Elections 2010 CCM yatoa tamko kuhusu kitendo cha wabunge wa CHADEMA

Nategemea kuwa wataenda kuwauliza Sitta na Mwakyembe kama wana uhalali wa kufanya hivyo, kwani huyu bibi kizee hajui kitu
 
WanaJF jamani hapa tunajadili nini sasa? Kwa kifungu gani kitatumika kuwalazimisha Chadema wamkubali raisi? Hao waandishi wa habari hawakuuliza maswali kwa huyu katibu muenezi? Kwamba anazijua sheria za bunge? Kama anazijua jee ni kifungu gani kitatumika?

1996 NCCR walitoka bungeni mara kadhaa, mbona hivyo vifungu havikutumika? Chadema hawana ugomvi na CCM wala JK, bali wana ugomvi na mfumo uliotumika kumchagua JK na baadhi ya wabunge wa CCM. Sasa Katibu mwenezi anatakiwa afahamu hilo, na sio kulia lia kama kasuku wakati hujui sheria.

Jana ilikuwa clear massage kwa CCM partners IMF, World Bank, ADB, USAID, Mabalozi na wengine kwamba mchakato ulitumika kumchagua JK sio mchakato wa haki. Hivyo basi japokuwa nyinyi mnamtambua lakini sisi wawakilishi wa watu wa Ubungo, Kawe, Arusha mjini, Mwanza mjini, Kigoma Kaskazini, Iringa mjini, mbeya mjini, musoma mjini, maswa, na sehemu zote Chadema walikuoshinda hatumtambui. Simple, kwamba JK hatambuliki na wawakilishi wa maeneo hayo na watu wa maeneo hayo.Sasa walio baki mle wanamtambua JK, na wamekubaliana na katiba ambayo inasema kwamba as long tume imesema fulani raisi, basi mahakama haiwezi kuchunguza. Maana ya kwamba ipo siku kuna mwehu ataweka partnership na tume kisha huyo mwehu atatangazwa kuwa raisi jee tutamshitakia nani? Chadema nawasupport kwa hili, msimtambue Mkwere simple.


Case close.
 
naomba kifungu cha kanuni za kudumu za bunge kitakachotumika kufanya hivyo, ustuletee ukihiyo wa kiccm hapa? Hata chiligati amesema kuwa wataomba chadema wamatambue raisi kwanza hayo wewe umeyatoa wapi?. nakupatia kanuni za kudumu za bunge letu ili ufute ukihiyo wako.

massage tayari imeshakuwa sent, by february 2011 wakati hotuba inajadiliwa hata wabunge wa ccm watakuwa hawapo makini kwa hotuba hiyo ila kujijenga kwa mawaziri wapya new emerging administration (urais 2015) .

Utaona hotuba hiyo itakuwa haina wachangiaji wengi.

Nashukuru kwa kanuni, zitanisaidia kuondoa ukihiyo kama ulivyosema.
 
Haya yalitarajiwa na nina imani kabisa kwamba Chadema watanyang'anywa hadhi ya kuongoza upinzani Bungeni.

Kwanza hali itakuwa mbaya sana kwa Chadema Bunge litakapoanza kujadili Hotuba ya JK.
Watajikuta katika wakati mgumu wa kuwepo Bungeni wakati wa majadiliano ya hotuba waliyoisusia.

Wakisusa kuwepo wakati wa mjadala huo ni sawa na kujipalia makaa zaidi.

Tulishauri tukapuuzwa. 'Negative implications' tulizokuwa tunazitolea angalizo ndio hizi sasa.

Thubutu,

Hotuba ya JK ijadiliwe Bungeni? Unafikiri serikali iko tayari kuumbuliwa? Sikumbuki kama ukiacha ile hotuba ya kuzindua lile bunge lililopita kuna nyingine ilojadiliwa.
 
