CCM Yaanza Rafu!, Yaandaa Zengwe Kuwapiga Panga Baadhi ya Wagombea!

Pasco anapaswa asome mara tatu au nne akuelewe, si kwa ugumu wa lugha, hasha! ni kwa ukweli wa maandishi mstari kwa mstari, neno kwa neno.
kwa kuongezea mfano, Mwigulu ambaye ni mhazina wa ccm, anajidai kumuuliza pinda kuhusu mpango wa chenji ya rada, kanakwamba hajui, usitegemee huyu kijana kuyatenda matakwa ya wananchi, atatufanyia ukanumba tu, kumbe mzinzi mkubwa.
Mkuu Jogi, kweli mimi ni mzito kuelewa hivyo nimesoma mara 3 ndio kwanza naanza kuelewa ndio maana mpaka sasa sijamjibu Keil!.
 
pasco mbona hugombei??nimemuliza william, kwenye ile thread yake ya kumsifu nasari lakini hakujibu'nataka kujua next step kama akishindwa hizo mbio zake''atarudi new york au tumtafutie kazi hapa hapa??
Sigombei kwa sababu sina chama!. 2015 nagombea mahali kama mgombea binafsi!.
 
Pasco,

Title na contents haviendani ... mimi nilidhani ni Uongozi wa CCM, kumbe ni rafu za wagombea wao kwa wao? Hilo ni kawaida sana ndani ya CCM.

Hoja ya elimu inaweza kuwa na mashiko, ingawa mwakilishi yeyote wa CCM huwa ninamchukulia kwamba anawakilisha maslahi ya chama chake kwanza. Kwa hiyo kwangu mimi sioni tofauti whether ni kijana au mzee, wote ni wale wale tu, "opportunists".

Mfano mzuri ni kwenye mswada wa Katiba sikuona hata kijana mmoja kati hao mnaowaita waleta mabadiliko ndani ya CCM aliyesimama na kutetea maslahi ya Taifa. Sana sana huwa tunawaona wako kimya, wakitoka kwenye vikao wakiwa huku kitaa ndo wanakuja na tambo za kufa mtu kwamba wao ndo wataleta mabadiliko ndani ya chama. Mabadiliko my foot!

Piga ua galagaza, kuna vijana ambao hata wafanye nini hawatavuka kiunzi, Papaa Mkulu Mamvi hatawaachia wapenye. Wao wakomae na kura za kutoka kwa wapinzani. Lakini wanachoniboa hao vijana, wakishaingia huko ndani hawaleti mabadiliko tunayoyataka, wanaishia kuwa akina ndiyo mzee na kuanza kutumia lugha ya kejeri kwa wapinzani na huku ni wabunge hao hao wa upinzani waliowasaidia kuingia kwenye EALA.

Naomba nikukumbushe picha ya Nape Nnauye kwenye kile kikao cha NEC ambacho Lowassa alimnyooshea kidole JK. Ile picha ya Nape akisalimiana na Lowassa na pembeni yuko Sumaye, ilikuwa na mengi sana. Yule hakuwa Nape ambaye alikuwa anatamba kwenye majukwaa, siku hiyo alikuwa mdogo kama piriton. Juzi kati hapa kwenye mgomo wa Madaktari, Kigwangalla walitaka kumtoa macho wabunge wenzake wa magamba. Baada ya hapo Kigwa hakuongelea tena swala la mgomo wa madaktari. Hawa ndio vijana wa kuleta mabadiliko kweli?

Kijana yeyote ambaye yuko CCM akiwa na ndoto ya kuleta mabadiliko, anaota ndoto ya mchana. CCM hawataki mabadiliko na hata Katiba Mpya wamelazimishwa, hata hizi kauli za Taifa kwanza wanazitoa kwa kujilazimisha. CCM wanataka kila kitu kibaki kama kilivyo, ndo maana hata kwenye hizi kampeni za chaguzi ndogo akina Mwigulu wanatuhumiwa kumwaga hela nyingi ili washinde. Sasa vijana kama hao wana tofauti yoyote na status quo ambayo inanunua uongozi? Hapa tunadanganyana tu.

