CCM: Tujisahihishe au Tugawane Chama

Ujamaa una mapungufu makubwa..sana kwenye mfumo wa kuendesha maisha ya watu huru na kufanya kazi kwa bidii..
Ujamaa hauna mapugufu makubwa ni mtazamo hasina finyu watu ndio wanaouona hivyo ujamaa. Hata Sera kama za afya UK NHS ni sehemu ya sera za ujamaa. Obama naye kaingiza fya ya USA kwenye ujamaa fulani.

Baadhi ya mapungufu makubwa yaliyokuwepo kwenye ujama wetu Tanzania ni
  • ubinafsi wa viongozi amabao hata kwenye uchumi huria upo......
  • Wakubwa wa dunia kutofurahishwa na mfumo huo hivyo kutoupa support ya kupaa na kuuminya.
Kampuni ya samsung ya korea imefanikiwa dunia sababu mwanzo wake imebebwa bebwa na kuwezeshwa kwa namna mbali mbali kijamaa na serikali.kwanza mpak ikaweza kuingia soko shindani. ufagii tu sera za IMF WB bila kujiuliza ni mtatizo.

Lengo la WB/WB ni kutfanya tuwe consumers tu. Ona hata kiwanda cha baiskeli hatuna eti Soko huria. China na Korea wangefuata hayo wasingekuwa hivyo.
 
Nakubaliana na wewe; Mwenyekiti taifa - Kikwete alipokuja na wazo la kujivua gamba, ni jambo lisilo na ubishi kwamba alilenga suala la party's rebirth kwa ujumla, na kama mafisadi kwa njia ya ushahidi wapo, vikao vingefanyia kazi suala hilo kwa utaratibu uliopo; lakini kwa sababu mwenyekiti ni msimamizi tu wa shughuli zote za chama na sio mtendaji, suala la gamba likawa spinned na makundi mawili ambayo ni wazi yamemwelemea Kikwete kwani wao ndio ndio party machinery - kwani hawa ndio watendaji na watekelezaji wa maamuzi ya vikao; sina maana kwamba suala la ufisadi lisipewe uzito, ila suala nalozungumza hapa ni kwamba inakuwaje miaka ya nyuma masuala yote ya ufisadi na yale ambayo yalionekana ni ya kuasi chama yalikuwa yanashughulikia kimya kimya na vikao maalum bila kuharibu hali ya hewa ya nchi na kuwapotezea wananchi muda? Mfano, tuliona jinsi gani Mzee Jumbe na Seif Sherrif walishughulikiwa kwa kuonekana waasiwa CCM; na ndani ya mfumo wa vyama vingi, tumeona jinsi gani kina Kiula, Mramba, Yona wameshughulikiwa na CCM na serikali yake; Tujiulize, kwanini mapambano dhidi ya Yona na Mramba hayakuwa majukwaani na badala yake yalikuwa kwenye vikao na matokeo yake tumeyaona – watuhumiwa kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu hoja huku Chama kikiendelea na shughuli zake nyingine bila bugudha? Watuhumiwa ufisadi wa sasahivi wana tofauti gani mpaka vita dhidi yao ziende majukwaani na sio vikao maalum? Kuna nini hapa?? Kwa hili Nape amekosea na kama atapewa adhabu au kuteuliwa ubunge, au ubalozi ili aachie nafasi yake ya sasa, anastahili; kwani kama kweli wanaotajwa kwa ufisadi wana tuhuma za kujibu, njia iliyotumiwa Nape na wenzake ya kupeleka vita hivi majukwaani badala ya kwenye vikao, kama kweli walikuwa na tuhuma za kujibu, basi ndio wamepona kwani tafsiri ya wengi hivi sasa juu ya Nape na wenzake kukiuka taratibu inawapa hisia wengi kuangalia hili suala kama ni la visasi, fitina, chuki, na ubinafsi zaidi ya kitu kingine chochote; inawezekana Nape na wenzake walikuwa na nia safi, lakini kukiuka taratibu za chama juu ya hili ndio kimewaokoa watuhumiwa - 'kama walikuwa na kesi ya kujibu'

Vinginevyo Nape angerudia his job description:
  1. Kusimamia, kueneza na kufafanua masuala yote ya itikadi, siasa na sera kitaifa;
  2. Kupanga na kusimamia mafunzo na maandalizi ya makada na wanachama kitaifa;
  3. Kufuatilia utekelezaji wa sera za chama za kijamii na ilani za uchaguzi wa CCM;
  4. Kudumisha uhusiano mzuri na vyombo vya habari na kuwa na mipango ya mawasiliano na uhamasishaji wa umma kwa jumla;
  5. Kufuatilia hali ya siasa;
  6. Kufuatilia mwenendo wa jumuiya za kijamii;
Mengine nje ya haya angeshiriki kwa nafasi yake kwenye vikao au kamati; ila asisahau kwamba ufisadi mama yake ni Azimio la Zanzibar ambalo liliruhusu viongozi kuwa na mshahara zaidi ya mmoja, nyumba ya (za) kupanga, na kuwa na hisa katika makampuni binafsi, bila ya mipaka maalum; ndio maana nasisitiza tugawane chama ili wa azimio la Zanzibar wachague upande wao na sisi wengine wa azimio la Arusha tuchue upande wetu, tulifanyie marekebisho kidogo na pia tuchukue mwongozo wetu wa chama wa 1981 tusonge mbele; hakika huu utakuwa ni ushujaa; nipo tayari kuthubutu na kuwa mwanachama wa kwanza wa kambi hii;

Mkuu mimi sina tena neno umenena yote. Umenikumbusha mbali. Akina Choga, Kasanga Tumbo, Masha, Jumbe, Hamad Rashid Mohamed, Seif Sharif Hamad: Hao walishughulikiwa kimya kimya bila kelele wala kokoro na Chama kikabaki imara ila hili la sasa kweli nadhani kuna kupotoka.
 
