CCM yapigwa Stop ujenzi ardhi yenye mgogoro na Kanisa Katoliki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,992
Na MWANDISHI WETU, KIGOMA

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Kigoma, imetoa amri kwa Bodi ya Wadhamini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wadaiwa wengine kusitisha shughuli zote katika eneo lenye mgogoro kati yao na Kanisa Katoliki wilayani Uvinza.

Amri hiyo ya Mahakama ilitolewa jana Februari 15, 2023 mbele ya Jaji Mfawidhi, Lameck Mlacha baada ya muombaji Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma kuwasilisha maombi chini ya hati ya dharura wakidai ni wamiliki halali wa eneo hilo lililopo eneo la Nyambutwe, wilayani Uvinza mkoani Kigoma.

Mleta maombi katika shauri hilo anawakilishwa na Wakili Method Kabuguzi akishirikiana na Wakili Mgaya Mtaki na wajibu maombi wanawakilishwa na Wakili Fabian Donatus na Hamis Kimilomilo huku upande wa
Serikali ukiwakilishwa na Wakili Allan Shija.

Waombaji katika shauri hilo wanadai mjibu maombi namba mbili, Wizara na Halmashauri ya Uvinza wamepanga kuchukua eneo lao kuwapa CCM bila ridhaa yao kwa ajili ya kujenga madarasa ya Shule ya Sekondari ya Chumvi.

Kanisa Katoliki waliiomba Mahakama ikubali kutoa amri ya zuio la muda kwa wajibu maombi na mawakala wao au watu wengine kujenga au kuendeleza eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 39.6.

Baada ya kusikiliza maombi hayo Mahakama iliyakubali na kutoa amri tatu kwamba kuanzia jana CCM na wengine wote kwenye eneo lenye mgogoro hawaruhusiwi kujenga ama kuendeleza kitu chochote mpaka kesi itakaposikilizwa na kuamriwa.

Mahakama imezuia upande wa Serikali kufanya ama kuendelea na upimaji katika eneo lenye mgogoro.

Pia Serikali hairuhusiwi kufanya ugawaji ama umilikishaji wowote kwenye eneo lenye mgogoro.

Upande wa Serikali uliwasilisha majibu ya madai yanayowakabili lakini CCM walikuwa hawana majibu yoyote waliomba wapewe muda, hivyo Mahakama iliwaamuru kuwasilisha majibu yao ndani ya siku saba.

Awali Wakili wa CCM, Fabian Donatus alidai nyaraka zilihifadhiwa katika Ofisi ya Kigoma na kwa bahati mbaya zilichelewa kuwafikia Dodoma hivyo wakaomba siku saba ili kuweza kuwasilisha majibu ya kiapo kinzani na kuendelea na kesi hiyo.

Wakili wa Mleta maombi, Mgaya Mtaki alidai ni haki yao ya msingi kuwasilisha hati ya kiapo kinzani mahakamani hapo na kwamba wao hawana pingamizi.

Shauri limepangwa kuendelea Machi 3 mwaka huu.

Shauri hilo liliwasilishwa chini ya hati ya dharura na kupewa namba 42/2022 dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya CCM, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

IMG-20230216-WA0006.jpg
Lori likimwaga mawe ya ujenzi ya Shule ya Sekondari Chumvi inayomilikiwa na CCM. Mahakama imepiga marufuku shughuli zozote kufanyika kwenye eneo hilo hadi kesi ya msingi itakapoamriwa.

IMG-20230216-WA0007.jpg
Madarasa ya Shule ya Sekondari Chumvi yanayoendelea kujengwa eneo lenye mgogoro kabla ya Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma kupiga marufuku shughuli zozote kuendelea kwenye eneo hilo.

IMG-20230216-WA0005.jpg
Moja ya hosteli ya Shule ya Sekondari Chumvi Uvinza inayomilikiwa na CCM kwenye eneo la mgogoro na Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma. Mahakama imetoa zuio la kutoendelea kwa shughuli yoyote kwenye eneo hilo hadi kesi ya msingi itakapoamriwa.
 
Wanachokitafuta watakipata. Awamu ya sita kwa kupora maeneo ya umma wanatisha.

