CHADEMA Iitishe Maandamano dhidi ya Jeshi la Polisi?

This is the climax huwezi kuwa unaua watu kama zama za ukoloni!
Ivi hawa polisi hawajui kuwa we are customers to them

Inauma sana tuliwafukuza wakoloni kwa kishindo halafu tunauwawa na wenzetu!!!
 
Hakuna haja ya kuwa hata na rafiki polisi ni washenzi kabisa na hawa wanaoishi mitaani hakika ni kuwafanyia unyama tu tumewachoka
 
miezi michache iliyopita waandishi wa habari Iringa waliandamana wakidai kutoingiliwa na Polisi,tukumbuke Marehemu alikuwa mwenyekiti na kwa ninavyomfahamu ni mtu mwenye misimamo iliyosimama,nimefanya naye kazi Tanesco Iringa miaka ya 90 ninamjua vizuri,Mwangosi alikuwa anatafutiwa nafasi na wameipata,damu yake haitakwenda bure,Mwangosi ametuingiza kwenye level nyingine ya mabadiliko
 
Si chadema tu, wanahabari, na wanaharakati wa haki za binadamu. Wananchi tutawaunga mkono kwa nguvu zote, mauaji yamekuwa mengi mno sasa.
 
Tatizo hili naona ni kubwa kwa cdm.Pia hawajui matokeo halisi ya hicho wafanyacho.Haya hata kama cdm wakajua kwa asilimia mia kuwa it is a well planned stratregy to kick their ass,cdm watafanya nini
What cdm is prepared to do,say if their party is deregesterd.To me it looks cdm is short of stratergies.

Hakikufutwa UNITA, chama cha savimbi, pamoja na mauaji halisi kichofanya kwa wananchi wa Angola! ije kufutwa chadema kwa mauaji yanayofanywa na polisi!!! KUWA MUELEWA, NI WANANCHI NDIO HATUITAKI CCM, HATUBADILISHI LUGHA.
 
Mkuu Mwanakijiji naunga mkono hoja yako. CHADEMA iitishe maandamano nchi nzima haraka iwezekanavyo ili kupinga mauaji ya kinyama yanayofanywa na vyombo vya dola ambayo yanazidi kushamiri siku hadi siku.
 
CDM watakaa na kuanza kutoa hotuba zao zilizochoka; it is about time to confront evil!! Ikibidi kuitisha siku ya mgomo baridi!! Kwamba Said Mwema na Chagonja waondolewe na serikali ikikataa basi utakuwa ni mgomo wa nchi nzima. Hadi auawe mbunge wa CDM ndio watajua kuwa tulipofika ni 'tipping point'?
 
Hili la polisi linaanzia juu kwa viongozi wa jeshi; ni wao ndio wanatoa na kuonesha uongozi. Kuna kitu ambacho kwenye mashirika kinaitwa "corporate culture" yaani "utamaduni wa shirika". Karibu kila shirika lina utamaduni wake yaani namna ya kuangalia mambo, kufanya na kujionesha. Inajumuisha jinsi watu wanavyohusiana na jinsi watu wanatendeana. Ukiwa na 'corrupt corporate culture" utaona shirika linajihusisha na vitendo vya kifisadi kiasi kwamba inakuwa ni sehemu ya utamaduni wake.

Naamini hili sasa hivi linaweza kuelezewa juu ya jeshi letu la polisi. Wapo maafisa wengi tu ambao wanajitahidi kulitumikia jeshi hili kwa weledi na uaminifu (yule aliyejiua wa Morogoro ni mfano mmoja) lakini wanakwamishwa na utamaduni huu wa kulindana na kuwa na uadui na upinzani. Ni utamaduni ambao umejengwa chini ya Mwema na kulifanya jeshi hili liwe ni la kisasi (vengeful) na vile vile lenye mtazamo hasi na upinzani wa kisiasa. Matokeo yake makamanda wake karibu wote wana mawazo kuwa upinzani ukitaka kuandamana basi la msingi ni kudhibiti siyo kuhakikisha wanaandamana kwa amani! Hili linatokea kwa sababu Mwema, Chagonja na maafisa wa juuwa jeshi hilo wamejenga utamaduni huu wa kuwa na lengo la kulinda 'serikali' kutokana na ukosoaji mkali wa kisiasa.
 