Upo sahihi; vijana wengini (SIO WOTE) wanaingia kwenye siasa kutafuta uongozi ili wajitengenezee mazingira ya kuvuna pesa aidha kwa kununuliwa na viongozi au kutumia nafasi zao kuhujumu nchi; hawana dhamira ya kuweka nchi kwanza, tumbo baadae bali tumbo kwanza, nchi baadae; inabidi vijana tufikie hatua ya kusema sasa basi, sasa nataka kulinda heshima yangu na pia maslahi ya vizazi vya baadae; kama kijana una nia ya kutafuta pesa, kwanini usitafute huko kwenye soko huria, kwa kuuza mbao, kufuga kuku, mbuzi, kulima ufuta n.k? na kama una elimu nzuri, una nafasi ya kufanya makubwa zaidi kwani ujasiriamali pia unajenga nchi yako – utaajiri vijana wenzako, utalipa kodi, na utaweza changia chama chako kifedha hata bila kujikita kwenye siasa; binafsi sioni kosa kwa kijana kuwa na biashara zako halali na kuzitumia kujenga chama chako kwa njia ya uongozi au kwa njia nje ya uongozi; ili mradi fedha ziwe safi; lakini sio sahihi kuingia kwenye chama na kutafuta uongozi kwa matarajio ya kujijenga ki-uchumi; watu wa namna hii ndio wanaokiharibu chama;
Inasikitisha vjjana wa umri wa miaka 30-35 kukubali kushabikia upande fulani wa kisiasa na kutumika na wazee wanaotafuta uongozi, wazee ambao vita vyao ni fitina tupu, sio ufisadi; wazee/wanasiasa ambao miaka 15 ijayo watakuwa wastaafu wakati wewe kijana ndio kwanza utakuwa na umri wa miaka 45-50, mchanga kabisa kisiasa; litakuwa jambo la fedheha sana iwapo by mwaka 2025 utajikuta njia panda na kujuta kwanini ulichagua the wrong side of history, especially kama utakuwa bado na interest za siasa; hili litawakuta wale wanaoshabikia upande mmoja wa siasa bila kuelewa kiini cha vita hivyo ni nini; ushabiki unao base on personalities za viongozi hao badala ya sera na dira fulani kwa taifa; ushabiki huu ni short lived; by the time wazee hao wanaachia ngazi kisiasa kutokana na umri, vijana hawa ambao watakuwa umri wa miaka 45-50 wakati huo most likely wataishia aidha kwa Ocampo kujibu tuhuma za mauaji ya alaiki kwani itakuwa dhahiri kwamba walishiriki iwapo siasa zao zitatupeleka kwenye machafuko; kama sio kwa ocampo, basi vijana hawa wataishia kutuletea tu vurugu nchini aidha kwa harakati zao za kujinasua na kashfa (kwani tayari watakuwa wananuka) au kutafuta kukubalika kisiasa kwa nguvu; wakati huo, wazee wa sasa wanaopigana vijembe vya fitina wote watakuwa wanastarehe miguu juu kama wastaafu na familia zao; Sina maana kwamba wazee katika chama hawana nafasi au hawana maana; hoja yangu hapa ni kwamba kuna wazee wa maana sana wana CCM ambao tunawahitaji kimawazo lakini wengi ya hawa wapo kimya katika nyakati hizi kuwashauri vijana ipasavyo; wazee walio active ni wale ambao wanatumia siasa kwa manufaa yao binafsi na kuwateka vijana wasiokuwa na dira; ni dhahiri kwamba wakimalizana na siasa, watawatupa vijana wanaobebana nao sasa na badala yake kuepuka siasa za migongano na kujikita na shughuli za familia zao; This applies to kambi zote zinazohasimiana sasa ndani ya CCM; we should start learning how to think ahead;


Naona nawewe mkuu umeingia kichwakichwa kwenye the well orchestrated trap ya kuwaaminisha watu wote kwamba vita ya kupambana na UFISADI inayoendelea ndani ya CCM, ni vita ya kuelekea uchaguzi wa 2015.

If you have been caught in that bandwagon, then CCM has a long way to go kujikomboa, maana now its 2011 but people are talking of uchaguzi wa 2015 na watu munaamini. What happened to common sense jamani?... Hapohapo umeacknowledge somewhere kuwa CDM waliweza kuvuna kura nyingi uchaguzi wa mwaka jana kwa sera ya "UFISADI"... CCM sasa wanastuka wanataka wawashugulikie hili tatizo, then inaitwa ni vita ya 2015.... Hizi spin nyingine nilitegemea vichwa kama wewe uweze kuzitambua na kutofall in.

Mramba, Yona, Kiula hawakuwa na uongozi wowote wa kitaifa ndani ya chama,na mambo yao yalishughulikiwa kiserikali zaidi na kimahakama. Kwenye siasa perceptions za public can make or break a party. Hawa walioambiwa wajivue gamba ni wajumbe wa chombo cha juu kabisa cha maamuzi kitaifa NEC. Sasa kama hukuanza na kwenye chombo cha juu kabisa kukisafisha sijui ulishauri wangeanza wapi.

Ni kweli CCM haiwezi kusafishika kwa kuwaondoa makada watatu, lakini hao makada nao wameshaonesha uchu wa ajabu wa madaraka kiasi kwamba maslahi yao binafsi wameyaweka juu ya maslahi ya chama, na hata kuhatarisha uhai wa chama. Kumbuka kila safari ya kilomita 10 inaanza na hatua moja.

Tatizo lingine la CCM ni Mwenyekiti. Kwa mtizamo wangu ni mtu anayeyumba kwa kila dhoruba litakalompiga, ilihali ana vyombo vya kumpa tahadhari ya madhoruba yanayokuja mbele yake. Mpaka mjumbe anapata ujasiri wa kumvurumushia tuhuma mwenyekiti nayeye akabaki anacheka, ni mambo yaliokuwa hayafikiriki kwa Wenyeviti wote waliotangulia.

KUTOCHUKUA MAAMUZI MAGUMU bado ni tatizo kubwa litakaloiangamiza CCM, tena mwaka wa uchaguzi wao 2012.

Kwa vile wewe bado ni mwanaCCM hai, nakushauri umwandikie waraka huu uliouweka hapa Mwenyekiti wako(hoping atausoma).
 
Ujamaa hauna mapugufu makubwa ni mtazamo hasina finyu watu ndio wanaouona hivyo ujamaa. Hata Sera kama za afya UK NHS ni sehemu ya sera za ujamaa. Obama naye kaingiza fya ya USA kwenye ujamaa fulani.

Baadhi ya mapungufu makubwa yaliyokuwepo kwenye ujama wetu Tanzania ni
  • ubinafsi wa viongozi amabao hata kwenye uchumi huria upo......
  • Wakubwa wa dunia kutofurahishwa na mfumo huo hivyo kutoupa support ya kupaa na kuuminya.
Kampuni ya samsung ya korea imefanikiwa dunia sababu mwanzo wake imebebwa bebwa na kuwezeshwa kwa namna mbali mbali kijamaa na serikali.kwanza mpak ikaweza kuingia soko shindani. ufagii tu sera za IMF WB bila kujiuliza ni mtatizo.

Lengo la WB/WB ni kutfanya tuwe consumers tu. Ona hata kiwanda cha baiskeli hatuna eti Soko huria. China na Korea wangefuata hayo wasingekuwa hivyo.

Kilichofanya hizo kampuni kuwa succesfuly siyo ujamaa (mfumo) ila watu wanaosimamia shughuli hilo ndio tatizo letu Tanzania..

Ujamaa/ubepari siyo mifumo mibaya wala siyo kwamba ni perfect..

Tatizo ni kwamba mfumo wowote ule bila watu wazuri utakuwa mbaya tu...

na kila mfumo una fursa zake ambazo ni nzuri sana..

hapa kwetu ni vigumu sana kurudi kwenye fikra za nyerere trust me..
 
Tatizo ni kwamba mfumo wowote ule bila watu wazuri utakuwa mbaya tu...

na kila mfumo una fursa zake ambazo ni nzuri sana..

hapa kwetu ni vigumu sana kurudi kwenye fikra za nyerere trust me..

MKuu Topical
Ni gumu lakini Bank ngapi huko UK na USA hivi sasa ni za ujamaa?

Kumbe unaona yale waliyotukataza sie wajamaa ndiyo yae yae imebidi wayatumie baada ya wao kupata matatizo ya kiuchumi

Kuziita fikra za nyerere ni kosa lingine zile fkira zinatakwia kufanyiwa marekebsiho kwenda na nyakati hizi. Zile ni fikra sahihi.
 
MKuu Topical
Ni gumu lakini Bank ngapi huko UK na USA hivi sasa ni za ujamaa?

