CCM yaishukia CHADEMA suala la TUHUMA za Rushwa kwa wabunge

UJINGA MTUPU na GIZA LA UFISADI NDILO LINAWATAWALA WATU WA CCM, nafikiri kama anadhani kuwa hao watu CHADEMA wametajwa wasio sahihi au kwa upendeleo naye ANGETAJA ANAOJUA NI CDM au wapinzani wengine.

Imeandikwa "watu wangu hufa kwa kukosa maarifa",

kwanini NAPE NNAUYE asitaje
WALA RUSHWA WA CDM?

Nani atasikia KILIO chako NAPE hata kama ni KWELI kuwa wamehongwna a lakini unashindwa kuthibitisha tuhuma zao.....PUMBAVU MWANADAMU USIYEJUA WAKATI WAKO na ULAANIWE wewe usiyejua MAJIRA yako.
 
"Tunamtaka Lissu na wengine wanaofanya juhudi hizo kuacha mara moja, na badala yake tuvipe nafasi vyombo vinavyohusika vichunguze na matokeo ya uchunguzi huo yatangazwe hadharani ili tuwajue wabunge waliotusaliti", alisena Nape.

Alisema CCM inalaani vitendo vya rushwa hasa vinapohusishwa na viongozi ambao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kwamba rushwa ya namna hiyo inavuruga sana uchumi wa nchi, hivyo wanaohusika nayo haitoshi kuwaita wala rushwa tu bali ni zaidi ya wahujumu uchumi.
"Wakikithibitika ni muhimu hatua kali zichukuliwe kulikomesha kabisa hili na iwe fundisho kwa wengine", alisema Nape.

Kwa maoni yangu, Bw. Nape hakutakiwa kuyasema hayo aliyoyasema.
Au labda alitaka watu wajue uwepo wake, kwa maana kwamba hata lisilotakiwa kutolewa tamko basi atalitolea tu ili uwepo wake na nafasi ya cheo chake katika CCM ionekane.

Ninasema hivyo kwa sababu mbili zifuatazo.
1. Kwa vile amesema vyombo vinavyohusika vipewe nafasi ya kuchunguza, orodha ya Mhe. Lisu inavurugaje? Nadhani angeshukuru kwa kuwa ikidhihirika sivyo na Mhe. Lisu alishawataja basi Lisu ndiye atakayeumbuka japo hakusema kwamba ni wala rushwa.
2. Kama kweli Bw. Nape anaichukia rushwa, na kama kweli kauli hii "rushwa ya namna hiyo inavuruga sana uchumi wa nchi", imetoka mdomoni mwake, basi inatia shaka. Ni rushwa gani ambayo yeye anaiafiki? ameziwekea madaraja "categorized"?, kwamba hizi ruksa na zile si ruksa?

Namshauri awe makini katika kujibu hoja. Si lazima kila hoja kuitolea tamko, anajiangusha.
 
Kwa hiyo Nape amekubaliana na TL kuhusu Wabunge wa CCM aliowataja? Kwa hiyo anacholalamika yeye ni kutajwa wahusika wa CCM tu? Basi kama yeye anawajua wa Chadema, basi naye ATIRIRIKE!!!
 
Kauli ya Nape ni sawa na mwizi anapojitetea kuwa "sikuiba peke yangu". Sasa ndugu mwizi, kutuambia hukuiba peke yako kunakuondolea kosa lako? Nadhani mtego wa TL upo hapo, na leo Nape amenaswa na mtego kwa kukubali kuwa wale wabunge wa CCM aliowataja TL ni kweli walikula rushwa, ila tu anachoongezea Nape ni kuwa 'na wengine wapo' ambao hakuna anayethubutu kuwataja kwa kutokuwa na either ukweli au ushahidi!
 
wanaongea nini hawa mafisadi wala rushwa na wasioweza kukemea rushwa??!
tuangalie historia............
karamagi
msabaha
balali
ngeleja
mkulo
nyoni
......
......
sijui wanakataa nini sasa?
Mkuu unatumia kipimo kisichofaa kabisa,kwani unataka chadema wawepo kwenye mashindano ya nani ni fisadi zaidi ama kidogo kuliko mwenzake?kama wote mko uchi,haijalishi ni upande upi kati ya nyuma na mbele uko exposed,bottomline wote mko uchi,that's the way I look at it...
Rushwa ni rushwa,haijalishi tokea chama gani wala uwingi wake,wala nature yake,ni rushwa,period.
 
nape aje hapa atuambie ccm imemfanya nini omary baduwel aliyekamatwa red hended na m1 ya mlungula?
au atuambie ni tume ipi au ni uchunguzi upi ccm, iliwahi kuufanya kazi?
hapo ndipo tofauti ya chadema na ccm ilipo.
 
