CHADEMA ili mchukue nchi 2015 zingatieni haya

Chadema kwa sasa ndiyo tumaini la ukombozi kwa watanzania wengi na kinakua kwa kasi ya ajabu, hivyo basi ccm wanatafuta mbinu za kukisambaratisha. Ushauri wangu: 1. Tumtangulize MUNGU katika kila jambo. 2. Katika kila mkutano kuwe na watu maalumu walioandaliwa kuongea, wangine watambulishwe tu. 3. Akipokewa kiongozi kutoka ccm asipewe madaraka yoyote ndani ya chama hata ktk ngazi ya kata kwa muda wa miaka5. 4. Katika mikutano kusiwe na kauli zozote za kikanda, kikabila, kitabaka au kidini, kuwe na kauli za kisisasa tu. 5. Kiongozi anapokosea viongozi wengine wasimkosoe kwa kauli zao binafsi, bali akosolewe au kuadhibiwa kupitia vikao halali vya Chama. 5. Viongozi au wanachama tunapoonewa na serikali au taasisi zake tusilete vurugu bali tuwasubiri kwenye kupiga kura tuwapige chini vibaya. Chama/wanachama tukizingatia hayo, hakuna kitu kitaweza sambaratisha Chadema. Long live Chadema.

RED: Tuache kuchanganya dini na siasa - siasa na dini ni sawa na maji na mafuta, havichangamani!
1. Dini ni imani ya mtu binafsi!
2. CHAMA kama nchi, hakina dini!

Ushauri namba mmoja haufai kuendekezwa. kila mtu ana dini yake, imani yake, mungu wake na namna yake ya kumwabudu mungu wake.
Ondoeni kabisa kuchanganya dini na siasa.
 
Soma vizuri ndugu, hakuna hata sehemu moja niliyoandika neno dini, sijui umelitoa wapi? Je, unajua wimbo wa taifa la Tanzania unavyoanza? Au na wimbo huo ni wa kidini? Au wewe ni matokeo ya shule za kata?
 
Ya Mungu mpeni mungu na ya kaisari mpeni kaisari!
Mnapotaka madaraka mnamtafuta Mungu, mkiyapata hammkumbuki!
Nani asiyejua bunge linaanza na sala ya kumwomba mungu lakini baada ya hapo kinachoendelea mnakijua wenyewe.
Unafiki mtupu!

Shule za kata ni matokeo ya hao ambao kila wanapokutana wanasema, Ee mwenyezi Mungu ....
ila baada ya hapo kila mtu na biashara yake ...
 
Ni hivi jana nilimsikia Mheshimiwa Mbowe akiwa bungeni alilalamika kuwa chadema "wanakesha" kushughulia maoni yao ya bajeti maofisini kwao bila ya kuwa na makamishna kama ilivyo Serikali. Hilo ni kweli kabisa, wala sina ubishi nalo, malalamiko yalielekezwa kwa kitendo cha kuchanwa na kutupwa nakala ya maoni yao ya bajeti.

Baada ya muda kidogo nikamsikia Halima Mdee akisema kuwa hiyo ilikuwa makosa ya ku taipu na yalishatolewa ufafanuzi yalipogundulika (baada ya kuwasilishwa bungeni).

Kabla sijatoa ushauri, nna maswali haya:

1) Jee, CHADEMA mnataka kutudanganya au mnafikiri kuwa Watanzania wote ni wajinga kiasi cha kutaka kutuaminisha kuwa hesabu kubwa kama za kwenye maoni ya bajeti huwa zinapigwa taipu? na hamtumii "software" za mahesabu kama "excel", "Tally", "Quick books" au zinginezo?

2) Kuna mtu, kama sikosei anajiita TUNTEMEKE aliwahi kuleta nyuzi humu ikielezea kuwa hapo ofisi za CHADEMA, alipewa kazi "Mchumba" wa Dokta Slaa kuweka "custom software" ya kudhibiti mahesabu ya chadema. Jee, kuna uwezekano kuwa hiyo "software" ina matatizo na huwa haioneshi vyanzo vya mapato na ina inaonesha "0" (sifuri) kwenye mapato.

3) Kama maoni yenu ya bajeti yalikuwa na makosa kama hayo mliyoyaombea radhi, Jee, nyinyi mlitaka zisichanwe na kutupwa hizo kopi zenye makosa?

Ushauri:

Naomba ili Watanzania wachache, wanaojuwa jinsi mahesabu yanavyowekwa na kufanywa siku hizi, ili wasiwaelewe vibaya, muwakinaishe kuwa nyie ni kweli bado mnatumia taipu kama mlivyoeleza bungeni na si hizi "software" za mahesabu.