Kumbe unaona yale waliyotukataza sie wajamaa ndiyo yae yae imebidi wayatumie baada ya wao kupata matatizo ya kiuchumi

Kuziita fikra za nyerere ni kosa lingine zile fkira zinatakwia kufanyiwa marekebsiho kwenda na nyakati hizi. Zile ni fikra sahihi.[/QUOTE]

Siyo sahihi ndio maana hatukuwa matajiri kwakuwa tumekuwa na hizo fikra zake 24 yrs mkuu..hatuwezi kurudi huko

Hakuna bank za kijamaa UK, naomba mfano..lol
 
Mchambuzi,

..nadhani hujamtendea haki Mzee Mtei kuhusu mchango wake ktk kushulikia matatizo ya uchumi tuliyokuwa tukikabiliana nayo miaka ya themanini.

..kumbuka kwamba ni Mtei huyohuyo alikuwa waziri wa fedha wa Mwalimu Nyerere during the "old good days", era ambayo unasema wakulima walikuwa na hali nzuri.

..nchi ilikuwa kwenye some serious economic problems. haya siyo mambo ya kuyasoma kwenye mabuku na maripoti. ungekuwa na umri mkubwa wa ku-experience jinsi uchumi wetu ulivyo-shrink wakati ule usingekuwa hapa ukimlaumu Mtei kwa kutoa ushauri alioutoa.

..matatizo yale yangeendelea kuna uwezekano kabisa yangetokea machafuko nchini. Hali ilishaanza kujionyesha kidogo kidogo ambapo wananchi walishaanza kuchoshwa na hali ile na kuna uwezekano kabisa wangechukua hatua. nakumbusha jaribio la kina Hatty McGhee[Hatibu Gandhi], Mohamed Tamimu, Eugene Maganga, etc la kutaka kupindua serikali ya Mwalimu.

..kila alichojaribu Mwalimu Nyerere kilishindikana na ilichobakia ilikuwa ni kukubaliana na IMF/WB ili kunusuru kidogo tulichokuwa tumebakia nacho.

..sasa hivi uchumi wetu una matatizo lakini huwezi kuyalinganisha na yale ya mwaka 1982--1986. matatizo tuliyonayo sasa tunaweza kuya-manage sisi wenyewe ikiwa tutajipanga vizuri, yale ya wakati ule yalihitaji MISAADA toka nje. ukinishikia bunduki kichwani ukaniambia nichague kuishi ktk matatizo ya miaka 80 au haya ya sasa hivi i would choose haya ya sasa hivi.

NB:

..nakushauri usome kitabu cha maisha ya Mzee Mtei. Yapo mambo mengi sana ameyaeleza mle ndani. kuna crisis zaidi ya moja ambazo alipambana nazo akiwa waziri wa fedha chini ya Mwalimu Nyerere.

..Mzee Mtei alikwenda kufanya kazi IMF kwa mapendekezo na baraka za serikali ya Tanzania wakati huo ikiongozwa na Mwalimu Nyerere. Ilikuwa zamu ya Tanzania kuongoza idara ya Afrika IMF na Mwalimu akampendekeza Edwin Mtei. majuzi nafasi hiyo ilijitokeza tena na Raisi Mkapa akampendekeza Mzee Peter Ngumbulu.

..akiwa IMF Mtei alikuwa akifanya kazi kwa karibu na viongozi wa Tanzania kama Mwalimu Nyerere, Edward Sokoine, Mzee Alhaj Ali Mwinyi, Mzee Joseph Warioba, Mzee Cleopa Msuya etc etc.

..alipomaliza mkataba wake na IMF, Mzee Mtei aliongoza Tume ya serikali ya kurekebisha mfumo wa ukusanyaji kodi nchi. Ripoti ya Tume hiyo na mapendekezo yake ndiyo iliyopelekea kuanzishwa kwa TRA.

JokaKuu,
Nashukuru sana kwa mchango wako mzuri; kwanza na awali ya yote, sipo hapa kumlaumu mzee wetu Edwin Mtei kwani haitakuwa haki; ninamheshimu sana mzee wetu na ninathamini sana mchango wake kwa taifa hili kiuchumi na kisiasa; hoja yangu ya msingi ni kwamba CDM na CCM wote ni wale wale na nilishaeleza kwanini; real change kwa mtanzania aliyepo kijijini haipo katika CDM ya sasa iliyoasisiwa na Mtei wala CCM ya sasa iliyolitupa azimio la Arusha; ukombozi wa kweli wa Mtanzania kijijini ni chama kingine au hivihivi kama vitageuka na kuwa radical in terms of demanding hawa mabwana IMF/WorldBank kwamba sasa tunataka to ‘own our development agenda’;

Katika kujenga hoja, kuna uwezekano mkubwa nikatafsirika kama namlaumu au kumsema vibaya mzee wetu Mtei; la msigi katika hoja yangu ni kwamba by now, nina uhakka Mzee Mtei sees it clearly kwamba IMF/WorldBank haven’t made mtanzania kijijini better; Na chama chake CDM na CCM wote ni failure on that front; and a refurbishing of Nyerere’s agenda is the only way ahead for maskini vijijini; pia niseme tena kwamba, bila yeye (mzee Mtei) kujua au kutojua, ana mkono katika matatizo yanayotukumba sasa kutokana na ujio holela wa sera za IMF/WorldBank;

Ningependa kujibu hoja zako katika vipengele vifuatavyo:
Kwanza, kuhusu suala la umri wangu kuwa mdogo kujua kilichojiri, sidhani kama inahitaji umri mkubwa kujua nini kilijiri nyakati zile kiuchumi – vitabu vingi sana vimeandikwa juu ya nini kilitokea; kinachohitajika kwa kijana ni utamaduni wa kujisomea; nimejitahidi kusoma vingi na ninavyo hapa, mfano:
  • Beyond Structural Adjustement Programmes in Tanzania: Success, Failures and New Perspectives, by Msambichaka, Kilindo, Mjema (1995)
  • Economic Shocks and National Policy Making: Tanzania in the 1970s, by Green, Rwegasira and Van Arkadie (1982);
  • What Went Right in Tanzania: People’s Response to Directed Development, by Marja Swantz and Ali Tripp (1996), na humu wachumi kama Benno Ndullu na wengineo wana articles nzuri sana;
  • The IMF and Tanzania, edited by Horace Campbell & Howard Stein (1991);
  • Beyond Ujamaa In Tanzania: Underdevelopment and Uncaptured Peasantry, by Goran Hyden (1980);
Kwa ujumla wao wote, kilichopelekea Ujamaa kuanguka ilikuwa ni uwezo mdogo wa fedha kufanikisha sera na malengo ya Ujamaa kutokana na ukweli kwamba nchi ilikuwa bado changa sana kuendelea kushiriki katika international economic system isiyokuwa na haki - by Tanzanians producing what they do not consume and consume what they do not produce, kitu ambacho kililetwa na ukoloni na kuzidi kukuzwa ndani ya ukoloni mamboleo; Jitiada za Mwalimu zililenga kujaribu kugeuza hali hii kwa nia nzuri kabisa kupitia sera ya Ujamaa ili tuanze wote katika kiwango sawa kama jamii na vilevile kuhimiza sera ya kujitegemea kichumi, lakini lack of finance to support malengo haya ndio yakawa kikwazo;

