CCM waibiana kura, anayedaiwa kuhujumu kura hizo ni katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Hayo ndiyo maisha ya ccm, wote wamekosa maarifa na ufahamu. Wao rushwa ni sehemu ya maisha yao ya kila siku. Ccm imewaharibu sana watanzania, tulifanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi wa wajumbe wa serekali za mitaa, baada ya uchaguzi cdm ilishinda, cha ajabu wana ccm walioipigia cdm walikuja kudai rushwa kuwa tumeichagua cdm, tupeni fedha. Yote hayo shauri ya mazoea toka ccm. Ccm ni janga la taifa, hawaaminiki tena!
 
nahisi yeye ndio alikua anabebwa na Nappe.!

Aloo......



‎@ mUTUZ Good Morning FB: It is Friday you Know! ha! ha! ha! Well, My Babe F is here with me, So! ni Mpango Wangu Mzima, you know I Love the Baby!
- Well, off to the JFK Airport Wazee are leaving today, and So is My Great Friend Mheshimiwa Nape, it was nice to have them here: MBARIKIWE NA MUNGU WA MBINGUNI PEOPLE! - Will Mutuz!


386456_289782994376454_100000342668655_1028823_1598867757_n.jpg
 
Wameshindwa kuiba za chadema sasa wanaibiana wenyewe kwa wenyewe...huku malecela anataka maombi wakati nape anamwibia kura....ccm wamekuwa wabaya zaidi ya mashetani !
 
Kwa kawaida NWIZI ANAPOKOSA MTU WA KUMUIBIA HUJIIBIA MWENYEWE. wizi upo kwenye damu hawezi kuacha. hao ndio wanaotawala nchi hii ya maziwa na asali.
 
UCHAGUZI wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeingia doa.

Chanzo chetu cha habari kilichokuwa katika uchaguzi huo, kilisema jana kuwa, uchaguzi huo uliofanyika juzi kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, ulijaa kasoro kwa baadhi ya wagombea kuibiwa kura..........


Story kumbe tayari ipo JF
 
Mtoa habari kajichanganya mara yeye alikuwa na kinana mara yeye alikuwa wakala mara yeye alikuwa mtazamaji.
Inshort habari ni ya kutungwa!
Zanzibar will be free soon!
 
nahisi yeye ndio alikua anabebwa na Nappe.!

Kama alibebwa na vuvuzela Nape Karimjee basi huko Dodoma Nape hatakuwepo kwenye chumba cha kuhesabia kura hivyo kule jamaa ajitayalishe kuangua kilio!!
 
Siku moja JF wataandika Nape anatembelea kichwa badala ya miguu nao utakuwa mjadala..........kazi kwelikweli....



Imeandikwa na Maregesi Paul | Dar es Salaam
Thursday, April 05, 2012

UCHAGUZI wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeingia doa. Chanzo chetu cha habari kilichokuwa katika uchaguzi huo, kilisema jana kuwa, uchaguzi huo uliofanyika juzi kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, ulijaa kasoro kwa baadhi ya wagombea kuibiwa kura.

Chanzo hicho kilisema kuwa, mmoja wa wanaodaiwa kuhujumu kura hizo ni aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi huo, ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye. Nape alikuwa akisaidiana na kada wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.

Chanzo hicho kilisema kuwa, dalili za kuwapo hujuma katika uchaguzi huo, zilianza baada ya wabunge kukataa kura kuhesabiwa chini ya usimamizi wa meza kuu iliyokuwa ikiongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

"Mimi nilikuwapo ukumbini na niliingia kama mmoja wa mawakala waliokuwa katika chumba cha kuhesabia kura, kwani nilikwenda kumsimamia jamaa yangu ambaye alikuwa anagombea.

"Kwanza kabisa kabla ya kuingia katika chumba cha kuhesabia kura, kura zilipigwa kama kawaida, zoezi hilo lilipokamilika, ukafika wakati wa kwenda kuhesabu kura.

"Kabla ya hapo, Kinana alisimama na kutueleza kwamba, kura za wagombea zitasimamiwa na meza kuu, aliposema hivyo, wabunge wakalipuka kwa kusema hatutaki na wengine walidiriki hata kuzomea.

"Wakasema wagombea wenyewe wasimamie kura zao au kama kuna wasiotaka kuzisimamia, waweke mawakala kwa sababu meza haiaminiki.

"Baada ya kuvutana kwa muda, ukapitishwa uamuzi, kwamba wagombea ambao wakati huo walikuwa nje ya ukumbi, waitwe ili waulizwe wao wanataka utaratibu gani utumike.

"Walipoitwa, Kinana akaanza kuwaeleza kwamba, hapa kuna mambo matatu, mtu kusimamia kura zake, kuweka wakala au kuamini meza isimamie kura kwa sababu meza inaaminika.

"Alipouliza hivyo, wagombea wakawa kimya, nadhani ni kwa sababu ya ugeni katika masuala hayo.

Lakini mama mmoja nadhani ni yule wanayemuita Shyrose, akasema mimi nitasimamia kura zangu, kisha wengine nao wakaanza kusema watasimamia za kwao na baadhi wakasema wataiamini meza.