Hakikufutwa UNITA, chama cha savimbi, pamoja na mauaji halisi kichofanya kwa wananchi wa msumbiji! ije kufutwa chadema kwa mauaji yanayofanywa na polisi!!! KUWA MUELEWA, NI WANANCHI NDIO HATUITAKI CCM, HATUBADILISHI LUGHA.


SAVIMBI - UNITA - MSUMBIJI!... Hii historia yaelekea ipo mabwepande!..
 
CDM watakaa na kuanza kutoa hotuba zao zilizochoka; it is about time to confront evil!! Ikibidi kuitisha siku ya mgomo baridi!! Kwamba Said Mwema na Chagonja waondolewe na serikali ikikataa basi utakuwa ni mgomo wa nchi nzima. Hadi auawe mbunge wa CDM ndio watajua kuwa tulipofika ni 'tipping point'?

Maneno haya niliyazungumza siku ya mauwaji ya Morogoro,ama ni kwavile ni mwandishi?Na sasa tusubiri hadi mbunge ama kiongozi ndo auwawe?Hili la leo ni tippin point kwasababu picha ziko zinaonyesha tukio live lilipotokea!na nasikia walitoa kauli eti bomu lilimwangukia,wakitaka kuyeyusha kama lile tukio la morogoro, eti "a flying object"

Halafu tukisema tujadiliane ni kivipi wananchi wanaweza kujilinda thread inafutwa,huu si ndo ukondoo wenyewe?wananchi hawana haki ya kujilinda endapo hawana ulinzi?

Polisi wenyewe wanaofanya unyama kwani si wako miongoni mwetu?ndo maana kuna nchi nyingine kunakuwa na militia za kulinda wananchi.

Kama polisi wa wananchi wanaolipwa kwa kodi za wananchi,wanatumia pesa hizo hizo kuwauwa kwasababu wametumwa na wanasiasa wanategemea kitu gani?
 
Mzee Mwanakijiji,kwanza pole kwa kupoteza ndugu yako katika tasnia ya habari,ndugu yetu,mwananchi mwenzetu...nashukuru kwa bandiko hili pia,pengine tutapata maoni ya wananchi nini kifanyike.Nilianzisha thread ambayo nilitaka wananchi watoe maoni yao ni kivipi wanaweza kujilinda.

Ni wazi hatuwezi tena kutegemea ulinzi wa polisi.Polisi walikuwa wakiwauwa raia wema toka kitambo tu,sema hii ni kwasababu wameanza kuuwa kwasababu za kisiasa wazi wazi!

Maandamano ya kulilaani jeshi la polisi ni mwanzo tu.Lakini siyo solution ya tatizo.

Mimi naliona tatizo pia kwa wanahabari wenyewe ambao baadhi wananunulika kwa bei poa kabisa na serikali dhalimu hii kwa kuhongwa vyeo kama u-DC na -RC. Kwa kweli niliumia sana kuwaona waandishi, tena wahariri wa vyombo vya habari wakijikomba kule Magogoni walikoitwa na kinara wa ugandamizaji wa haki kwenda "kuzungumza" naye siku chache tu baada ya kulifungia gazeti lililokuwa likitoa ukweli bila kubabaisha la Mwanahalisi. Kwa mfano mauaji ya jana ya Mwanahabari kule Iringa ni well documented na independent sources, sasa ni wakati waandishi wangeweka wazi unyama huu wa polisi. nimeangalia hatua kwa hatua picha za jinsi mwandishi yule alivyohujumiwa, tena mbele ya gari la RPC (Inasemekana alikuwepo kwenye tukio) na ipo U-tube ya ku-support habari juu ya uhalifu uliotendwa na watu hawa walioapa kuwalinda wananchi, lakini utashangaa hao hao wanahabari wakieneza theories watakazopewa na CCM na Polisi! Ama kweli gawanya utawale! Wanahabaeri amkeni sasa, teteeni haki zenu, kataeni kununuliwa na madhalimu hawa CCM na semeni hapana kwa sauti moja ili Tanzania na dunia nzima iwasikie. A luta continua.
 
kwa kuanzia,picha za unyama huu zisambazwe kwenye balozi zote,especially zile ambazo serikali dhalimu hupendelea kutembeza bakuli.Zisambazwe kwenye mashirika na taasisi zote za haki za binadamu.Maandamano ya kudai haki yaanze right away,huku wananchi wakifikiri na kujadili namna ya kujilinda dhidi ya udhalimu huu.
 