Saivi maeneo mengi yameshagawanwa hadi unashindwa kuelewa miaka yote walikuwa wa
 
CHAMA TAWALA kinapora ARDHI ya KANISA AIBU SANA CCM kugombania Ardhi na Kanisa
Hata VIWANJA vya MICHEZO vilijengwa na WANANCHI lakini CCM imejimilikisha kinyemela inadai ni VYAKE

20220508_225536.jpg
 
Na MWANDISHI WETU, KIGOMA

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Kigoma, imetoa amri kwa Bodi ya Wadhamini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wadaiwa wengine kusitisha shughuli zote katika eneo lenye mgogoro kati yao na Kanisa Katoliki wilayani Uvinza.

Amri hiyo ya Mahakama ilitolewa jana Februari 15, 2023 mbele ya Jaji Mfawidhi, Lameck Mlacha baada ya muombaji Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma kuwasilisha maombi chini ya hati ya dharura wakidai ni wamiliki halali wa eneo hilo lililopo eneo la Nyambutwe, wilayani Uvinza mkoani Kigoma.

Mleta maombi katika shauri hilo anawakilishwa na Wakili Method Kabuguzi akishirikiana na Wakili Mgaya Mtaki na wajibu maombi wanawakilishwa na Wakili Fabian Donatus na Hamis Kimilomilo huku upande wa
Serikali ukiwakilishwa na Wakili Allan Shija.

Waombaji katika shauri hilo wanadai mjibu maombi namba mbili, Wizara na Halmashauri ya Uvinza wamepanga kuchukua eneo lao kuwapa CCM bila ridhaa yao kwa ajili ya kujenga madarasa ya Shule ya Sekondari ya Chumvi.

Kanisa Katoliki waliiomba Mahakama ikubali kutoa amri ya zuio la muda kwa wajibu maombi na mawakala wao au watu wengine kujenga au kuendeleza eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 39.6.

Baada ya kusikiliza maombi hayo Mahakama iliyakubali na kutoa amri tatu kwamba kuanzia jana CCM na wengine wote kwenye eneo lenye mgogoro hawaruhusiwi kujenga ama kuendeleza kitu chochote mpaka kesi itakaposikilizwa na kuamriwa.

Mahakama imezuia upande wa Serikali kufanya ama kuendelea na upimaji katika eneo lenye mgogoro.

Pia Serikali hairuhusiwi kufanya ugawaji ama umilikishaji wowote kwenye eneo lenye mgogoro.

Upande wa Serikali uliwasilisha majibu ya madai yanayowakabili lakini CCM walikuwa hawana majibu yoyote waliomba wapewe muda, hivyo Mahakama iliwaamuru kuwasilisha majibu yao ndani ya siku saba.

Awali Wakili wa CCM, Fabian Donatus alidai nyaraka zilihifadhiwa katika Ofisi ya Kigoma na kwa bahati mbaya zilichelewa kuwafikia Dodoma hivyo wakaomba siku saba ili kuweza kuwasilisha majibu ya kiapo kinzani na kuendelea na kesi hiyo.

Wakili wa Mleta maombi, Mgaya Mtaki alidai ni haki yao ya msingi kuwasilisha hati ya kiapo kinzani mahakamani hapo na kwamba wao hawana pingamizi.

Shauri limepangwa kuendelea Machi 3 mwaka huu.

Shauri hilo liliwasilishwa chini ya hati ya dharura na kupewa namba 42/2022 dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya CCM, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Lori likimwaga mawe ya ujenzi ya Shule ya Sekondari Chumvi inayomilikiwa na CCM. Mahakama imepiga marufuku shughuli zozote kufanyika kwenye eneo hilo hadi kesi ya msingi itakapoamriwa.

Madarasa ya Shule ya Sekondari Chumvi yanayoendelea kujengwa eneo lenye mgogoro kabla ya Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma kupiga marufuku shughuli zozote kuendelea kwenye eneo hilo.

Moja ya hosteli ya Shule ya Sekondari Chumvi Uvinza inayomilikiwa na CCM kwenye eneo la mgogoro na Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma. Mahakama imetoa zuio la kutoendelea kwa shughuli yoyote kwenye eneo hilo hadi kesi ya msingi itakapoamriwa.
Ccm utapeli na dhulma ndio sifa yenu
 
Ndugu katika ushirika wa kutawala Wazanzibara wanagombania ardhi tena!
 
Na MWANDISHI WETU, KIGOMA

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Kigoma, imetoa amri kwa Bodi ya Wadhamini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wadaiwa wengine kusitisha shughuli zote katika eneo lenye mgogoro kati yao na Kanisa Katoliki wilayani Uvinza.
Huu ni uamuzi mzuri!.
P
 
Back
Top Bottom