Jatropha
JF-Expert Member
- Apr 9, 2009
- 1,151
- 199
chama cha mapinduzi, ccm, kinaandaa tamko na mkakati rasmi kuhusiana na kitendo cha wabunge wa chama cha demokrasia na maendeleo, chadema, kuondoka katika ukumbi wa bunge hapo jana wakati rais alipokuwa akilifungua bunge hilo rasmi kwa ajili ya vikao vya awamu ya 2010 - 2015.
Katibu wa itikadi na uenezi wa ccm, kapteni mstaafu john chiligati amekutana na waandishi wa habari leo huko dodoma na kusema ccm inapindana na hatua ya wabunge wa chadema kuondoka bungeni.
Amesema kwamba chama chake kitapeleka tamko rami bungeni ili ikiwezekana kwa mujibu wa sheria, kanuni na taraibu za bunge, basi wabunge wa chadema waondoshwe katika ushiriki wa shughuli na vikao vyote vya bunge hadi hapo watakapotambua kuwa aliyechaguliwa kwa asilimia nyingi zaidi katika uchaguzi uliopita ni jakaya mrisho kikwete na ndiye rais halali wa jamhuri ya muungano wa tanzania.
hapo ndio pazuri chadema ilipopataka tuingie katika mgogoro wa kikatiba, ili kila upande utoe madukuduku yake. Kwa wale wote waliokuwa wakionyesha wasi wasi na hatua hii ya chadema mnaona we nyewe jinsi ilivyowagusa? Mpaka wantaka kukaa na vyama walivyowaulia wanachama wao 2001. Big up chadema!!!!!!!!!!!!!!!