Miaka ya late 1960s to mid 70s, Tanzania ilikuwa ni nchi ya pili duniani kwa kupata misaada mingi (AID) kutoka mataifa tajiri; Tanzania was only second to Israel duniani. WorldBank Chief wa wakati ule ‘McManara” alipenda sana na kuelewa philosophy ya Ujamaa hivyo alisaidia sana sera za Mwalimu kifedha; vilevile Scandinavian and Nordic Countries pia walikuwa mstari wa mbele kusaidia kufanikisha Ujamaa; tusisahau kwamba Sweden leo hii ni the top in the world in terms of quality of life kwa wananchi wake kutokana na sera zake za kijamaa, Kwahiyo hawakuona ubaya kuisaidia Tanzania kufika huko; kilichopelekea wakubwa hawa kuanza kuachana na sera za Mwalimu miaka ile haikuwa kitu kingine zaidi ya kugundua kwamba pamoja na nia nzuri ya sera za Mwalimu, ili zifanye kazi it needed an overhaul of the entire international economic system ambayo ina favor matajiri tu kwani we were are still are participating in such a world order from the periphery, not from the centre; hii ilipelekea nchi maskini kama sisi kuzidi kuwa marginalized; kwahivyo kufanikisha Ujamaa katika mazingira yale yalihitaji marekebisho ya such a system kitu ambacho ni kigumu kufanikisha; so when crisis hit, wakubwa abandoned Mwalimu and his Ujamaa philosophy; kuruhusu IMF waje kiholela holela ikawa a grave mistake and this has been argued elsewhere;

Hoja yako kwamba alichojaribu kufanya Nyerere kilishindikana thereby ujio wa WorldBank/IMF to come to rescue the situation ni sahihi; ila ni muhimu tuelewe why Nyerere failed na kwamba pamoja na yote, wakubwa (WorldBank under MCmanara, Sweden, Denmark) walikuwa bado wanajua the end result of sera za Mwalimu was good; only problem was the means towards that end;

Pili, simlaumu Mtei kwa ushauri aliotoa; nachosema hapa ni kwamba ana mkono juu ya madhara ya ujio wa IMF na WorldBank kwa kasi kubwa kiasi kile; kupata blessings za Mwalimu kwenda kufanya kazi IMF was just a formality, how could Nyerere say no? Na miaka yote Nyerere aliendelea kupiga kelele kwamba hawa wajomba mtakuja kuona madhara yao baadae; na kweli tukayaona na tunayaona hadi sasa; Hoja kwamba Mzee Mtei did what he did because there was no other alternative, sikubaliani moja kwa moja; mabadiliko yalikuwa hayakwepeki lakini sio kwa pupa ile Mzee Mtei aliyoiunga mkono; Mtei had a chance to negotiate further na sio just to embrace IMF/WorldBank reforms kiholela;

Tatu, hoja kuhusu wewe kuchagua kuishi katika matatizo ya sasa kuliko yale ya kipindi cha 1982- 1986, – kwa wewe binafsi ni sahihi; hata mimi ningechagua hivyo kama sina Uzalendo na nchi yangu, hasa hasa huruma kwa watanzania zaidi ya asilimia 70 vijijini; hoja yangu hapa ni kwamba – ukienda kwa mwanakijiji Ruvuma, Singida, Shinyanga na kumuuliza je, hali yako ya uchumi miaka ya 1982 – 1986 na ya miaka ya sasa ipi ni nafuu? Unadhani jibu la mwanakijiji wa kawaida litakuwa lipi? Kama unalenga ubora wa hali ya 25% ya watanzania wanaoishi mijini, unaweza kuwa sahihi, mimi I am addressing the issue of 75% of the population;

Nne, kuhusu mzee mtei kupambana na mambo mbalimbali ya uchumi ambayo ameyainisha kwenye kitabu chake, sikatai, kinachonitatiza hapa was his ‘exit strategy’; na baadae kuunda chama cha chadema ambacho kimsingi kina implement au kina kiu ya kui implement the Washington consensus ile ile CCM inayo implement ambayo kwa kweli, kwa watanzania wengi wa vijijini, hali yao between 1967 – 1985 when Mtei took the exit, na kipindi cha 1986 – hadi sasa (2011), wananchi hawa vijijini hawaja experience any major change katika maisha yao kama sio kuzidi didimia; Nikuulize, Je unakubaliana na kauli ya miaka 50 ya uhuru kwamba tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele? Iwapo jibu la haraka haraka akilini kwako halikuwa NDIO baada ya kunisoma hapa, ni ishara kwamba tunaongea lugha moja, lafudhi tofauti;

Na Tano, kuhusu Mwalimu kuingia wakati mgumu kisiasa na kutaka kupinduliwa, zote hizi zilikuwa njama za mabeberu na mabepari ambao walikuwemo humu nchini tena wenye ngozi hizi hizi kama zetu ambao walikuwa vibaraka wa mabepari; hawa waliumizwa sana na sera za Ujamaa - hawakuwa wanakubaliana na sera za ‘tuinuke wote kwa pamoja’, hawakuwa na muda huo, wao walijali zaidi sera za kuwaendeleza wao binafsi na familia zao; na leo hii wapo wengi katika makundi yetu haya haya; kwa wao, mtanzania wa kijijini kuendelea kiuchumi ni kikwazo cha Maendeleo yao (mabepari);

Vinginevyo, ukiangalia na kufananisha takwimu za miaka 1967 – 1985 na 1986 – 2011 kwenye sekta ya Maendeleo vijijini – kilimo, viwanda, na sekta mbali mbali za kijamii, ni wazi kwamba hakuna tofauti yoyote kubwa kati ya Tanzania chini ya Nyerere na ile chini ya IMF/WorldBank; Maendeleo vijijini kama yapo ni ya bahati mbaya; enzi za Mwalimu, sekta ya viwanda ilifikia mafanikio ya juu kuliko sasa katika mazingira haya ya soko huria; kilimo mchango wake wakati ule na sasa katika GDP tofauti ni ndogo sana; muhimu hapa ni kwamba bado about 75% ya watanzania leo hii ni wakulima wa jembe la kuungua juani na kupinag mgongo;

Hata Mzee Mtei lazima anajua fika kwamba miaka 19 ya siasa ya Ujamaa (1967 – 1985) na miaka 25 ya soko huria (1986 – 2011) linalolazimishwa kimabavu na IMF (bila ya sisi kuamua the terms) haijaleta tofauti yoyote ya maana kwa Mtanzania anaeishi kijijini kiuchumi; na kwamba CDM ya sasa na CCM ya sasa haina jipya kubadili ukweli huu;

Sera za IMF na Mzee Mtei; sera amabzo hata CCM hivi sasa inazipakata kwa mbwembwe na kurembua zimempotezea muda wa bure mwanakijiji;
 
Mchambuzi, umetoa mawazo mazuri sana. Nataka tu nichangie kipengele cha World Bank na IMF. Ni ukweli ulio wazi kwamba taasisi hizi zinatunyonya sana kupitia mikopo na masharti magumu. Hata hivyo, kuna mambo mawili muhimu katika hili.

