Kigoma: Kisa mgogoro wa ardhi, Kanisa Katoliki laishitaki CCM Mahakamani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,991
Mgogoro wa ardhi ambao umekuwa ukiendelea kwa muda umesababisha Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma kuamua peleka Mahakamani mashitaka dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Shitaka hilo lililofunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma, Kanisa limewashtaki Bodi ya Wadhamini wa CCM, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halmashauri ya Uvinza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuchukua eneo lao wanalodai kulimiliki tangu Mwaka 1920.

Wamewasilisha shitaka hilo chini ya hati ya dharura na yamepangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Lameck Mlacha.
a44c22a3-9846-4d6e-8431-25c9a7ab90d1.jpg

Askofu Joseph Mlola wa Jimbo Katoliki la Kigoma

Waombaji katika shauri hilo wanadai mjibu maombi namba mbili Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Halmashauri ya Uvinza wamepanga kuchukua eneo lao kuwapa CCM bila ridhaa yao kwa ajili ya kujenga madarasa ya Shule ya Sekondari ya Chumvi.

Kupitia kwa Method R.G Kabuguzi ambaye ni Wakili wa Kujitegemea, Kanisa linaomba Mahakama izuie kwa muda uendelezwaji wa eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 39.6 hadi shauri la msingi litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Kanisa limewasilisha hati 3 za viapo zilizosainiwa na Christopher Mibanda, Emmanuel Kimpanti na Padri Esperius Hamenyande. Mahakama imepanga shauri hilo litajwe Februari 15, 2023

Padri Hamenyande ni Mweka hazina wa Jimbo Katoliki la Kigoma na Christopher Mibanda ni Katekista mstaafu huku Emmanuel Mibanda akiwa ni Mzee maarufu Uvinza.
 
Mshasema tangu 1920. More than 99 years lease.
Hiyo ardhi washamaliza lease. Back to the Government.
 
Ni aibu kubwa sana kwa CCM, mwenyekiti wake na Rais wa nchi hili jambo hapo lilipo linabaraka zote za Vatican. Na CCM inatumika kwa Kivuli cha wivu wa waislamu dhidi ya kanisa katoliki.
 
Chama tawala kimekuwa na huu tabia ya kunyang'anya maeneo ya taasisi zingine na kudai ni yao kwa kurudisha umiliki miaka ya nyuma. Hili pia lilijitokeza Geita Shule ya msingi Kalangalala ilipata ufadhilii wa GGM wa kuboreshewa uwanja mwa kuchezea watoto. Walipoona tu mashine zimeanza kufanya kazi wakaanza kudai uwanja ni wao. Ikabidi mfadhili ajitoe hadi watakapoelewana. Niseme tu hivi tabia CCM wanayo na hawamuogopi hata Mungu.
 
Shitaka hilo lililofunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma, Kanisa limewashtaki Bodi ya Wadhamini wa CCM, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halmashauri ya Uvinza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuchukua eneo lao wanalodai kulimiliki tangu Mwaka 1920.
Vatcan at work
 
Back
Top Bottom