Mimi ninawaona ni vijana "opportunists" tu ambao wanataka ulaji na ndio maana hata wakiwa Bungeni huwezi kuwasikia wakikemea uozo au uovu. Mtu anayetanguliza Taifa kwanza angewapasha wabunge wenzake wa magamba ambao walikuwa wajadili mswaada wa sheria ya kuandika katiba kwa mipasho na ushabiki.

Hakuna mabadiliko yatakuja kutokea ndani ya CCM, mwaka mzima sasa tangu secretariat ibadilishwe, hakuna kipya nilichokiona. Walijitutumua mwanzo, sasa wamerudi kwenye status quo na hakuna ambaye anaongelea kuvua gamba wala mabadiliko.
Keil, nakubaliana na wewe, but in an event you are stuck somewhere in between two devils, and you have no choice, choose the lesser!. CCM are devils, we have no choice we have to live with them!. Kwenye uchaguzi huu wa EALA, wether we love or we don't, we have to choose 3 devils alongside an angel!, better are the young and energetic devils than the old dying devils!.

And on the devils, we are supposed not only to choose the lesser, but better a devil we know (young), than a devil we don't know!.
 
Wanabodi,

Nyakati za uchaguzi mjini Dodoma, ni nyakati, za harakati kubwa na pilika pilika nyingi katika mji wa Dodoma, hivyo sisi wenye interest na siasa za nyumbani, tupatapo nafasi, hupenda kupeleka pua japo kidogo mjini Dodoma japo kunusa tuu kile kinachoendelea.

Miongoni mwa pilika pilika kubwa za kisiasa mjini Dodoma kwa sasa, ni harakati za kugombea ubunge wa Afrika Mashariki ambapo vikao vya wazi na vya siri vimekuwa vikiendelea mjini hapa, huku wagombea wakijitahidi kuandaa "the winning coalition", huku wabunge ambao ndio walengwa wakijikuta katika wakati mgumu kuchagua kambi ya mgombea gani waiunge mkono!.

Mvutano mkubwa wa vuta nikuvute, shika nikushike ni miongoni mwa wagombea 9 wa CCM wanaogombea nafasi 3, hivyo ushindani ni mkubwa kuliko huku kila mmoja akiepuka kudondokea miangoni mwa wale 6 wataopigwa chini, hivyo pia kuna harakati za chini chini kila mmoja wao akifanya jitihada za kujinusuru.

Ushindani mkubwa ni kati ya wale wanaowaunga mkono vijana wa kisasa ambao wana uughwaji mkubwa na wana CCM wanaotaka mageuzi ya ukweli dhidi ya wagombea wazee ambao tayari ni spent force, watakuwa hawana jipya la kuleta zaidi ya kumendea fungu la kustaafu kwa heshima!.

Kufuatia upepo kuwavumia vizuri wagombea vijana, kuna tetesi kuwa wagombea wazee kwa kuwatumia wazee wa CCM, wamejipanga kuwaundia zengwe wagombea vijana ili kuwapiga panga la kimtindo!.

Zengwe hili linapikwa chini kwa chini ambapo kwa kuamua kuandaa vigezo vitatu vya sifa mpya za wagombea wa CCM ambavyo wata lobby kuvipeleka kwenye caucus ya CCM over the weekend ili vipitishwe hivyo kuwapiga panga wagombea vijana wenye uugwaji mkubwa wa wabunge wengi.

Zengwe hilo ambalo msingi wake mkubwa ni kupiga fitna ili kuwapiga chini wagombea vijana.

Wazee hao wamekuja na viogezo vipya vitatu ambavyo sikuwahi kuvisikia kwenye sifa za uongozi za CCM hata mara moja!.

1. Umri- eti CCM ichague wagombea wenye umri mkubwa kama uthibitisho wa long expiriance ya uzoefu wa muda
mrefu! .
2. Awe na shahada ya Chuo Kikuu ama ya Sheria, ama ya Uchumi kwa hoja kuwa kule kuna issues za kisheria na
issues za kiuchumi!.
3. Uzoefu wa kidplomasia.