Kwanza, ni vema tukubali kwamba vyombo hivyo ni vya kibiashara, na biashara yenyewe ni ya kibepari. Hakuna hata siku moja tutakaa tutegemee kwamba watatupa masharti laini. Masharti wanayotoa ni ya kulinda mitaji yao, kitu ambacho kinafanyika hata kwenye benki zetu za ndani kwa wakopaji wa Tz (CRDB, NBC, n.k.). Hakuna taasisi inayoweza kugawa rasilimali zake bila masharti. Na hili ni muhimu sana kwa nchi zetu ambazo risk ya kukopa iko juu, mfano vurugu za kisiasa, ufisadi, n.k. Ni lazima waweke masharti ili wawe na uhakika wa kurudisha fedha zao.

Pili, wenye shida ni sisi na ni sisi wenyewe ndio tunawatafuta hao WB na IMF. Hayo masharti yao huwa hayaji kwa kushtukiza, bali huwa tunaingia hiyo mikopo tukijua kabisa kitakachofuata. Kwa hiyo ni jukumu letu kuhakikisha kwamba tunakopa kwa malengo na kufanyia mambo ya maana, ili hata tukianza kulipa, basi tuwe tumefaidika kiasi fulani. Ni kweli kwamba hakuna nchi yoyote duniani iliyoendelea kwa kutegemea rasilimali zake yenyewe. Hata Marekani na China nao ni wakopaji wazuri tu. Tofauti ni kwamba wao wanakopa kwa ajili ya kupanua uzalishaji mali na kuongeza ajira. Sisi tunakopa halafu tunashindwa kusimamia, mwisho wake ni ufisadi, kulipana posho, safari za nje, n.k.

Hatuwezi kuzuia kukopa. Lakini, tukope kwa malengo maalum ya kujenga uwezo wa ndani, halafu baada ya muda tuachane na mikopo tujitegemee. Malengo tunayo mazuri sana. Udhaifu wetu ni kwenye usimamizi. Mpaka miaka ya '70, nchi yetu haikuwa tofauti sana na China, Brazil, na Singapore. Lakini hao jamaa ghafla wakatupita kwa kasi na kutuacha tumeduwaa. Hakuna uchawi wala mazingaombwe. Ni uchapakazi, utawala wa sheria, na kuzalisha. Nadhani unajua vizuri adhabu ya wala rushwa na mafisadi China. Ni kunyongwa. Ilimradi tumeamua kucheka na mafisadi, tusahau maendeleo. Tukiamua kupambana na ufisadi utaona nchi hii inaendelea kwa kasi licha ya hayo masharti ya WB na IMF.

Mafisadi wanaifuja hii nchi kuliko hata WB na IMF. Halafu, kibaya zaidi, ufisadi unaua uzalendo na moyo wa utumishi. Si kweli kwamba migomo wa walimu, manesi, madaktari, vyuo vikuu, n.k. inatokana na maslahi duni tu. Hiyo ni sababu mojawapo, tena ndogo. Ukweli ni kwamba watu hawaoni tena sababu ya kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya nchi wakati wenzao wanafyonza nchi bila jasho. Wakati wa Nyerere uzalendo ulikuwa juu, si kwa sababu watu walikuwa wanalipwa mishahara mikubwa, bali viongozi walikuwa bega kwa bega kushirikiana na wananchi kwenye shida na raha. Leo hii shida ni ya wananchi, viongozi wao wako peponi, halafu tutegemee uzalendo?

Hoja yangu ya msingi ni kwamba tuache kuwalaumu WB na IMF. Wao ni wafanyabiashara, na kila mtu anajua hayo ni mashirika ya kibepari. Hakuna hata siku moja watashusha masharti kwa ajili yetu sisi wanyonge. Ni jukumu letu kukopa kwa malengo ili huko mbeleni tujitegemee. Tusipopata akili ya namna hii, tutaendelea kulia kila siku huku tukiendelea kubaki mafukara na nchi nyingine zikitupita na kutuacha hapa hapa.

Lakini pia, kwa hali ya sasa ya kimataifa, sioni uwezekano wa kurejesha Ujamaa ule wa Mwalimu. Rasilimali zote za nchi tumeshauza, huo Ujamaa utaanzia wapi? Tukubali kwamba mambo yamebadilika, na tuwe wepesi kutumia fursa zinazopatikana kwenye mfumo wa kimataifa uliopo kwa sasa. Kuendelea kuwaza Ujamaa ni kupoteza muda. Kama ni Ujamaa, tutoe tafsiri mpya inayoendana na hali halisi ya sasa. Ujamaa ule wa 1967 usingetufikisha popote kwa sababu mazingira na mahitaji ya leo kijamii na kimataifa ni tofauti sana na ya wakati ule.
 
Naona nawewe mkuu umeingia kichwakichwa kwenye the well orchestrated trap ya kuwaaminisha watu wote kwamba vita ya kupambana na UFISADI inayoendelea ndani ya CCM, ni vita ya kuelekea uchaguzi wa 2015.

If you have been caught in that bandwagon, then CCM has a long way to go kujikomboa, maana now its 2011 but people are talking of uchaguzi wa 2015 na watu munaamini. What happened to common sense jamani?... Hapohapo umeacknowledge somewhere kuwa CDM waliweza kuvuna kura nyingi uchaguzi wa mwaka jana kwa sera ya "UFISADI"... CCM sasa wanastuka wanataka wawashugulikie hili tatizo, then inaitwa ni vita ya 2015.... Hizi spin nyingine nilitegemea vichwa kama wewe uweze kuzitambua na kutofall in.

Mramba, Yona, Kiula hawakuwa na uongozi wowote wa kitaifa ndani ya chama,na mambo yao yalishughulikiwa kiserikali zaidi na kimahakama. Kwenye siasa perceptions za public can make or break a party. Hawa walioambiwa wajivue gamba ni wajumbe wa chombo cha juu kabisa cha maamuzi kitaifa NEC. Sasa kama hukuanza na kwenye chombo cha juu kabisa kukisafisha sijui ulishauri wangeanza wapi.

Ni kweli CCM haiwezi kusafishika kwa kuwaondoa makada watatu, lakini hao makada nao wameshaonesha uchu wa ajabu wa madaraka kiasi kwamba maslahi yao binafsi wameyaweka juu ya maslahi ya chama, na hata kuhatarisha uhai wa chama. Kumbuka kila safari ya kilomita 10 inaanza na hatua moja.

Tatizo lingine la CCM ni Mwenyekiti. Kwa mtizamo wangu ni mtu anayeyumba kwa kila dhoruba litakalompiga, ilihali ana vyombo vya kumpa tahadhari ya madhoruba yanayokuja mbele yake. Mpaka mjumbe anapata ujasiri wa kumvurumushia tuhuma mwenyekiti nayeye akabaki anacheka, ni mambo yaliokuwa hayafikiriki kwa Wenyeviti wote waliotangulia.

KUTOCHUKUA MAAMUZI MAGUMU bado ni tatizo kubwa litakaloiangamiza CCM, tena mwaka wa uchaguzi wao 2012.