"Baada ya hatua hiyo, suala hilo likaonekana kutaka kumalizwa kiaina, sasa Mkuchika akasimama na kuuliza ni utaratibu gani utatumika kuhesabu kura.

"Baadaye ikaamuliwa kwamba, wanaotaka kwenda wenyewe kusimamia kura zao wafanye hivyo, wanaoweka mawakala, wawaweke na wakati huo huo wanaoiamini meza, waiachie itawasimamia," kilisema chanzo hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho ambacho kiliingia katika chumba cha kuhesabia kura, baada ya kuingia katika chumba hicho, mazingira ya kuhujumiana yalianza, kwani Nape alisimama mbele ya wagombea na kuanza kusoma jina moja moja na kura alizopata mgombea.

"Alipoanza kusoma hivyo, watu wakaanza kulalamika, wakamwambia wataamini vipi kura anazosoma ni za kweli wakati hawaoni anachosoma? Yeye akakataa, akasema ataendelea kusoma tu.

"Alipomaliza kusoma, lawama zikazidi, wagombea wakasema hawakubaliani na matokeo, wakataka kura zihesabiwe upya, lakini yeye akagoma, akasema matokeo yako kama alivyokuwa amesoma awali.

"Wagombea walipoona wanachakachuliwa, vurugu zikaanza, wengine wakaandika barua harakaharaka kwa Kinana ili kumweleza kilichokuwa kikijiri huko ndani.

"Kinana akaamua kuja, alipoelezwa mambo aliyokuwa ameyafanya Nape, akaamuru kura zihesabiwe upya na wakati huo huo, Serukamba (Peter Serukamba, Mbunge wa Kigoma Mjini), Zambi (Godfrey Zambi, Mbunge wa Mbozi Mashariki), Shaha (Abdulkarim Shaha, Mbunge wa Mafia), Martha Mlata (Mbunge wa Viti Maalum) na Mbunge wa Mufindi Kusini, Mahmud Mgimwa, waliingia pia.

"Walipofika, kura zikaanza kuhesabiwa, sasa vituko vikaanza kujidhihirisha kwa sababu baadhi ya wagombea waliokuwa na kura chache, kura zilipohesabiwa kwa mara ya pili wakapata kura nyingi.

"Kwa mfano, kuna mgombea mmoja ambaye awali alikuwa na kura 149, chini ya usimamizi wa Nape, lakini kura ziliporudiwa, amini usiamini, aliambulia kura 40.

"Mwingine chini ya usimamizi wa Nape alikuwa na kura 32, lakini ziliporudiwa mgombea huyo akazoa kura 136.

"Si hilo tu, kuna dada mmoja alikuwa akimsimamia ndugu yake, kura za kwanza alikuwa amepata kura 114, ziliporudiwa akapata kura 126, lakini matokeo yakabadilishwa kwamba amepata kura 107, wakati yeye mwenyewe alikuwa akihesabu kura hizo.

"Sasa angalia haya madudu, wao wanasema chama kiko imara, uimara wake uko wapi, mambo yanapelekwa kienyeji na ndiyo maana hata wabunge tulipoulizwa mwanzoni kama meza inaweza kusimamia kura tulikataa, kwa sababu sisi wenyewe hatuaminiani.

"Pamoja na kwamba washindi wameshapatikana, bado tunasema uchaguzi haukuwa huru na wa haki, yaani mtu kama Nape anaingia katika uchaguzi akiwa na watu wake, huu siyo utaratibu kabisa, chama tunakiua wenyewe," kilisema chanzo chetu.

Nape alipozungumza na MTANZANIA kwa simu jana, alisema uchaguzi ulikwenda vizuri tangu kura zilipopigwa hadi uhesabuji wa kura, ingawa kulitokea kasoro ndogondogo ambazo ni za kawaida.

"Nadhani mmelishwa stori kwa sababu mimi na Kinana ndiyo tuliokuwa wasimamizi wa uchaguzi huo, uchaguzi ulikwenda vizuri na hata kura zilipohesabiwa kwa mara ya pili, washindi waliokuwa wameshinda awali ndiyo hao hao walioendelea kushinda.

"Kwa hiyo mtu anaposema hayo, anadanganya kwa sababu hakuna aliyelalamika, lakini kama kuna ambaye hakuridhishwa na matokeo angegomea matokeo.

"Pamoja na hayo sishangai malalamiko haya kuletwa kwenu kwa sababu najua aliyeyaleta anajua mtayaandika kwa ajili ya kumwandika Nape vibaya," alisema Nape.


Source: Mtanzania
 
Siku moja JF wataandika Nape anatembelea kichwa badala ya miguu nao utakuwa mjadala..........kazi kwelikweli....

jaribu kufikiri kabla ujatupa comment broo ihi story ni copy and paste ya news paper we unashoboka jf wanakuandka.jaribu kutembea kwa kichwa ina weza kuwa laana we uoni nyoka hadi leo bado anatambaa
 
Back
Top Bottom