Lengo la vigezo hivi ni kuwaengua wagombea vijana!

Baadhi ya wabunge wa EALA ambao ambao hawagombei tena, wamepiga kambi bungeni hapa wakiwa na wagombea wao kwapani, wengi wakiwa ni hawa wazee ambao ni spent force!.

Wakati huo huo, nimehudhuria tafrija moja mahali, usiku huu hapa Dodoma, kufumba kufumbua, kumbe ni tafrija ya kampeni ya wazee fulani wawili, ambao walituamkia wote kwa shikamoo!.

My Take.
CCM kama chama, kimekaa mkao wa kifo, watu pekee wanaoweza kukinusuru CCM na kifo cha aibu, ni hawa wagombea vijana wa kileo ambao sasa wanataka kupigwa zengwe. Kama kweli itatokea CCM ikawapiga zengwe hawa vijana, hiyo ndio itakuwa uthibitisho wa CCM ni chama mfu, hakiwahitaji vijana wa kisasa, wito wangu kwa vijana hawa ni kuwa baada ya kupingwa panga, hameni CCM, achaneni na CCM ili mjiokoe nafsi zenu kwa 2015, jiungeni na vyama vinavyo kubali nguvu ya vijana, vinginevyo down the drain, mtakwenda chini na CCM yenu!.

Asante.

Pasco.[/QUOTE

Hakuna cha vijana wala wazee. Km bado unaamini CCM inaweza kubadilishwa na vijana unajidanganya. Lichama limeshakufa hilo, hakuna cha vijana wala wazee. Yeyote anayeshabikia CCM kwa nyakati hizi ama ana maslahi binafsi na anafaidika na huo mfumo mbovu wake ama ni kichaa anapaswa aende milembe. Hakuna cha kuwahurumia hao vijana wanaojichafua kutafuta njia nyepesi ya kupata hela kupitia lichama mfu. Acha wawafanyie mizengwe ndo wawe na adabu
 
Wagombea wote wa CCM bila kujali umri wao wanatabia zianazofanana za mizengwe, ufisadi na hujuma katika chaguzi, wala huwezi kuwatofautisha!
 
1. Umri- eti CCM ichague wagombea wenye umri mkubwa kama uthibitisho wa long expiriance ya uzoefu wa muda
mrefu! .
2. Awe na shahada ya Chuo Kikuu ama ya Sheria, ama ya Uchumi kwa hoja kuwa kule kuna issues za kisheria na
issues za kiuchumi!.
3. Uzoefu wa kidplomasia.

Ndio maana William alikuja fasta fasta huku JF jana akiomba kura za wapinzani kwa kumfagilia Nassari.
Yaani hivyo vigezo hapo juu ha-meet hata kimoja.
Hana shahada ya sheria ama uchumi.
Kwenye thread yake alisema haendekezi diplomasia
Labda kigezo cha umri anaweza akafanya kama Lulu.
 
Wagombea wote wa CCM bila kujali umri wao wanatabia zianazofanana za mizengwe, ufisadi na hujuma katika chaguzi, wala huwezi kuwatofautisha!


eg....pale waliposema Seleli hana mvuto then wakapiga chini na kumchukua mshindi wa chini yake Mhesh Kigwangalla
 
William Malecela anaweza kupigiwa debe kwa kuwa ni kijana, lakini hana hadhi hata punje ya kuwa Mbunge wa EAC
 
Keil, nakubaliana na wewe, but in an event you are stuck somewhere in between two devils, and you have no choice, choose the lesser!. CCM are devils, we have no choice we have to live with them!. Kwenye uchaguzi huu wa EALA, wether we love or we don't, we have to choose 3 devils alongside an angel!, better are the young and energetic devils than the old dying devils!.

And on the devils, we are supposed not only to choose the lesser, but better a devil we know (young), than a devil we don't know!.

Ndugu yangu Pasco,

Bado nasimama pale pale, kwamba hakuna mwenye afadhali, awe mzee au kijana. Hao unaosema kwamba wana nafuu kwa kuwa tunawafahamu, nadhani unawafahamu nusu nusu.