Kwa vile wewe bado ni mwanaCCM hai, nakushauri umwandikie waraka huu uliouweka hapa Mwenyekiti wako(hoping atausoma).

kwani Mramba na Yona wamepelekwa mbele ya sheria kwa ajili gani, si kuonyesha umma kwamba CCM na serikali yake wanapingana na ufisadi? haijalishi kama walikuwa kwenye uongozi wa CCM au lah;
Okay, lets say that matters - cheo gani kikubwa zaidi kati ya ujumbe wa NEC na Ubunge? Jibu ni Ubunge; sasa kwanini Chama kinachotaka ni kuwatoa watuhumiwa kwenye nafasi zao za NEC na kuwaachia ubunge wao kama ulivyo? haikuingii akilini kwamba kisiasa na ushindani wa 2015 NEC hata kama ni nafasi inferior to ubunge inalipa zaidi kama una nia ya kugombea urais?

Suala hapa sio la spin, ni suala lililo wazi kwamba CCM tangia mwaka 2008 haina lolote la maana inalolifanya zaidi ya makada wake kujipanga kikambi kumpokea Kikwete kijiti 2015; nashangaa kwanini hauoni hilo; vinginevyo naomba nisaidia maelezo kwamba siasa za CCM sasahivi ni zipi; hata katibu mwenezi wa chama Nape Mnauye hafanyi kazi based on his job description, amejikita katika vita dhidi ya wale wanaodhaniwa watatia nia kupitia CCM uchaguzi mkuu 2015;

CDM nakubali bado kwamba wamevuna kura nyingi sana kupitia kelele za ufisadi, lakini unashindwa kujiuliza kwanini? ni kwa sababu sera za CDM haziuziki kwani kama sio kwamba zinafanana na za CCM, basi kuna nyingine CCM ilizifuata na hazikufanikiwa miaka ya nyuma; na given hali mbaya ya kiuchumi ya watanzania wengi ambayo imepelekea jamii kugawanyika kati ya walio nacho na wasio nacho, siasa za ufisadi makujwaani zitavuna kura nyingi sana, whether by perception or reality;

Kuhusu mwenyekiti kuyumba, lazima ayumbe kama machinery yake inalegalega na imegawanyika; kumbuka mwenyekiti ni msimamizi tu, NEC ina nguvu sana katika siasa za CCM na ndio maana suala la gamba limetolewa huko na kupelekwa kamati maalum; vinginevyo ni desturi yetu watanzania kumsema mwenyekiti vibaya akiamua kutoa maamuzi magumu kama vile alivyofanya mkapa wakati fulani, lakini pia tunalaumu anapo yumba kutokana na udhaifu ulio bayana; nina uhakika kama akijipanga, atautumia uchaguzi mkuu ujao wa chama kurekebisha hilo;
 
Hoja yangu ya msingi ni kwamba tuache kuwalaumu WB na IMF. Wao ni wafanyabiashara, na kila mtu anajua hayo ni mashirika ya kibepari. Hakuna hata siku moja watashusha masharti kwa ajili yetu sisi wanyonge. Ni jukumu letu kukopa kwa malengo ili huko mbeleni tujitegemee. Tusipopata akili ya namna hii, tutaendelea kulia kila siku huku tukiendelea kubaki mafukara na nchi nyingine zikitupita na kutuacha hapa hapa.

Lakini pia, kwa hali ya sasa ya kimataifa, sioni uwezekano wa kurejesha Ujamaa ule wa Mwalimu. Rasilimali zote za nchi tumeshauza, huo Ujamaa utaanzia wapi? Tukubali kwamba mambo yamebadilika, na tuwe wepesi kutumia fursa zinazopatikana kwenye mfumo wa kimataifa uliopo kwa sasa. Kuendelea kuwaza Ujamaa ni kupoteza muda. Kama ni Ujamaa, tutoe tafsiri mpya inayoendana na hali halisi ya sasa. Ujamaa ule wa 1967 usingetufikisha popote kwa sababu mazingira na mahitaji ya leo kijamii na kimataifa ni tofauti sana na ya wakati ule.

Upo sahihi kabisa kuhusu existence ya WorldBank na IMF kama tools za mabepari kwani ni kweli worldbank is just like CRDB, NBC, etc, tofauti yao kubwa ni clients; otherwise ukiangalia stakeholders wa WorldBank kwa mfano ni wa aina gani, haraka utagundua kwamba kwao risk ni kitu wasichokitaka, so maskini hawezi pewa kipaumbele unless ni kupitia serikali yake na kwa masharti huo mkopo ufanye kazi gani ili urudi, mfano kuruhusu soko huria, kufuta kodi za aina fulani fulani, kufungua milango sekta za madini kiholela etc ili mradi tu stakeholders wa Worldbank (directly and indirectly) wanufaike;

Ni sahihi pia kwamba kurudisha ujamaa wa Mwalimu per Se kwa sasa haiwezekani; lakini sera ambazo zinalenga watanzania to own their development agenda; sera za social ownership katika maeneo kadhaa zinawezekana kabisa kama viongozi wetu wataamua kuthubutu;
 
..alipomaliza mkataba wake na IMF, Mzee Mtei aliongoza Tume ya serikali ya kurekebisha mfumo wa ukusanyaji kodi nchi. Ripoti ya Tume hiyo na mapendekezo yake ndiyo iliyopelekea kuanzishwa kwa TRA.

haya ndio nayoyazungumza; TRA kuundwa kwake haikutokana na viongozi wetu kukunwa na umuhimu wake bali hao ha IMF na WorldBank kuchoshwa na tabia ya Tanzania na nchi nyingi maskini kutojiweza kifedha kwa ajili ya maendeleo yao na badala yake misaada ya walipa kodi wa nchi tajiri na vilevile baada ya kuona kwamba nchi maskini kama Tanzania watarundika tu deni lao la nje na kupelekea defaults; wakubwa hawa wakaona njia bora ya kuwafanya wakusanye mapato yao ili watulipe madeni yetu na chenji zibaki kwa ajili ya matumizi yao ni reforming their tax system; lakini angalia matatizo yaliyopo ndani ya hizo reforms; na pia angalia kiasi gani cha kodi kinapotea from tax exemptions ambazo hao hao Worldbank/IMF wanabariki;
 
Mchambuzi,

..Thanks for ur response.

..kama ulivyoelekeza, inawezekana tunazungumzia suala hilohilo ila kwa "lafudhi" tofauti!!!

..lakini kuna wanaosema, wanaotusifia wa-Tanzania, kwamba sisi tulipata very "favorable terms" kulinganisha na wenzetu walio-negotiate na IMF/World Bank.

..I dont know why u think we need to negotiate with IMF/WB even further. Kwa mtizamo wangu, the more we kept dragging our feet in implementing IMF/WB proposals the more we compounded our economic problems.

..mimi kwa kifupi naomba nisisitize kwamba yeyote yule ambaye angekuwa ktk nafasi ya Edwin Mtei huenda angetoa ushauri uleule aliotoa Mzee wetu huyu.

..nadhani ni makosa kufikiria kwamba uchumi wetu unaweza kutengemaa kabisa kabisa kwa kupitia misaada na policies za IMF/WB peke yake. kwa mtizamo wangu mashirika hayo yanaweza kusaidia tu kuleta " nafuu/ahueni " ya kiuchumi to the point kwamba nchi inaweza kutekeleza policies zake yenyewe.

..now, tuki-fast forward mpaka 2000; je ni kitu gani kinatuzuia kuteleza sera zetu wenyewe zitakazowanufaisha mpaka na 75% ya wakulima kule vijijini?

