Elections 2010 CCM yatoa tamko kuhusu kitendo cha wabunge wa CHADEMA

Unajua wabunge wa CCM ni wa chache sana wanaozijua sheria na kanuni za bunge, ukimuondoa Sitta, Harrison Mwakyembe na wengine wachache sana ndiyo wanakubalika kuwa wanazisoma sheria hizo wengine ni wauza sura, ni watu wa vijiweni wanaongea lolote litokalo kinywani wakidhani watanzania wa leo ni wale wa 1995.Chiligati ni mmoja wa vilaza ndani ya CCM press conference yake kapotezea muda waandishi hana jipya.Nahisi kina mwakyembe watamuambia baadae kuwa ametokota hakuna adhabu hapo Chiligati ni mmoja ya wabunge waliogawiwa masanduku ya kura za wizi kama Mahanga lazima alopoke kutetea ujambazi wao.HANA MPYA .Chadema haina kipimo bungeni hakuna wa kupammbana na figures zile.CHILIGATI ARUDI CHUONI AKANOE UBONGO KWANZA

Ngoja wajaribu yale ya kumsimamisha Zitto tu na ishu ya Buzwagi yaliwatoa jasho, hii sasa wataiingiza nchi kwenye mgogoro rasmi ambao Chadema waliuepusha kwa kuamua tu kutumia haki yao ya kujieleza kwa kutoka nchi. Wakileta hoja ya kuwasimamisha Chadema itabidi pia ijadiliwe hoja ya kwa nini (na hata ushahidi uwasilishwe) hawamtambui JK. Hapo chill na wenzake watakuwa wamejiumbua.
 
Chadema si CCM, CHADEMA imejipanga kila kitu, na kabla ya kufanya maamuzi yake waliangalia kila inshu yoyote kuhusu sheria, KIUFUPI CHADEMA HAWAKURUPUKI.
 
Yahya usijilipue basi!!!!!!!!! Tatizo ni mswahili asiye na akili na uchungu na walalahoi kazi yake ngonao tu
 
Haya yalitarajiwa na nina imani kabisa kwamba Chadema watanyang'anywa hadhi ya kuongoza upinzani Bungeni.

Kwanza hali itakuwa mbaya sana kwa Chadema Bunge litakapoanza kujadili Hotuba ya JK.
Watajikuta katika wakati mgumu wa kuwepo Bungeni wakati wa majadiliano ya hotuba waliyoisusia.

Wakisusa kuwepo wakati wa mjadala huo ni sawa na kujipalia makaa zaidi.




Tulishauri tukapuuzwa. 'Negative implications' tulizokuwa tunazitolea angalizo ndio hizi sasa.

Kuchangia hotuba au Hoja yoyote BUNGENI ni maamuzi ya mtu, wa hulazimishwi, ndo maana bunge la TISA kuna watu hawajawahi kuchangia hata hoja moja, mfano ROSTAM AZIZI
 
Hawa walivyozoea kukurupuka kujibu tuhuma, hebu tusikie watajibu nini. Kama mkuu wa Usalama wa Taifa naye alikurupuka basi hata huyu hatumshangai.
 
Chama Cha Mapinduzi, CCM, kinaandaa tamko na mkakati rasmi kuhusiana na kitendo cha Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kuondoka katika ukumbi wa Bunge hapo jana wakati Rais alipokuwa akilifungua bunge hilo rasmi kwa ajili ya vikao vya awamu ya 2010 - 2015.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni mstaafu John Chiligati amekutana na waandishi wa Habari leo huko Dodoma na kusema CCM inapindana na hatua ya Wabunge wa CHADEMA kuondoka Bungeni.

Amesema kwamba chama chake kitapeleka tamko rami Bungeni ili ikiwezekana kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taraibu za Bunge, basi Wabunge wa CHADEMA waondoshwe katika ushiriki wa shughuli na vikao vyote vya Bunge hadi hapo watakapotambua kuwa aliyechaguliwa kwa asilimia nyingi zaidi katika uchaguzi uliopita ni Jakaya Mrisho Kikwete na ndiye Rais halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Duh!! Wamesahau zomea zomea ziliwapata walivyomfungia Zitto, wajaribu wataona.
 
Haya yalitarajiwa na nina imani kabisa kwamba Chadema watanyang'anywa hadhi ya kuongoza upinzani Bungeni.

Kwanza hali itakuwa mbaya sana kwa Chadema Bunge litakapoanza kujadili Hotuba ya JK.
Watajikuta katika wakati mgumu wa kuwepo Bungeni wakati wa majadiliano ya hotuba waliyoisusia.

Wakisusa kuwepo wakati wa mjadala huo ni sawa na kujipalia makaa zaidi.

Tulishauri tukapuuzwa. 'Negative implications' tulizokuwa tunazitolea angalizo ndio hizi sasa.

Wacha kubabaika Ndg CHADEMA kuna vichwa pale. Hawa watu walifikiri hizo imprications kabla ya kufikia huo uamuzi. Tulia uone mambo ngoma ndo imeanza mdundo.
What matters most massage sent.
 
John chiligati wa CCM ndo ameongea hizo pumba mbele ya waandishi wa habari (this guy must be mad) eti kasema chama chake na kushirikiana na vyama vingine vinapeleka pendekezo lao bungeni waone uwezekano wa kuwazuia hawa wapiganaji

Hazuiliki mtu, hawatujui nini?

This is our strength "we know them in&out, but they don't know even our out"

... irrevesible change has began
 
Wana Matatizo ya kiakili badala wafikilie kujipanga upya kukabiliana na hizi changamoto .cjui ndo wanawaza revenge:embarrassed:
 
Lazima CCM waonekane wamereact kwa issue ya jana, cause ni aibu kwa wageni wa kimataifa walioalikwa jamani
 
Ni haki yao kikatiba na hakuna kanuni wala sheria ya bunge iliyovunjwa kwa hiyo ccm a na ccm b hawana hoja ya msingi katika hili na swala la kujadili hoja ya msela ni wao kuamua kuchangia au kutokuchangia kutokuwepo kusikiliza sio hoja hansard za kazi gani kila neno litamkwalo bungeni huwa linarekodiwa wajameni!
 
Hivi mtoto wa kike kavunja ungo unafanya sherehe anabebwa mabegani na binamu yake matiti nje na kavaa kanga moja wewe baba unashangilia mtoto kakua kwa kumzunguka hiyo inakuja akilini, hivi ilikuwa mtu akili hii akapewa nchi?
 
Haya yalitarajiwa na nina imani kabisa kwamba Chadema watanyang'anywa hadhi ya kuongoza upinzani Bungeni.

Kwanza hali itakuwa mbaya sana kwa Chadema Bunge litakapoanza kujadili Hotuba ya JK.
Watajikuta katika wakati mgumu wa kuwepo Bungeni wakati wa majadiliano ya hotuba waliyoisusia.

Wakisusa kuwepo wakati wa mjadala huo ni sawa na kujipalia makaa zaidi.

Jamani mapambano is not for the faint-hearted kama bwana Kishongo. Sio mara ya kwanza chama hapa nchini kususia na kutomtambua Rais. CUF ni mfano halisi na matokeo yake tumeyaona. Kama kususia na kutomtambua Rais ni inconsequential kama alivyo ashiria Rais mwenyewe na Waziri Mkuu katika hotuba zao; Why such a panic now?
 
Back
Top Bottom