Young and energetic, but Very ARROGANT! Mifano tunayo hapa hapa akina Lau Masha, Ngeleja na vijana wengineo, wamefanya nini? Sana sana naona wanaishia kutisha watu na wanazidi kushiriki kuifisadi nchi.

Halafu hawa vijana ndo balaa, wakiitwa na kufokewa, wananywea na kuufyata wala huwasikii tena. Kwa hiyo hata kama hoja yake ina mashiko hawezi kuendelea nayo kwa kuwa anajua anaweza kushughulikiwa na vikao vya chama.

Hao wazee angalau wana nafuu, wakishakuwa frustrated na system wanajiropokea/fyatuka watakavyo, liwalo na liwe na hawawezi kumwita na kumfokea kwenye vikao vya chama. Tangu Sitta anyimwe Uspika, kwa yale yote ambayo ameisharopoka/fyatuka, mpaka sasa angekuwa alishatemwa uanachama na kupokwa ubunge wake.

Nape anaamini Lowassa ni fisadi ,,,, wenye chama wanaamini Lowassa ni msafi. Baada ya hapo Nape kimyaaaaaaaaaaaaaa!
 
Hivi from nowhere kumpeleka "a fresh graduate" kuwakilisha interest za Taifa kwenye Bunge la Afrika Mashariki tunajitendea haki kama Taifa? Mfano madhara ya ardhi kuingizwa au kutoingizwa kwenye Jumuia huyo kijana aliyetoka chuo anafahamu? Unapozungumza kuwa na sarafu moja ndani ya mataifa yanayotofautiana sana katika pato la Taifa "GDP, "skilled labour", "balance of payment", "Industries" n.k. huyo mtoto anafahamu madhara ya hayo yote kwa ukuaji wa Taifa? Iweje "Government Bonds denominated in Euro" ziuzwe Jamhuri ya Ireland na Ujermani za Ujermani zifanye vizuri lakini Ireland zisifanye vizuri wakati sarafu ni moja?


Kwa ajili ya ustawi wa Taifa ni vizuri hivyo vigezo vikazingatiwa na kama waliopitishwa hawana hivyo vigezo, zoezi zima lirudiwe. Kwa maana nyingine ilitakiwa vigezo viwekwe hadharani kabla ya waombaji kujaza fomu.
 
Hivi ule utafiti wa Mukama kuhusu CCM kupoteza mvuto ulisemaje?

Hivi Mukama ametekeleza kwa kiasi gani mapendekezo yaliiyotolewa kwenye utafiti huo? Au ndio amekuja kukimaliza chama?
 
Mkuu Jogi, kweli mimi ni mzito kuelewa hivyo nimesoma mara 3 ndio kwanza naanza kuelewa ndio maana mpaka sasa sijamjibu Keil!.

"Nimekarudiaaa, nimekarudiaaa sijaona tatizo" by Julius K. Nyerere akikielezea kitabu "Azimio la arusha" kwa hiyo mkuu Pasco, usifadhaike moyoni mwako, kurudia kupasoma hakutoi ujumbe wa uzito wa kuelewa.
 
Hivi from nowhere kumpeleka "a fresh graduate" kuwakilisha interest za Taifa kwenye Bunge la Afrika Mashariki tunajitendea haki kama Taifa? Mfano madhara ya ardhi kuingizwa au kutoingizwa kwenye Jumuia huyo kijana aliyetoka chuo anafahamu? Unapozungumza kuwa na sarafu moja ndani ya mataifa yanayotofautiana sana katika pato la Taifa "GDP, "skilled labour", "balance of payment", "Industries" n.k. huyo mtoto anafahamu madhara ya hayo yote kwa ukuaji wa Taifa? Iweje "Government Bonds denominated in Euro" ziuzwe Jamhuri ya Ireland na Ujermani za Ujermani zifanye vizuri lakini Ireland zisifanye vizuri wakati sarafu ni moja?


Kwa ajili ya ustawi wa Taifa ni vizuri hivyo vigezo vikazingatiwa na kama waliopitishwa hawana hivyo vigezo, zoezi zima lirudiwe. Kwa maana nyingine ilitakiwa vigezo viwekwe hadharani kabla ya waombaji kujaza fomu.