..binafsi nadhani kinachokosekana ni NIDHAMU na UZALENDO ktk kuhakikisha kwamba tunatumia MISAADA tunayopewa, na RASILIMALI zetu, kujiletea maendeleo ambayo ni EQUITABLE and SUSTAINABLE.

..asante kwa mchango wako, sasa turejee kwenye hoja yako ya CCM kujisahihisha.
 
Mchambuzi,

..sasa hoja yako ya CCM kujirekebisha.

..hivi huoni kwamba wananchi nao wanawaponza kwa kuendelea kuwachagua?

..kwa kweli CCM isiposhindwa uchaguzi basi hili suala la kujisahihisha litakuwa gumu sana.

..CCM unayoitaka lazima itanguliwa na matokeo mabaya ya uchaguzi kwa kiasi fulani.
 
Mchambuzi,

..Thanks for ur response.

..kama ulivyoelekeza, inawezekana tunazungumzia suala hilohilo ila kwa "lafudhi" tofauti!!!

..lakini kuna wanaosema, wanaotusifia wa-Tanzania, kwamba sisi tulipata very "favorable terms" kulinganisha na wenzetu walio-negotiate na IMF/World Bank.

..I dont know why u think we need to negotiate with IMF/WB even further. Kwa mtizamo wangu, the more we kept dragging our feet in implementing IMF/WB proposals the more we compounded our economic problems.

..mimi kwa kifupi naomba nisisitize kwamba yeyote yule ambaye angekuwa ktk nafasi ya Edwin Mtei huenda angetoa ushauri uleule aliotoa Mzee wetu huyu.

..nadhani ni makosa kufikiria kwamba uchumi wetu unaweza kutengemaa kabisa kabisa kwa kupitia misaada na policies za IMF/WB peke yake. kwa mtizamo wangu mashirika hayo yanaweza kusaidia tu kuleta " nafuu/ahueni " ya kiuchumi to the point kwamba nchi inaweza kutekeleza policies zake yenyewe.

..now, tuki-fast forward mpaka 2000; je ni kitu gani kinatuzuia kuteleza sera zetu wenyewe zitakazowanufaisha mpaka na 75% ya wakulima kule vijijini?

..binafsi nadhani kinachokosekana ni NIDHAMU na UZALENDO ktk kuhakikisha kwamba tunatumia MISAADA tunayopewa, na RASILIMALI zetu, kujiletea maendeleo ambayo ni EQUITABLE and SUSTAINABLE.

..asante kwa mchango wako, sasa turejee kwenye hoja yako ya CCM kujisahihisha.

Kimsingi nipo na wewe; kwa miaka ile, nakubaliana na wewe kwamba Gavana yoyote asingefanya maamuzi tofauti sana na ya Mzee wetu mtei; kinachinifanya niwe na uwezo wa kusema haya ninayosema ni kwa sababu kweli sikuwa mtu mzima miaka ile, nimesoma tu kwenye vitabu n.k, na nimepata muda wa kuchambua kitu ambacho kilishatokea na hivyo kuwa kwenye nafasi ya kuangalia prons and cons; kimsingi, hicho ndicho kinanipa uwezo wa kuweza kusema mzee mtei alikosea wapi n.k na sio vinginevyo;

Kuhusu sisi kupewa better terms than other countries, hata mimi nimesoma sehemu juu ya hilo; tukubali ukweli kwamba baada ya Nyerere kuondoka, awamu ya pili ilikurupuka sana, na viongozi wake wengi walikuwa busy wakijaribu ku catch up maisha ya kifahari ya majirani zetu kina njonjo n.k; hapo ndipo suala la uzalendo na nidhamu unalolizungumza linaingia; hata hii leo, nimewahi kusikia wakubwa fulani fulani wakiteta malengo yao kuwa na utajiri mkubwa kama wa waziri mkuu wa Italy - Silvio Berlusconi nikabaki kujikuna kichwa;


Nakubaliana na wewe kwamba inabidi ifikie mahali hawa IMF/Worldbank waje just to complement on our own agenda, kama wanavyoingia na kutoka huko Greece na kadhalika; Kenya wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika hili, nadhani kwa sasa hawategemei misaada katika bajeti zao, sana sana labda ni mikopo tu toka IFC kwenye miradi na miundo mbinu, lakini fedha kusaidia afya, elimu, mishahara watumishiwa umma? wakenya wameshafuzu katika hilo; na njia sahihi wa sisi ni kutumia rasilimali zetu ipasavyo kujiletea maendeleo ambayo ni both kaam unavyonena - equitable and sustainable; ila kufika huko lazima tuwe kitu kikuu kimoja - chama chenye nia ya dhati katika hilo ambacho sio CDM wala CCM ya sasa (hawa wanahitaji badilika);

mabadiliko kupitia NEC - CCM kwenda huko hayawezekani; lazima tuvunjike kama chama na hili ni jambo zuri tu; linatia hofu wale wenye kuweka matumbo mbele kwani chama kikivunjika, wanashindwa la kuwaeleza wazee na vijana huko matawini na kwenye kata nini kimetokea kwani huko mpaka leo wanabeba azimio la arusha kwenye vikao; na vijana wakiwa kwenye mikutano kumpokea nape etc wanaimba kwa madaha "kauli yetu ni kulinda ujamaa na kujitegemea", huku nape anatabasamu na kupiga makofi;
 
Mchambuzi,

..sasa hoja yako ya CCM kujirekebisha.

..hivi huoni kwamba wananchi nao wanawaponza kwa kuendelea kuwachagua?

..kwa kweli CCM isiposhindwa uchaguzi basi hili suala la kujisahihisha litakuwa gumu sana.

..CCM unayoitaka lazima itanguliwa na matokeo mabaya ya uchaguzi kwa kiasi fulani.

Ni sahihi Joka Kuu, wananchi wanakiponza chama kwa kuzidi kukichagua lakini viongozi wengi hawajali hilo kwani mpaka mambo yabadilike wao watakuwa tayari wastaafu wanakula pension;

Nakubaliana na hoja yako kwamba bila CCM kushindwa uchaguzi suala la chama kujirekebisha gumu sana; lakini litajirekebisha kwa njia gani sustainable zaidi ya kuvunjika? merekebisho lazima yaanzie kwenye itikadi ambayo hadi sasa inasomeka UJAMAA NA KUJITEGEMEA; ndani ya NEC na CC, wapo wengi sana ambao wanajisikia kichefuchefu kuhusu neno 'ujamaa' lakini kwa sababu wanajua ndio njia pekee ya kuzidi kumdanganya mtanzania wa kijijini juu ya ukweli juu ya hali yake kimaisha, wanabutua ili mradi mpira uende;vinginevyo binafsi nadhani tabia ya viongozi ambao wengi ni mabepari kuwaongoza wanachama na viongozi wa chini wanaoamini bado chama kipo kwenye ujamaa ni dhambi kubwa zaidi ya ufisadi; and this is a timing bomb;

Kuhusu CCM itakayokuwa tofauti ni lazima iwe ile itakayotanguliwa na matokeo mabaya ya uchaguzi, kwa kiasi fukani upo sahihi lakini navyosoma hali ya hewa, viongozi wengi wa CCM wanazidi kuelekea kuwekeza na kujali zaidi kushinda kwenye majimbo yao kuliko kushinda urais mwaka 2015 kwani wimbi la CDM haligeuziki kirahisi; kuna baadhi ya wabunge huwa nawasikia wanatamani kuwa na status kama ya Mzee Cheyo wa UDP ambapo mtu unakuwa mbunge bila compromise zozote za ajabu, unapokea posho yako, na maisha yanasonga mbele; hii inaashiria nini? ni vigumu kuja na jibu moja sahihi;
 
Mchambuzi,

..naomba nikuulize swali personal kidogo.