Na kama bado mnatumia "custom software" zilizowekwa na Josephine, mpeleke wataalaam wakachunguze kwanini zinaonesha mapato "0" kiasi cha kuwa aibisha bungeni na muwaombe tena radhi Watanzania kwa kuwadanganya kuwa lilikuwa ni kosa la ku taipu.

Mchunguze vile vile kama na mapato yenu pia ya chama yanaonesha hivyo hivyo?

Huo ni ushuri wa bure kama nilivyowapa siku mlioibandika bajeti yenu hapa JF, siku hiyo hiyo iliyosomwa, saa sita na robo mkawa mmeshaibadika hapa, kabla ya saa tisa mchana nikawaonesha hayo makosa kwenye post zangu zaidi ya moja. Mpaka wengine ( kaa la moto mmoja wapo) wakanishutumu kuwa nnajibu tu bila kuisoma hiyo bajeti. Nadhani yaliojiri bungeni yanajitosheleza na inabidi muufanyie kazi ya ziada huu uzembe.

Bajeti yenu: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-kambi-ya-upinzani-bungeni-2.html#post4074739

Moja ya post zangu ya kuyaonesha hayo makosa:

quote_icon.png
By zomba

Nimeipitia, juu huko inasema tunataka fedha za wahisani ziwekeze sio zitumike kwa matumizi ya kawaida, chini kwenye jedwali pesa za wafadhili kwenye maendeleo ni 0.

What a contradiction.

Jamani msifanye upuuzi kuhusu haya kwani haiingii akilini kuwa Waziri kivuli ambae aliweka rekodi siku za nyuma kwa kuwa mbunge wa mwanzo kusoma hoja zake bungeni kwa kutumia Ipad, leo asiwe anatumia "software" za mahesabu awe ana tumia "taipu" kufanya mahesabu yake.

zomba, kwa haraka haraka naweza kutaja maeneo ambayo unaweza kutoa ushauri;
1. Utatuzi wa mgogoro wa madakatri
2. Matumizi makubwa ya serikali ya CCM (magari ya ths 5trillion, ths 3 trillion kwa ajili ya mawaziri vs ths 700 kwa Halmashauri)
3. Kupunguza umasikini wa watanzania.
4. Majibu sahihi kuhusu Kiwira (hii inakuja bungeni kwa kishindo)

NB: hoja yako ina tofauti gani ya Ngeleja aliyehujumu uchumi wa nchi kwa kuiweka gizani ili wakubwa zake wafaidi? Ushauri gani unatoa hapa na sio kwa ngeleja kuhudhuria vikao vya bunge badala ya kuongea mambo yaliyokuwisha tolewa ufafanuzi? No wonder aliruga sekta nzima ya madini.
 
Fungulia nyuzi, ntatoa ushauri.
 
Ni hivi jana nilimsikia Mheshimiwa Mbowe akiwa bungeni alilalamika kuwa chadema "wanakesha" kushughulia maoni yao ya bajeti maofisini kwao bila ya kuwa na makamishna kama ilivyo Serikali. Hilo ni kweli kabisa, wala sina ubishi nalo, malalamiko yalielekezwa kwa kitendo cha kuchanwa na kutupwa nakala ya maoni yao ya bajeti.

Baada ya muda kidogo nikamsikia Halima Mdee akisema kuwa hiyo ilikuwa makosa ya ku taipu na yalishatolewa ufafanuzi yalipogundulika (baada ya kuwasilishwa bungeni).

Kabla sijatoa ushauri, nna maswali haya:

1) Jee, CHADEMA mnataka kutudanganya au mnafikiri kuwa Watanzania wote ni wajinga kiasi cha kutaka kutuaminisha kuwa hesabu kubwa kama za kwenye maoni ya bajeti huwa zinapigwa taipu? na hamtumii "software" za mahesabu kama "excel", "Tally", "Quick books" au zinginezo?

2) Kuna mtu, kama sikosei anajiita TUNTEMEKE aliwahi kuleta nyuzi humu ikielezea kuwa hapo ofisi za CHADEMA, alipewa kazi "Mchumba" wa Dokta Slaa kuweka "custom software" ya kudhibiti mahesabu ya chadema. Jee, kuna uwezekano kuwa hiyo "software" ina matatizo na huwa haioneshi vyanzo vya mapato na ina inaonesha "0" (sifuri) kwenye mapato.

3) Kama maoni yenu ya bajeti yalikuwa na makosa kama hayo mliyoyaombea radhi, Jee, nyinyi mlitaka zisichanwe na kutupwa hizo kopi zenye makosa?