Mkuu Mzee Mwanakijii pole kwa kuandika hii thread ambayo inanizidishia uchungu jinsi hii nchi inavyoendeshwa kibabe wamemaliza kuuza rasilimali sasa za nchi sasa wameanza kututoa uhai

Kamanda Precise pangolin;
wacha kamba kama ungekuwa unasikia uchungu ungekuwa Mufindi kuziba pengo la kamanda Mwangosi (R.I.P), inasikitisha na kuhuzunisha sana kuona kijana wa watu amepoteza maisha kwa sababu ya upuuzi wa mtu kam Dr. Slaa kulikuwa na ulazima gani wakati serikali ilishakataza, kama haitoshi baada ya tukio hili badala ya kuungana na familia ya marehemu bado alijitia kudai Chadema watafanya mkutano hivi tuseme angekufa mtoto wake au kaka yake Josephine bado angeyasema hayo? Leo kuna wazazi hawatalala, kwa majonzi, leo kuna watoto maisha yao yatabadilika kwa kumkosa baba, yote sababu ya nini kwa sababu ya mshenzi mmoja aliyekosa busara; mtailaumu polisi lakini kama huo ushindani wa kipuuzi usingeshinikizwa na mpumbavu Dr. Slaa Mwangosi (R.I.P) angekuwa hai, yeye amaeshinikiza akiwa hotelini kazi nyake ni kutoa vyambo watoto watu.
Makamanda akili kichwani mwenu hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindana na nguvu ya serikali.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
POLISI%2B2.JPG


Kwa miaka sasa CDM wamekuwa wakionewa, kunyanyaswa na kukandamizwa na jeshi la polisi la Tanzania linaloongozawa na IGP Said Mwema. Na kwa miaka sasa CDM imekuwa ikitoa hutuba za motomoto kilaa wanachama au mashabiki wake wanapouawa na jeshi hilo huku viongozi wake wakinyanyaswa (mnakumbuka Mbowe alivyobebwa kwa ndege ya jeshi kupelekwa Arusha?). Sasa imekuwa ni tabia kuwa CDM hawawezi kufanya maandamano au mkutano wowote wa kisiasa bila kufikiria polisi watafanya nini 'this time'.

Jeshi la Polisi (kuanzia juu hadi chini) limeendelea kuwachukulia CDM with contempt; haliamini wana haki yakupinga serikali na kwa hakika linaamini linaweza kuwanyamazisha ilimradi tu. Matokeo yake CDM wako chini ya huruma ya jeshi la polisi. Makala hii ya Februari 2012 iligusia kitu hicho hicho: Bwagamoyo: Polisi wataendelea kutuua mpaka lini? Kuna haja ya kufanyika kitu.

a. CDM iache kulionea aibu jeshi la polisi na mchezo wao huu wa kuwahutubia polisi kwenye mkutano yao. Wakati umefika wa kuanzisha maandamano dhidi ya jeshi la polisi na uongozi wake wa juu ili kutaka kina Mwema, Chagonja na wenzake waondolewe kwani ni watuhumiwa nambari moja hawa wa uvunjaji wa haki za msingi za raia!

b. Maandamano haya yawe na lengo la kuonesha dunia juu ya ukatili wa jeshi letu la polisi kwa raia.

c. CDM waliambie taifa mapema kabisa na viongozi wote wa polisi wajue kuwa itakapoingia madarakani kazi ya kwanza itakuwa ni kulivunja jeshi la polisi na kuliunda upya. Katika kulivinja kuna viongozi ambao watashtakiwa kwa yale anbayo wanayafanya sasa dhidi ya raia. Viongozi wa polisi wajue kabisa kuwa "nilikuwa nafuata amri" siyo utetezi pale maisha ya wananchi yanatoweshwa. Watanzania wajue kabisa kuwa jeshi lao la polisi linahitaji kuvunjwa siyo kufanyiwa tu marekebisho. CDM angalieni ilani yenu inasema nini kuhusu jeshi la polisi!!!