Nanusa syndicate kwenye jumuiya hii wanayogombea uwakilishi(ubunge) inataka kuonekana hawa madogo wanaweza kupata nafasi ambazo hawajui kilicho nyuma ya pazia la jumuiya (kama lusinde ambavyo alijikuta kapewa jukumu asilojua mustakabali wake)
 
"Nimekarudiaaa, nimekarudiaaa sijaona tatizo" by Julius K. Nyerere akikielezea kitabu "Azimio la arusha" kwa hiyo mkuu Pasco, usifadhaike moyoni mwako, kurudia kupasoma hakutoi ujumbe wa uzito wa kuelewa.

Mkuu hiyo nukuu ya mwalimu we acha tu!
 
Hivi ule utafiti wa Mukama kuhusu CCM kupoteza mvuto ulisemaje?

Hivi Mukama ametekeleza kwa kiasi gani mapendekezo yaliiyotolewa kwenye utafiti huo? Au ndio amekuja kukimaliza chama?

Utafiti ulisema mambo makuu yafuatayo:
1. Mafisadi wachache ndani ya CCM wamesababisha CCM nzima ipoteze mvuto kwa kuwa kinaonekana ni chama cha mafisadi na kwamba mafisadi hao ndio wanakipaka matope. Suggestion - Fukuza kwenye uongozi. Rostam pekee ndo alitoka

2. Mitandao ya Kijamii ilitumika sana kukipaka matope Chama cha Mapinduzi, na hasa JamiiForum - Suggestion teuwa vijana ili watumie mitandao ya jamii kujibu hoja za kukipaka matope chama.

3. Utaratibu wa Kura za maoni katika kuteua wagombea ubunge, ulikigharimu chama kwa kuwa sehemu nyingi ambako upinzani ulikuwa mkali kulikuwa na matatizo ya uteuzi wa wagombea. Suggestion - maamuzi ya wapiga kura za maoni yaheshimiwe, NEC na CC wakate jina la mgombea iwapo wana ushahidi wa kutosha

Operation Vua Gamba imedunda. Walipoona imedunda wakagundua kwamba EL ana nguvu/support kubwa kwenye NEC na CC, ndipo wakaamua kuvunja CC. Baada ya kuvunja CCM wakasema wanabadilisha baadhi ya vipengele vya Katiba kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu, kuzuwia wabunge wasigombee na pia ujumbe wa NEC iwe ni full time job na kwamba watakuwa wanatoka wilayani. Hapa wanafikiri wanamzuwia Lowassa lakini naona wanakinga upepo usipite kwenye dirisha la nyavu.

Kwa hiyo wakasema operation vua gamba haikueleweka, ilimaanisha kwamba ni mabadiliko ndani ya chama kuanzia kwenye shina mpaka Taifa. Sasa wale waliokuwa wanawa-refer kwamba ni viongozi wajitoe wenyewe, wako huko kwenye mashina? Hivi wanaweza kupoteza muda kubembeleza kiongozi wa tawi au shina kumfukuza eti wamwambie ajitoe mwenyewe? Mbona Katibu wa CCM wa Mkoa wa Singida walimtosa? Mbona Kilumbe Ng'enda wamemtosa bila hata kumwomba ajitoe?

Kwa kifupi, Mukama hajaweza kutekeleza hata moja kati ya yote yale aliyopendekeza. Mzee Makamba huko aliko nadhani anacheka tu na kushangilia. Sana sana nana wamejuzia jamii ya Malaria Sugu hapa ndani ambao hata hawawezi kujenga hoja zenye mashiko.

Nadhani Mukama amepewa chama ili akichimbie kaburi, sisi tutamsadia kukizika. Kilishakufa tayari kinachosubiriwa ni maziko tu na wazazi wa chama (TANU na ASP) walishatangulia mbele ya haki, sisi wapambe tutasaidia kuweka matanga na kuchemsha chai kuwapa akina Rejao na wenzake.
 
Back
Top Bottom