CCM watelekeza mamia ya watu Mwanza waliowachukua vijijini kuwaleta kwenye maadhimisho yao

mabasi yatakuwa yamelipwa trip moja wakaambiwa kurudi itakula kwao.
nchi imewashinda adhabu wanapewa masikini na ngombe,kweli ccm ina wenyewe.
 
chadema kwa wivu ya CCM yanawawashia nini?

Sio ya ccm kumbaff weee hao ni wanamchi fukara waliodanganyika sio kwa mapenzi yao kwa ccm bali kwa njaa umasikini na ujinga waliopandikiziwa na ccm. Hivyo unafikiri wakipata matatizo sisi kama wananchi tusihoji?kwa kuwa eti ni ya ccm?hao ni baba na mama zetu pia kaka na dada zetu. Ucheni ukatili huo!!
 
Tutasikia mengi sana Baada ya sherehe za miaka 35 ya magamba.Ukweli utabainika tuuu
 
Baadhi yao walikuwa pale kona ya furahisha mida ya saa moja usiku wanashangaa tu cha kusikitisha watu walikuwa wanawazomea tu huku makonda wa daladala wakikataa kuwabeba kwenye magari yao,yaani inatia huruma na wengi walikuwa peku na wachache na ndala miguuni ila juu tisheti na kofia za ccm kama kawa

Mnh! hii ni njia nzuri kujifunza kwa mtu mzima.
 
mkuu unajua CDM walifanya mikutano ya siri na katika maadhimio ya kikao walikubaliana kuwasomba makada wao kwa malori kutoka bukwimba, ngudu, misungwi,magu na sengerema iliionekana ccm ndio imefanya hivyo halafu baada ya sherehe waliwatawanya watu wao mitaani ilikuonyesha ccm imewatelekeza, mimi nipo hapa mkuyuni ndio napata hizi habari
 
Lazima kamati ya usafiri imefanya vitu vyake hapa. naamini uongozi wa juu ulitenga fedha ya kuwarudisha pia.
Nape yuko wapi aje athibitishe humu?
Chama kimezungukwa na ufisadi kila kona.
 
mkuu unajua CDM walifanya mikutano ya siri na katika maadhimio ya kikao walikubaliana kuwasomba makada wao kwa malori kutoka bukwimba, ngudu, misungwi,magu na sengerema iliionekana ccm ndio imefanya hivyo halafu baada ya sherehe waliwatawanya watu wao mitaani ilikuonyesha ccm imewatelekeza, mimi nipo hapa mkuyuni ndio napata hizi habari

Na je kama habari hiyo ni propaganda ya CCM dhidi ya CDM? sidhani kama CDM wanaweza fanya ujinga huo.
 
Watoto wa mjini waniita kuwa WATALIJUA JIJI,nimeshamkosa mwenyji wangu stand ya mabasi,utawasilimia mpaka Watoto. Anyway ni siku nyingine wawe makini.
 
ukiona hali halisi ya wanachama ama kweli ni yakusikitisha kwa vile wengi walivalia tshirt za ccm Miguuni ni ndala na viatu vilivyochanika kwa keli inatia uchungu. anyway wanatumika kama kondom sasa hiyo ni adhabu yao
 
....Wamethubutu wameweza na sasa wanasonga mbele!!!! Wameshatimiza mradi wao wa kutaka kuujaza uwanja wa Kirumba na umati wa watu 20,000 baada ya kukamilisha mradi wao kila aliyekuja atajiju!!! Magamba wamefilisika hivyo ni lazima wabane matumizi na hivyo kutowajali maelfu ya Wananchi waliowatelekeza.
 
Wakuu;

Nipo mwanza na habari ni kuwa ccm wamewatelekeza watu wengi sana bila ya kuwapatia usafiri wa kurudi makwao.

Hii ni baada ya kuwasomba jana kuwaleta kwenye maadhimisho ya miaka 35 ya chama chao.