Sara Msafiri na Munde Tambwe wote wawili ni wabunge viti maalum.....hebu ona hasara kubwa inayotakana na sheria na mifumo iliyooza. Mzigo mzito wa mishahara na marupuru yao ni hasara kubwa kwa Taifa.

Na kama haitoshi, si tu kwamba hawana tija in any positive way, bali wana huge negative impact in a costly way; ni MAFISADI.

Jamani, ni nani aliyeilaani nchi hii?

Ronal Reagan,

..binafsi siamini kama hao kina mama/dada wana ujanja wa kufanya ufisadi walioufanya.

..kwa mtizamo wangu wapo vigogo nyuma ya mradi huo, na inawezekana hata huo ubunge wameupata kwa nguvu ya vigogo hao.

NB:

..kwa nini Nape hazunguki nchi nzima kushinikiza wabunge wala rushwa wajivue gamba, na kutimuliwa ubunge??
 
Huyu Nape akili ni za kushikiwa,, Omar Badwel kakamatwa na rushwa Live tena peke yake lakini Nape hatatoa hata tamko la kumlaani mbunge wake, leo kapima upepo anakuja na unafiki wake
 
--Yadai orodha yake inalenga kupotosha tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.
--yadaiwa kutaka kuwaokoa wabunge wa Chadema katika sakata hilo.
--Yasema suala la tuhuma za rushwa kwa wabunge lisigeuzwe kuwa la kisiasa.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelaani juhudi zinazofanywa na baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kupotosha na kuuficha ukweli juu ya tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.

Akizungumza na waandishi a habari leo mjini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, zipo juhudi za baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kulifanya suala la tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wabunge kuwa la kisiasa kwa malengo yao.

"Mfano mzuri wa juhudi hizi ni kitendo cha Tundu Lissu, ambaye ni mbunge wa Chadema na Mnadhimu Mkuu wa Kkambi ya upinzani Bungeni cha kutoa aliyoiita orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kufanya biashara na TANESCO na kwamba ndio watuhumiwa wa rushwa inayozungumziwa", Alisema Nape na kuongeza;

"Cha kushangaza orodha yake ilikuwa na wabunge wa CCM peke yake wakati wote tunajua kuwa yapo majina ya baadhi ya wabunge wa vyama vingine hasa Chadema, yanayotajwa katika orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa hii".

Nape alisema juhudi hizo za Lissu na wenzake zinalengo la kuuficha ukweli na kujaribu kuwalinda watuhumiwa wa uhalifu wanaotokana na Chadema.

"Tunamtaka Lissu na wengine wanaofanya juhudi hizo kuacha mara moja, na badala yake tuvipe nafasi vyombo vinavyohusika vichunguze na matokeo ya uchunguzi huo yatangazwe hadharani ili tuwajue wabunge waliotusaliti", alisena Nape.

Alisema CCM inalaani vitendo vya rushwa hasa vinapohusishwa na viongozi ambao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kwamba rushwa ya namna hiyo inavuruga sana uchumi wa nchi, hivyo wanaohusika nayo haitoshi kuwaita wala rushwa tu bali ni zaidi ya wahujumu uchumi.

"Wakikithibitika ni muhimu hatua kali zichukuliwe kulikomesha kabisa hili na iwe fundisho kwa wengine", alisema Nape.

Nape alisema CCM inawapongeza watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na Waziri wao Prof. Sospeter Muhongo, Manaibu wake, Massele na Simbachawene na Katibu Mkuu, Maswi kwa uzalendo, ujasiri na umahiri wao mkubwa waliouonyesha kwa muda mfupi waliokaa kwenye wizara hiyo.

"Tunaamini uzalendo walioonyesha katika kusimamia wizara hii,utaigwa na watumishi wengine wa umma katika kuhakikisha matumizi mazuri ya rasilimali za nchi zinalindwa ili kuhakikisha maisha bora kwa kila Mtanzania yanatimia. Tunaunga mkono jitihada zao", alisema Nape.

Alisema, pia CCM inalipongeza bunge kwa kuendelea kusimamia serikali na rasilimali za nchi katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa ya maendeleo.

"Tunawaomba waheshimiwa wabunge wazidi kutanguliza masilahi ya taifa mbele na uzalendo mkubwa katika shughuli zao za kila siku", alimalizia.

Kimsingi nape nnauye huwa anakurupuka hayuko makini,kama mtakuwa mmemsikia Lissu vizuri kabisa jana amewataja wabunge ambao anaushahidi nao na mwisho akasema kuhusu mh. zitto kabwe achunguzwe na hajazungumza kauli hata moja kuhusu tuhuma za wabunge wa chadema akimaanisha kuwatetea wabunge wa chadema....nape akae kimya tena asituudhi kabisa wabunge wangapi wa ccm wanatajwa , wanapelekwa kuchunguza takukuru taarifa hazionekani...mimi binafsi ninachoamini ni kwamba ccm inajikanyaga yenyewe chondechonde watanzania tushirikiane kuiua ccm.....
 