..kinachokuzuia kujiunga na vyama vingine tofauti na CCM ni kitu gani?

..u have a better chance ya kujenga kitu uchokitaka from foundation up ukiwa kwenye upinzani kuliko CCM.

..CCM imeshabadilika. labda wenye matatizo ni wewe na wenye mawazo kama yako. siyo chama cha wakulima na wafanyakazi tena, ni chama cha matajiri wafanyabiashara.
 
Mchambuzi,

..naomba nikuulize swali personal kidogo.

..kinachokuzuia kujiunga na vyama vingine tofauti na CCM ni kitu gani?

..u have a better chance ya kujenga kitu uchokitaka from foundation up ukiwa kwenye upinzani kuliko CCM.

..CCM imeshabadilika. labda wenye matatizo ni wewe na wenye mawazo kama yako. siyo chama cha wakulima na wafanyakazi tena, ni chama cha matajiri wafanyabiashara.

Una kila haki ya kuniuliza swali hili kwani mwisho wa siku ni muhimu kujua mtoa hoja anasimamia wapi na analenga wapi; lakini nilishalielezea hili, mimi nina amini kwamba CCM kuvunjika isn't only inevitable but also it is desirable, kwani kama msingi wa chama ni itikadi, CCM ya sasa haina itikadi ya kweli; nipo tayari kuwa mwanachama wa kwanza wa CCM itakayomeguka na kuchukua mazuri ya azimio la Arusha, CCM ambayo itarudia kama unavyosema kuwa Chama cha wakulima na wafanyakazi; Nina imani kubwa saba kwamba hatupo mbali sana kufikia huko; suala la msingi ni je, litatokana na top – bottow approach whereby viongozi kadhaa watameguka? Au litatokana na bottom – up approach whereby wanachama hasa vijana watapata ukweli juu ya umuhimu wa kugawanya chama ili kiwe na dira na malengo yanayoeleweka, na kupelekea wanachama hawa to demand a new & different wing and then kuvuta viongozi wenye mtazamo tofauti na CCM ya sasa, mmoja baada ya mwingine; nipo tayari kuwa mmoja wa wanachama wa mwanzo wa CCM mgawanyiko;

Vinginevyo kuhamia chama cha upinzani kwa kweli zaidi ya kukupa a better chance ya kushinda ubunge au udiwani kuliko kuwa ndani ya CCM kuna nini cha zaidi? Angalau hata huko upinzani basi kungekuwa na sera mbadala za kikweli; labda kama mpango uwe kujiunga huko ili kwenda kuongeza kelele na kususa bungeni; nje ya hapo bado hakuna la maana la kumwokoa mtanzania wa kijijini; kinachohitajika ni kuwaelimisha vijana wa CCM juu ya hali halisi ilivyo ili wawe in a position kuchagua upande likotokea litakalotokea, na hilo linawezekana hata huku huku vijiweni tukiwa tunacheza bao, tukinywa kahawa na kashata; wanaobisha kuvunjika kwa chama ni wale ambao matumbo yapo mbele kuliko chochote kile, wale ambao wakienda kwenye vikao vyao majimboni wanapokelewa na salaam za siasa za Ujamaa na kujitegemea huku wazee wakipepea vitabu vya azimio la Arusha;

Kuhusu chama kuwa cha wafanyabiashara, hili ni suala inevitable; before 1992, CCM ilikuwa inajichotea fedha hazina inavyotaka lakini mfumo wa vyama vingi umepelekea chama kukaukiwa fedha; ndio maana mbadala ukawa kuegemea waanyabiashara kufadhili chaguzi na shuguli za chama kwani miradi na vitega uchumi vilivyopo havikidhi mahitaji ya chama kifedha – uendeshaji wa miradi hii ni ya kifisadi, kuanzia tawini hadi taifa;
 
@machambuzi
Lakini sijui wewe kama unaiona hili

Binafsi naona siasa zimeachngia zaidi ya 90% ya matatizo yetu lakini siasa sio hata 15% ya suluisho la matatizo yetu

Kwa hiyo hata CCM ikuvunjika mfumo na Kasumba wanasiasa kutaka kutoa suluisho a matatizo bila kuskiliza watalaam na washauri ni tatizo sugu.

Angalia sasa wabunge wa CCM wakisaidiana na wa upinzani . Wako busy kujenga heshima ya bunge na wabunge badala ya ujenga heshima ya wananchi na wapiga kurawa vijijini

Ni wabunge wacahache wanatumia japo siku 60 kati ya 360 za mwaka kuwa kwenye wilaya zao.
 
@machambuzi
Lakini sijui wewe kama unaiona hili

Binafsi naona siasa zimeachngia zaidi ya 90% ya matatizo yetu lakini siasa sio hata 15% ya suluisho la matatizo yetu

Kwa hiyo hata CCM ikuvunjika mfumo na Kasumba wanasiasa kutaka kutoa suluisho a matatizo bila kuskiliza watalaam na washauri ni tatizo sugu.

Angalia sasa wabunge wa CCM wakisaidiana na wa upinzani . Wako busy kujenga heshima ya bunge na wabunge badala ya ujenga heshima ya wananchi na wapiga kurawa vijijini

Ni wabunge wacahache wanatumia japo siku 60 kati ya 360 za mwaka kuwa kwenye wilaya zao.

Upo sahihi; Chama ni watu, sio Viongozi. Viongozi wa CCM wakiwa na mtazamo huo na wakiwajibika kwa mtazamo huo, ni dhahiri Chama kitakuwa karibu zaidi na watu kuliko ilivyo sasa; Katika Hotuba Mwalimu aliyotoa kwenye mkutano wa Uganda People's Congress mwaka 1968 alisema hivi:

"Chama si Chombo Cha Serikali. Serikali ndio chombo ambacho chama hujaribu kutekeleza matakwa ya watu na kuyahudumia masilahi yao. Kwahiyo ni wajibu wa chama kuamua misingi mikuu ambayo serikali itaendesha shughuli zake; ni wajibu wake kuamua siasa ambazo serikali yake itazifuata; bila shaka, chama hakiwezi kuwa mbadala wa serikali, hakiwezi kuifanya ile kazi iliyotafsiriwa ya kutunga sheria na kuzitekeleza, ambayo ni wajibu wa serikali kuifanya; lakini chama chenye mizizi yake katika mioyo ya watu tu, chenye wafanyakazi wenye ari vijijini na kwenye miji nchini mote – chama cha namna hiyo tu ndicho kinachoweza kuiambia serikali ni nini malengo ya watu, na kama malengo hayo yanatekelezwa kwa njia ya kuridhisha; kuwepo chama kama hicho ndiko kunakoweza kuhakikisha kwamba serikali na watu wanashirikiana kutekeleza malengo ya watu;"
--
CCM ya namna hii inawezekana;
 
Back
Top Bottom