Ushauri:

Naomba ili Watanzania wachache, wanaojuwa jinsi mahesabu yanavyowekwa na kufanywa siku hizi, ili wasiwaelewe vibaya, muwakinaishe kuwa nyie ni kweli bado mnatumia taipu kama mlivyoeleza bungeni na si hizi "software" za mahesabu.

Na kama bado mnatumia "custom software" zilizowekwa na Josephine, mpeleke wataalaam wakachunguze kwanini zinaonesha mapato "0" kiasi cha kuwa aibisha bungeni na muwaombe tena radhi Watanzania kwa kuwadanganya kuwa lilikuwa ni kosa la ku taipu.

Mchunguze vile vile kama na mapato yenu pia ya chama yanaonesha hivyo hivyo?

Huo ni ushuri wa bure kama nilivyowapa siku mlioibandika bajeti yenu hapa JF, siku hiyo hiyo iliyosomwa, saa sita na robo mkawa mmeshaibadika hapa, kabla ya saa tisa mchana nikawaonesha hayo makosa kwenye post zangu zaidi ya moja. Mpaka wengine ( kaa la moto mmoja wapo) wakanishutumu kuwa nnajibu tu bila kuisoma hiyo bajeti. Nadhani yaliojiri bungeni yanajitosheleza na inabidi muufanyie kazi ya ziada huu uzembe.

Bajeti yenu: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-kambi-ya-upinzani-bungeni-2.html#post4074739

Moja ya post zangu ya kuyaonesha hayo makosa:

Jamani msifanye upuuzi kuhusu haya kwani haiingii akilini kuwa Waziri kivuli ambae aliweka rekodi siku za nyuma kwa kuwa mbunge wa mwanzo kusoma hoja zake bungeni kwa kutumia Ipad, leo asiwe anatumia "software" za mahesabu awe ana tumia "taipu" kufanya mahesabu yake.

Ile ilikuwa ujanja wa manguli wa mahesabu wa CDM. Waliweka 0 makusudi ili wabunge wengi wa ccMafisi na Watanganyika wote wasome na wajue kuwa tunaweza kuwa na vyanzo vya mapato hapa hapa nchini pasipo kutegemea sana wafadhili. Bila ya hivyo ccMafisi wasingeisoma kabisa Bajeti ya wapinzani. Na kwa wanauchumi wa CDM Wameweza kwani kila mwanaTanganyika kaelewa kuwa tunaweza tusipowaachia mafisadi wakashirikiana na watu wao kukwepa kodi. CDM CHAMA MAKINI BANA. SIO RAHISI KUSAHAU ETI TYPING ERROR.
 
Kwi kwi kwi teh teh teh, hata mapato ya nchini yalikuwa "0".

Nilioutoa ni ushauri wa bure, zingatieni.
 
Du hapa leo napita mitusi itaniangukia mradi Bajeti ya Wizara Fedha imepita basi sasa zote
 
Si unajuwa magwanda ya khaki yakirowa jasho huwa yanatoa harufu ya kikwapa? Na hapa jasho lazima liwatoke na kikwapa leo hakikwepeki.
 
Swala la soft ware unalijua wewe that was typing error!

Mbona huongelei swala la bajeti kuwa na matumizi mengi kwaajili ya vitafunwa na chai za wakubwa!

Toa ushauri wako kwa hilo basi.

Zomba chama kinakupa posho zaidi ya Nape
 
Sasa hivi nilikuwa nasoma nyuzi ya mwenzako (kimagwanda) mmoja nae ametoa ushauri ingawa kachelewa na kautoa baada yangu, lakini cha msingi, si mimi tu mwenye kuwapa ushauri. Nna uhakika mtakapokuwa mmeondoa uzembe unaojionesha wazi wazi (Wabunge wote ni wazembe - Mnyika) mtaweza kuwa wasimamizi wazuri pale bungeni.

Msome huyu mwenzako anaeitwa Mag3, nae anataka hii kitu itazamwe "seriously" kwenye post # 58: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...%92s-shadow-budget-blunder-2.html#post4104322
 
Bado mpaka leo hamjajua kwanini software ya Josephine imetoa mapato "0"?
 
Kosamoja haliwezi kuondoa mazuri 99 yaliyofanywa na cdm. Na wala kosa moja haliwezi kupunguza kasi ya kuing,oa ccm madarakani. Ushauri wako tumeupokea na inaonesha unaipenda chadema ndio maana umetushauri maana tunahitaji kusonga mbele.
 
Hujajibu swali:

Back
Top Bottom