CCM yaishukia CHADEMA suala la TUHUMA za Rushwa kwa wabunge

UJINGA MTUPU na GIZA LA UFISADI NDILO LINAWATAWALA WATU WA CCM, nafikiri kama anadhani kuwa hao watu CHADEMA wametajwa wasio sahihi au kwa upendeleo naye ANGETAJA ANAOJUA NI CDM au wapinzani wengine.

Imeandikwa "watu wangu hufa kwa kukosa maarifa",

kwanini NAPE NNAUYE asitaje
WALA RUSHWA WA CDM?

Nani atasikia KILIO chako NAPE hata kama ni KWELI kuwa wamehongwna a lakini unashindwa kuthibitisha tuhuma zao.....PUMBAVU MWANADAMU USIYEJUA WAKATI WAKO na ULAANIWE wewe usiyejua MAJIRA yako.
is this all u have got in ur mind....?
 
naona watu hawajiamini kabisa kwa kujihami wakataja list ya uongo..jamani hao watu wenu mnaowaamini hawapo smart ...ndio maana kauli zao hazieleweki...kama siasa tufanye siasa na kama kujenga nchi tuijenge....usione kuna watu wako kimya ukadhani hawatambui uozo wenu wanatambua na sasa hukumu ndio inakuja.
 
--Yadai orodha yake inalenga kupotosha tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.
--yadaiwa kutaka kuwaokoa wabunge wa Chadema katika sakata hilo.
--Yasema suala la tuhuma za rushwa kwa wabunge lisigeuzwe kuwa la kisiasa.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelaani juhudi zinazofanywa na baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kupotosha na kuuficha ukweli juu ya tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.

Akizungumza na waandishi a habari leo mjini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, zipo juhudi za baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kulifanya suala la tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wabunge kuwa la kisiasa kwa malengo yao.

"Tunamtaka Lissu na wengine wanaofanya juhudi hizo kuacha mara moja, na badala yake tuvipe nafasi vyombo vinavyohusika vichunguze na matokeo ya uchunguzi huo yatangazwe hadharani ili tuwajue wabunge waliotusaliti", alisena Nape.

Alisema CCM inalaani vitendo vya rushwa hasa vinapohusishwa na viongozi ambao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kwamba rushwa ya namna hiyo inavuruga sana uchumi wa nchi, hivyo wanaohusika nayo haitoshi kuwaita wala rushwa tu bali ni zaidi ya wahujumu uchumi.

"Wakikithibitika ni muhimu hatua kali zichukuliwe kulikomesha kabisa hili na iwe fundisho kwa wengine", alisema Nape.


"Tunawaomba waheshimiwa wabunge wazidi kutanguliza masilahi ya taifa mbele na uzalendo mkubwa katika shughuli zao za kila siku", alimalizia.

Huyu Nepi Naye ni mropokaji tu hana lolote huyu.

Je, anataka kuwaambi watanzania kuwa CCM ndiyo kwanza wameanza kusikia habari za rushwa??? Apeleke ujinga wake huko.Anasemaje kuhusu Fisadi na mla Rushwa Mkuu Bwana Andrew Chenge ambaye ni mtuhumiwa wa Chenji ya Rada lakini leo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi??Mbona CCM hawajamchukulia hatua kali kama anavyobwabwaja???Kuna mbunge Omari Badweli-Bahi CCM aliyekamatwa red handed na PCCB kwa kupokea Rushwa ya 1 milioni na bado anadunda Bungeni, mbona CCM hawajamchukulia hatua kali???

Kwanini vyombo vya habari huwa havihoji maswali kama haya wanapokuwa kwenye Press conference na hawa viongozi vihiyo aina ya kina Nepi???

Siasa bwana kweli mchezo mchafu!!!!
 
wanaongea nini hawa mafisadi wala rushwa na wasioweza kukemea rushwa??!
tuangalie historia............
karamagi
msabaha
balali
ngeleja
mkulo
nyoni
......
......
sijui wanakataa nini sasa?
Nalaila Kiula
Lowasa
Chenge
Yona
Mramba
..........
..........
.........
endeleeni wapo wengi
 
Jamani kamati ya BUNGE vp kuhusu utetezi wa Mnyika kumtaja Nchema kwenye tuuma za EPA? napata shida sana na utendaji wa serikali hii pamoja na Bunge lake!!!!!!!! wabunge wote wa ccm wangeuwawa kwa bomu ili tuanze nchi mpya
 
it will take so much for the people of this national to realize there self worth...!
 
RUSHWA Bungeni wahusika ni CCM na CHADEMA
VIWANJA gezaulole wahusika ni CCM,CHADEMA n.k
Haya tuendelee kuwatetea CCM na CHADEMA huku wao wanatafuna kwa chinichini
 
Wako wapi wote hao uliowataja.CCM imewashughulikia kwa staili tofauti. Tafuta hoja nyingine
 
Wewe Makoye unaakili za kimakoye makoye (matatizo tatizo hv). Uliambiwa CCM ni Mahakama au Takukuru. Unataka CCM wawe wakurupukaji kama CDM! Lazima CCM ya watanzania ionyeshe ukomavu na utawala/uongozi wa sheria. CCM haiwezi kuwa polisi, mahakama na magereza. Nyinyi CDM ya wachagga(na wewe msukuma sijui umetoka nayo wapi) endeleeni kuwadanganya watanzania kuwa UFISADI ni SERA japo ukweli umedhihiri kuwa ufisadi ni hulka/ubinafsi.
 
Kuna Mbunge alikamatwa majuzi akiomba rushwa hapa jijini sijui anaitwa nanin naye kesi yake Nape anasemaje ? Yaani Nape akili zake sijui vipi .Chadema wamewataja CCM now Nape nawe jifanye unafanya siasa wataje wa Chadema tuanzie happo
 
Jamii forum liko biased, ukitoa maoni mazito ya kupinga kauli za wana cdm, hutaiona thread hewani lakini matusi ya wana cdm yanapewa kipaumbele. Naomba yeyote ambaye si pro-cdm aniunganishe na mtandao mwingine wa uwazi zaidi ambao unatoa fursa sawa kwa wote kutoa na kujibu huja hasa za wapuuzi hawa wa cdm. I HATE JAMII FORUM FOR THEIR BIASNESS. Fu*&*&*
 
Sasa mbona hamna alichosema nape,kama amekanusha aanike ukweli ili sisi ambao tuko mbali na screen tujue sterling wa movie nan?
 
wanaongea nini hawa mafisadi wala rushwa na wasioweza kukemea rushwa??!
tuangalie historia............
karamagi
msabaha
balali
ngeleja
mkulo
nyoni
......
......
sijui wanakataa nini sasa?

lowasa
ben mkapa
 
Swala la kuwavua magamba Lowasa na Chenge amemaliza? Mbona ameanza kurukia mengine!?
 
The same OLD STORY, Debe tupu haliachi KUTIKA!

Kama TL ametaja Wabunge tu wa CCM na kuacha wa CDM, kwanini Nape naye asiwataje wa CDM waliochwa?

Kati ya TL na Nape nani anayelinda ufisadi? TL aliyewataja kwa majina watuhumiwa au Yeye Nape
anayeficha majina ya watuhumiwa?.

Hivi mpaka hapa Nape na CCM bado hawajaona tofauti ya utendaji kazi wa CDM na CCM. Endeleeni kutumia vichwa vyenu kufunga nywele wakati wenzenu CDM wanatumia pia kwa kufikiri!

well said
 
Back
Top Bottom