dhana kuwa nchi hii bila CCM haiweazekaniki nendeni kawaaambieeni INAWEZEKANA
 
Regia Magari mitumba musinunue kabisa nunueni hata moja lakini liwe jipya,mukinunua mitumba mutashwindwa kujitetea kwamba mumeenda kinyume na yale munayootuaminisha

Kitengo chenu cha mawasiliano kiwe live kutoa habari vijana wa Bavicha wanaweza kufanya kazi hiyo ya kutuhabarisha na kutuwekea picha hapa kila la heri mukawasalimie Akina Mbombo ngafu huko Mbeya

Hahahahaha!!
 
inaonekana haujui maana ya MWANAUME. Ili usirudie uupuuzi, vilevile tafuta maana ya MVULANA.
 
Back
Top Bottom