CCM watelekeza mamia ya watu Mwanza waliowachukua vijijini kuwaleta kwenye maadhimisho yao

leteni picha wakuu maana hii ni ishu kubwa sana , ni ulaghani mkubwa wa kisiasa
 
Sijui kwanini huwa hawakomi, miaka yote huwa wanasombwa hivyohivyo halafu wanatelekezwa lakini hawajifunzi wala hawakomi, afadhali waliotoka Mag, misungwi na kwimba wanaweza kutembea haya nie kina bageshi mliotoka Sengerema na Geita mtarudije, sijui mtakatiza ziwani
 
Bado wanasherekea mradi wa Nape wa Miaka 35 ya Magamba kwa matembezi ya hiari hapo jijini Mwanza.
 
mkuu unajua CDM walifanya mikutano ya siri na katika maadhimio ya kikao walikubaliana kuwasomba makada wao kwa malori kutoka bukwimba, ngudu, misungwi,magu na sengerema iliionekana ccm ndio imefanya hivyo halafu baada ya sherehe waliwatawanya watu wao mitaani ilikuonyesha ccm imewatelekeza, mimi nipo hapa mkuyuni ndio napata hizi habari

Chadema wako bize kutoa elimu ya uraia, hawana muda wa kupoteza kufanya mambo ya kitaahira kama hayo yaliyofanywa na CCM jana
 
Ila jana CCM imejaza watu sana! Yani ukifikiria CCM imepoteza umaarufu gafla inajaza watu wakutosha! Halafu jana ilikua CCM! CCM! CCM CCM! CCM!
 
CCM wanajua mjini hawawezi mpata mtu kwa kua tunajua maovu yao yote sasa hao malimbukeni walio tolewa makwao wakanyage na mguu kama Enzi la azimio la Arusha, ukweli mamluki wamejaaa sana kweny mikutano ya CCM
 
Tatizo la wana CCM ni kuwa bado hajamfahamu JK hadi leo kuwa ni mtu sampuli gani, huyu kamwingiza chaka WM Pinda kwenye sakata la posho za wazomeaji kule bungeni atashindwa kuwaacha solemba hao sungu sungu? Safi saaaaaaaaaaaaaana, wakome uroho wa pilau la nyama pori.
 
Hivi nyie huwa hamna uwezo wa kugawa hayo mapilau na kofia au? Hela huwa mnapeleka wapi wakati hata kodi huwa mnakwepa kulipa?
si tunauza sera na kumwaga ukweli tu mambo ya pilau,kanga, kofia ni ya chama kizee kilichokosa mvuto
 
Ukiwasaidia hao watasahau haraka sana na 2015 watapewa tena vi t-shirt na kofia. Bora kuwaacha hapo wasote mpaka kila mtu afike kwake kwa nguvu zake mwenyewe. Kweli Tanzania bado sana.

Trust me, Chadema needs to gain the Lake Zone rural trust. For historical reasons, CCM is the trusted party in most rural areas in the Lake Zone. Mjini wameweza chukua CDM sababu vijana ni wengi and from all over Tanzania. But ukitaka kura ya msukuma, lazima akuamini kwanza. Huu ndio wakati muafaka wa kujenga imani.
CCM inasambaza sumu ya ukanda.
Kwa historia, baada ya uhuru na wakati wa vijiji vya ujamaa na kujitegemea, wafanyabiashara wa vioski toka kanda ya kaskazini as well as wahindi na warabu ndio waliokuwa na maduka. Nasikia hawa watu walivyoamia huko usukumani, waliwadharau sana wasukuma. Tena msukuma au mzinza akifungua duka enzi za 60s, alikuwa anafanyiwa njama. Hizo ni historia zilizofanywa na baba na babu zetu.
Sasa wasukuma kawaida wanakuwa wazito.
Mambo yameshabadirika kwa sasa lakini CCM inawadanganya wasukuma wa vijijini kuwa CDM ni ya Kaskazini.

Ndio maana ni muhimu kwenda kuonyesha kwa vitendo kuwa CDM ni chama cha watu na kina jali watu wakati wa dhiki.
 
umaskini ni mmbaya sana , lakini watu atukomi na hawa jamaaa kama ni mganga wanaye mtumia basi ni balaaaaaaaaaaaa, huduma mbovu mahospitalini poa tu, umeme juu, bidhaa zimepanda poa tu, posho za wabunge kuongeza poa tu, lakini jana ni ccccccccccccccm ccccccccccccm sijui kama tutafika:hatari:
 
nimefurahishwa na kitendo cha hao watu kutelekezwa labda watapta akili. kauli mbiu ilikuwa kula nyama unyamaze
 
Ni kweli kabisa tuko la kairo hapa wanapita mamia kwa mamia kwa miguu na mabegi yao huku wakilaumiana wenyewe kwa wenyewe kuwa kwa nini walikuja! Wanatoka sengerema, bunda na vijiji vya karibu.

Duu hi kweli kali.... jamani kwanini msiwashauri waite waandishi wa habari waongee nao, ili tuweke kwenye kumbu kumbu! Nape bana.... eti Watu walijaa wakiwa na furaha... uwanja ulitapika .. watu walionyesha mapenzi yao ya kweli kwa chama hiki... Waambie sasa mume wao CCM aliyewawowa, kawatosa.....
 
Hawa hakuna haja ya kuwapa pole, si kwani jk keshawapa vipande vyao jana kuwa ulafi ndio unaowasumbua, sasa acha kwanza wajifunze kwa sababu funzo la mjinga ni kupigika tu
 
Inaonekana Chadema umati wa jana wa CCM hamkutarajia bado mna weweweseka! Acheni propaganda za Kitoto Chadema na Uzushi wenu! Hao watu wapo uwanjani? Upuuuuuuuzi tu mnaendekeza hapa JF

Tunawasubiri kwenye uchaguzu mdogo wa diwani pale Kirumba Mwaloni kwa hamu,halafu ndiyo utajua vizuri cdm ni nini hapa Mwanza.
 
mkuu unajua CDM walifanya mikutano ya siri na katika maadhimio ya kikao walikubaliana kuwasomba makada wao kwa malori kutoka bukwimba, ngudu, misungwi,magu na sengerema iliionekana ccm ndio imefanya hivyo halafu baada ya sherehe waliwatawanya watu wao mitaani ilikuonyesha ccm imewatelekeza, mimi nipo hapa mkuyuni ndio napata hizi habari

Na wakajawavalisha Nguo za CCM kweli hoja yako inaweza kusikika zaidi kama utaipa mashiko
 
Jana nimeshuhudia mkazi wa kahama akiwa jijini mwanza akisema kuwa kakodiwa kuja mwanza na ccm.. na kupewd posho... Ala alifunguka na kusema yeye ni mwanachama wa chama pinzani..
 
Jana nimeshuhudia mkazi wa kahama akiwa jijini mwanza akisema kuwa kakodiwa kuja mwanza na ccm.. na kupewd posho... Ala alifunguka na kusema yeye ni mwanachama wa chama pinzani..
Hakika kipigo cha jana kwa cdm ilikuwa over doose!! Poleni sana watani na hii ni hang'over ya jana!!! Endeleeni kujifariji!
 
Back
Top Bottom