Chadema kwa sasa ndiyo tumaini la ukombozi kwa watanzania wengi na kinakua kwa kasi ya ajabu, hivyo basi ccm wanatafuta mbinu za kukisambaratisha. Ushauri wangu: 1. Tumtangulize MUNGU katika kila jambo. 2. Katika kila mkutano kuwe na watu maalumu walioandaliwa kuongea, wangine watambulishwe tu. 3. Akipokewa kiongozi kutoka ccm asipewe madaraka yoyote ndani ya chama hata ktk ngazi ya kata kwa muda wa miaka5. 4. Katika mikutano kusiwe na kauli zozote za kikanda, kikabila, kitabaka au kidini, kuwe na kauli za kisisasa tu. 5. Kiongozi anapokosea viongozi wengine wasimkosoe kwa kauli zao binafsi, bali akosolewe au kuadhibiwa kupitia vikao halali vya Chama. 5. Viongozi au wanachama tunapoonewa na serikali au taasisi zake tusilete vurugu bali tuwasubiri kwenye kupiga kura tuwapige chini vibaya. Chama/wanachama tukizingatia hayo, hakuna kitu kitaweza sambaratisha Chadema. Long live Chadema.
RED: Tuache kuchanganya dini na siasa - siasa na dini ni sawa na maji na mafuta, havichangamani!
1. Dini ni imani ya mtu binafsi!
2. CHAMA kama nchi, hakina dini!
Ushauri namba mmoja haufai kuendekezwa. kila mtu ana dini yake, imani yake, mungu wake na namna yake ya kumwabudu mungu wake.
Ondoeni kabisa kuchanganya dini na siasa.