ntagunga
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 654
- 256
Mi sioni haja ya CDM kuwaambia yote hayo polisi maana itakuwa kama ni mkwara.
Dawa ni kufanya vitendo. CDM iwe na subira mpaka hapo itakapoingia madarakani kisha iwashughulikie vibaraka wote wa polisi wanaotumiwa kwa maslahi ya watu wachache.
Waanze na shemeji yake rais (Said Mwema) kisha ma'RPC na wengine wa chini yao.
HATA MIMI SIRIDHISHWI NA UTENDAJI WA BAADHI YA MAKAMANDA, NA KWA KUWA IGP NI OFISA MWENZAO, NAONA NDO SABABU YA YEYE KUTOKUCHUKUA HATUA. HAWATISHI KWA LOLOTE, KWANI KAMA NI MWAJIRI NA MWANGALIZI WA MAFILE YAO NI MMOJA, YAANI RAIS NA OFISI YAKE.
SASA SWALI LANGU NI KWA WALE MAKAMANDA AMBAO WAMEFANYA VIZURI, WANATUMIA WELEDI NA WAKO MAKINI KATIKA KUTEKELEZA KAZI ZAO, TUNAWAWEKA KATIKA KUNDI LIPI?
JANA CHADEMA HAPA MWANZA WALIKUWA NA MKUTANO WA HADHARA, WATU WALIKUWA NI WENGI NA HAWAKUWA NA KIBALI HADI WALIPOAAMBIWA WASUBIRI SENSA IMALIZIKE.
CHADEMA WALIPUUZA AGIZO HILO, NA JESHI MKOAN HAPA LIKAWAPUUZA, MBONA MAMBO YAMEENDA VIZURI? MBONA MKUTANO ULIMALIZIKA SALAMA NA WATU KURUDI MAKWAO KWA AMANI?
kWA NINI MWANZA IWEZEKANE LAKINI MIKOA MINGINE ISHINDIKANE?