CHADEMA Kuitikisa Nyanda za Juu Kusini; Safari Kuanza kesho

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Wana JF.

Heshima kwa wote.

Ile Ziara ya Maandamano ya Nyanda za Juu Kusini imewadia.Maandalizi yanaendelea vizuri na kesho ndio msafara unaoondoka kwa Convoy kuelekea Mkoani Mbeya.

Maandamano yenyewe yatazinduliwa Mbeya Mjini Siku ya Ijumaa tarehe 6 Mei, tunatarajia kufanya Ziara kwenye Mikoa ya Mbeya,Rukwa,Ruvuma na Iringa respectively.

Mkoa wa Morogoro tumeuondoa kwa sasa kwa kuwa kuna mvua nyingi na sehemu nyingine kuna mafuriko hivyo hatutaweza kufika maeneo yote, Morogoro tutakwenda baada ya Bunge la Bajeti.

Maandamano hayo kuongozwa na Viongozi Wakuu wa Chama. Makamanda Mbowe, Dr Slaa, Zitto na Arfi tukifuatiwa na Wabunge, Watendaji Makao Makuu, Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Majimbo.

Ziara inatarajiwa kuwa ya Siku 12 kila Mkoa ni siku tatu.

Kama kawaida nitajitahidi kuwahabarisha kila kitakachojiri kadiri ya uwezo wangu.
Nitaanza na Msafara wa kesho.

Aluta Continua

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
 
Safi sana mheshimiwa Regia Mtema,2nawaomba Chadema waendelee na moyo huo huo wa kuwapa elimu ya uraia watanzania wa maeneo mbali mbali.
 
Wana JF.Heshima kwa wote.

Ile Ziara ya Maandamano ya Nyanda za Juu Kusini imewadia.Maandalizi yanaendelea vizuri na kesho ndio msafara unaoondoka kwa Convoy kuelekea Mkoani Mbeya.Maandamano yenyewe yatazinduliwa Mbeya Mjini Siku ya Ijumaa tarehe 6 Mei.Tunatarajia kufanya Ziara kwenye Mikoa ya Mbeya,Rukwa,Ruvuma na Iringa respectively.Mkoa wa Morogoro tumeuondoa kwa sasa kwa kuwa kuna mvua nyingi na sehemu nyingine kuna mafuriko hivyo hatutaweza kufika maeneo yote.Morogoro tutakwenda baada ya Bunge la Bajeti.
Maandamano hayo kuongozwa na Viongozi Wakuu wa Chama. Makamanda Mbowe,Dr Slaa,Zitto na Arfi tukifuatiwa na Wabunge,Watendaji Makao Makuu,Viongozi wa Mikoa,Wilaya na Majimbo.

Ziara inatarajiwa kuwa ya Siku 12 kila Mkoa ni siku tatu.

Kama kawaida nitajitahidi kuwahabarisha kila kitakachojiri kadiri ya uwezo wangu.Nitaanza na Msafara wa kesho.

Aluta Continua

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
Usisahau kutuwekea picha. Kule Mwanza tulikudai picha sana hukutuwekea inawezekana hukuwa na kamera. Picha pia huzungumza sana wakati fulani hata kuzidi maneno. Kabla hamjaondoka tayarisha kabisa kamera.
 
Asante Dada Regia,ziara kama hizo ndizo zinazokijenga chama kwa kukiongezea idadi ya wanachama.Tupo pamoja nanyi,tutashukuru sana kama utakua unatujuza mapema kila kitakachojiri katika hiyo ziara.
 
Usisahau kutuwekea picha. Kule Mwanza tulikudai picha sana hukutuwekea inawezekana hukuwa na kamera. Picha pia huzungumza sana wakati fulani hata kuzidi maneno. Kabla hamjaondoka tayarisha kabisa kamera.


Ziara yote ya Kanda ya Ziwa niliweka picha ingawa zilikuwa zinachelewa.Refer my threads Kanda ya Ziwa.
 
Safi sana, ila nashauri uwepo utaratibu mzuri wa kupata feedback ya hiki kinachofanyika, nilitamani uwepo ufunguzi wa matawi na mashina jamani.kwani tusikae kuelea hewani na huku chini hatuna muundo,chama sio masikini hivi sasa.
 
waambieni watu huko kwamba mnamlipa slaa milioni 15 na mnanunua magari mitumba ya mbowe
Mr.II aka Sugu anakukaribisha kwenye kampeni yake ya KUTWANGA NA KUKOBOA ukimwona Makamba na Mkama wape taarifa hii tafadhali you are all welcome.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mh. Mtema na viongozi wengine karibuni sana Mbeya, tunawasubiri kwa hamu. Peoples Power!
 
Tunashukuru kwa taarifa.Tunawasubiri huku Ruvuma mje mfungue matawi ya wanachama wapya.hamasisheni wananchi kujiunga na chama.kumbukeni kwenda vijijini.Japo si mada yake kwa leo lakini naomba nikufikishie manung'uniko yangu kwenu,kuwa msijaribu kununua magari yaliyochakaa.nunueni mapya hata kama ni mawili ni better zaid.Nilimwuliza majuzi hapa katibu wa chadema wilaya ya songea, vipi mpango wa kununua magari yatakayo rahisisha kwenda vijijini kuhamasisha chama?akanijibu kuwa kuna mpango wa kununua magari 20 kwanza.sawa.lakini taarifa tunazozipata za kununua magari machakavu while tunapiga vita ufisadi,hili sio sawasawa.Nakipebda chadema na ndio maana mimi ni mwanachama hai.Samahani kwa kuingilia hili.
 
Ziara yote ya Kanda ya Ziwa niliweka picha ingawa zilikuwa zinachelewa.Refer my threads Kanda ya Ziwa.

picha za kanda ya ziwa tulizipata swadakta. ila picha za shinyanga kwenye mazishi ya comrade Shilembi haukuzirusha mh. Tafadhali bado tunazisubiri. Many thanks Regia. Aluta...........
 
Mkuu Regia akhsante saaana kwa taarifa muhimu. Moto ni huo huo hadi kieleweke.
Kwa upande wa Morogoro ni kweli kabisa haitawezekana kwani kuna mvua nyingi na mafuriko katika maeneo kama vile Kilosa, Mvomero na maeneo kadhaa ya Morogoro vijijini. Na hili ni tatizo kubwa sana kwa mkoa huo kwani viongozi wa ccm ambao wamepewa madaraka wamejisahau kwa muda mref na kuacha maeneo hayo maskini wa kutupwa, madhara ya mafuriko ni makubwa na hakuna anayejali. Tazama ufisadi unaofanyika wilayani Kilosa, viongozi wamejigeuza miungu....Anyway mtakaporudi tena, Morogoro iunganishwe na mikoa ya Singida na Dodoma, then kampeni iendelee mikoa ya kusini...Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Na Kitaeleweka.
 
Back
Top Bottom