Utawahurumia akina mama wengi na baadhi ya wanaume jinsi walivyokosa matumaini kwa sababu mabasi yaliyowaleta hawayaoni na wala viongoz wa ccm hawaonekani, yaani wanahangaika kwelikweli

Ni aibu sana kwao pamoja na kujikomba bungeni kwa naibu spika kuwa uwanja ulitapika.
Saaafi sana. Na ule ubwabwa waliokula jana leo wamesha u post...kazi kwao. CCM oyee...!
 
mkuu unajua CDM walifanya mikutano ya siri na katika maadhimio ya kikao walikubaliana kuwasomba makada wao kwa malori kutoka bukwimba, ngudu, misungwi,magu na sengerema iliionekana ccm ndio imefanya hivyo halafu baada ya sherehe waliwatawanya watu wao mitaani ilikuonyesha ccm imewatelekeza, mimi nipo hapa mkuyuni ndio napata hizi habari
Mbavu sina. Lakini yote hayo ni kupenda dezo!
 
Baadhi yao walikuwa pale kona ya furahisha mida ya saa moja usiku wanashangaa tu cha kusikitisha watu walikuwa wanawazomea tu huku makonda wa daladala wakikataa kuwabeba kwenye magari yao,yaani inatia huruma na wengi walikuwa peku na wachache na ndala miguuni ila juu tisheti na kofia za ccm kama kawa
hahahaaa kiukweli siwahurumii hata kidogo mana hawa ndo wanatuangushaga kwenye uchaguzi kwa kupenda kwao mapilau na kofia za bwerere, wakome tena wakome kbs
 
mkuu unajua CDM walifanya mikutano ya siri na katika maadhimio ya kikao walikubaliana kuwasomba makada wao kwa malori kutoka bukwimba, ngudu, misungwi,magu na sengerema iliionekana ccm ndio imefanya hivyo halafu baada ya sherehe waliwatawanya watu wao mitaani ilikuonyesha ccm imewatelekeza, mimi nipo hapa mkuyuni ndio napata hizi habari
Mkuyuni wapi wewe! njoo maeneo ya Kirumba,Mwaloni na Ghana uone kumetapakaa mashati na kanga za kijani na watu wamechoka kwa njaa na kiu wanadhurura bila kujua uelekeo. Kwa kweli ukiangalia sura zao zimekata tamaa kwa kutokujua nini wafanye maana waliowaleta wame ingia mitini.
Mbaya zaidi wameanza kujisaidia hovyo maana vyoo ni vya kulipia na walio wapa ubwabwa jana hawakuwapa pesa za kulipia vyoo. Sasa hivi ni saa tisa kasoro, kuna dalili za wengi wao kushindwa kuondoka tena leo hii na hali ni mbaya sana.
 
Okay, here is a suggestion: CDM wachangamkie kuwasaidia hawa watu kurudi makwao. Ili wakifika vijijini wakasimulie jinsi CCM ilivyowapeleka mjini na kuwatekeleza, hadi chama kinachojali watu cha CDM kilipojitolea kuwasaidia kurudi nyumbani.
Hakika CDM itavuna mara dufu!
Dada Leticia changamkia hii tenda ya wanaoenda Kwimba, mtaji wa imani for 2015.
 
Wakuu;

Nipo mwanza na habari ni kuwa ccm wamewatelekeza watu wengi sana bila ya kuwapatia usafiri wa kurudi makwao.

Hii ni baada ya kuwasomba jana kuwaleta kwenye maadhimisho ya miaka 35 ya chama chao.

Utawahurumia akina mama wengi na baadhi ya wanaume jinsi walivyokosa matumaini kwa sababu mabasi yaliyowaleta hawayaoni na wala viongoz wa ccm hawaonekani, yaani wanahangaika kwelikweli

Ni aibu sana kwao pamoja na kujikomba bungeni kwa naibu spika kuwa uwanja ulitapika.

Hongera CCM kwa kuanza kutekeleza hotuba ya Rais kwa vitendo. Well done CCM! JK jana amewakumbusha maneno ya hekima ya Hayati Ditopile wa Mzuzuri ambaye aliulizwa na wapiga kura kama anayaelewa wazi matatizo yao, naye aliwajibu,'TATIZO LENU NI ULOFA. BABA MZIMA UNAMWACHA MKEO NA WATOTO NYUMBANI UNAENDA KUKAA MAHALI USIKU KUCHA KUSUBIRIA UBWABWA WA BURE, NA SH 2,000!'. CCM imewafundisha hao kuwa wasiwe malofa kwenda kupoteza muda wao kuishangilia CCM kwa malipo ya Ubwabwa na michezo mbalimbali ya kuwaburudisha. Waliletwa, wakalishwa, bado wanataka warudishwe?
 
Back
Top Bottom