CCM mnaota ninyi nani anawadanganya namna hii??? Wabunge wa CHADEMA walitumia HAKI yao sasa kuwaondoa bungeni halafu bunge liwe la CCM na CUF sasa mnataka kuwaamsha waliolala. Mimi nawaambia MSITHUBUTU mtaona machungu yasiyotarajika. Haya mambo yataendelea sasa kwani kumkataa rais ni jambo la kulazimishwa si hiari ya mtu. Ndugu yangu kikwete mtanzania mwenzangu kumbuka miaka mitano sio mingi kama unavyofikiri utarudi kijiweni sijui utaficha wapi uso wako. Waache CHADEMA WATUMIE HAKI YAO ACHA KUTUENDESHA KIDIKTETA HAPA. SIO WATANZANIA WOTE WALIKUCHAGUA JUA NA FAHAMU HILO.
 
mmh.. kama kitendo kile kilikuwa ni cha kijinga, cha kitoto na kisicho na maana kwani hakibadilishi aliyetangazwa mshindi.. kwanini hili linawasumbua? I don't understand. Mimi nadhani CCM wangepuuzia tu.. si walisema "wataenda, watarudi? au kuna kitu ninamiss?
 
Hazuiliki mtu, hawatujui nini?

This is our strength "we know them in&out, but they don't know even our out"

... irrevesible change has began

wawazuie bungeni kwao wao ndio wamewapeleka pale! Hayo makapi anayoongea chiligati atakayeyatilia maanani nae ni kiazi. Ajaribu kuwaondoa aone mziki. Jk jana yalimshuka wanaume walipokua wanaondoka ye akabaki anakenua tu
 
Njia ya kuzuia hili tatizo siyo kwenda kuiburuza Chadema as if siyo chama cha siasa ambacho kinajua sheria za nchi. Muhimu ni kufanyia kazi mabadiliko ya katiba na tume huru ya uchaguzi. Tukumbuke mabadiliko huwa hayana njia rahisi.Ila haraka haraka za CCM kuvuruga vyama vingine inaweza kurahisisha sana mabadiliko kuliko tunavuotegemea.
 
Nchi inaongozwa kwa sheria na sio kwa maamuzi binafsi, watanzania wengi hawana kawaida ya kufanya maamuzi ndani ya sheria na ya kisomi kwa kuwa vitu hivi vililetwa na wazungu kwetu, havikuibikia africa. Siamini kwamba tindu lissu, mabere na huyo dr ndiyo wasomi wakuu wa sheria, tupo kwenye century ya 21, kila kitu kipo wazi kwenye mtandao na kimaandishi, tunauwezo wa kuzisoma na kuvielewa na kufanya maamuzi sahihi. Kivyovyote vile, chadema wanafanya maamuzi ndani ya sheria zilizopo, wanajua, wakizivunja wanalo.

Naamini, kuwa ni busara kuita press conference na kufanya informed decision ndani ya sheria. Sio kukurupuka na kuacha vitabu pembeni na kufanya maamuzi, kila siku utachekwa kwa ufinyu wa akili zako iwapo unataka kuendesha nchi, taasisi, chama, au kampuni kwa kutokea kijiweni,( aristottle na wenzake ndo walileta elimu hii ya kisasa duniani kutokea greece, sasa watanzania hatutaki kutumia, kuamini kwamba, ni kwa usomi na science ndipo tutaweza kuiendesha nchi, siamini kuwa mtu akiwa anaumri mkubwa na ana phd ndo anajua kila kitu, ni lazima usome kila siku kujua, dunia iko wapi na imetoka wapi).
 
Wanaandaa tamko la nini wakati "waziri mkuu' alitamka kuwa kitendo cha wabunge wa chadema kususia speeech ya mkwere ilikuwa 'geresha' tu!! I hope Pinda knows the meaning of 'geresha"
 
JF msipende kurukia kila hoja kwa kufikiri mnauelewa wa kila kitu kinacholetwa hapa jukwaani. Kitendo cha wabunge wa Chadema kutoka nje ni haki yao kimsingi sijui kama mnalifahamu hilo? Ooh Chadema kutoka nje ya Bunge si sahihi etc ndio maana wengine bado mnafikiri kuwa anayepaswa kushinda ubunge ni mwana CCM pekee.

This time it is business unusual. Mmezoea bunge lenye mtazamo mmoja tu. This time kuna watu ambao wakiona kuna kuonewa wananchi wanaowawakilisha watapaza sauti tu. Kutoka nje ya ukumbi ni njia moja ya kupaza sauti loud and clear. Kama wewe unadhani si njia nzuri its well and good. Let be those who think CHADEMA's move is good.
 
mmh.. kama kitendo kile kilikuwa ni cha kijinga, cha kitoto na kisicho na maana kwani hakibadilishi aliyetangazwa mshindi.. kwanini hili linawasumbua? I don't understand. Mimi nadhani CCM wangepuuzia tu.. si walisema "wataenda, watarudi? au kuna kitu ninamiss?

