CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Matokea ya uchaguzi jimbo la Busanda, yameanza kutoka ambako katika miji mikuu yote ya jimbo hilo, ni Chadcema inaongoza na kuiacha CCM kwa mbali wakati huko vijijini ni CCM inaongoza.

Shamra shamra za kusherehekea ushindi ni mijini kwa kuwafanya wafuasi na washabi wa Chadema kufurika mitaani kusherehekea ushindi hali inayoashiria wakijaambia matokeo ya jumla sio wao, mijini kutakuwa hapatoshi na hakukaliki.

Mpaka sasa Mji mkuu wa Busanda ni Chadema wakati kata maarufu ya Nyarugusu ni CCM.

Nitawaletea matokeo ya kata kwa kata kadri ninavyoyapata.
 
Last edited by a moderator:
Ka nzi ka kijiji kametua Busanda tangu jana, na taarifa za matokeo ya uchaguzi zimeanza kutiririka sasa hivi. Kura zimemalizwa karibu masaa matatu yaliyopita.

a. Chadema kama ilivyotabiriwa inaelekea kuchukua ushindi eneo la Katoro (mjini) kwa ushindi wa tsunami. Hata hivyo ngoma yote inaonekana kuwa iko kijijini. Utabiri wangu wa Chadema kushinda jimbo zima kati ya asilimia 50-55 bado unasimama.

b. Naibu waziri mmoja (Mwantuma Mahiza) na diwani wadaiwa kukutwa na shahada ambazo hazijatumika na haieleweki kwanini amekutwa nazo. Chanzo kingine kinasema ni karatasi zilizokwishapigiwa kura ingawa chanzo cha awali is more authoritative (non-partisan).

will keep u updated every half hour..
 
Asante Babu MKJJ!

Noooooooooooooooo It cant be . . . Then kuna uwezekano mkubwa sana CCM wameiba kura.

Sipati picha Mwantumu naye kaingia katika Ufisadi pamoja na kujionyesha kuwa yeye ni mtu safi na Ushungi Masaa 24!

Ngoma Nzito, bado kiza kinene!
 
Kazi ipo leo kwa wasomaji, Ka-inzi vs Pasco...
Yote heri, maadam CCM inaibuka mshindi, kama ilivyowashangaza CUF kule Magogoni.
 
Ka nzi ka kijiji kametua Busanda tangu jana, na taarifa za matokeo ya uchaguzi zimeanza kutiririka sasa hivi. Kura zimemalizwa karibu masaa matatu yaliyopita.

a. Chadema kama ilivyotabiriwa inaelekea kuchukua ushindi eneo la Katoro (mjini) kwa ushindi wa tsunami. Hata hivyo ngoma yote inaonekana kuwa iko kijijini. Utabiri wangu wa Chadema kushinda jimbo zima kati ya asilimia 50-55 bado unasimama.

b. Naibu waziri mmoja (Mwantuma Mahiza) na diwani wadaiwa kukutwa na shahada ambazo hazijatumika na haieleweki kwanini amekutwa nazo. Chanzo kingine kinasema ni karatasi zilizokwishapigiwa kura ingawa chanzo cha awali is more authoritative (non-partisan).

will keep u updated every half hour..

What a shame, sasa waziri na wizi wa kura jama?
 
Pasco na MMKJJ (na ka-nzi kako); Poleni na kazi....

Tunashukuru sana kwa updates, ila angalieni usalama wenu aisee, tunahitaji kuwa pamoja hata kesho na keshokutwa

Pia kama mngeweza kuwasiliana zaidi na ku-complement hizo nyuz ingekuwa poa

...anyway, the most important is that you are giving us wonderful piece of info [i hope hakuna kulala leo]
 
Mkuu omarilyas

waache wafu wazike wafu wao.....

Mwaka wa mungu huu............watajuta kuwadanganya watanzania huko nyuma
 
Kazi ipo leo kwa wasomaji, Ka-inzi vs Pasco...
Yote heri, maadam CCM inaibuka mshindi, kama ilivyowashangaza CUF kule Magogoni.

Inaibuka mshindi ama inafanikisha wizi? by the way sijui hii aibu chama cha mafisadi mtaiweka wapi? waziri anakamatwa ameiba shahada za kupigia kura? yaani huyo ndo kiongozi mwenye dhamana anaye diriki kupora haki za raia aliokabidhiwa kuwaongoza?

Mi siku zote nilidhani walau mafisadi huwatumia vijana wenye njaa kufanya vitendo hivi vya kihuni, kumbe wenye dhamana wenyewe wanaingia mitamboni?
 
MKKJ na Pasco,

Asante kwa updates. Leo nitakuwa macho usiku mzima nikifuatilia matokeo haya. Chupa ya whisky iko tayari tayari kufanywa vibaya endapo Chama Cha Mafisadi kitalazwa chali Busanda.

Keep it up.

Tiba
 
Ngoma ikilia sana mwisho wake upasuka. Na huu ni wakati hasa wa Ngoma kupasuka.

CCM Must go now! Hata kama wameiba kura, they will never go away with it.

Hizo kura za Kijijini haziwezi kuwa nyingi kwa idadi kuliko za mjini. Labda waibe!
 
Back
Top Bottom