jogi
JF-Expert Member
- Sep 25, 2010
- 25,558
- 25,323
Mkuu hiyo nukuu ya mwalimu we acha tu!
Kiukweli Mwalimu aliipenda nchi yake.
Mkuu hiyo nukuu ya mwalimu we acha tu!
Pasco, Ulivyoileta thread yako inaonyesha wazi uko upande gani, vijana hawatatusaidia chochote kama hawana vigezo vinavyohitajika, na uzuri wake umevitaja. Lile bunge si bunge la kisiasa kama bunge letu la ndani la NDIYOO na kupiga meza, linahitaji mtu mwenye uwezo wa kuchambua sheria na mchumi.Wanabodi, Wazee hao wamekuja na viogezo vipya vitatu ambavyo sikuwahi kuvisikia kwenye sifa za uongozi za CCM hata mara moja!.
1. Umri- eti CCM ichague wagombea wenye umri mkubwa kama uthibitisho wa long expiriance ya uzoefu wa muda
mrefu! .
2. Awe na shahada ya Chuo Kikuu ama ya Sheria, ama ya Uchumi kwa hoja kuwa kule kuna issues za kisheria na
issues za kiuchumi!.
3. Uzoefu wa kidplomasia.
Lengo la vigezo hivi ni kuwaengua wagombea vijana!
unamaana vijana wa cccm wamelelewa kama lulu
Hivi from nowhere kumpeleka "a fresh graduate" kuwakilisha interest za Taifa kwenye Bunge la Afrika Mashariki tunajitendea haki kama Taifa? Mfano madhara ya ardhi kuingizwa au kutoingizwa kwenye Jumuia huyo kijana aliyetoka chuo anafahamu? Unapozungumza kuwa na sarafu moja ndani ya mataifa yanayotofautiana sana katika pato la Taifa "GDP, "skilled labour", "balance of payment", "Industries" n.k. huyo mtoto anafahamu madhara ya hayo yote kwa ukuaji wa Taifa? Iweje "Government Bonds denominated in Euro" ziuzwe Jamhuri ya Ireland na Ujermani za Ujermani zifanye vizuri lakini Ireland zisifanye vizuri wakati sarafu ni moja?
Kwa ajili ya ustawi wa Taifa ni vizuri hivyo vigezo vikazingatiwa na kama waliopitishwa hawana hivyo vigezo, zoezi zima lirudiwe. Kwa maana nyingine ilitakiwa vigezo viwekwe hadharani kabla ya waombaji kujaza fomu.
Wanabodi,
Nyakati za uchaguzi mjini Dodoma, ni nyakati, za harakati kubwa na pilika pilika nyingi katika mji wa Dodoma, hivyo sisi wenye interest na siasa za nyumbani, tupatapo nafasi, hupenda kupeleka pua japo kidogo mjini Dodoma japo kunusa tuu kile kinachoendelea.
Miongoni mwa pilika pilika kubwa za kisiasa mjini Dodoma kwa sasa, ni harakati za kugombea ubunge wa Afrika Mashariki ambapo vikao vya wazi na vya siri vimekuwa vikiendelea mjini hapa, huku wagombea wakijitahidi kuandaa "the winning coalition", huku wabunge ambao ndio walengwa wakijikuta katika wakati mgumu kuchagua kambi ya mgombea gani waiunge mkono!.
Mvutano mkubwa wa vuta nikuvute, shika nikushike ni miongoni mwa wagombea 9 wa CCM wanaogombea nafasi 3, hivyo ushindani ni mkubwa kuliko huku kila mmoja akiepuka kudondokea miangoni mwa wale 6 wataopigwa chini, hivyo pia kuna harakati za chini chini kila mmoja wao akifanya jitihada za kujinusuru.
Ushindani mkubwa ni kati ya wale wanaowaunga mkono vijana wa kisasa ambao wana uughwaji mkubwa na wana CCM wanaotaka mageuzi ya ukweli dhidi ya wagombea wazee ambao tayari ni spent force, watakuwa hawana jipya la kuleta zaidi ya kumendea fungu la kustaafu kwa heshima!.
Kufuatia upepo kuwavumia vizuri wagombea vijana, kuna tetesi kuwa wagombea wazee kwa kuwatumia wazee wa CCM, wamejipanga kuwaundia zengwe wagombea vijana ili kuwapiga panga la kimtindo!.
Zengwe hili linapikwa chini kwa chini ambapo kwa kuamua kuandaa vigezo vitatu vya sifa mpya za wagombea wa CCM ambavyo wata lobby kuvipeleka kwenye caucus ya CCM over the weekend ili vipitishwe hivyo kuwapiga panga wagombea vijana wenye uugwaji mkubwa wa wabunge wengi.
Zengwe hilo ambalo msingi wake mkubwa ni kupiga fitna ili kuwapiga chini wagombea vijana.
Wazee hao wamekuja na viogezo vipya vitatu ambavyo sikuwahi kuvisikia kwenye sifa za uongozi za CCM hata mara moja!.
1. Umri- eti CCM ichague wagombea wenye umri mkubwa kama uthibitisho wa long expiriance ya uzoefu wa muda
mrefu! .
2. Awe na shahada ya Chuo Kikuu ama ya Sheria, ama ya Uchumi kwa hoja kuwa kule kuna issues za kisheria na
issues za kiuchumi!.
3. Uzoefu wa kidplomasia.
Lengo la vigezo hivi ni kuwaengua wagombea vijana!
Baadhi ya wabunge wa EALA ambao ambao hawagombei tena, wamepiga kambi bungeni hapa wakiwa na wagombea wao kwapani, wengi wakiwa ni hawa wazee ambao ni spent force!.
Wakati huo huo, nimehudhuria tafrija moja mahali, usiku huu hapa Dodoma, kufumba kufumbua, kumbe ni tafrija ya kampeni ya wazee fulani wawili, ambao walituamkia wote kwa shikamoo!.
My Take.
CCM kama chama, kimekaa mkao wa kifo, watu pekee wanaoweza kukinusuru CCM na kifo cha aibu, ni hawa wagombea vijana wa kileo ambao sasa wanataka kupigwa zengwe. Kama kweli itatokea CCM ikawapiga zengwe hawa vijana, hiyo ndio itakuwa uthibitisho wa CCM ni chama mfu, hakiwahitaji vijana wa kisasa, wito wangu kwa vijana hawa ni kuwa baada ya kupingwa panga, hameni CCM, achaneni na CCM ili mjiokoe nafsi zenu kwa 2015, jiungeni na vyama vinavyo kubali nguvu ya vijana, vinginevyo down the drain, mtakwenda chini na CCM yenu!.
Asante.
Pasco.
Ni type ya akina wema, Lulu....unamaana vijana wa cccm wamelelewa kama lulu
Naomba nikukumbushe picha ya Nape Nnauye kwenye kile kikao cha NEC ambacho Lowassa alimnyooshea kidole JK. Ile picha ya Nape akisalimiana na Lowassa na pembeni yuko Sumaye, ilikuwa na mengi sana. Yule hakuwa Nape ambaye alikuwa anatamba kwenye majukwaa, siku hiyo alikuwa mdogo kama piriton.