Mwanakijiji, hujakosea kabisa, walisema hivyohivyo, wataenda watarudi. Ukweli ni kwamba, CCM ktk mambo ambayo hawakuyategemea ni lile la wajumbe wa CDM kutoka hotuba ya JK. Walipigwa na Butwaa na hata JK mwenyewe. Lile somo la CDM ni somo ambalo watanzania wote jana wamejifunza na hata kudhubutu kufahamu kuwa, kumbe mtanzania ana uhuru wa kutokukubaliana na Rais, kitu ambacho wengi wao walikuwa hawakijui. Kama ni somo la Uraia (Civics) basi CDM wataingia ktk historia ya watanzania.

MY TAKE: CCM naomba wasome alama za nyakati.....ukweli ni kwamba ugumu na ubishi wao ktk kukubaliana na hali halisi, kutatuletea matatizo hapa nchini. Na ikiwa kama watafanya hayo ya kutaka Bunge liwasimamishe wabunge wa CDM, wafahamu kuwa, wanawanyanganya mamillioni ya watanzania haki yako ya kuwakilishwa Bungeni na wala si wale wabunge 56 wa CDM. Na hapo sasa, itabidi watanzania watafute njia muafaka nyingine ya kudai haki zao. Kama NEC ilichakachua kura, wasidhani inawezekana kuchakachua pia wabunge wa CDM pale mjengoni: Naona hali inavyozidi kwenda, waliowengi wanachoshwa na mambo haya ya ukandamizaji, chonde chonde, watu wakipoteza uvumilivu hapatakalika hapa. Na kwanini tufike huko?? Kwa ukweli, kila siku matamko ya hao waheshimiwa, yanaifanya hali ya siasa nchini kuwa tete...., Wenye masikio ya kusikia na wasikie kwani wasidhani watakuwa salama!
 
mtatumia maneno yote lakini ukweli utabaki palepale. To the party chadema is right to the public they are wrong. Wananchi wanajua rais yupo. Lakini rais wa Chadema hayupo. Vikao wanahurudhuria vya nini. Wasuse kila kitu mpaka 2015 tutawaelewa kweli hawana serikali. Wabunge wametumwa kuwakilisha wananchi si chama. Tatizo la JF ni kutaka kuona kila mtu anasurpot chadema whis is imposible.
 
Huyu Chili sijui pilipili gati si ndio alisema bashe si raia, na kesho yake wakasema ni raia, msimsikilize huyu ni mropokaji, hawana lolote chama cha majambazi wanatapatapa tu, msimjali mpuuzi Pilipiligati na wenzake ndani ya ccm
 
Ati watachukua hatua - Thubutu! Wajaribu waone si wanasema hii ni nchi ya amani. Hawa Wezi waliachiwa sana na wanafikiri kutumia pesa ya walipa kodi wanavyotaka ni halali yao. Sasa wamepigwa jamba jamba wanahaha.
 
Haya yalitarajiwa na nina imani kabisa kwamba Chadema watanyang'anywa hadhi ya kuongoza upinzani Bungeni.

Kwanza hali itakuwa mbaya sana kwa Chadema Bunge litakapoanza kujadili Hotuba ya JK.
Watajikuta katika wakati mgumu wa kuwepo Bungeni wakati wa majadiliano ya hotuba waliyoisusia.

Wakisusa kuwepo wakati wa mjadala huo ni sawa na kujipalia makaa zaidi.

Tulishauri tukapuuzwa. 'Negative implications' tulizokuwa tunazitolea angalizo ndio hizi sasa.

Kwenye ile hotuba hakuna cha kujadili ni upupu tu.... haimusaidii mtanganyika yeyote..... kanda ya ziwa tutajitenga sasa.
 
Ole wao wajaribu kutufukuzia wabunge wetu,watakiona cha mtema kuni..wao si watakuwa Dodoma na wanalindwa na polisi,sisi tutaanza na hawa hawa wenzao waliopo karibu yetu...nna hasiraa! Ole wao
 
Back
Top Bottom