CCM watelekeza mamia ya watu Mwanza waliowachukua vijijini kuwaleta kwenye maadhimisho yao

ithangaledi

Member
Jun 4, 2011
84
57
Wakuu;

Nipo mwanza na habari ni kuwa ccm wamewatelekeza watu wengi sana bila ya kuwapatia usafiri wa kurudi makwao.

Hii ni baada ya kuwasomba jana kuwaleta kwenye maadhimisho ya miaka 35 ya chama chao.

Utawahurumia akina mama wengi na baadhi ya wanaume jinsi walivyokosa matumaini kwa sababu mabasi yaliyowaleta hawayaoni na wala viongoz wa ccm hawaonekani, yaani wanahangaika kwelikweli

Ni aibu sana kwao pamoja na kujikomba bungeni kwa naibu spika kuwa uwanja ulitapika.
 
Pole zao kama hawaijui CCm ndiyo hiyo sasa lakini si walitazama concert la bwerere na ubwabwa pamoja na t-shirt...
 
Ni aibu kwa hao akina Baba na mama kuacha familia zao na kazi zao kuja kula nyama na Ubwabwa wa CCM!!! Sasa CCM wameamua kuwaonyesha their true colors!!
 
Baadhi yao walikuwa pale kona ya furahisha mida ya saa moja usiku wanashangaa tu cha kusikitisha watu walikuwa wanawazomea tu huku makonda wa daladala wakikataa kuwabeba kwenye magari yao,yaani inatia huruma na wengi walikuwa peku na wachache na ndala miguuni ila juu tisheti na kofia za ccm kama kawa
 
Ni kweli kabisa tuko la kairo hapa wanapita mamia kwa mamia kwa miguu na mabegi yao huku wakilaumiana wenyewe kwa wenyewe kuwa kwa nini walikuja! Wanatoka sengerema, bunda na vijiji vya karibu.
 
Ndugu zangu wasukuma nao bana, teh teh teh tehe teh teh, mpaka Nape na Magamba wanawaingiza mjini kiasi hicho!! fungukeni bana.....Lake zone walishakwisha hawana jipya so tusiwape ujiko kabisa. Pamoja tutashinda.
 
Baadhi yao walikuwa pale kona ya furahisha mida ya saa moja usiku wanashangaa tu cha kusikitisha watu walikuwa wanawazomea tu huku makonda wa daladala wakikataa kuwabeba kwenye magari yao,yaani inatia huruma na wengi walikuwa peku na wachache na ndala miguuni ila juu tisheti na kofia za ccm kama kawa

du! hizi ni habari za kusikitisha sana jamani, sipati picha kama mtu hana nauli ya kurudi kwao
 
Ni kweli kabisa tuko la kairo hapa wanapita mamia kwa mamia kwa miguu na mabegi yao huku wakilaumiana wenyewe kwa wenyewe kuwa kwa nini walikuja! Wanatoka sengerema, bunda na vijiji vya karibu.

Makubwa!! Mimi ni kama Thomaso, siamini bila kuona, itakuwaje Chama kongwe, Chama Tawala kilete watu jijini halafu kiwatelekeze? Siamini kabisa, Au ndiyo yanaanza kutimia yale aliyoimba mdogo wetu Vic kamata jana. Any way, mimi niko hapa Tarime natokea Kenya ndiyo nataka kuanza safari ya kuja jijini Mwanza na nafikia hapo La Kairo, sijui nitawawahi hao akina mama na akina baba wanaohangaika ili nitengeneze case study, wajua tena No Research, No right to speak!!.
 
ccm nacho chama kama wanaweza kuwaacha wagönjwa wafe mahospitalini licha ya watu walio waleta na malori vipi han ndio ccm ya leo wa magamba
 
Mbona kila siku wanatekelezwa kila siku na hawakomi,huruma kweli kuingizwa mjini mchana kweupe namna hiyo ,CCM na serikali yake ni majambazi unaaambiwa wale madaktari wanajeshi walioshikiria muhimbili hawajalipwa posho wanatupiana mpira kati ya wizara ya afya na ulinzi ,hawa jamaa hovyo kweli kweli
 
Safi sana CCM! Wakome kushangilia chama cha magamba. Hiyo ndiyo CCM Bwanaaaa! Njaa ya siku moja tu inakudhalilisha. Sisi CDM hatuna haja ya malori wala akina Suma Lee. Muziki wetu sisi ni hotuba zenye msisimko za viongozi wetu. Malori yetu ni miguu yetu wenyewe hata kilomita 50 tunatembea. Hiyo ndio nguvu ya umma Bwnaaaaaa!
 
No comments, nasepa. Watu huwa hatukomi na ni wepesi kusahau.
 
Safi sana CCM! Wakome kushangilia chama cha magamba. Hiyo ndiyo CCM Bwanaaaa! Njaa ya siku moja tu inakudhalilisha. Sisi CDM hatuna haja ya malori wala akina Suma Lee. Muziki wetu sisi ni hotuba zenye msisimko za viongozi wetu. Malori yetu ni miguu yetu wenyewe hata kilomita 50 tunatembea. Hiyo ndio nguvu ya umma Bwnaaaaaa!
Waambie bwanaaaaaaa alaaa!1
 
Raia mwema, uwe mwema kiukweli. Acha uchama, watu wameachwa solemba bila huduma, tujadili hilo. Acha uchama, utakupeleka pabaya. Utaacha nduguyi wa chama kingine afe njiani wakati ungeweza kumsaidia.

chadema kwa wivu ya CCM yanawawashia nini?
 
Back
Top Bottom