Ikumbukwe kuwa wafadhili wamekuwa wakitoa misaada mingi kwa jeshi la polisi vikiwemo vile vya mafunzo, silaha na vifaa. CDM imulike wafadhili hawa vile vile!! Iweje waendelee kufadhili jeshi linalokandamiza upinzani wa kisiasa nchini.



Nitadharau nikisikia tena viongozi wa CDM wanazungumzia mambo yale yale, kuhusu jeshi lile lile na kwa namna ile ile!! hawatokuwa tofauti na watawala wa sasa!

baadhi ya viongozi wa chadema (about 20%) ni mamluki na kamwe haitatokea wakakumbwa na dhahma yoyote ya polisi...... tafakari
 
Kamanda Precise pangolin;
wacha kamba kama ungekuwa unasikia uchungu ungekuwa Mufindi kuziba pengo la kamanda Mwangosi (R.I.P), inasikitisha na kuhuzunisha sana kuona kijana wa watu amepoteza maisha kwa sababu ya upuuzi wa mtu kam Dr. Slaa kulikuwa na ulazima gani wakati serikali ilishakataza, kama haitoshi baada ya tukio hili badala ya kuungana na familia ya marehemu bado alijitia kudai Chadema watafanya mkutano hivi tuseme angekufa mtoto wake au kaka yake Josephine bado angeyasema hayo? Leo kuna wazazi hawatalala, kwa majonzi, leo kuna watoto maisha yao yatabadilika kwa kumkosa baba, yote sababu ya nini kwa sababu ya mshenzi mmoja aliyekosa busara; mtailaumu polisi lakini kama huo ushindani wa kipuuzi usingeshinikizwa na mpumbavu Dr. Slaa Mwangosi (R.I.P) angekuwa hai, yeye amaeshinikiza akiwa hotelini kazi nyake ni kutoa vyambo watoto watu.
Makamanda akili kichwani mwenu hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindana na nguvu ya serikali.

Chama
Gongo la mboto DSM

Walikuwepo watu wenye fikra hizi wakati wa utawala wa makaburu au wakati wa harakati za hai za raia. Waliamini kabisa kuwa serikali haitakiwi kupingwa, haitakiwi kuhojiwa, na haitakiwi kugomewa. Kwamba ukigoma serikali itakuua. Na ilikuwa kweli. Serili ziliua wananchi wake na kutumia nguvu nyingi sana kuwakandamiza. Kumbe kwa kufanya hivyo serikali inajipatia wapinzani wengi zaidi! Badala ya kuilaumu serikali kwa mauaji haya unalaumu CHADEMA. Kana kwamba CDM ndiyo ilishika bunduki na kumlipua Mwangosi.

Oh pity!
 
CDM watakaa na kuanza kutoa hotuba zao zilizochoka; it is about time to confront evil!! Ikibidi kuitisha siku ya mgomo baridi!! Kwamba Said Mwema na Chagonja waondolewe na serikali ikikataa basi utakuwa ni mgomo wa nchi nzima. Hadi auawe mbunge wa CDM ndio watajua kuwa tulipofika ni 'tipping point'?

Serikali hipi iwaondoe ndugu yangu? Binafsi naamini serikali ndio inawatumia Polisi kuua raia wake.
Kinachotakiwa ni serikali kung'oka kwa kuteketeza raia. Katiba (hii mbofumbofu)inatoa fursa sawa kwa raia na wakaazi kuishi ihali serikali yenye jukumu la kulinda wananchi linateketeza mmoja baada ya mwingine ili watakaobahatika kubaki waendeleze uoga. Bado hatujafikia tipping point tunaikaribia, wengi wataendelea kumeagwa damu kabla uoga wawaTanzani haujaondoka.
Nashauri tutengeneze kumbukumbu za waanga wote wanaopigania uhuru wa kweli ili siku ya siku ikifika waorodheshwe kama mashujaaa wa kweli. Bila documentary, historia itasahaulika.
 
Back
Top Bottom