Jamani, au mimi sikuelewa? Mbona Lissu alizungumzia mgongano wa kimaslahi kwa baadhi ya wajumbe wa kamati. Sikuona tamko kuwa wamepewa rushwa! Sasa hili suala la rushwa limetoka wapi?

Labda anachezea akili za wananchi kama walivyozoea,kwasababu nimeona double standards zake kwenye hiyo habari.Upande mmoja akionekana kusema Lissu alichotaja si majina ya wanaotuhumiwa kwa rushwa,bali wale wenye migongano ya kimaslahi.Lakini at the same time ni kama anamlaumu kwa kutokuwataja na wa chadema kuwa wala rushwa,very confusing kwa wengine ambao hatukumwelewa alivyotaka.Kwa upande mwingine,ninaamini migongano ya kimaslahi inaweza kuwa chachu ya rushwa.
 
Katibu Uenezi Taifa CCM Ndg.Nape si unaona ujasiri wa CHADEMA kutaja wala rushwa bila chenga sasa ya nini kuzunguka mbuyu wataje watuhumiwa kama wabunge wanavyoona sasa tuhuma zinawachafua hata wale ambao hawahusiki:



VIdeo kwa hisani ya ITV TANZANIA ya YOUTUBE
 
Last edited by a moderator:
--
..........................................
Nape alisema CCM inawapongeza watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na Waziri wao Prof. Sospeter Muhongo, Manaibu wake, Massele na Simbachawene na Katibu Mkuu, Maswi kwa uzalendo, ujasiri .................


hivi huyu bwana mdogo nape...anajua kitu kinachoitwa consistency (au kinyume chake) kweli?
hivi lile bango alilombembea lowassa kuhusu richmond lina tofauti gani kimantiki na hao aliowataja hapo juu?

my point is.... kama kuna mtu aliharamisha kitendo cha lowassa wakati ule, tunategemea aendelee kuharamisha pia kitendo cha akina prof muhongo. halikadhalika kinyume chake.

siasa zisizokuwa na akili nchi hii zitaendelea kutufanya tudumae. we really need some crazy guy to occupy that white magogoni house at least for a term in order whip our asses kidogo!
 
:israel:Mwoga ni mwoga, jasiri haogopi kusema ukweli daima! Wenzako wamewataja na wewe kwa maslai ya taifa hili na namna unavyopigania chama chako wataje wahusika unaowafahamu!

"Time will tell and you will never walk alone"
 
Sasa Nape mbona unashindwa kutumia logic, Mwenzako Lissu kawataja wake na mpaka leo hakuna mtuhumiwa hata mmoja kati ya wale waliotajwa amejitokeza na kukanusha, sasa ww unaogopa nini kuja na vithibitisho?

THINK BIG
 
CCM ni aibu hata kuitaja.Inanuka na kuchekesha. TL kataja anaowafahamu bila woga kwa vile ushahidi upo,Nape kama kuna nyongeza na ushahidi upo si awataje kigugumizi na kulialia inasaidia nini?
 
Go Nape go nape waambie hao mabwege wanakurupuka tu wametoka baa na kutaja list Once there was a young girl who decided to take a short cut home from school. The fastest way to her house was to cut through an alley. The girl approached the alley way. She saw a man standing like he was waiting for someone. She said a prayer:"Dear God please lead me through this alleyway, safe and unharmed. Amen." The girl walked through the alley and past the man. Later on that night the girl decided to watch the news. She saw that man had murdered and raped a young girl. The police said the man told them another girl had passed through the alley 10 minutes before. They asked him why he didn't attack the first girl. He said there was a man walking beside her...
God walks with us. We deny His presences but He is always there. 95% of people will just read this and shut their phones, but be among the 5% that will read & send to friends! Don't be ashamed to admit you're a Child of God..
 
The same OLD STORY, Debe tupu haliachi KUTIKA!

Kama TL ametaja Wabunge tu wa CCM na kuacha wa CDM, kwanini Nape naye asiwataje wa CDM waliochwa?

Kati ya TL na Nape nani anayelinda ufisadi? TL aliyewataja kwa majina watuhumiwa au Yeye Nape
anayeficha majina ya watuhumiwa?.

Hivi mpaka hapa Nape na CCM bado hawajaona tofauti ya utendaji kazi wa CDM na CCM. Endeleeni kutumia vichwa vyenu kufunga nywele wakati wenzenu CDM wanatumia pia kwa kufikiri!

Mh, unanikumbusha Werema mtaalam wa kutumia kichwa kwa kufuga nywele. Naamini Nape ameelewa, maana naona hoja hapo juu ni kama darasa tosha.
 
Nape acha kulialia, kama unawajua hao wabunge wa chadema wala rushwa wataje ili twende sambamba
 
Back
Top Bottom